Pre GE2025 Siasa za uwakilishi za Arusha mjini zimeharibika sana na kukosa ustaarabu kabisa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Kuna habari nimieona ambapo madiwani wa Arusha mjini walikuwa kwenye kikao rasmi cha kazi. Jambo la kusikitisha ni kwamba hicho kikao kilikuwa kama kikao cha chama huku watu wenye maslahi yao binafsi wakifanya siasa za minyukano.

Mambo mengine ya ajabu katika hiko kikao ni pamoja na diwani kulia machozi kabisa eti mbunge wao wa Arusha wanayetoka katika chama kimoja hashirikiani na madiwani! Alienda mbele zaidi akasema alikuwepo kwenye kikao hicho akakimbia aliposikia mkuu wa mkoa anakuja.

Kuna diwani amemuomba mkuu wa mkoa msamaha kwa wananchi kumchagua mbunge wa sasa wa Arusha!

Kuna diwani amemfananisha mkuu wa mkoa wa Arusha na Mfalme!

Pia nimeona madiwani wengi katika hiko kikao sarufi ya lugha ya kiswahili ni tatizo, kuna mmoja amenyoa O anasema Makonda anapambania "dhidi" ya maendeleo ya maslahi ya watu Arusha akimaanisha anipaginia maendeleo ya Arusha! Kikako kizima ni kituko kitupu.

Pia soma

Kuna habari nimieona ambapo madiwani wa Arusha mjini walikuwa kwenye kikao rasmi cha kazi. Jambo la kusikitisha ni kwamba hicho kikao kilikuwa kama kikao cha chama huku watu wenye maslahi yao binafsi wakifanya siasa za minyukano.

Mambo mengine ya ajabu katika hiko kikao ni pamoja na diwani kulia machozi kabisa eti mbunge wao wa Arusha wanayetoka katika chama kimoja hashirikiani na madiwani! Alienda mbele zaidi akasema alikuwepo kwenye kikao hicho akakimbia aliposikia mkuu wa mkoa anakuja.

Kuna diwani amemuomba mkuu wa mkoa msamaha kwa wananchi kumchagua mbunge wa sasa wa Arusha!

Kuna diwani amemfananisha mkuu wa mkoa wa Arusha na Mfalme!

Pia nimeona madiwani wengi katika hiko kikao sarufi ya lugha ya kiswahili ni tatizo, kuna mmoja amenyoa O anasema Makonda anapambania "dhidi" ya maendeleo ya maslahi ya watu Arusha akimaanisha anipaginia maendeleo ya Arusha! Kikako kizima ni kituko kitupu

Tambua tu kwamba nchi ikitawaliwa na mambumbumbu lazima umbumbumbu huo utajionyesha dhahiri katika nyanja zote maisha ya Watu waliopo katika nchi husika.
 
Paulo ame target uwaziri tuu hana lolote yule 🥴🥴, makatibu wakuu wajiandae "kama " watakutana nae
 
Kuna diwani anaitwa Lobora, wa kata ya themi, kiukweli huyu jamaa anamchukia gambo kupita kiasi, japo gambo ana mapungufu mengi ila chuki ya lobora kwa gambo imezidi kipimo, btw, hakuna mtu anayempenda gambo huko Arusha, hakuna.
 
Wana shida gani na Gambo?
 
Back
Top Bottom