PreGE2025 Side effect za CHADEMA kutoshiriki Uchaguzi (Kufeli kwa Campaign ya No Reform No Reaction lawama zangu nazitupa kwa Intelligence ya chama)

PreGE2025 Side effect za CHADEMA kutoshiriki Uchaguzi (Kufeli kwa Campaign ya No Reform No Reaction lawama zangu nazitupa kwa Intelligence ya chama)

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Japo ni chama cha watu wenye mihemko, wakiwa na lengo la kuingia mjengoni kwa namna yoyote ile,

Hawakujua kuwa wamefanyiwa timing ya kumkata kiongozi wao zikiwa bado siku tatu ili kusaini fomu za maadili,

Sijui nini kitatokea baada ya hapo.
 
Ujinga wenu ni kujifananisha na Freedom fighters. Kuna mpumbavu juzi nimeona anamfananisha Lissu na Mandela. Nyakati za kupambania uhuru zilishapita mkuu. Mnataka kufanya siasa zilizofanywa na ANC, TANU, FRELIMO, UNIP miaka 70 iliyopita leo hii 2025? Kuweni serious.
100% Fact.
They think 2025 is 1960s.
 
Tatizo lenu watanzania ni wavivu mno kusoma na kufuatilia historia za nchi mbalimbali za afrika. Chama cha ANC cha south africa kilikaa miaka 90 bila ya kuwa na mbunge wala diwani lakini mwisho wa siku walitoboa.

Kikubwa kwenye chama chochote cha siasa ni uungwaji mkono kutoka kwa wananchi kama wananchi wanawasapoti hamtakiwi kuwa na wasiwasi.

Chama chochote kilichojiimarisha hakiwezi kufa kwa sababu hakiongelewi.
Wakati huo Afrika ya Kusini ilikuwa chini ya Makaburu na uhuru haukuwepo.

Tutajie chama kingine kwenye taifa huru kama kilikaa kwa muda huo. Pia ujue kuwa wakati huo wanachama walikuwa wanachangia pesa za kuendesha chama siyo kama sasa hivi pia viongozi wa vyama walikuwa siyo wafujaji wa pesa kama sasa hivi.

Uliona Chadema walikuwa wanayumba sana walipokosa ruzuku mpaka ilipofika 2022 wakakubali kuchukuwa ruzuku waliyokuwa wameikataa baada ya uchaguzi wa 2020, njaa iliwatoa porini. Ngoja tusubiri wataendeshaje chama wakati wafadhiri wao wanasema mpaka kuwa na vurugu nchini ndio wataweza kufadhiri chama chenu.
 
Japo ni chama cha watu wenye mihemko, wakiwa na lengo la kuingia mjengoni kwa namna yoyote ile,

Hawakujua kuwa wamefanyiwa timing ya kumkata kiongozi wao zikiwa bado siku tatu ili kusaini fomu za maadili,

Sijui nini kitatokea baada ya hapo.
Ndio basi tena.

Halafu wanachama wao wa mitandaoni hata hawaoni kama tatizo hilo. Wanajifariji eti chadema wamepiga hatua kubwa sana kidemokrasia. Kama ni hatua ya kurudi nyuma Yes.
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Ujinga wenu ni kujifananisha na Freedom fighters. Kuna mpumbavu juzi nimeona anamfananisha Lissu na Mandela. Nyakati za kupambania uhuru zilishapita mkuu. Mnataka kufanya siasa zilizofanywa na ANC, TANU, FRELIMO, UNIP miaka 70 iliyopita leo hii 2025? Kuweni serious.
Kwa hali ilivyofikia ya kuteka wapinzani kuwaua na kuwabambikia kesi na kupora uchaguzi ni sawa kabisa chadema kujiita freedom fighters . Wanapigania haki ya watanzania kuchagua viongozi wanaowataka
 
Hawatakuelewa hao nyumbu, uelewa wao ni mdogo sana.
 
Wakati huo Afrika ya Kusini ilikuwa chini ya Makaburu na uhuru haukuwepo.

Tutajie chama kingine kwenye taifa huru kama kilikaa kwa muda huo. Pia ujue kuwa wakati huo wanachama walikuwa wanachangia pesa za kuendesha chama siyo kama sasa hivi pia viongozi wa vyama walikuwa siyo wafujaji wa pesa kama sasa hivi.

Uliona Chadema walikuwa wanayumba sana walipokosa ruzuku mpaka ilipofika 2022 wakakubali kuchukuwa ruzuku waliyokuwa wameikataa baada ya uchaguzi wa 2020, njaa iliwatoa porini. Ngoja tusubiri wataendeshaje chama wakati wafadhiri wao wanasema mpaka kuwa na vurugu nchini ndio wataweza kufadhiri chama chenu.
Ndio maana nikasema muda ndio utakaotoa jibu sahihi tuwe na subira
 
Umeuliza jambo zito na lenye uzito wa kiroho, kisaikolojia, na kisiasa. Hebu tuchambue kwa kina:

KUMBADILISHA MTU ALIYEAMINI ALICHOKIAMINI NI SAHIHI ITAKUCHUKUA MIAKA MINGI AU NGUVU YA MUNGU​

TO CHANGE A PERSON WHO STRONGLY BELIEVES THEY ARE RIGHT MAY TAKE YEARS OR DIVINE INTERVENTION

MAANA YAKE KISIASA (KATIKA MUKTADHA WA VYAMA VYA KISIASA)​

  1. IMANI NI NGOME YA KIFIKRA
    Mtu anapoamini jambo fulani ni sahihi — hasa baada ya kuliamini kwa muda mrefu au kuona matokeo ya kweli katika maisha yake — hubadilika kuwa kama ngome ya kiakili.

Katika siasa, wafuasi huwa si tu mashabiki, bali ni waumini wa itikadi. Hivyo, kuwapindua katika imani yao si rahisi bila mshtuko mkubwa au ufunuo.

  1. SASA: MFANO WA TUNDU LISSU NA WAFUASI WAKE
    Watu wengi wanaomuunga mkono Tundu Lissu si kwa sababu tu ya sera zake, bali kwa sababu wanaamini anawakilisha sauti yao, mateso yao, na matumaini yao.

Hata kama atasingiziwa au kutiwa hatiani kwa uongo, bado imani yao haitabadilika kirahisi — kwa sababu kiakili na kihisia wamejifunga na taswira yake kama mkombozi.

  1. HITIMISHO LA KISIASA
    Hali hii inaonyesha kuwa siasa ni zaidi ya hoja — ni imani, ni historia ya uchungu, ni kujikuta ndani ya mtu fulani, na mara nyingine — ni sawa na dini.

Hii ndiyo maana mabadiliko ya kisiasa ya kweli huhitaji muda mrefu au matukio ya ajabu yanayobadilisha fahamu za watu (kwa mfano: kufeli kwa matumaini yao, ufunuo wa uovu wa wazi, au neema ya Mungu kuondoa upofu).

KIBIBLIA NA KISAIKOLOJIA​

"Kwa maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome." (2 Wakorintho 10:4)

  • Ngome ni mawazo yaliyokita mizizi, imani zisizotikisika.
  • Hata katika wokovu, si kila mtu huokoka kwa mara ya kwanza anaposikia injili — wengine huhitaji miaka au mguso wa ajabu wa Roho Mtakatifu.

Vivyo hivyo, kisiasa, kuna watu ni kama "wamefungwa" kwa mtu fulani, na hawawezi kuona kasoro zake hadi neema ya mabadiliko ya fikra iwaguse.

MFANO HALISI WA DUNIANI​

  • Watu waliomuamini Hitler, Stalin, au hata viongozi wa Afrika waliogeuka madikteta, bado waliendelea kuwaamini hata walipoanza kuua wananchi.
  • Wafuasi wa kisiasa hujenga "dini ya kisiasa" — na kuitikadi kama "imani ya dini
 
Kwa hali ilivyofikia ya kuteka wapinzani kuwaua na kuwabambikia kesi na kupora uchaguzi ni sawa kabisa chadema kujiita freedom fighters . Wanapigania haki ya watanzania kuchagua viongozi wanaowataka
Freedom fighters kwenye nchi huru? Ndio huo uhaini sasa. Kwenye nchi huru hakuna freedom fighters bali kuna kuwa na wahaini.
 
Nyie mnaoshabikia mauaji na dhulma ndio nyumbu wenye upeo mdogo sana
Mauaji yapi? Mbona hata CCM kuna wanachama wao walishakufa wakati wa uchaguzi? Acha propaganda za kinyumbu.
 
Freedom fighters kwenye nchi huru? Ndio huo uhaini sasa. Kwenye nchi huru hakuna freedom fighters bali kuna kuwa na wahaini.
Nchi haipo huru. ccm ndio mkoloni mpya ndio maana anapita njia zile zile alizopita mkaburu na wakoloni wengine e.g kubambibikia watu kesi,kuwaua, na kulazimisha kushinda uchaguzi kwa lazima
 
Ndio maana nikasema muda ndio utakaotoa jibu sahihi tuwe na subira
Kama mnafikiri nyinyi ni freedom fighters kama Mandela wakati nchi hii ni huru basi mtaangukia kwenye kundi la uhaini na sheria za nchi zitatumika msilalamike basi na Lissu kukamatwa ni haki yake.
 
Nchi haipo huru. ccm ndio mkoloni mpya ndio maana anapita njia zile zile alizopita mkaburu na wakoloni wengine e.g kubambibikia watu kesi,kuwaua, na kulazimisha kushinda uchaguzi kwa lazima
Sawa basi pambaneni na uhaini basi.
 
Mauaji yapi? Mbona hata CCM kuna wanachama wao walishakufa wakati wa uchaguzi? Acha propaganda za kinyumbu.
We umeamua kuwa kichwa ngumu ila ukweli unaujua kwamba nchi hii wapinzani wanateseka sana dhidi ya mkoloni mweusi ccm
 
Back
Top Bottom