Siasa za kuegemea Ukabila, Dini na Ukanda ni tatizo linalokuja


Hiyo ni hoja mfu kabisa...!!
Tanzania tuna AMANI kwa vile tumeunganishwa na LUGHA MOJA YA KISWAHILI.....!!!
Kutetea kuomba Kura kwa KISUKUMA NI UHUNI na Ni kuonesha jinsi MAGUFULI ALIVO MTUPU KICHWANI.....!!!

Yamkini ndo maana hata KIINGREZA KINAMPA SHIDA kwa kuendekeza kilugha.....So rubbish!!!
 
Wapare huwa wako vizuri kichwani nashangaa wewe sijui Ni mpare wa wapi kwa hii logic yako kutetea vitu visivo faa au unatafta uteuzi
 
Sasa hivi Ni ukabila kwa kwenda mbele ndio sera ya Sasa kugawa taifa vipande pande, tangu nchi ipate Uhuru awamu hii watu wanaji proud kikabila bila woga Wala aibu, gwajima mwenyewe alishauri viundwe vikundi vya kikabila kumtetea mheshimiwa, Sasa kila kabila likianza kuji organize kikabila na kuchagua watu wao nchi itatawalika kweli.
Maana moja ya tatizo kubwa Africa Ni ukabila ndio unaoleta Hadi Vita, huku Rwanda wakipiga marufuku sisi huku ndio watu wanaanza kuleta ukabila kwa Kasi, I feel sorry for my country
 
Na sisi ccm chini kiongozi wetu jemedari Magufuli tutahakikisha watanzania mnagwanyila kikanda kidini na kikabila.
 
Kwasababu tumekosa akili na busara mambo kama haya tunayaona rahisi na niyakawaida ila yatakuja kutugharimu uko mbele.
 
k

Kinachokutesa wewe ni kwamba idadi ya wasukuma ni kubwa kuliko kabila lolote afica mashariki na kati katika watu ishirini watano ni wasukuma, sasa ukilalamika uongozi wamepewa kikabila utakufa siku si zako kinachowabeba wasukuma ni wingi wao siyo ukabila utamruka msukuma umchukue nani wakati wameuzunguka pote tena hata hivyo mshukuru Mungu wasukuma wengi walikalia kuchunga ng'ombe na kuchimba madini wangesoma kama shemeji zangu wachagga na wahaya sasa hivi tungeongea mengine. unachopaswa kufanya sasa jitahidi angalau uwe na watoto wanane ili ubalance na sisi lakini kwa staili hiyo ya chips mayai na nyota ya kijani miaka ijayo kila watu kumi 7 watakuwa wasukuma jiandae hatulembi sisi mwaume umekamilika eti una watoto watatu au wawili una akili au matope ?
 
Wapare huwa wako vizuri kichwani nashangaa wewe sijui Ni mpare wa wapi kwa hii logic yako kutetea vitu visivo faa au unatafta uteuzi
Sasa natetea nini ? Ukabila au nini? au pia ni mtu haupendi kupata general knowledge kuhusu kabila ? Kuna ukweli hatuwezi kuuzuia kuwa wao ni wengi ? Kumchukia Magufuli kusitufanye tujinyime uwezo wa tukafahamu ukweli ambao utatupa uwezo wa kukabili tatizo.

Bila kujua tatizo lolote lile lilivyo huwezi kulikabili. Jee umejaribu hata siku moja kujiuliza baada ya Magufuli, voting block hii itarithiwa na nani? Jee iachwe ibaki CCM? Haya ndio maswali muhimu sana upinzani kujiuliza kisiasa.
 
Hizi siasa za kikanda na ukabilia zipo sana chadema,safari mmemkuta mtu anayejua hizo siasa mnakuja kulialia kuwa mnavutwa shati.
 
Siwezi kuteswa na kabila nasimamia kilicho sahihi and not otherwise kamwe siwezi kuteswa ukisema wingi hata mbugani nyumbu Ni wengi kwa idadi Ila hawana akili na wanaliwa Sana na wanyama, so uwingi sio tija if usipokuwa smart na kuwa proactive, so for that fact kila kabila lianze kujitetea na kuestablish Kanda zake unafikri ka taifa tutafika wapi, refer case nyingi za Africa na matatizo yake, kuanzia huko Rwanda, Nigeria Hadi kukawa na Biafra war, so kuongelea uwingi doesn't make sense ingekuwa waasisi wetu wamesimamia ukabila tungefika kweli?
Think out of the box so akija Raisi kabila jingine na yeye aanze kutumia ukabila?
 
Huna hoja zaidi ya ujinga tu unaoendelea kuandika hapa jukwaani. Huyo utopolo anatumia kigezo cha ukabila kutafuta kura. Hata Nyerere alipinga huu uwendawazimu.
 
Umeelewa kilichoandikiwa?
 
Alafu tume ya uchaguzi ipo kimyaaa... Badala ya kukemea maneno na uchochezi wa ubaguzi...
 
Nyerere:"Hatumchagui mtu kuwa Rais kwa kabila lake wala dini yake"!

Magufuli:"Nichagueni mimi msukuma mwenzenu,mtoto wa nyumbani"

Kuweni serious na mtakeni radhi Nyerere.
Kuna kabila moja linataka kuona kila mtu ni mshamba na limetengeneza wapambe kibao!!
 
Hongera kwa kufika ujerumani!
 
Nakuongezea tena labda huelewi unachokililia Magufuli kuongea kisukuma akiwa usukumani kosa liko wapi lakini pia ametumia lugha ya wasukuma kufikisha ujumbe alioukusudia kwao kama vile kuna bible za kigogo na makabila mengine lengo ni kufikisha ujumbe kwa njia sahihi ukabila unakuwa hivi Ma dc na wengine wote ni wasukuma lakini haliko hivyo sasa kusema lugha ya kwenu ukiwa kwenu nayo iwe hoja ya ukabila pole sana kwa hilo unalolitaka kulipanda pia zingatia kuwa Rais ni kama wewe yuko huru kuongea na jamii alikotoka usimpangie kila kitu heshimu uhuru wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…