Sidumu kwenye mahusiano

Sidumu kwenye mahusiano

Kama kichwa cha hapo imeandika, mimi sijawahi kudumu na mwanamke zaidi ya miezi sita nitaeleza kwa visa vya wanawake watatu.

Wa kwanza nilidumu nae kwa mwezi mmoja, wakaenda kwao likizo baada ya hapo mahusiano yakaisha akawa ana dharau hata nikimwita mara anisimamishe njiani. Kama siku moja aliniambia nisubiri akatoe hela kwa wakala nikasimama kama robo saa hajatokeza. Kila nikimsemesha hajibu message baadae kabisa akanijibu eti alikuwa bado anatoa hela, huyu demu alikuwa analeta dharau sana

Wa pili alikuwa akiishi Magomeni, basi sasa nikadumu nae kwa miezi kama mitatu. Mwanzoni alikuwa yupo na heshima ila baadae akaanza madharau mpaka kufikia kunitukana, nikaacha a nae.

Wa tatu ndio nilimpenda sanaaaa sijawahi kupenda demu kiasi hiki, nilijitahidi kadri niwezavyo tufurahi pamoja na heshima nilimpa kama zote mwanzo alikuwa na wivu nilichelewa kujibu message anakasirika, nilidumu nae almost 6 months tukaja kuachana kisa simjibu message nikajitetea yakaisha. Sasa miezi kama minne imepita nimesafiri hajawahi kuniulizia chochote nilivyo mwambia kama amezingua akaleta kelele nyingi kwamba simpendi namchezea tu, akasema tuachane kwakuwa sina future nae basi na mimi nikamuitikia na sijawahi kumtafuta tena, ila uliniumiza sana kuachana nae.

Wanawake wote hao na wengine wengi niliowahi kuachana nao sijawahi kuona hata mmoja akinisemesha kunijulia hali

Swali?

Kosa langu ni lipi. Au ni focus kwenye mambo ya maana kama Lusaka noti niachane na mademu daima?
Utoto.
 
Tukuulize swali uliingia nao kwenye mahusiano ya sirias umuoe?
Nakushauri tafuta pesa wanawake wana nyenyekea sana kama wakijua unajiweza.. sasa ww unaombwa 20k unaanza sababu kibao unategemea nn?

Ushauri wangu achana mahusiano sirias ya mapenz unapoteza muda wako na pesa zako, tafuta pesa mkuu. Ukijiskia unachukua wa kupiga mnaachana hapo hapo unaendelea mishe zako.

Mapenz ya kugandana ni ya kipuuzi sana
 
Tatizo demu anaonyesha dharau
Ngoja nikupe ramani ya vita ya hawa viumbe wakati unamtaka inatakiwa uwe mnyenyekevu akikupanga unapangika la sio kwenye ELERI na narudia sio kwenye ELERI ukishamjaza au akishakaa ndani unamwambia sasa mimi utaratibu wangu upo hivi wakati anazungukia mbali yaan MJAMZITO
 
Ni hivi bro, mwanzo uwa tupo kwenye mapenzi deep ila baadae kuna mmoja alisema namchezea au nitamuoa nikamwambia nitamuoa ingawa niliona nimwambie tu sikua na malengo nae sana, baadae akaanza kusema namchezea na Wala sina nia ya kumuoa eti nitaoa mwingine nitakae tafutiwa
 
Ngoja nikupe ramani ya vita ya hawa viumbe wakati unamtaka inatakiwa uwe mnyenyekevu akikupanga unapangika la sio kwenye ELERI na narudia sio kwenye ELERI ukishamjaza au akishakaa ndani unamwambia sasa mimi utaratibu wangu upo hivi wakati anazungukia mbali yaan MJAMZITO
Bro kwamba nimpe mimba? Sitamani kua na mtoto kabla sijao, kuwala uwa na Wala tatizo baadae visa vinakua vingi mpaka tunaachana
 
Dah.....🤔🤔! Nimeandika na kufuta kama mara ishirini, ila umedai una 23yrs bado kinda sana. Take it slow na ukiwa na partner hakikisha unamuuliza ni kitu/vitu gani angetamani ubadilike/ubadilishe, ukijua matatizo yako na ukayaacha nadhani suala la kutodumu kwenye mahusiano litabaki kuwa historia.
 
Demu wangu wa mara ya mwisho nilimheshimu sana mpaka vilevi niliacha kwasababu yake nilimjali na kumheshimu sana, tatizo alisisitiza kwamba nitamchezea na sita muoa, nishauri bro nitafute demu mkubwa kwangu au demu gani nitadumu nae
 
Back
Top Bottom