Sielewi kwanini mtu aliyechakachua msaada wa serikali na kujimilikisha enzi za Kikwete, akaondolewa leo anateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa

Sielewi kwanini mtu aliyechakachua msaada wa serikali na kujimilikisha enzi za Kikwete, akaondolewa leo anateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa

yawezekana wengi mnaohoji hii mada ni either mna umri mdogo au mlikuwa kijijini mnalima.
Sasa wewe umetoka wapi na unaenda wapi?

Unaongea vitu vya hewani hewani tu. Funguka nani ni "wenye umri mdogo" hapa (mtoto) na umejuaje. Kisha fafanua sababu ya kusema hivi ni nini...!

Kwa sababu, kwa namna hii, mimi pia unaweza nifanya nione kuwa hata ninyi wazee wa zamani sometimes ni kama "hamnazo" fulani...

Maana unarusha mipasho tu hapa badala ujenge hoja ya kuwa disqualify hao vijana ili kweli tuone busara na kujua kwako...
 
Tatizo kubwa tulilonalo ni hilo la watu kutuhumiwa, halafu uchunguzi haufanyiki kuhusu wanayotuhumiwa juu yake; wanapumzishwa au wanapangiwa kwingine. Hili ndilo tatizo la msingi. Kwa nini iendelee kuwa hivi?
Kiini cha matatizo yote ya nchi hii kinaeleweka...unafiki na kulindana ambazo ndizo nguzo kuu za chama tawala CCM. Kumtafuta kiongozi msafi ndani ya CCM ni sawa na kutafuta nguo safi ndani ya dampo la taka. CCM wanajuana...kila moja anajua uchafu wa mwenzie na uoga wa kufichuana ndio msingi mkuu wa kulindana.

Usemi wa you scratch my back, and I’ll scratch yours (nikune mgongo na mimi nikukune) ndiyo falsafa kuu katika chama hicho kikongwe na zipo sababu nzito zinazozuia makada fulani kuadhibiwa...wanajua mengi! Kama tukifanya kosa tupeni adhabu ndogo ili nasi tuje tuwape adhabu ndogo makosa yenu yatakapofichuliwa!
 
Na bado muandika jina lake kwenye mawe anaimba nyimbo za pambio huku walio chini yake wamekwapua mamilioni siku ya May day na bado yupo tu anadunda kisa mtu wa mtandao!
 
Maarufu pande za Arusha huku ni Gidbless Lema tu, wengine HAPANA hakuna kitu....SIYO MAARUFU...

Amtaje au mtaje wewe kwa kuwa umeshamjua. Wengine sure kabisa, bado hatumjui...
kwani mabadiliko ya jana ya ukuu wa mikoa hukuyasikia?
 
Ndiyo maana mnapowaitaga wazungu Ni mabeberu nawaonaga kuwa Ni wapumbavu wakubwa.
 
Kiini cha matatizo yote ya nchi hii kinaeleweka...unafiki na kulindana ambazo ndizo nguzo kuu za chama tawala CCM. Kutafuta kiongozi safi ndani ya CCM ni sawa na kutafuta nguo safi ndani ya dampo la taka. CCM wanajuana...kila moja anajua uchafu wa mwenzie na uoga wa kufichuana ndio msingi mkuu wa kulindana.

Usemi wa you scratch my back, and I’ll scratch yours (nikune mgongo na mimi nikukune) ndiyo falsafa kuu katika chama hicho kikongwe na zipo sababu nzito zinazozuia makada fulani kuadhibiwa...wanajua mengi! Kama tukifanya kosa tupeni adhabu ndogo ili nasi tuje tuwape adhabu ndogo makosa yenu yatakapofichuliwa!
Unanikumbusha sinema aliyo i'direct' Marehemu Magufuli kuhusu mali za CCM, 'stelingi' wake akiwa Bashiru!

Hili jambo la "Huyu ni Mwenzetu" naona litakuwa tatizo ndani ya nchi hii kwa muda mrefu.
Kama sikosei, ni kama CHADEMA nao wanaelekea huko huko na matamshi yao ya hivi karibuni kuhusu wanachama wao wanaokisaliti chama hicho.

Pengine ni wakati mwafaka sasa wa kuruhusu watu binafsi wasiotegemea chama na makundi maalum kusimama kama wao kwa wanachokiamini na kusaka uongozi wa nchi.
Wakipewa ridhaa ya kuongoza, waunde serikali bila kujali huo 'uwenzetu' wao.
 
Mkuu walengwa wa hii thread wanaelewa. Unapotaja majina una-risk moderators kuifuta thread yako maana nao hupewa sana shinikizo. Nikitaja majina inabidi nieleze kisa chote, jinsi walivyoomba msaada wa magari kwa niaba ya serikali, wakapewa, kisha wao na watu wa wizara ya Mambo ya Nje wakaamua kujimilikisha. Haikugundulika hadi wahisani walipoongelea huo msaada kwa JK, wakakuta JK anashangaa, msaada upi wa magari mlitupa, mbona haukufika!!!
Usitaje jina ila utuambie baada ya kuwajibishwa na JK aliendelea kuwa mtumishi wa umma kwa nafasi tofauti au aliondolewa/ alifukuzwa kazi kwenye utumishi wa umma? Kama alifukuzwa kazi kwenye utumishi wa umma, hapo kuteuliwa kwake sasa kwenye nafasi hiyo (ungaliitaja) kutakuwa kuna tatizo - washauri wa rais inabidi walaumiwe kwa kutochunguza records za wateule hao kabla hawajateuliwa. Kama hakufukuzwa kazi kwenye utumishi wa umma, hakuna tatizo la kuteuliwa tena kwenye nafasi hiyo kuu ya utumishi wa umma. Kuwajibishwa kazini haina maana kwamba wewe ndiye uliyetenda hilo kosa.
 
Aya ni majungu tu, maana ujamtaja uyo mtu,Kama Ni Sabaya tayari ananyea ndoo.
Kiswahili kigumu jamani: Aya = Haya, ujamtaja = hujamtaja, uyo = huyo, na ujinga mwingine kama huo. Hovyo kabisa. Oni Sigala ingilia kati, aibu Sana, ukute mtu kama huyo ni graduate!!
 
Kiswahili kigumu jamani: Aya = Haya, ujamtaja = hujamtaja, uyo = huyo, na ujinga mwingine kama huo. Hovyo kabisa. Oni Sigala ingilia kati, aibu Sana, ukute mtu kama huyo ni graduate!!
We bakia na kiswahili chako Kama ni dili sana,unadhani kila mtu kazaliwa kilipoanzia kiswahili
 
Si mlisema alipoteuliwa uRas kwamba nafasi hiyo ilikuwa ndogo kulingana na Cv yake. Kumbe kimsingi hakustahili uteuzi wowote!! Haya bwana.

Tafuta popote niliposema huyo tapeli nafasi aliyopewa ni ndogo.
 
Pamoja na kuhoji kutokutaja jina la mhusika, sehemu pana ya mada iliyowasilishwa ina mantiki sana.

Hawa wateuwaji, hivi wanakosa watu wa kuwateuwa katika nafasi mbalimbali za uongozi, kiasi kwamba watu wale wale, tena walio na rekodi mbaya katika utumishi wao ndio waendelee kuteuliwa?

Tatizo kubwa tulilonalo ni hilo la watu kutuhumiwa, halafu uchunguzi haufanyiki kuhusu wanayotuhumiwa juu yake; wanapumzishwa au wanapangiwa kwingine. Hili ndilo tatizo la msingi. Kwa nini iendelee kuwa hivi?
Fisiemu ni ileile na watu ni walewale... na wao ndio wenyewe... waacheni wale nchi maana wengine si wenzao!!
Kwanini huwa hamuelewi? Au hamjui bungeni na SM kuna kina nani? MSITUKWAMISHE!!!
 
Pigania katiba mpya hizo nafasi ziwe za kuchaguliwa na wananchi badala ya uteuzi
 
Pigania katiba mpya itakayokupa fursa ya kuchagua mkuu wako wa mkoa kwa kura yako mwenyewe badala ya kuteuliwa Bashite au Sabaya.
Pamoja na kuhoji kutokutaja jina la mhusika, sehemu pana ya mada iliyowasilishwa ina mantiki sana...
 
Back
Top Bottom