Siasa za Kukurupuka: Hatimaye Zimbabwe Yaanza Kuwafidia Mabilioni Wakulima wa Kizungu Walioporwa Mashamba Yao na Mugabe

Baada ya aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Marehemu Mugabe kuwapora Walowezi wa Kizungu na ambao walikuwa raia wa Zimbabwe wenye Asili ya Uingereza,hatimaye Serikali imetangaza kuanza kuwalipa mabilioni ya fidia kutokana na kuporwa Mali Yao.

Uporaji wa mashamba ya Walowezi wa Kizungu ulifanyika kama kete ya Kisiasa ya Mugabe kushinda uchaguzi na ilipelekea Nchi hiyo kuwekewa vikwazo Vikali na kuporomoka Kwa Uchumi na kuigeuza Zimbabwe ambayo ilikuwa na usatwi kuwa Moja ya Mataifa ya kishenzi yaani failed state.

View: https://twitter.com/BloombergAfrica/status/1791501940385317125?t=O5kGCm3t2SSf7HdDHvEqKw&s=19

My Take
Hizo ndio hasara za siasa za Kukurupuka na mihemko.Kiko wapi Sasa? Unalipa na fidia Juu.

Kunae yule wa makinikia nae alitaka afanye hayo hayo kabla ya kurudi nyuma japo aliwafanyia wafanyabiashara wa Beureu De Change ambao Samia kawarudishia pesa zao.

Pia soma Zimbabwe: Mamia ya Wakulima wa Kizungu Waliotimuliwa na Hayati Mugabe Warejea kwa wingi kuendeleza kilimo chao

Ni ujinga, nchi imekuwa fukara sababu ya maamuzi ya mjinga mmoja
 
hata kama alikuwa dikteta lakini na waingereza walimwingiza chaka kwa wazungu. Nadhani walitaka asifanikiwe kwa vyo vyote vile. Ila na wao walikumbana na kisiki cha mpingo.
Angekuwa mzalendo angetawala Zimbabwe hata miaka kumi na mitano halafu angefanya uchaguzi huru mtu mwingine atawale na kuendeleza mazuri aliyoyaanzisha ya kuwafukuza Wazungu,Lakini hakuamini katika akili za wengine na ndiyo maana muda ulipofika wa kumtema chini aliugua na kufa kwa sababu alikuwa na tamaa ya kuabudiwa kama mtu muhimu sana kuwahi kutokea Zimbabwe.Huu ulikuwa udhaifu wa dikteta Mugabe kama vile udhaifu wa Yoeri Mseveni na Kagame.
 
Zimbabwe ilipokuwa inatawaliwa na Mzungu ilikuwa nchi tajiri sana hata kuzidi nchi yetu.Kulikuwa kama Ulaya maisha yalikuwa mazuri.Wazimbabwe hawakuwa na njaa,walisoma bure,walitibiwa bure.Walikuwa na viwanda ila baada ya mshenzi Mugabe kutawala kila kitu kiliharibika Zimbabwe.
Achana na hoja mufisilisi wazibabwe sio wajinga kudai uhuru kwaiyo wewe ukibiwa ufanyiwe kinyume kisa huduma za Bure utakubali?
 
Wazimbabwe wapi walifanywa kinyume? Mbona wanawalilia tena hao Wazungu na wanawalipa pesa Juu?

Wazimbabwe walikuwa na shida zipo kabla ya yule tapeli Mugabe kuvurunda uchumi wao?

Ni kama nyie mlivyokuwa mnawaimbia watu uzalendo na unyonge wakati mnafisadi keki ya Taifa.
 
Achana na hoja mufisilisi wazibabwe sio wajinga kudai uhuru kwaiyo wewe ukibiwa ufanyiwe kinyume kisa huduma za Bure utakubali?
Wangedai uhuru kwa Haki Mugabe asingetawala miaka yote ile kwa sababu wangemtoa na kumweka mwingine wa kuwavusha kwenye dimbwi la umaskini.
 
Mkuu Chukua soda nakuja kulipa

Mugabe na huyo aliyewarudishia mashamba na fidia wazungu mjinga ni huyu aliyewarudisha wazungu, sijui kahongwa nini Waafrika wengi ni useless
Tunatanguliza maslahi ya watu weupe kuzidi ya kwetu

Tumekaa tu hapa na utapiamlo, baadhi wanaona wanapesa lakini tukizigeuza in terms of dollar Sisi ni Makapuku..!🚮
Ni ujinga kupora ardhi mtu anayelima kwa kutumia zana za kisasa, kisha kumpa mtu anayetumia jembe la mkono eti ni uzalendo. Hayo mashamba wakati Mugabe anawapota wazungu yalikuwa yanazakisha Hadi ziada, wakapewa weusi yakiwa na miundombinu yote ikaishia kufa. Huu ujinga ndio alifanya Nyerere kupora wazungu Mali zao, viwanda wakapewa makada wa ccm vikafa vyote.
 
Tangu Balozi wa Marekani ate mbelen ofisi za makao makuu ya JF siku chache zilizopita, nahisi kabisa moderators na wamiliki mnashikiwa akili na Mabeberu, na hili jukwaa ni mradi tukufu wa mabeberu against Africanism.

Maana kazi yenu ni kuwaponda viongozi wa kiafrika hasa waliodiriki kuonesha uzalendo wao kwa kutanguliza maslahi ya waafrika kwanza.
Kwangu mimi hii ni aibu hasa kwa mleta maada maana ni wazi uko upande wa hao mabwana zenu.
Mkuu Sio kweli Kwa balozi anahusika Kwa lolote hapa 👆.
Alichokufanya Mugabe ni siasa za chuki juu ya jamii Fulani, kumbuka Hao anao waita white ni raia wa Zimbabwe.
Kabla ya Hapo Zimbabwe ilikuwa na uchumi mzur Sana , Sasa Leo Kiko wapi?,
Acheni wivu wa kijinga wawezesheni vijana wenu waweze kumiliki sectors mbalimbali za uchumi na Sio kwenda kupora Mali za watu
 
Ushauri mzuri huu uliyoenda shule.Asante mkuu.
 
Ni ujinga kupora ardhi mtu anayelima kwa kutumia zana za kisasa, kisha kumpa mtu anayetumia jembe la mkono eti ni uzalendo. Hayo mashamba wakati Mugabe anawapota wazungu yalikuwa yanazakisha Hadi ziada, wakapewa weusi yakiwa na miundombinu yote ikaishia kufa. Huu ujinga ndio alifanya Nyerere kupora wazungu Mali zao, viwanda wakapewa makada wa ccm vikafa vyote.
Ni kweli kabisa ,Hao anao waita White's wamefanya Zimbabwe uchumi wake ukawa Imara, alivyo wafukuza nn kimetokea,
 
Baada ya aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Marehemu Mugabe kuwapora Walowezi wa Kizungu na ambao walikuwa raia wa Zimbabwe wenye Asili ya Uingereza,hatimaye Serikali imetangaza kuanza kuwalipa mabilioni ya fidia kutokana na kuporwa Mali Yao.

Uporaji wa mashamba ya Walowezi wa Kizungu ulifanyika kama kete ya Kisiasa ya Mugabe kushinda uchaguzi na ilipelekea Nchi hiyo kuwekewa vikwazo Vikali na kuporomoka Kwa Uchumi na kuigeuza Zimbabwe ambayo ilikuwa na usatwi kuwa Moja ya Mataifa ya kishenzi yaani failed state.

View: https://twitter.com/BloombergAfrica/status/1791501940385317125?t=O5kGCm3t2SSf7HdDHvEqKw&s=19

My Take
Hizo ndio hasara za siasa za Kukurupuka na mihemko.Kiko wapi Sasa? Unalipa na fidia Juu.

Kunae yule wa makinikia nae alitaka afanye hayo hayo kabla ya kurudi nyuma japo aliwafanyia wafanyabiashara wa Beureu De Change ambao Samia kawarudishia pesa zao.

Pia soma Zimbabwe: Mamia ya Wakulima wa Kizungu Waliotimuliwa na Hayati Mugabe Warejea kwa wingi kuendeleza kilimo chao

Nasikia wa vyeti fake nao wapo njiani!
 
Back
Top Bottom