Siasa za Tanzania zinapitia upepo mbaya sana

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Ukiangalia mwenendo wa uchangiaji wa hoja humu ndani ni vigumu sana kupambanua kama mchangiaji ameegemea mrengo gani wa kisiasa yaani kaegemea upinzani ama ccm. Tungekua na magenious ya game za kisiasa basi huu ndio uliokua muda muafaka kujijenga na kutengeneza mkondo mpya.
Na nikiri kwamba nashindwa kubashiri kua upepo huu utavuma mpaka lini! Maana umewageuza wanasiasa kua mithili ya samaki walio kwenye maji yaliyochafuka sana!
 
Ni kweli CDM wengi wapo upande wa mama hata hawajielewi tena?
 
Mungu ni mwema, tunajenga taifa moja.Jiwe aliharibu sana umoja na ustawi wa taifa letu.Binafsi nilikuwa naguswa sana na kuandika kwa uchungu zama zile.
 
Kwa maoni yangu umeanza vyema ukamaliza fyongo. CDM wanajielewa kuliko unavyodai.

Ungeandika hivi ungestahili likes za kutosha:

"Ni kweli CDM wengi wapo upande wa mama."
 
Watu ni lazima wabadilike kutokana mazingira. Kiongozi akiwa na dhamira ya dhat katika kuleta umoja na utengamano wa kitaifa ni lazima aungwe mkono na watu wenye itikadi tofauti.
 
Mahitaji ya msingi ya taifa yapo palepale sioni sababu ya watu kuyumba kimsimamo, ni kutojielewa tu, issue kama Katiba Mpya na Tume Huru ya uchaguzi zinahitajika miaka yote.
 
Ni kweli CDM wengi wapo upande wa mama hata hawajielewi tena?

Huu ni ushahidi mojawapo mkubwa kabisa kwamba Bi Mkubwa ni mpinzani, ila tu hakuwa anafurukuta. Sijajua Katiba inasemaje kuhusu kureshuffle presidents wa nchi ila Dkt Hussein Jr aje bara halafu huyu aende kuhutubia mipasho hukooooo ya taarabu visiwani!???
 
Ukiangalia mwenendo wa uchangiaji wa hoja humu ndani ni vigumu sana kupambanua kama mchangiaji ameegemea mrengo gani wa kisiasa yaani kaegemea upinzani ama ccm. Tungekua na magenious ya game za kisiasa basi huu ndio uliokua muda muafaka kujijenga na kutengeneza mkondo mpya.
Na nikiri kwamba nashindwa kubashiri kua upepo huu utavuma mpaka lini! Maana umewageuza wanasiasa kua mithili ya samaki walio kwenye maji yaliyochafuka sana!
Shida ni kwamba atakaechangia ata akiwa si wa ccm au upinzani ila akichangia lazima kuna upande ataendanao sawa lakini itategemea we upeo wako utamwangaliaje
 
Back
Top Bottom