Sidhani kama kuna ukweli kuwa Waarabu walikuwa wakihasi watumwa wanaume

Sidhani kama kuna ukweli kuwa Waarabu walikuwa wakihasi watumwa wanaume

Ninachokumbuka tulisoma kwenye History form 3 kuwa kizazi cha watumwa weusi waliokuwa wakienda Uarabuni walikuwa wakihasiwa ili kutozaliana kule.

Kutokea hapo niliwachukia sana Waarabu kwa kuwa miongoni mwa Watumwa walioenda kwao Babu zangu watatu walienda na hawakufanikiwa kuacha watoto hadi wanakufa.

Isingekuwa kuhasiwa ina maana leo hii ningekuwa na Wajomba Oman 😎
 
Ni kweli kuwa kuna baadhi ya watumwa wa kiume walihasiwa kama ulivyosema. Lakini inawezekana pia kwa sababu hapakuwa na mahitaji makubwa ya nguvu kazi ya watumwa wa kiume kama ilivyokuwa Marekani ( Kaskazini, kusini na visiwani) wengi waliuzwa tena kwa wenye kuwahitaji. Vitu vingine ambavyo vilichangia kupungua kwa idadi ya watumwa ni:

1. Waarabu hawakunyang'anya utu wa watumwa kama walivyofanya wamarekani weupe. Kwa waarabu mtumwa ( pamoja na ukatili mkubwa waliomfanyia) alikuwa ni binadamu na alikuwa na nafasi ya kujikomboa na baadhi yao walifanya hivyo. Kuna watumwa walikuwa na nafasi za juu tuu katika jamii na waliaminiwa sana na walio wa own. Lakini haikuwa hivi kwa waarabu wote. Baadhi ya nchi za Afrika Kaskazini na Sahel zilikuwa kama wamarekani na waliwatendea na wanaendelea ukatili mkubwa watu weusi.

2. Tofauti na Marekani, mtoto wa mtumwa mwanamke na muarabu alikuwa muarabu. Hii imefanya wengi ambao ni weusi kujihesabu kuwa ni waarabu. Kwa Marekani, mtoto yeyote aliyezaliwa na mwanamke mtumwa alikuwa mtumwa. Hali hii ndio ilichangia kwa kiasi kikubwa kwa utumwa kuendelea kwa vizazi na vizazi. Ndio maana Marekani unaweza kumuona mtu ana rangi nyeupe lakini anahesabiwa mweusi kwa sababu tu babu yake alikuwa mweusi. Katiba ya Marekani ilisema thamani ya mtu mweusi aliye mtumwa ni 3/5 ya mtu mweupe. Marekani mtumwa alikuwa mali ghafi kama alivyokuwa ng'ombe na tajiri wake alikuwa na haki ya kumtendea chochote anachotaka.

Watu weusi wapo uarabuni lakini wanajitambua kama ni waarabu. Janjaweed wengi walikuwa weusi Lakini walijiona kuwa ni waarabu kuliko waarabu weupe.

Huu ni mjadala mzuri kama hatutauharibu kwa kuingiza masuala ya dini.

Amandla....
Umeelezea vizuri
 
Ninachokumbuka tulisoma kwenye History form 3 kuwa kizazi cha watumwa weusi waliokuwa wakienda Uarabuni walikuwa wakihasiwa ili kutozaliana kule.

Kutokea hapo niliwachukia sana Waarabu kwa kuwa miongoni mwa Watumwa walioenda kwao Babu zangu watatu walienda na hawakufanikiwa kuacha watoto hadi wanakufa.

Isingekuwa kuhasiwa ina maana leo hii ningekuwa na Wajomba Oman 😎

Elimu elimu elimu
 
Wazungu wame edit history kuweka chuki ...na kujiondoa lawama ..
Utaona mostly Christians Africans Wana wachukia waarabu Kwa utumwa lakini wanaamini wazungu walikuwa watu wema waliokuja kueneza Tu dini...maovu ya wazungu kwenye utumwa hawajui wala hawataki kusikia....

Lynching Kwa mfano haipo kabisa kwenye history za waafrika
 
Umemaliza mkuu, na mjadala ufungwe
 
Hii ni propaganda kidogo japo kuna ukweli mdogo.
Waliohasiwa ni watumishwa haswa kwenye majumba ya wafalme lakini watumwa wengine hawakuwa wanahasiwa.
2. Kitu kingine hapa ni watoto waliozaliwa na hawa watumwa walikuwa huru hawakurithi utumwa as long as mzazi alisilimu
3. Kuna jambo lingine watu weusi uarabu wako under represented kwenye media na politics hivi jamii ya kimataifa kuamini hawapo au ni wachache (tawala nyingi hapa mfahamu ni za koo za kifalme za kiaarabu.
4. Bado wanafanywa raia daraja la pili na wanakosa fursa nyingi ukiondoa michezo haswa kandanda (Saudi Arabia 🇸🇦) team yao almost wote ni weusi, utashangaa hapa wametoka wapi??
5. 10% ya wasaudi ni watu weusi ambao either ni vizazi vya watumwa au migrants workers
40-50% ya wa Oman ni weusi au machotara toka zanzibar
Yemen 🇾🇪 pia kuna idadi kubwa ya hawa weusi
Iraq kuna zanj arabs ambao bado wanafanya matambiko ya Kiswahili hii ni dhahiri watumwa walisalia hawakuwa wanahasiwa
 
Wazungu wame edit history kuweka chuki ...na kujiondoa lawama ..
Utaona mostly Christians Africans Wana wachukia waarabu Kwa utumwa lakini wanaamini wazungu walikuwa watu wema waliokuja kueneza Tu dini...maovu ya wazungu kwenye utumwa hawajui wala hawataki kusikia....

Lynching Kwa mfano haipo kabisa kwenye history za waafrika
Likewise Muslim Africans wanachukia wazungu
Sababu ni zile zile
 
Mwarabu asili yake ni mweusi:
,mababu zao,kwa kuoana na wazungu watuma wa mashariki ya ulaya,ndio kukapatikana waarabu weupe🙂machotara wa kizungu wa mashariki na waarabu(weusi).
Wapo waarabu wa asili (weusi),sehemu nyingi duniani,hata Yemen kiko kisiwa kinaitwa Scotra,wapo wengi,kiasi).
Waarabu (weusi),ndio kabila pekee duniani,lilipotea kwa kasi,kwa kuoana na mtaifa mbali mbali duniani,hawa weupe waarabu,unaowaona,ni mchanganyiko wa watumwa wazungu wa mashariki ya ulaya na waarabu wenyewe wa asili weupe.
Huo ni uongo hujui kaa kimya
 
Uarabuni ipi isio na machotara? Tuamze hapa, huu ni uongo ambao unarudiwa kila siku na kila siku unakuwa exposed kwa evidence na bado watu wanaendelea kuuongea.

Arabuni Kuna weusi kibao, hadi Familia za Kifalme Zina watu weusi, sultan tu wa Oman aliefariki karibuni ni kati ya hao machotara ila hamuoni.

View attachment 2556344

Asilimia 10 ya Saudi Arabia ama 3.5 million ni Afro Arabs, wapo mpaka Royal family, World cup mumewaoma kibao,

Na unlike Marekani na sehemu nyengine Arabuni Systematic Racism si kubwa hivyo weusi wengi Arabuni wanakuwa matajiri.

AL amoud ni mfano mzuri Mara kwa mara anachuana na Dangote kama mtu mweusi Tajiri zaidi duniani

View attachment 2556353

Hapo bado hujaenda sector nyengine kama muziki, michezo etc.
Weusi wa marekani ni matajiri kuliko weusi wa uarabuni mkuu
 
O
Another explanation ni;
Idadi ya watumwa weusi walopelekwa Arabuni haikua kubwa ukilinganisha na waliopelekwa Amerika

Sababu
Hakukua na shughuli iliyohitajia watumwa wengi huko jangwani Arabunk kama alivyohitajia huko Amerika kulikokuwa na mashamba makubwa makubwa ya kila aina ya mazao

Je watumwa walihasiwa?
Sina shaka walihasiwa ila sijui ni wangapi au ka kiwango gani

Na Ukiangalia population ya baadhi ya nchi za Arabuni kwa sasa utaona bado percentage-wise watu wenye asili ya weusi wapo kwa kiwango fulani

Saudi Arabia 10%
Oman 15%
Yemen 13%
Iraq 4%
Oman ni zaidi ya hiyo idadi
Hata Qabus alikuwa mweusi
 
Uarabuni ipi isio na machotara? Tuamze hapa, huu ni uongo ambao unarudiwa kila siku na kila siku unakuwa exposed kwa evidence na bado watu wanaendelea kuuongea.

Arabuni Kuna weusi kibao, hadi Familia za Kifalme Zina watu weusi, sultan tu wa Oman aliefariki karibuni ni kati ya hao machotara ila hamuoni.

View attachment 2556344

Asilimia 10 ya Saudi Arabia ama 3.5 million ni Afro Arabs, wapo mpaka Royal family, World cup mumewaoma kibao,

Na unlike Marekani na sehemu nyengine Arabuni Systematic Racism si kubwa hivyo weusi wengi Arabuni wanakuwa matajiri.

AL amoud ni mfano mzuri Mara kwa mara anachuana na Dangote kama mtu mweusi Tajiri zaidi duniani

View attachment 2556353

Hapo bado hujaenda sector nyengine kama muziki, michezo etc.
Hawa Wana weusi gani sasa
 
Unachosema ni kweli. Machotara wengi wa kiarabu walikuwa assimilated. Hata Anwar Sadat alikuwa uzao wa watumwa. Au ukiangalia huyu Sultan wa Oman.
3IN2PEGHX5HCRK5FB4GLVF6DW4.jpg

20170123092636omanroyalwedding.JPG
Anwar Saddat ni mnubi mkuu sio chotara wala matokeo ya utumwa

Saddat na field Marshall Mohammed Hussein tantawi are nubians
 
Hata urusi....bamdogo alienda kupiga kitabu akahasiwa hukohuko.....so huenda ni kweli yasemwayo
Si kweli, kama alihasiwa basi itakua aliingilia anga za wenyewe.
Kuna watanzania wengi wamesoma urusi wakarudi na wanywa Vodka kama wake zao
 
Weusi wa marekani ni matajiri kuliko weusi wa uarabuni mkuu
Si kweli Anaepishana na Dangote kila siku kama mtu mweusi mwenye Utajiri zaidi ni Msaudi, siku zote weusi Matajiri wanatoka Arabuni ama Africa na sio Marekani ama Ulaya.

images (23).jpeg

Al amoud Huyo.

Nchi nyingi za Kiarabu weusi wanakua hadi wafalme.
 
Back
Top Bottom