The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,541
Sasa wewe umetoka wapi na unaenda wapi?yawezekana wengi mnaohoji hii mada ni either mna umri mdogo au mlikuwa kijijini mnalima.
Kiini cha matatizo yote ya nchi hii kinaeleweka...unafiki na kulindana ambazo ndizo nguzo kuu za chama tawala CCM. Kumtafuta kiongozi msafi ndani ya CCM ni sawa na kutafuta nguo safi ndani ya dampo la taka. CCM wanajuana...kila moja anajua uchafu wa mwenzie na uoga wa kufichuana ndio msingi mkuu wa kulindana.Tatizo kubwa tulilonalo ni hilo la watu kutuhumiwa, halafu uchunguzi haufanyiki kuhusu wanayotuhumiwa juu yake; wanapumzishwa au wanapangiwa kwingine. Hili ndilo tatizo la msingi. Kwa nini iendelee kuwa hivi?
kwani mabadiliko ya jana ya ukuu wa mikoa hukuyasikia?Maarufu pande za Arusha huku ni Gidbless Lema tu, wengine HAPANA hakuna kitu....SIYO MAARUFU...
Amtaje au mtaje wewe kwa kuwa umeshamjua. Wengine sure kabisa, bado hatumjui...
Unanikumbusha sinema aliyo i'direct' Marehemu Magufuli kuhusu mali za CCM, 'stelingi' wake akiwa Bashiru!Kiini cha matatizo yote ya nchi hii kinaeleweka...unafiki na kulindana ambazo ndizo nguzo kuu za chama tawala CCM. Kutafuta kiongozi safi ndani ya CCM ni sawa na kutafuta nguo safi ndani ya dampo la taka. CCM wanajuana...kila moja anajua uchafu wa mwenzie na uoga wa kufichuana ndio msingi mkuu wa kulindana.
Usemi wa you scratch my back, and I’ll scratch yours (nikune mgongo na mimi nikukune) ndiyo falsafa kuu katika chama hicho kikongwe na zipo sababu nzito zinazozuia makada fulani kuadhibiwa...wanajua mengi! Kama tukifanya kosa tupeni adhabu ndogo ili nasi tuje tuwape adhabu ndogo makosa yenu yatakapofichuliwa!
Usitaje jina ila utuambie baada ya kuwajibishwa na JK aliendelea kuwa mtumishi wa umma kwa nafasi tofauti au aliondolewa/ alifukuzwa kazi kwenye utumishi wa umma? Kama alifukuzwa kazi kwenye utumishi wa umma, hapo kuteuliwa kwake sasa kwenye nafasi hiyo (ungaliitaja) kutakuwa kuna tatizo - washauri wa rais inabidi walaumiwe kwa kutochunguza records za wateule hao kabla hawajateuliwa. Kama hakufukuzwa kazi kwenye utumishi wa umma, hakuna tatizo la kuteuliwa tena kwenye nafasi hiyo kuu ya utumishi wa umma. Kuwajibishwa kazini haina maana kwamba wewe ndiye uliyetenda hilo kosa.Mkuu walengwa wa hii thread wanaelewa. Unapotaja majina una-risk moderators kuifuta thread yako maana nao hupewa sana shinikizo. Nikitaja majina inabidi nieleze kisa chote, jinsi walivyoomba msaada wa magari kwa niaba ya serikali, wakapewa, kisha wao na watu wa wizara ya Mambo ya Nje wakaamua kujimilikisha. Haikugundulika hadi wahisani walipoongelea huo msaada kwa JK, wakakuta JK anashangaa, msaada upi wa magari mlitupa, mbona haukufika!!!
Kiswahili kigumu jamani: Aya = Haya, ujamtaja = hujamtaja, uyo = huyo, na ujinga mwingine kama huo. Hovyo kabisa. Oni Sigala ingilia kati, aibu Sana, ukute mtu kama huyo ni graduate!!Aya ni majungu tu, maana ujamtaja uyo mtu,Kama Ni Sabaya tayari ananyea ndoo.
We bakia na kiswahili chako Kama ni dili sana,unadhani kila mtu kazaliwa kilipoanzia kiswahiliKiswahili kigumu jamani: Aya = Haya, ujamtaja = hujamtaja, uyo = huyo, na ujinga mwingine kama huo. Hovyo kabisa. Oni Sigala ingilia kati, aibu Sana, ukute mtu kama huyo ni graduate!!
Taja jina vinginevyo ni majungu yaliyozoeleka.
Team JK imerudi kwa kasi, lakini matumaini ni kwamba hao wanaorudishwa hawatarudi na madudu ya awamu ile.
Matumaini ni Rais Samia kuwa na sauti, maana inakuwa haina faida kwa taifa kama wanarudishwa wanamtandao halafu wakarudi na akili zile zile za wakati ule.
Si mlisema alipoteuliwa uRas kwamba nafasi hiyo ilikuwa ndogo kulingana na Cv yake. Kumbe kimsingi hakustahili uteuzi wowote!! Haya bwana.Batilda Buriani. Je unataka kingine boss?
Si mlisema alipoteuliwa uRas kwamba nafasi hiyo ilikuwa ndogo kulingana na Cv yake. Kumbe kimsingi hakustahili uteuzi wowote!! Haya bwana.
Mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu.
Fisiemu ni ileile na watu ni walewale... na wao ndio wenyewe... waacheni wale nchi maana wengine si wenzao!!Pamoja na kuhoji kutokutaja jina la mhusika, sehemu pana ya mada iliyowasilishwa ina mantiki sana.
Hawa wateuwaji, hivi wanakosa watu wa kuwateuwa katika nafasi mbalimbali za uongozi, kiasi kwamba watu wale wale, tena walio na rekodi mbaya katika utumishi wao ndio waendelee kuteuliwa?
Tatizo kubwa tulilonalo ni hilo la watu kutuhumiwa, halafu uchunguzi haufanyiki kuhusu wanayotuhumiwa juu yake; wanapumzishwa au wanapangiwa kwingine. Hili ndilo tatizo la msingi. Kwa nini iendelee kuwa hivi?
Pamoja na kuhoji kutokutaja jina la mhusika, sehemu pana ya mada iliyowasilishwa ina mantiki sana...