Uchaguzi 2020 Sifa Bora alizonazo Tundu Lissu zitakazomfanya kuwa Rais wa JMT

Uchaguzi 2020 Sifa Bora alizonazo Tundu Lissu zitakazomfanya kuwa Rais wa JMT

Rasterman

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2015
Posts
33,894
Reaction score
44,117
Kama wewe ni mfatiliaji wa siasa za Tanzania na Afrika utakubaliana na mimi kuwa kwa muda mrefu sasa tumekuwa tukikosa kiongozi bora wakuongoza watanzania kwa maslahi ya taifa na wala sio vyama na wanaompa vyeo.

Tulipata janga kama taifa baada ya kuongozwa na Mh Rais Magufuli ambaye aliokota urais kama embe chini ya mnazi kwa kupewa na wale wanaoitwa wenye nguvu.

Matokeo yake nchi imekuwa ni vilio vitupu, hali mbaya ya uchumi na uliopo kuwa wa makaratasi tu. Hali mbaya ya amani, upendo kufifia na hofu kutawala nchini.

Sasa kila mtu anahaha namna ya kumwondoa huyu aliyeshika mizizi pasipo kuwa na mvuto kwa watanzania. Mwaka 2015 nchi yetu iliingia katika janga la kiurais kwa kumpata Rais asiyekuwa na uwezo wa kudumisha utawala wa kisheria, kuheshimu katiba na uhuru wa kisisasa, Kiuchumi na kijamii.

Baada ya kilio cha miaka 5 sasa, mwenyezi Mungu anatuletea rais bora kabisa mwenye sifa zifuatazo. Na ana uwezo wa kurejesha matumaini ya watanzania.

Si mwingine ni Tundu Antiphas Mugwai Lissu mbobevu ktk fani ya sheria, mwenye upendo na uzalendo wa kweli ktk nchi yake.

Sifa zifuatazo zitampa Urais TL kwani watanzania wote wanamjua na kumfahamu vizuri asiyekubaliana nazo ana lake binafsi.

1. Ni kiogozi shupavu na jasiri, hili litamwezesha kufabya maamuzi magumu na yenye tija kwa taifa. Wananchi wanaamini hataishia maneno ya majukwani tu bali atatenda kwavitendo na sio maigizo kama ya Rais Mafufuli.

2. Ana uzoefu unaohitajika kuwa Rais. Watanzania wanajua Mh Tundu Lissu ana uzoefu na serikali zote zilizopita kuanzia ya Mwinyi hadi ya Magufuli. Madhaifu ya kiuongozi ni yale yale miaka yote. Na hakuwahi kubadilika ktk misimamo yake ya kusimamia utawala bora, haki na wajibu.

3. Uwezo wa kutuvusha kiuchumi. Mhe Tundu Lissu anafahamika vyema kama mpambanaji wa maslahi kwa wananchi. Anajua vyema changamoto za maisha ya wananchi. Sio kujenga fly over ya mita 500 ubungo na kwenda kuimbia nyimbo tandahimba! INAHUSU!!

4. Yupo tayari kuwa amiri jeshi mkuu wa Tanzania. Kama anavyofahamika vema kwa vyombo vyote vya dola kuwa ni kiongozi shupavu. Asiyeyumbishwa na siasa za chuki, uhasama na kuburuzana. Ni mwanasheria aliyebarikiwa kuitendea haki taaluma yake. Ni mfano bora kwa wote wanaovutiwa kusoma taaluma ya sheria. Hata hivyo ni kiongozi mwema na mwenye ushirikiano, heshima, busara na utulivu wa kiakili kama sifa bora ya kuwa amiri jeshi mkuu.

5 . Ni msema kweli. Hili ni sifa bora kabisa ktk utawala wa dunia ya kwanza zilizoendelea. Hawezi kusema kuwa tatizo halipo kwa kulificha. Mdororo wa uchumi na uhusiano wa kimataifa umekuwa ndio wimbo wake siku zote kiasi mahasimu wake wasiopenda ukweli kumwinda na pengine kutaka kuondosha uhai wake. Lisu ni mpenzi wa Mungu kweli kweli.

Karibu Mh Tundu Lissu wewe ni yule ajaye Unayesubiliwa kwa miaka nenda Rudi.
 
Lissu is our saviour , I hope that after archived to rule this county, First we suppose to arrest Juma maharage and his family , and to keep them in jail without bell
No Lissu hana sifa ya Kisasi. Tutawasamehe lakini pia walioumizwa na utawala wake watalipwa compansation
 
Yes mkuu tutawasamehe wote ila tuwanyanganya Mali zote walizopola.
Mali wamepora nyingi sana kwa kulindana na magenge amya wenzao hizo zitarudi mikononi mwa Watanzania.

Lissi ataimarisha utawala bora kila mtanzania ataukubalim kutakuwa hakuna kuoneana wala kudhulimiana.
 
Mali wamepora nyingi sana kwa kulindana na magenge amya wenzao hizo zitarudi mikononi mwa Watanzania.

Lissi ataimarisha utawala bora kila mtanzania ataukubalim kutakuwa hakuna kuoneana wala kudhulimiana.

Yes for Sure Tz kwanza Mkapa na kikwete na Magufuli lazima Mali walizochuma zirudi kwa watz .
 
Back
Top Bottom