Siasa zimezidi The Law School of Tanzania. Hiki chuo kimulikwe!

nchi hii ngumu sana kila eneo lina vikwazo kibao pia kwa wahasibu ndo kabisa kuipata hiyo CPA (T) ujue si chini ya miaka 7 hata wanaosomea udaktari ni cha mtoto.wenzetu ulaya na marekani vitu kama hiyo ni rahisi sana kuvipata na wanafunzi wakifeli huyo mwalimu anajisikia vibaya sana kwani kufeli kwake ni sawa na kufeli kwa huyo mwalimu.
 
Pole mkuu kwa supp
 
Hatari sn
 
Hatari sn

Si kidogo. Utaratibu wa utahini vyuo vikuu ndiyo chanzo cha haya. Utaratibu wa utahini shule za msingi na sekondari ni muafaka zaidi.

Mtunga mtihani hapaswi kumfahamu mtahiniwa, hali kadhallika msahishaji hapaswi kuwa ndiye mtahini.

Imekuwa kusema hadi uvuke mto. Wa kumfunga paka kengele hayupo hadi mtu avuke mto kwanza.
Mtu ukivuka mto ya nini kujihusisha na yasiyomhusu?

Vicious cycle inaendelea.
 

Kupigania haki za watahiniwa ni jambo la msingi.

Mtunga mtihani, msahishaji na mtahiniwa zinapaswa kuwa pande tatu zisizofahamiana.

Vinginevyo u Mungu mtu itabakia kuwa ni matokeo tu.
 

Waungwana wanasema:

The way to hell is paved with good intentions.

Tatizo si mitihani. Tatizo ni mode ya examinations.

Gone are the days at MUCHS when barely 2 doctors could hardly pass, out of a batch of 40.

Walitanzua vipi utata kama huu pale?
 

Kwamba mtu kasoma sheria Hadi Ph.D lakini kafeli LST haya ni Tanzania tu no wonder:

"Ways to hell are paved with good intentions."
 
Umeandika ukweli sana yaani !! hongera kwa kuwasemea watu hawa

Hata website ya matokeo haIfanyi kazi. Ole wako ujitie kimbele mbele kuuliza.

Kwamba kuwa na Ph.D ni bure ila kuwa na cheti Cha TLS, na watu wote wameufyata?

Hii nchi ni ngumu sana.

Si bora watu wakasome law school peke yake waachane na yasiyokuwa na faida?
 
Mazingira wezeshi kabisa kwenye zile rushwa zetu pendwa za ngono na mauzo batili ya notes.

"Iweje kitabu 'original' kilichoandikwa na mwalimu husika kuruhisiwa kuingia nacho kwenye mtihani, lakini siyo photocopy ya kitabu hicho hicho?"
Mkuu, Africa has it's own ways of running things. Usiumize sana kichwa chako kwa watu ambao hawataki positive changes.

All in all, tungepata fursa ya kusikia upande wa mlalamikiwa ingekuwa vema zaidi ili tuweze kutoa huku iliyo sahihi.
 
HATA MATOKEO YAO HAYA YALIYOTOKA JUMATANO YANA WALAKINI INABIDI WARUDIE KUYASAHIHISHA MAANA KUNA WATU WAMEFELISHWA MAKUSUDI
 
Mkuu, Africa has it's own way of running things. Usiumize sana kichwa chako kwa watu ambao hawataki positive changes.

All in all, tungepata fursa ya kusikia upande wa mlalamikiwa ingekuwa vema zaidi ili tuweze kutoa huku iliyo sahihi.

Ngoja tuwasubirie labda walikuwa wanashughulikia Ile website ya matokeo ilivyokuwa inazidi kuwatolea uvundo zaidi.

Kweli Africa Ina namna yake. No wonder we are poor.
 
Kama umeamua kusoma soma jamani elimu ya kupeana. Sio poa
Kwa maana iyo mnataka hata walio feli wafaulishwe? Big NO
 
Hayo ni matokeo ya kawaida kabisa mkuu.

Kufaulu 30 kati ya 400.

Toka hiyo shule imeanza matokeo yapo hivyo.
 
Kama umeamua kusoma soma jamani elimu ya kupeana. Sio poa
Kwa maana iyo mnataka hata walio feli wafaulishwe? Big NO

Unayasoma wapi ya kutaka wafaulu waliofeli?
 
Hayo ni matokeo ya kawaida kabisa mkuu.

Kufaulu 30 kati ya 400.

Toka hiyo shule imeanza matokeo yapo hivyo.

30 kati ya 400 na hao LLB, LLM na Ph.D holders wewe waona ni kawaida?

Hata Muhimbili wakifaulu 2 au hamna kati ya 40 pana warusi wa pande za Buza hawakuchoka kudai ilikuwa ni kawaida hiyo. Hadi dua la kuku lilipomfika mwewe.
 
30 kati ya 400 na hao LLB, LLM na Ph.D holders wewe waona ni kawaida?

Hata Muhimbili wakifaulu 2 au hamna kati ya 40 pana warusi wa pande za Buza hawakuchoka kudai ilikuwa ni kawaida hiyo. Hadi dua la kuku lilipomfika mwewe.
Kawaida sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…