Sidhani kama kuna ukweli kuwa Waarabu walikuwa wakihasi watumwa wanaume

Sidhani kama kuna ukweli kuwa Waarabu walikuwa wakihasi watumwa wanaume

Mimi nimeishi nchi za kiarabu nyingi na zingine nimekaa kaa kwa muda mchache kama miezi mitatu mpaka mitano

Middle Eastern countries nazijua vizuri sana
Na zinazozizunguka
Kuna nchi ndogo sana inaitwa Kuwait ilipata uhuru 06/1961 ina wakazi kama 1m na kidogo ila tajiri sana
Kuna Sheikh Abdallah Al Salim Al Sabah alikuwa ni Mfalme (Amir) wa 11 katika utawala wa Kuwait alimuoa kijakazi au mtumwa na akamzalia watoto

Mtoto wake mkubwa alikuwa anaitwa Saad Abdallah Al Sabah akiwa mweusi kama sisi akifuata rangi ya mama yake

Naye akiwa Prince na baadae akawa crown prince halafu kuwa Amir wa Kuwait (I was there )

Hizi ni picha za Abdallah na mwanae Saad
Kwa hiyo tusiwashutumu tu kwa kila tunalolisikia
Screenshot_20230319_052006_Google.jpg
Screenshot_20230319_051448_Google.jpg
Screenshot_20230319_051351_Google.jpg
 
Inabidi tujiulize

? Waarabu walichukua watu weusi hapa Africa na kwenda kufanya watumwa je? Wako wapi? Mbona hawaeleweki wamepotelea wapi?

Wamewaua au ? Mbona hawana muendelezo wowote

Wamewahasi au ? Mbona hawaonekani na Mbona Waafrica walioenda mataifa mengine wanaonekana muendelezo wake na kama sio mwendelezo wake maelezo yapo kuwa waliwaua mfano ARGENTINA [emoji1033] - Kuna story ipo kuwa walikuwa wanawaua watu weusi yaani watumwa waliokuwepo au walioenda kwa kupelekwa Kama watumwa kwa hofu kuwa watazaliana na kuwa wengi na uwenda wakaja kutaka haki yao kama sehemu ya taifa?

Je? waarabu waliwafanya nn? Watu weusi walioenda/walio wachukua kama watumwa waliwaua au waliwahasi?

Hili swala sio la kidini isije? Ikaonekana kama kuna udini hapana ila ukweli usemwe ili tujue mababu zetu walifanyiwa nini?

Acha chuki dhidi yao, sasa ukweli usemwe ili tujue mababu zetu walifanyiwa nini! So what? Utafanya maamuzi yapi dhidi yao?

Halafu kwa taarifa yako tu mkuu, ARGENTINA 🇦🇷 tumetwaa kombe la dunia, tumewacharanga wasaliti 🇨🇵
 
Mimi nimeishi nchi za kiarabu nyingi na zingine nimekaa kaa kwa muda mchache kama miezi mitatu mpaka mitano

Middle Eastern countries nazijua vizuri sana
Na zinazozizunguka
Kuna nchi ndogo sana inaitwa Kuwait ilipata uhuru 06/1961 ina wakazi kama 1m na kidogo ila tajiri sana
Kuna Sheikh Abdallah Al Salim Al Sabah alikuwa ni Mfalme (Amir) wa 11 katika utawala wa Kuwait alimuoa kijakazi au mtumwa na akamzalia watoto

Mtoto wake mkubwa alikuwa anaitwa Saad Abdallah Al Sabah akiwa mweusi kama sisi akifuata rangi ya mama yake

Naye akiwa Prince na baadae akawa crown prince halafu kuwa Amir wa Kuwait (I was there )

Hizi ni picha za Abdallah na mwanae Saad
Kwa hiyo tusiwashutumu tu kwa kila tunalolisikia View attachment 2557485View attachment 2557486View attachment 2557487

Baadhi ya waswahili hawatakuelewa kwa hili, nasubiri now
 
Labda haujui maana ya kuhasiwa vizuri. Hata wanyama huwa wanahasiwa na wanaendelea kuishi fresh tu.

Kuhasiwa ni vitendo walikuwa wanafanyiwa sana watumwa enzi za mababu. Na jambo lingine la kujua ni kuwa kuhasiwa hakumfanyi mtumwa kushindwa kufanya kazi zake za kutumia nguvu ingawa kisaikolojia anakuwa wameshamharibu hayupo sawa kiakili.

Kuhusu waafrika kutokuzaliana na waarabu hili swala lilikuwa limekaa kibaguzi zaidi. Imagine hata sasa ukienda uarabuni ni ngumu kupata yule demu pure wa kiarabu wa kuzaa nae, sasa miaka hiyo ilikuwaje.
 
Ni kweli kuwa kuna baadhi ya watumwa wa kiume walihasiwa kama ulivyosema. Lakini inawezekana pia kwa sababu hapakuwa na mahitaji makubwa ya nguvu kazi ya watumwa wa kiume kama ilivyokuwa Marekani ( Kaskazini, kusini na visiwani) wengi waliuzwa tena kwa wenye kuwahitaji. Vitu vingine ambavyo vilichangia kupungua kwa idadi ya watumwa ni:

1. Waarabu hawakunyang'anya utu wa watumwa kama walivyofanya wamarekani weupe. Kwa waarabu mtumwa ( pamoja na ukatili mkubwa waliomfanyia) alikuwa ni binadamu na alikuwa na nafasi ya kujikomboa na baadhi yao walifanya hivyo. Kuna watumwa walikuwa na nafasi za juu tuu katika jamii na waliaminiwa sana na walio wa own. Lakini haikuwa hivi kwa waarabu wote. Baadhi ya nchi za Afrika Kaskazini na Sahel zilikuwa kama wamarekani na waliwatendea na wanaendelea ukatili mkubwa watu weusi.

2. Tofauti na Marekani, mtoto wa mtumwa mwanamke na muarabu alikuwa muarabu. Hii imefanya wengi ambao ni weusi kujihesabu kuwa ni waarabu. Kwa Marekani, mtoto yeyote aliyezaliwa na mwanamke mtumwa alikuwa mtumwa. Hali hii ndio ilichangia kwa kiasi kikubwa kwa utumwa kuendelea kwa vizazi na vizazi. Ndio maana Marekani unaweza kumuona mtu ana rangi nyeupe lakini anahesabiwa mweusi kwa sababu tu babu yake alikuwa mweusi. Katiba ya Marekani ilisema thamani ya mtu mweusi aliye mtumwa ni 3/5 ya mtu mweupe. Marekani mtumwa alikuwa mali ghafi kama alivyokuwa ng'ombe na tajiri wake alikuwa na haki ya kumtendea chochote anachotaka.

Watu weusi wapo uarabuni lakini wanajitambua kama ni waarabu. Janjaweed wengi walikuwa weusi Lakini walijiona kuwa ni waarabu kuliko waarabu weupe.

Huu ni mjadala mzuri kama hatutauharibu kwa kuingiza masuala ya dini.

Amandla....
Bado haujajibu swali tuanataka uzao wa kipemba kule uarabuni. Ukienda tu hapo mkoani Zanzibar utaona mchanganyiko wa muarabu na mwafrika, lakini mbona huko uarabuni hatuwaoni.
 
Bado haujajibu swali tuanataka uzao wa kipemba kule uarabuni. Ukienda tu hapo mkoani Zanzibar utaona mchanganyiko wa muarabu na mwafrika, lakini mbona huko uarabuni hatuwaoni.
Huwa mnataka jibu liwe lilelile kama la kutoka kwenye notisi za mwalimu alizofundisha,
 
Bado haujajibu swali tuanataka uzao wa kipemba kule uarabuni. Ukienda tu hapo mkoani Zanzibar utaona mchanganyiko wa muarabu na mwafrika, lakini mbona huko uarabuni hatuwaoni.
Inaelekea jibu unalo tayari na lolote utakaloambiwa hautalikubali kama ni tofauti na jibu lako. Ni kupotezeana muda tuu kuingia kwenye mjadala na mtu kama wewe. Mtu unaetaka uonyeshwe uzao wa kipemba uarabuni wakati wapemba hawakuuzwa kama watumwa uarabuni. Umeambiwa uarabuni sio tu kuwa kuna watu waliochanganya damu bali wako pia ambao ni weusi tii lakini bado unataka uonyeshwe wanaofanana na hao wa Ng'ambo Unguja! Ni kupotezeana tu wakati.

Amandla...
 
Bado haujajibu swali tuanataka uzao wa kipemba kule uarabuni. Ukienda tu hapo mkoani Zanzibar utaona mchanganyiko wa muarabu na mwafrika, lakini mbona huko uarabuni hatuwaoni.

Wewe hujatembea wala kuishi nchi za kiarabu, hivyo huu mjadala achananao
 
Back
Top Bottom