Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Ingawa tunajua kwamba chuki dhidi ya Lissu inatokana zaidi na uwezo wake wa kijasiri wa kusema kile anachokiamini dhidi ya watawala, lakini pia wapo watu wanaomchukia Lissu kwa kuwa tu yupo hai hata baada ya jaribio la kutaka kumuua kufanyika.
Kuna watu kila wakimuona Lissu anatembea na kuendeleza harakati zake za kisiasa, ghafla wanapandwa na hasira na kuchefukwa na baadhi yao huanza kuporomosha matusi na laana kwa Lissu. Unashangaa ni kwa nini watu wachukie manusura aliyopata Lissu?
Ukiweka mkatale kwamba hawa watu hawakufurahia waliposikia Lissu kashambuliwa na yupo kwenye gema (Brink) la uvuli wa mauti, itashangaza sana. Wanaochukia leo hii kwa Lissu kuwa hai, ni wale walioshangilia siku aliposhambuliwa kwa risasi.
Mpaka leo bado wanajifaragua hadharani kwamba eti Lissu hakupigwa hizo risasi zinazosemwa kapigwa na tukio zima ni maigizo tu ya kuongeza umaarufu wa kisiasa kwa Lissu na CHADEMA. Na wakati mwingine husema kwamba ni Mbowe ndiye aliyetaka kumuua Lissu kwa kuwa eti Lissu anatishia uenyekiti Mbowe CHADEMA!!
Lakini pia labda chuki yao inakuja kwa kuwa mtu wao Kafa na Lissu aliyekusudiwa kuuawa ndiye yupo mitaani anadunda. ACHENI MUNGU AITWE MUNGU!!