Kipondo Cha ugoko
JF-Expert Member
- Apr 12, 2023
- 1,411
- 2,700
Ndio maana mnaambiwa msitegemee siasa kuishi...! Mtu anaetegemea siasa kuendesha maisha yake ni rahisi sana kununuliwa, kula RUSHWA, kuishi kwa fikra za vyeo kama mtoa mada anavyofikilia nk. . mtu wa namna hiyo akivikosa hivyo chap anasaliti. Nawashauri hasa vijina jijengeni kiuchumi kwanza ndio mkimbilie siasa na hata kama unafanya siasa kuwa na vimiradi vya hapa na pale vitakupunguzia njaa njaa za kulamba watu miguu.Duniani hakuna kitu ambacho hakina side effects.
Mlevi mmoja huko nchini Uingereza, aliejulikana kwa jina la Isack Newton, siku moja baada ya kumaliza kufanya masterbation, alitamka maneno yafuatayo:👇👇
" To every action there is an equal and opposite reaction ".
Na hii ndio wasomi wa Afrika mnaiita " The third Law of Motion ".
Chadema kutoshiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu kuanzia ngazi ya udiwani hadi Urais, ni jambo ambalo litaleta side effects nyingi na kubwa Sana kwa maendeleo ya Chadema kama Chama.
Moja kati ya side effects hizo ni pamoja na kufifisha popularity ya Chadema kwa wananchi.
Umaarufu wa Chadema utapungua kwa kiasi kikubwa Sana.
Mimi sio mwanasiasa ila na yaamini maneno ya mlevi mwingine aitwae Lenin. Lenin aliwahi kusema kwamba
" The most best way to lead opposition is to control it ourselves ".
Kama Mimi ambae sio mwanasiasa ninayajua haya vipi kuhusu CCM? Watakuwa wanajua zaidi kuhusu hili, so obviously wata capitalize kwenye the absence of Chadema kwenye majukwaa rasmi ya kisiasa " Kutengeneza" chama kingine cha upinzani ambacho kitawafanya Chadema kuwa a " Surplus".
Tegemea Chama kama ACT wazalendo kupata viti vingi vya Ubunge na udiwani kama Chadema walivyo pata mwaka 2015. Hili litafanywa kimkakati ili kuprove kwa wananchi na jumuiya ya kimataifa kwamba hoja za Tundu Lissu kwenye "No Reform No Election" hazikuwa na mashiko.
Na hili linawezekana vizuri Sana. Tutegemee wana Chadema wengi ambao wamekuwa na ndoto za kuwa wabunge na madiwani kuhamia ACT wazalendo au vyama vingine vya upinzani kwa ajili ya kutimiza ndoto zao.
Lissu has nothing to loose na hategemei siasa kuishi, ndio maana hata asipo ingia bungeni haiwezi kumuathiri kiuchumi.
But on personal level, hakuna mtanzania wa kawaida mwenye uthubutu huo wa kuachilia fursa ya kujaribu kuingia bungeni akale hela za bure za wananchi kwa sababu tu ya kuwafurahisha mashabiki wa harakati za kisiasa...
Mwisho wa siku mwanasiasa anataka udiwani ama Ubunge kwa ajili ya tumbo lake na familia yake. Utakuwa mwendawazimu kama utakuwa unafikiri kwamba, mwanasiasa yupo kwa ajili yako..
LAWAMA ZANGU KWA INTELLIGENCE YA CHADEMA KU APPROVE " NO REFORM NO REACTION" 👇👇👇
Moja kati ya kazi za Intelligence Desk of any society or organization ni kuwa na uwezo wa "kutabiri" yatakayo tokea baada ya jambo fulani kufanyika au kutokufanyika.
Kutabiri sio taaluma ya uganga. Kutabiri ni taaluma inayo husisha kutumia akili yako vizuri based on experience and a very deep understanding of human psychology.
Unaposikia mfano FBI walitabiri kupinduliwa kwa let's say Robert Mugabe, usidhani ndani ya FBI kuna wapiga ramli. No!!
Ni watalaamu wa masuala ya intelligence waliyasoma matukio na Mambo yote yaliyokuwa yanaendelea kwenye utawala wa Mugabe wakapiga hesabu, wakafanya tathmini Yao wakaja na conclusion kwamba " Mugabe atapinduliwa ndani ya mwezi mmoja " ( Incase you are wondering of course yes Mugabe alipinduliwa)
So utabiri sio taaluma inayo husisha uchawi Ila taaluma inayo husisha matumizi sahihi ya akili, experience na basic human psychology.
Kwa mantiki hii hata wewe ni mtabiri. Una beef na mwanamke, then Ukamkuta yupo na vijana wake wa kiume, kabla hujampiga unatakiwa Uwe na uwezo wa kutabiri kwamba, watoto wake hawatokuacha salama. Watakupiga Sana. So wakikuua kosa ni lako wewe sio Lao . Ulishindwa kutabiri vizuri.
BACK TO CHADEMA'S INTELLIGENCE.
Ina maana kwenye intelligence ya Chadema hakuna wataalamu wa human psychology?
Ina maana kwenye intelligence ya Chadema hakuna watu ambao walikuwa na uwezo wa kutabiri kitakacho tokea kwa Lissu endapo No Reform No Election will be approved?
Ina maana ndani ya Chadema hakuna watu ambao wana uwezo wa kutabiri kwamba, kitendo cha Lissu kutembea kwa wananchi nchi nzima kuwaambia wasishiriki uchaguzi uliopo kisheria na kwamba siku ya uchaguzi waende kwenye vituo vya kura kuzuia uchaguzi, kingeweza kusababisha serikali iingilie Kati kwa kumkamata Lissu na kumfungulia mashtaka Jambo ambalo pia lingefifisha nguvu ya harakati yote kwa ujumla? Ni serikali gani duniani inayo weza kumuachia raia ane intice insurrection?
Ina maana ndani ya intelligence ya Chadema hakuna wataalamu wa Human Psychology and Behaviour ambao wangeweza kutabiri kwamba " No Reform No Reaction " Italeta mpasuko na mgawanyo kwenye chama kwa Sababu kwa human nature, kuna watu ndani ya chama ambao watahitaji kugombea nafasi mbali mbali kutimiza ndoto zao za kisiasa?
Maswali yapo mengi sana Ila sitaki kuamini kama Chadema haina watu hao kwa Sababu naamini Chadema ni chama cha wasomi wabobevu.
Ni nacho kiona ni kwamba watu hao wameshindwa kumshauri Lissu kwa Sababu kwa personality Yake anaonekana ni mtu asie weza kushauriwa pale anapokuwa ameamua Jambo lake.
Lissu ame uthibitishia umma kwamba yeye ni mtu anae amini Sana katika violence na people's power.
So he is running Chadema in his image and Likeness.
Yes " No Reform No Reaction " is in the image and likeness or Lissu's personality.
I see a lot of Tundu Lissu's personality in No Reform No Reaction Campaign.
Unajua watu hawajui tu; siasa ya huku kwetu bara giza ni sawa na vita hasa ukiwa umeamua kupambana na vyama vikongwe kama CCM ama madude kama museni,kagame n.k. Leo hii chalamira,makonda,makalla na watu wote wanaoitafuna nchi hii hawawezi kukubali uwashushe kwenye maisha ya V8 eti wakaanze maisha ya kujifunza kupanda boda boda. Ili uing'oe CCM madarakani inabidi ujikane nafsi Yako!!!!
Jambo Hilo ni wapinzani wachache wako tayari kulifanya, wengi lazma wahanye 🤣 na wanahanya kweli....!