Patriot
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 5,759
- 4,872
Katika kampeni zinazoendelea, tumeona sasa hata nyinbo za kisukuma zinatumika kueneza sera za chama. Kwa nini wa-TZ wanaanza kuona lugha za kienyeji ni muhimu kuliko ujumbe wa kitaifa? Je ni kufurahisha nafsi ya mkuu wa nchi bila kujali umma unaotawaliwa? Si mara ya kwanza. Kuna wakati tulilalamikia u-dini. Wakati wa rais Mwinyi, ilisadikiwa baadhi ya wanasiasa waliswali msikiti kwa kuhama kumfuata mkuu wa nchi ili awaone.
Mambo yakapamba moto, mabucha ya nguruwe yakabomolewa na kufikia awamu ya 4, makanisa yakachomwa moto na mapadri kushambuliwa. Baadhi walichoka na kupigia kelele udini. Kuna wale wanaoona kanda yao inatengwa na kusahau ndo walikowahi kutoka mawaziri wakuu 3 katika historia ya nchi hii, lakini hilo wanaona ni haki yao.
Watawala wanaweza kuwa ni wema sana, tatizo ni watawaliwa kuhangaikia urafiki na watawala kwa kuangalia nini wanachokipenda. Tuachane na hotuba za kikabila. Tuache kutumia lugha za kienyeji majukwaani. Tuache kuwatanguliza viongozi wa dini majukwaani kwa kisingizio cha kumuomba Mungu katika Siasa. Tuache kujitetea na kusema kanda yetu, kanda yetu! Haya hayatusaidii. Kilio kinakuja.