Siasa za kuegemea Ukabila, Dini na Ukanda ni tatizo linalokuja


Sisi ndio wenye taabu, wenzetu CCM wanawaelekezaji maalumu chumba cha kupiga kura, na kanda hiyo kwa kawaida wanakuwa wengi.
 

Huu utetezi sio mbaya, lakini hauridhishi na mjinga tu ndio anaweza kukubaliana nao. Huu ujinga wa kutetea makosa ya wazi kabisa ya rais unazidi kushika kasi kwa sasa. Kama huko kanda ya ziwa watu wengi hawafahamu kiswahili kwa kiwango hicho, kiasi kuwa lugha yao inahalalishwa kutumika nje ya sheria za uchaguzi, mbona fomu za serikali za kutolea huduma hazitolewi za kisukuma? Kama rais anavunja sheria za uchaguzi wazi wazi kwa kisingizio cha eneo aliloko, tunaposema huyo mtu anapandikiza ukabila nchi hii huwa mnatokwa na mishipa ya shingo kwanini.

Nimewahi kusema, na ninarudia tena, Magufuli watu wanamfumbia macho kwa haya anayoyafanya, lakini haya mambo yataleta shida ambayo itakuwa ngumu kutatulika. Nchi hii ina miaka almost 60, lugha ya taifa ni kiswahili miaka yote, iweje leo Magufuli kuingia madarakani ndio iwe lugha ya kiswahili huko kwao haieleweki?
 
Ukabila Ni ukabila tu awe mchagga, mpare msukuma, so kuutetea vile eti kabila flani limewazidi kielimu, au uchapakazi sio kigezo hicho, trend ikiwa hivi si hao wa vikabila vidogo wanabaki kuwa watumwa nchini mwao?
Ukabila, udini, Ni wa kukemewa na mtu yoyote mstaarabu, sikuhizi ka kabila lako hutakutana na mtu kupata huduma unateseka mpaka ujute, so usitetee ukabila Ni mubaya sana
 

Huwa napata tabu kubadilishana ufahamu na wewe, ni mgumu kuelewa.

Hakuna anaeunga mkono hali hii, lakini kiuhalisia ndio hali utakayo ikuta huko, sasa hauwezi ukaiondoa kwa kusema neno tuu "haikubaliki".

Lazima pawe na mbinu kitaifa kama sio kuondoa lugha ikishindikana basi iwe kufubaza. Lakini hawa jamaa wametapakaa mikoa ifuatayo na baadhi ya mikoa wanaimeza: Mara ( hasa wilaya ya Bunda na Serengeti, Hata Mbunge wetu Ester Bulaya ni Msukuma wa Bunda), Simiyu, Shinyanga, Tabora, Katavi, Geita, Songwe, Rukwa na magharibi yote ya Singida.

Na wana zaana sana, na wana uwezo mkubwa wa kujilisha bila kutegemea kusaidiwa sio watu tegemezi.

Mh. Magufuli inawaambia kila akiwa huko "mzaane sana na msiwe na uzazi wa majira" Msukuma mmoja kuwa na watoto 20 ni kawaida sanaaaa.

Mimi nina kufahamisha ni hali ilivyo kwa pamoja tutoe ushauri.
 
Bado hamjamjua jiwe ni mtu wa aina gani tu? Fanyeni kosa kumchagua tena, hayo mnayoona ya ukabila ni kwa juu juu tu ukijua undani wake pamoja na mipango yake utashangaa sana. Ni mtu hatari kabisa ondokaneni naye.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]TUME YA UCHAGUZI Ipo kimya Utadhani Haisikii Ila Tanzania
Nyerere:"Hatumchagui mtu kuwa Rais kwa kabila lake wala dini yake"!



Magufuli:"Nichagueni mimi msukuma mwenzenu,mtoto wa nyumbani"



Kuweni serious na mtakeni radhi Nyerere
John amejikita kanda ya ziwa....kwao. Ili aongee kilugha.

Kasimu Majaliwa amejikita Kusini....kwao.

Samia Suluhu (mswahili wa pwani)...amejikita pwani.

Huku ni kuendekeza ukabila na ukanda.

"Tuna rais wa ajabu haijawahi kutokea"..TAML
Sasa kila mtu akichaguliwa na Kanda yake nchi si itamegeuka vipande kila mtu ajitenge na watu wake, tutafika kweli, siasa za kikabila Ni za majitaka
Ukiwa kwa wachagga ongea kichaga, ukiwa kwa wahaya no mwiiko .
Sasa yuko usukumani , mwacheni aongee kisukuma
Thanks again


Ukabilaaaaa......!!
 

Inawezekana tatizo la ukabila, Udini na ukanda ww ndio umeliona sasa, au ulishaliona lakini ukaogopa kulisema. Sisi tulioko huru tuliliona mapema na kulisema, nyuzi za mambo hayo ziko zaidi ya moja. Kama umeamua kuwa mkweli basi tatizo hilo la ukanda sio kwamba ni tatizo lijalo, bali ni tatizo lilipo. Kwa sasa anachofanya rais analiweka wazi baada ya kulifanya muda huu wa miaka mitano na kukaliwa kimya, huku vyombo vya habari rasmi vikiogopa kulisema, na yeye anaona watu wanamuogopa, hivyo analifanya bila woga.

Kwa sasa ni juu yetu kuangalia linamalizwaje kama kuna nia njema. Lakini kwa jinsi katiba yetu ilivyo, sioni matatizo hayo yakiisha akiwa bado madarakani. Wasiwasi kwangu ni wakati anatoka madarakani, kama atakubali kutoka, haya matatizo yatakuwa makubwa kwa kiwango gani, na rais atayeingia atayatatua vipi.
 
SHERIA GANI YA NCHI IMEVUNJWA KWA MTU KUIMBA AU KUSEMA KISUKUMA ??
 

Huku kwetu kaskazini karibu yote Kilimanjaro, Arusha na Manyara kilimo cha trekta wamekwisha kukihodhi japo mashamba sio mali yao. Huku wapo kila mahala mashambani hasa muda wa kilimo. Ila ni watu wanaoweza kukaa na jamii yeyote bila usumbufu na ni wafuata sheria.
 
Tumetoa Wanne sio watatu umesahu, Tena mmoja amerudia awamu mbili
 
Huyu Jamaa tusipomkemea atatuachia taifa vipande vipande. Juzi pale Busega inajigamba eti Mkuu wa Majeshi ni msukuma mwenzangu nimemtoa hapa Busega. Yaani viongozi wote wakuu wa vyombo vikubwa vikubwa vya maamuzi ni ama wasukuma au wa kanda yake. Jaji Mkuu, IGP, DPP, wote ni wa kanda ya Ziwa. Hili halina afya kwa nchi yetu. Sikuelewa kumbe hata Mnyeti aliyejuwa mkuu wa Mkoa wa Manyara ni wa kwao! Makonda ni wa Kwao, Gwajima, ni wa kwao, Patrobasi Katambi huko huko. Hii ni hatari kubwa sana!
 
Nakuunga mkono asilimia zote
 

Mkuu hiyo kwamba unapata shida kubadilishana ufahamu na mimi hilo mbona halina mjadala. Na kwa bahati mbaya hata mimi sikubaliani na hoja zako wala kuzielewa, ila hilo sio kosa lako bali ni la kwangu.

Sasa twende pamoja kwenye huu utetezi wako dhaifu, kuwa watu wa huko wako hivyo, hivyo rais naye anapaswa kuvunja sheria ili aendane na watu wa huko. Huko kanda ya ziwa kuna mila za ukeketaji, mbona rais hapeleki vifaa vya kisasa vya kukeketea ili aendane na watu wa huko? Ni kweli watu wa huko wako hivyo, je sheria zina macho kwa udhaifu wa watu wa kabila la rais? kama rais anavunja sheria za uchaguzi waziwazi kwa udhaifu wa watu wa huko kwao, tukisema ana upendeleo na kwao kwanini mnakataa? Kama huu utetezi wako una mashiko, kwanini shule za msingi na sekondari respectively zifundishwe kwa kisukuma, ili haya anayofanya rais yapate uhalali? Ni hivi, acheni kuzunguka mbuyu, rais anavunja sheria, na anakaliwa kimya kwa sababu ya madaraka yake. Sasa hapo utapima ni wapi tunapishania kiufahamu.
 
Acha ubaguzi wa kikabila na kikanda wewe....! Hii nchi mtu yeyote na kabila lolote anaweza kuwa Rais..!!
Tunachokataa ni kuanza kuwagawa watu kwa Sera za kipuuzi za kuongea kilugha ATI unaomba kura Kama anavofanya Mfalme Jiwe😁
 

Kama watu wa huko ni wafuata sheria, je rais anakwama wapi wakati watu wa huko kwao ni wafuata sheria? Angewaambia kuwa anataka wamuelewe vizuri kwa kisukuma, ila sheria haziruhusu kuongea kisukuma, mbona wangemuelewa tu? Anapoongea kisukuma wakati anajua fika sheria za kampeni haziruhusu kisukuma, hicho ni kiburi cha madaraka. Kama hawezi kutii hata sheria za kawaida, je atakubali tume ya uchaguzi ifanye kazi yake kwa uhuru?
 

Nimekubali unalazimisha tutofautiane:

Hakuna anaeunga mkono ukabila hapa. hata kwa akili ya kawaida tuu, mimi Mpare tunaweza kufika million moja, nikiruhusu na kupenda ukabila hasara ni kwangu, Hao ni zaidi ya million 20, mtawala ni kwao, sisi wapare ni wachache tutapata wapi opportunities. Sikupenda kufika hapo.

Mkubwa asipo fuata sheria inakera zaidi: Sababu ni kawaida ya Wa afrika kuto kuchukua hatua kwa mkubwa. Na kinyume chake naona tume ingekuwa tayari ama imetoa tamko ama imechukua hatua.
 
John amejikita kanda ya ziwa....kwao. Ili aongee kilugha.

Kasimu Majaliwa amejikita Kusini....kwao.

Samia Suluhu (mswahili wa pwani)...amejikita pwani.

Huku ni kuendekeza ukabila na ukanda.

"Tuna rais wa ajabu haijawahi kutokea"..TAML

Utawala wa A5 utaiacha Tanzania ikiwa vipande vipande!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…