Siasa za Mwalimu Nyerere za Ujamaa wa kujitegemea na itikadi yake ya Azimio la Arusha ndio chanzo cha umaskini wa Tanzania

Dogo hujui usemalo wala hujui sera mbovu na siasa na uongozi mbaya ndio chanzo cha umasikini wa nchi na wananchi wenyewe

Serikali inatakiwa kutengeneza mazingira mazuri kwa raia wake kujifanyia shughuli zao na kupata vipato kisha walipe kodi nchi izidi kufanya maendeleo

Hao massikini wa nchi tajiri za kibepari wanatofauti kubwa sana na maskini wa nchi za kijamaa
 
Umenena vyema mkuu
 
Umekiri mwenyewe kuwa mfumo aliyotumia mwalimu Nyerere ni mfumo Na. 1 ambao ni ujamaa umeuleza mfumo huo kuwa ndio uliomkwamisha kuleta maendele umekiri mwenyewe hapo

Ndio kitu ambacho na mimi nimekieleza kwenye uzi wangu sasa hiyo mitusi yako yote uliyotukana umejitukana mwenyewe hongera dogo
 
Mbona nimekuambia kuwa hakuna nchi hata ambazo azikufuata mfumo wa ujamaa na kujitegemea zilizo fanikiwa kufanya vizuri kati ya nchi za waafrica ...makosa yalikuwepo ila nilichopinga mimi ni nyinyi mnaosema ujamaa na kujitegemea ....ukipima ufanisi wa tz na nchi zingine nyingi kipindi cha nyerere tulikuwa tumeziacha mbali sana . Hata shiling yetu ilikuwa sawa tu na kenya
 
Wakati wa ujamaa unaomlaumu Nyerere tulikuwa na viwanda vikubwa vya nguo, kuchakata na kusindika mazao, elimu bure, afya bure.
Tuje Sasa utueleze tangia mfumo ubadilike ni kitu gani kimeboreshwa, Sasa hivi taifa limekuwa la wachukuzi Kila kitu tunaagiza tumebaki kuongea miaka ya sitini Tanzania na nchi za Asia zilikuwa na uchumi sawa miaka ya 60.
Kilichomkwamisha Nyerere kinaeleweka mtu amekufa zaidi ya miaka 25 mmeshindwa Nini kufanya mabadiliko.
 
Mkuu, nadhani wataelewa tu, usikate taama; ni jukumu letu kuwa elimisha.
 
Hii mifumo utaibadilisha bila wahusika kukubali? mfano tu matumizi ya hovyo misafara kuanzia DC kwenda juu na wizi wa mali za umma, wewe una mahakama ako?
Sasa hapo Nyerere kosa lake liko wap yy aliweka mifumo yake kwa hicho kpnd na wanch kwa wakt huo aliaona n sawa aya saivi n kzaza kngne ya technology je kiongoz mkubwa ambayo n rais yy ndy anayo mamlaka kwa mujibu wa katba wa kuamua kubalisha baadh ya matumz ya umma mfano R I P magufuli yy alikuwa muwazi badh ya sera zake n kubana matumiz na tuliona ivyo ndy mamb yanapaswa ya fanyike kwa wakat uliopo kama unataka kwendanana na mifumo ya sasa
 
Rwanda wamepigana vita hati miaka ya tisini sasa hivi wanasonga mbele. Miaka 200 baadaye utaendelee kumlaumu Nyerere. Kisa kuwakingia kifua wahalifu waliopo madarakani. sasa.
 
Ukweli mchungu sana huu na.ukitaka kujua mapungufu ya mchonga msikilize TAL sana.
Utaelewa kwamba hayati hakuwa malaika bali kuna.mambo aliyafumbia macho makusudi.
 
Hii hata wanasiasa niliyokuwa nawaheshinu sana nawasikia wanaongea upumbavu huu!!
Mara tena ooh Nyrere ndiye katutia uoga wa kuandamana! Kweli? Uzembe wa vijana waliozaliwa wakati wa Mkapa wakakua enzi za Kikwette kasababisha Nyerere??!!

Wameshindwa katika zama zao wanamsingizia Mwalimu!!
 
Ni kama Mwl ,aliwahi kwenda kwenye Ujamaa kabla ya kupitia kwenye Ubepari mode of production..

Jingine hili la lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia elimu ya Msingi nadhani haikuwa sawa.. ona sasa tumekuwa kama KISIWA..though ana mazuri yake
 
Ukweli mchungu sana huu na.ukitaka kujua mapungufu ya mchonga msikilize TAL sana.
Utaelewa kwamba hayati hakuwa malaika bali kuna.mambo aliyafumbia macho makusudi.
Huyo TAL ndiyo kawa mwendawazimu kabisa!!

Kashindwa kushawishi wananchi ili aeleweke anataka nini kwa manufaa ya taifa, anaishia kumtukana Mwalimu!
Ni kukosa akili nani utaahira wa hali ya juu mno.

Hivi Nyerere wakati anadai uhuru angekuwa anawatunakana kina Mkwawa, Kimweri, Mirambo n.k kuwa walikuwa vibaraka tu wa wakoloni yeye ndiye ana akili...unadhani watanganyika wangemuunga mkono katika kudai uhuru!?
 
🤣🤣🤣 aiseee kwl kabsaa
 
Sahivi kuanzia DC kwenda juu kila mtu kwenye ziara anakuwa na msafara wake siyo chini ya gari 10 na hapo unakuta wameenda kuangalia kisima cha maji cha milioni 3, mpaka unajiuliza kuna hatari gari DC kwenda na polisi kwenye kisima jamani? utadhani nchi ipo vitani
 
Wawaulize ni akina nani waliyatoa madini yetu ya Dhahabu na Gesi kwa bei ya Bure kwenye mikataba Umiza !

Waliosaini hiyo mikataba ndio wametusababishia Umasikini !
 
Ili watu waendelee kupiga mkwanja ni lazima watafute mtu wa kumsukimia jumba bovu !
Tumewastukia Mazee !
Mikataba ya kimagumashi ya Madini ya Dhahabu na Gesi ndio iliyosababisha Nchi kuendelea kuwa Masikini !!

3% ! Kweli ???!! 😱🤦🏽‍♂️ Makinikia 😱🤦🏽‍♂️
Eti ni mchanga tu !!😳🙄
 
Kwa ujengaji hoja yako hitimisho lako ni kwamba Tanzania ni maskini kwasababu ya Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea iliyoletwa na Mwl. Nyerere sio? Swali langu sasa;
'Je, nchi zingine za Kiafrika ambazo HAZIKUFUATA siasa za Ujamaa na Kujitegemea za Mwl. Nyerere ziliendelea kimaendeleo kuliko Tanzania?
NB: Naomba unijibu swali langu ukizingatia Tanzania ni nchi ya tisa kwa maendeleo ya kiuchumi Afrika kati ya nchi zaidi ya arobaini na tisa Afrika.

Natanguliza shukrani!
 
Nyerere alitufelisha sana kama nchi basi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…