Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Imezoeleka sana kwa watu kusema kuwa Uarabuni hakuna watu weusi kama Amerika licha ya watumwa wengi kupelekwa huko. Wengi hudai kuwa waarabu walikuwa wajiwahasi watumwa wakiume ili wasizaliane. hili naona si jambo la kweli hata kidogo.
Sababu ni kuwa kitendo cha kuhasi mtu kilikuwa ni kitendo hatari sana. Zaidi ya nusu ya watu wote waliohasiwa walikufa kutokana na complications zilizotokana na kuhasiwa. Na watumwa walikuwa ni bidhaa ghali, hakuna ambaye alikuwa tayari kuhatarisha zaidi ya nusu ya mali yake kwa mtindo huo.
Pia kawaida watumwa wengi waliohasiwa walikuwa ni wangali bado watoto. Lengo ni wakahudumie wake wa wafalme au matajiri, au wawe wanamuziki(Wanaume waliohasiwa huimba sauti nyororo). Uhitaji wao haukuwa mkubwa kiasi hicho.
Nafikiri kuna explanation nyingione ya kwa nini watu wanaona 'hakuna' watu weusi uarabuni kama Amerika licha ya watumwa kupelekwa huko.