Sifa ya kwanza ya kiongozi mbovu wa Afrika ni kusifiwa na wazungu

Sifa ya kwanza ya kiongozi mbovu wa Afrika ni kusifiwa na wazungu

Ukitaka kujua sifa ya kwanza ya kiongozi mbovu kwa Africa ni kusifiwa na Wazungu.

Kiongozi yoyote wa Afrika anaesifiwa na wazungu ujue huyo ni bure kabisa, ni bomu.

Hakuna kiongozi wa Afrika ambae analinda rasilimali na maslahi ya wananchi wake akasifiwa na wazungu, hayupo.

Na wazungu hata uwe dikteta vipi, kama huathiri maslahi yao huwezi kusemwa vibaya hata siku moja. Mfano mzuri ni Kagame. Umewahi kusikia Kagame anasemwa vibaya pamoja na kufunga wapinzani wake wote?

Wazungu wanajua, tabia ya kwanza ya viongozi wa Afrika ni kupenda sifa, kwa hiyo wanajua wakimsifia kwenye media zao na kumpamba basi yeye hukenua meno na kuchanua mapaja watu wajichotee malighafi wanazotaka bila shida.

Ukiona kiongozi wenu anasifiwa na wazungu ujue mmepigwa na kitu kizito kichwani.

Kama kupigwa na wazungu kunaleta uchumi mzuri kama wa Rwanda basi acha na sisi tupigwe. Miaka 60 ya uhuru nchi bado hovyo si afadhali tungewaacha wakoloni wabaki?
 
Lakini kama kuna ukweli fulani ndani ya haya maneno,

kwa sababu huwa ni kama kosa la jinai kwa kiongozi wa kiafrika ku tofautiana mawazo na wazungu,

yani watamchukia na watalazimisha na raia wake wamchukie,

adui yetu mkubwa waafrika ni sisi wenyewe kuendekeza njaa matokeo yake tunafanya yasiyo stahili kwa ahadi ya pesa
 
Upo sahihi mkuu, hakuna kiongozi makini wa afrika atakayependwa na mabeberu historia inadhihirisha hilo. Katika freedom fighters wa afrika Mandela pekee ndiye anayeimbwa sana na mabeberu na hii ni kwwa sababu alilinda maslahi yao, huwezi kumskia Nyerere, Lumumba,Sankara na wazalendo wengine wakipewa sifa zao na mabeberu.
 
Back
Top Bottom