Tetesi: SIDO kuunda ndege ya kubeba abiria 500

Tetesi: SIDO kuunda ndege ya kubeba abiria 500

Sikatai ni wazo zuri, lakini ndege ya abiria 500 ni kubwa sana, ile ndege ya rais wa USA boeing 777(Air force One) ni kubwa kuizidi hata dreamliner 787-8 ya kwetu, na ile 777 inabeba abiria 400, sasa hii ya abiria 500 itakuwaje?

Ni wazo zuri la uthubutu, lakini kwanini wasianze na ndege ndogo ndogo, au watengeneze mabasi ya mwendo kasi, bajaji, au coaster za abiria.

Airbus au boeing wakimaliza kutengeneza ndege huwa inapigwa tests za kufa mtu, wana fridge moja kubwa sana ndege inaingia yote ndani, boeing na ukubwa wake inaingizwa kwenye fridge kutizama kama engines zinaweza handle baridi... wanafanya tests za kila aina, usicheze na uhai wa watu...

Wakimaliza kutengeneza wapande wafanya kazi wote wa SIDO waliotengeneza na familia zao watoto na wake zao.
 
Are you serious?SIDO hii ninayoijua mimi!acheni utani kwanza itatakiwa ivunjwe itengenezewe taasisi nyingine yenye vision na si hii taasisi mufilisi ya wanasiasa,majungu,upendeleo ,ulinzi isiyo na expertise.
Umewaambia UKWELI HALISI japokuwa najua watakuja hapa watakaounga mkono hoja hiyo ya ajabu ili kodi zetu hizi kiduchu zinazokusanywa kwa mitulinga zipigwe.
 
Mkuu hatuwezi kufika kwa kudharau kila kinachofanywa na Watanzania wenzetu. Waungwe mkono waongezewe wataalamu watafanikisha.
Kwa staili hii hatutafika au tukifika tutakuwa tumechoka sana au tuseme tumeshapotea njia???
Eti una anza kwa kuomba:
1. Uungwe mkono i.e. unatushawishi na hujui kwamba ombi laweza kukubaliwa au kukataliwa.
2. Uongezewe wataalam i.e. huna uwezo peke yako kwa sasa tena Hujui kinachoendelea kwa sasa (Huendi na wakati) kwamba ajira hakuna.
Kwa kifupi ni kwamba unaanza kwa kufeli. Kwa maana unaweza usiungwe mkono na usiongezewe wataalam.
 
Labda kuku 500. Wachina wapo mbele yetu hata mara 1,000 lakini hakuna shirika la ndege lolote Duniani, hata ya huko China yanayotumia ndege ya abiria iliyotengenezwa China.
Una uhakika?
 
Au UNGO? ... kwanza aerodynamics kuna engineer wa kufanya hayo mafekeche?
 
Back
Top Bottom