Siasa za Mwalimu Nyerere za Ujamaa wa kujitegemea na itikadi yake ya Azimio la Arusha ndio chanzo cha umaskini wa Tanzania

Hilo liko Hilo.liko wazi lakini ilikuaje mkamuacha Magufuli akaanza kuleta siasa za kipuuzi kama hizo?
 
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anatembea na vitabu viwili , Bible na Azimio la Arusha, tatizo ni utekelezaji tuu wa ujamaa wetu.
P
Nyerere mwenyewe alishindwaje utekelezaji wa ujamaa? Hakuwa na upinzani wa kisiasa, vyombo vyote vya habari vilikuwa vinamilikiwa na serikali yake, vyombo vya usalama vilikuwa chini yake na vilimtii, katiba ilimpa nguvu ya kufanya mambo mengi, sasa kilichomkwamisha ni nini?

Kama jibu ni vita ya Kagera ndiyo ilitukwamisha, kwa nini vita ya Kenya na Somalia ambayo ni ya muda mrefu zaidi ya vita ya Kagera, haikwamishi uchumi wa Kenya?
 
Sababu ni moja tuu na niliisha itajaga kwenye uzi huu Je, maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu au vitu? Wachumi tusaidieni, uchumi wa Awamu ya 5, unalisaidia Taifa au utaliangamiza?
Nilisema

P
 
Ujinga na uongo mtupu. Kazi hamfanyi, Magufuli alikuwa serious kwa miaka 4 tu nchi ikaingia uchumi wa kati na mamiradi ya maana kibao
 
Tatizo ni mfumo aliyoweka hautoi fursa ya maendeleo na wote wanaokuja mbele yako wanaogopa kuufumua mfumo wa siasa za hovyo zilizoasisiwa a mwalimu hawataki katiba mpya ambayo ndio dira ya maendeleo ya nchi
 
Huo ndiyo ujamaa wa kiserikali na ujamaa wa umma (kiraia)kamwe auwezi kufanikiwa kiuchumi kwa njia hiyo ila taifa linakuwa halina stress sana unapo fuata mfumo huo... watu wanakuwa very slow wasio na masindano ya kimaendeleo ...kitu kilicho takiwa hapo ni nyerere kukubali secta binafsi iwe ya kibepari ila serikali iwe ya kijamaa ....
 
Ukweli mchungu sana huu na.ukitaka kujua mapungufu ya mchonga msikilize TAL sana.
Utaelewa kwamba hayati hakuwa malaika bali kuna.mambo aliyafumbia macho makusudi.
mwite huyo tundulisu aje tukutane na mimi hapa kama utaendelea tena kumsifu...Huyo tundu lisu ndiyo kiazi mbatata kabisa ...hata kama yupo humu muite... huyo ni mpuuzi tu kama zitto
 
Wamekuja marais wengine wanne mpaka kufikia Samia, na wao unawalaumu kwa umaskini huu wa leo?

Huoni aibu kumlaumu hayati aliyekwisha kulala usingizi wa milele?.
 
Walalamikaji wengi ni hawa mashujaa wa nyuma ya keyboard, hawajui yanayoendelea katika nchi yao wenyewe.

Watamlaumu kila mwanasiasa wanayeweza kumlaumu, watamlaumu kila mtu isipokuwa wao wenyewe. Hawana utashi wa kujitazama wamekosea wapi na wafanye nini ili wayafute makosa yao.
 
Ukweli maovu yote ya watawala yanatokana na yeye
Mkuu Nyerere kafariki siku nyingi mno. Kama walifuatilia wangekuwa viongozi wazuri wangeweza kurekebisha zamani sana. Mimi kwanza naona kadiri siku zinavyokwenda ndivyo viongozi wanavyozidi kuwa wa hovyo kulinganisha na Nyerere. Ila sisemi kuwa hakuwa na makosa, la hasha. Kwa mfano elimu, aliiharibu kwa kuingiza mifumo ya majaribio na elimu kwa lugha ya kiswahili kitu kilichofanya tuzalishe wahitimu vilaza. Kenya waliendelea na mfumo wa elimu wa kikoloni ona walivyo na wasomi wengi wenye weledi.
 
Nchi ngapi ambazo hazikufuata ujamaa hapa Africa, unaweza kusema zimetuacha kimaendeleo?

Kenya tu hapo, wana uchumi mkubwa kuliko sisi, lakini kimaendeleo tuko nao sambamba.

Mifumo ya kiuchumi ya kimataifa ni ya kibeberu na imewekwa katika hali ambayo NYERERE au kiongozi yeyote wa kiafrica ANGEFANYA VYOVYOTE, bado kulikuwa hamna kutoboa. Mifumo inataka muda wote sisi tuendelee kuwa wategemezi, na mabeberu yazidi kunufaika.
Baya lolote likitokea, mabeberu na media zao wanaandika na kutufundisha baadhi yetu wajinga, kuwa sisi, na siasa zetu ndio sababu. Na kwa ujinga tulionao tunaamini hivyo.
 
Sii kweli, China ni wajamaa na ni matajiri

Sii kweli, alitaka the gap between the haves
and the havenot iwe small.

Kulikuwa na mistake moja kubwa kwenye ujamaa wa Nyerere.

Sii kweli, waliokamatwa ni wahujumu uch

Asante
P
Asante
 
Naamanisha viongozi wote wanaotutawala ni zao lake, wamesoma kipindi chake, ni kweli alileta mfumo wa elimu wa hovyo kabisa ambao hauna faida yoyote, waliomfuata ni majangili tupu wametengenezwa na hii katiba mbovu ambayo hata yeye alikiri kuwa ni ya hovyo haswa, alishindwa nini kuibadili na uwezo alikuwa nao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…