Sifa ya kwanza ya kiongozi mbovu wa Afrika ni kusifiwa na wazungu


Kama kupigwa na wazungu kunaleta uchumi mzuri kama wa Rwanda basi acha na sisi tupigwe. Miaka 60 ya uhuru nchi bado hovyo si afadhali tungewaacha wakoloni wabaki?
 
Lakini kama kuna ukweli fulani ndani ya haya maneno,

kwa sababu huwa ni kama kosa la jinai kwa kiongozi wa kiafrika ku tofautiana mawazo na wazungu,

yani watamchukia na watalazimisha na raia wake wamchukie,

adui yetu mkubwa waafrika ni sisi wenyewe kuendekeza njaa matokeo yake tunafanya yasiyo stahili kwa ahadi ya pesa
 
Upo sahihi mkuu, hakuna kiongozi makini wa afrika atakayependwa na mabeberu historia inadhihirisha hilo. Katika freedom fighters wa afrika Mandela pekee ndiye anayeimbwa sana na mabeberu na hii ni kwwa sababu alilinda maslahi yao, huwezi kumskia Nyerere, Lumumba,Sankara na wazalendo wengine wakipewa sifa zao na mabeberu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…