Yaani kwa CCM yetu ni kama vile hakuna MAISHA nje ya madaraka. Mazoea mabaya kweli hayo. Yamevuruga hadi chaguzi zetu. Sasa wanataka vyote kabisa. Urais, Bunge na Halmashauri zote kabisa. Vijiji na mitaa walishachukua vyote.k
Kinachokutesa wewe ni kwamba idadi ya wasukuma ni kubwa kuliko kabila lolote afica mashariki na kati katika watu ishirini watano ni wasukuma, sasa ukilalamika uongozi wamepewa kikabila utakufa siku si zako kinachowabeba wasukuma ni wingi wao siyo ukabila utamruka msukuma umchukue nani wakati wameuzunguka pote tena hata hivyo mshukuru Mungu wasukuma wengi walikalia kuchunga ng'ombe na kuchimba madini wangesoma kama shemeji zangu wachagga na wahaya sasa hivi tungeongea mengine. unachopaswa kufanya sasa jitahidi angalau uwe na watoto wanane ili ubalance na sisi lakini kwa staili hiyo ya chips mayai na nyota ya kijani miaka ijayo kila watu kumi 7 watakuwa wasukuma jiandae hatulembi sisi mwaume umekamilika eti una watoto watatu au wawili una akili au matope ?
Mkuu unatumia nguvu nyingi kumuelewesha mtu mambo ambayo yanazidi uwezo wake kufikiri.Siwezi kuteswa na kabila nasimamia kilicho sahihi and not otherwise kamwe siwezi kuteswa ukisema wingi hata mbugani nyumbu Ni wengi kwa idadi Ila hawana akili na wanaliwa Sana na wanyama, so uwingi sio tija if usipokuwa smart na kuwa proactive, so for that fact kila kabila lianze kujitetea na kuestablish Kanda zake unafikri ka taifa tutafika wapi, refer case nyingi za Africa na matatizo yake, kuanzia huko Rwanda, Nigeria Hadi kukawa na Biafra war, so kuongelea uwingi doesn't make sense ingekuwa waasisi wetu wamesimamia ukabila tungefika kweli?
Think out of the box so akija Raisi kabila jingine na yeye aanze kutumia ukabila?
Kuongea kikabila hairuhusiwi kwenye official matters na hii imeanza awamu hii why tangu mwanzo haikuwepo maana sikuhizi sio ukabila tu hata kuvunja na kutokufata Sheria imekuwa Ni Jambo la kawaida, ukabila haufai Sasa kila mtu akianza kuvutia upande wa kabila lake tutafika, mbona Jakaya alikuwa Raisi hatukuona akiongea kikwere, Mara muje na hoja ya wingi sijui Nini eti kufikisha ujumbe, Ina maana awamu hii wasukuma ndio hawajui kiswahili mpaka kianze kikabila, na nchi hii kila mahali watu wanaongea kiswahili Hadi huko ndani ndani, why nowdays.Nakuongezea tena labda huelewi unachokililia Magufuli kuongea kisukuma akiwa usukumani kosa liko wapi lakini pia ametumia lugha ya wasukuma kufikisha ujumbe alioukusudia kwao kama vile kuna bible za kigogo na makabila mengine lengo ni kufikisha ujumbe kwa njia sahihi ukabila unakuwa hivi Ma dc na wengine wote ni wasukuma lakini haliko hivyo sasa kusema lugha ya kwenu ukiwa kwenu nayo iwe hoja ya ukabila pole sana kwa hilo unalolitaka kulipanda pia zingatia kuwa Rais ni kama wewe yuko huru kuongea na jamii alikotoka usimpangie kila kitu heshimu uhuru wake.
Lazima aeleweshe maana hajui kiongozi kuwa kabila flani haimaanishi kila Jambo awe sahihiMkuu unatumia nguvu nyingi kumuelewesha mtu mambo ambayo yanazidi uwezo wake kufikiri.
Katika kampeni zinazoendelea, tumeona sasa hata nyinbo za kisukuma zinatumika kueneza sera za chama. Kwa nini wa-TZ wanaanza kuona lugha za kienyeji ni muhimu kuliko ujumbe wa kitaifa? Je ni kufurahisha nafsi ya mkuu wa nchi bila kujali umma unaotawaliwa? Si mara ya kwanza. Kuna wakati tulilalamikia u-dini. Wakati wa rais Mwinyi, ilisadikiwa baadhi ya wanasiasa waliswali msikiti kwa kuhama kumfuata mkuu wa nchi ili awaone.
Mambo yakapamba moto, mabucha ya nguruwe yakabomolewa na kufikia awamu ya 4, makanisa yakachomwa moto na mapadri kushambuliwa. Baadhi walichoka na kupigia kelele udini. Kuna wale wanaoona kanda yao inatengwa na kusahau ndo walikowahi kutoka mawaziri wakuu 3 katika historia ya nchi hii, lakini hilo wanaona ni haki yao.
Watawala wanaweza kuwa ni wema sana, tatizo ni watawaliwa kuhangaikia urafiki na watawala kwa kuangalia nini wanachokipenda. Tuachane na hotuba za kikabila. Tuache kutumia lugha za kienyeji majukwaani. Tuache kuwatanguliza viongozi wa dini majukwaani kwa kisingizio cha kumuomba Mungu katika Siasa. Tuache kujitetea na kusema kanda yetu, kanda yetu! Haya hayatusaidii. Kilio kinakuja.
Sasa kila mtu akichaguliwa na Kanda yake nchi si itamegeuka vipande kila mtu ajitenge na watu wake, tutafika kweli, siasa za kikabila Ni za majitaka.
Kuhusu matumizi ya Kisukuma kwa kanda ya magharibi:
Tatizo kubwa lipo kwenye eneo husika, unaweza kutoka Shelui Singida zaidi ya kilomita 450 kwenda Bunda, na zaidi ya kilomita 750 na kutoka Simiyu mpaka Mpanda unaongea kisukuma tuu na ukafanya karibu shuguli zote za kijamii.
Kama hautaki kuwa na masiliano na jamii zingine chache zinazo kuzunguruka ambazo huongea lugha nyingine na sio Kisukuma, lugha ya kiswahili hautoijua.
Kinacho endelea sasa hivi ni lugha nyingine ndogo ndogo zimemezwa na zinaendelea kupotea.
Sasa hivi Kisukuma ni lugha inayotumika na idadi kubwa ya wakazi wa kanda ya magharibi na wengine sio Wasukuma kabisa ili waweze kuwa na mawasiliano na wazungumzaji.
Na kuna maeneo inatumika kama lugha ya kwanza na sio kiswahili kwa baadi ya wakazi wa Magharibi mwa Tanzania. Na wageni kutoka maeneo mbali mbali hasa wafanya biashara bila Kisukuma katika hayo maeneo biashara yake haito kwenda vizuri, sababu atashindwa kuwasiliana na wateja.
Na mbaya zaidi wenzetu hawataki kujifundisha lugha nyingine mbali na Kisukuma.
Bila kusahau mkoa wa Kagera wilaya ya Biharamulo 3/4 ya wakazi wa wilaya hiyo ni wasukuma, Muleba nayo maeneo ya Shimwanyi na Kyamuyolwa ni wasukuma watupu. Wilaya ya Ngara sasa robo ni wasukuma huku Wilaya za Kakonko na Uvinza mkoani Kigoma zikibadilika chapuchapu kuwa SukumalandHuwa napata tabu kubadilishana ufahamu na wewe, ni mgumu kuelewa.
Hakuna anaeunga mkono hali hii, lakini kiuhalisia ndio hali utakayo ikuta huko, sasa hauwezi ukaiondoa kwa kusema neno tuu "haikubaliki".
Lazima pawe na mbinu kitaifa kama sio kuondoa lugha ikishindikana basi iwe kufubaza. Lakini hawa jamaa wametapakaa mikoa ifuatayo na baadhi ya mikoa wanaimeza: Mara ( hasa wilaya ya Bunda na Serengeti, Hata Mbunge wetu Ester Bulaya ni Msukuma wa Bunda), Simiyu, Shinyanga, Tabora, Katavi, Geita, Songwe, Rukwa na magharibi yote ya Singida.
Na wana zaana sana, na wana uwezo mkubwa wa kujilisha bila kutegemea kusaidiwa sio watu tegemezi.
Mh. Magufuli inawaambia kila akiwa huko "mzaane sana na msiwe na uzazi wa majira" Msukuma mmoja kuwa na watoto 20 ni kawaida sanaaaa.
Mimi nina kufahamisha ni hali ilivyo kwa pamoja tutoe ushauri.
Ila wangeimba kwaito wangeshangilia !SHERIA GANI YA NCHI IMEVUNJWA KWA MTU KUIMBA AU KUSEMA KISUKUMA ??
Siwezi kuteswa na kabila nasimamia kilicho sahihi and not otherwise kamwe siwezi kuteswa ukisema wingi hata mbugani nyumbu Ni wengi kwa idadi Ila hawana akili na wanaliwa Sana na wanyama, so uwingi sio tija if usipokuwa smart na kuwa proactive, so for that fact kila kabila lianze kujitetea na kuestablish Kanda zake unafikri ka taifa tutafika wapi, refer case nyingi za Africa na matatizo yake, kuanzia huko Rwanda, Nigeria Hadi kukawa na Biafra war, so kuongelea uwingi doesn't make sense ingekuwa waasisi wetu wamesimamia ukabila tungefika kweli?
Think out of the box so akija Raisi kabila jingine na yeye aanze kutumia ukabila?
Huna hoja zaidi ya ujinga tu unaoendelea kuandika hapa jukwaani. Huyo utopolo anatumia kigezo cha ukabila kutafuta kura. Hata Nyerere alipinga huu uwendawazimu.
Naunga mkono hoja.Katika kampeni zinazoendelea, tumeona sasa hata nyinbo za kisukuma zinatumika kueneza sera za chama. Kwa nini wa-TZ wanaanza kuona lugha za kienyeji ni muhimu kuliko ujumbe wa kitaifa? Je ni kufurahisha nafsi ya mkuu wa nchi bila kujali umma unaotawaliwa? Si mara ya kwanza. Kuna wakati tulilalamikia u-dini. Wakati wa rais Mwinyi, ilisadikiwa baadhi ya wanasiasa waliswali msikiti kwa kuhama kumfuata mkuu wa nchi ili awaone.
Mambo yakapamba moto, mabucha ya nguruwe yakabomolewa na kufikia awamu ya 4, makanisa yakachomwa moto na mapadri kushambuliwa. Baadhi walichoka na kupigia kelele udini. Kuna wale wanaoona kanda yao inatengwa na kusahau ndo walikowahi kutoka mawaziri wakuu 3 katika historia ya nchi hii, lakini hilo wanaona ni haki yao.
Watawala wanaweza kuwa ni wema sana, tatizo ni watawaliwa kuhangaikia urafiki na watawala kwa kuangalia nini wanachokipenda. Tuachane na hotuba za kikabila. Tuache kutumia lugha za kienyeji majukwaani. Tuache kuwatanguliza viongozi wa dini majukwaani kwa kisingizio cha kumuomba Mungu katika Siasa. Tuache kujitetea na kusema kanda yetu, kanda yetu! Haya hayatusaidii. Kilio kinakuja.
Wasukuma kunyanyaswa ilikuwa lini na wapi walinyamyaswa, na Hilo zimwi lilikuwa wapi kuamka siku zote, all I see ni inferiority complex tu na kuhalalisha uvunjifu wa vitu ambavyo havikuwepo.Leo ndio umelijua hilo ? Mlizoea kuwanyanyasa wasukuma, sasa zimwi limeamka na kumbuka wako ml 9 nchi hii.
Ni lini ulikuta mhaya, mchagga au mnyakusa anaongea kikabila ili kupata pity votes, let's accept they are smart and ahead of you, kamwe huwezi kukuta wanafanya Mambo ya ajabu hadharani, hata ka kubebeana Ni kwa u smart wa Hali ya juu Hadi watu kushtukia Ni ngumu.Acha hizo wewe nani mkabila ? Wachagga, wahaya na wanyakyusa ndio waendekeza ukabila nchi hii ila mmeshikwa pabaya awamu hii kazi kulia lia tu.
Huko ujerumani walikuwa wanagombea nafasi ya kitaifa kwa kisukuma?Mwaka 2004 nilienda Ujerumani, Nilishangaa kukuta wasukuma kule na wanapiga Lugha Lao kama kawaida! Sembuse mahali walikozaliwa!
Ingawa sio vema kuendekeza mi Lugha asili kwenye mambo ya kitaifa, lakini tusiwe na nongwa watu wakikutana wakaanza kuchapa Lugha zao za Asili, Nawapenda Waha hawaogopi kupiga Lugha Yao mahali popote pale