Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi, Mhandisi Ezra Chiwelesa ameikataa Bungeni taarifa iliyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum Sigrada Mligo, aliyesimama katikati ya mchango wake na kupinga kauli kuhusu kuachiliwa huru kwa wote waliokamatwa baada ya vurugu za Oktoba 29, 2026.
Chiwelesa ameikataa taarifa hiyo wakati akichangia mjadala wa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa Bunge la 13 akisisitiza kuwa hatua za Rais za kuunda tume na kukusanya maoni ni jitihada za kuleta maridhiano na mshikamano wa kitaifa.
Akizungumza Bungeni Chiwelesa amesema “Wote ni mashahidi tunaona wale vijana wote wapo nje leo tunataka mama afanye nini sasa? Na aliahidi kuunda tume tumeona inazunguka ikichukua maoni yote ni juhudi ya Rais kurudisha hili Taifa pamoja na ametoa ahadi ya kutoa mkono wa ushirikiano na kuelekea kwenye maridhiano bila kuchoka nasema hivi kwa sababu hatuwezi kujenga hili Taifa kama kuna baadhi ya watu wanasimama ‘the way’ wanavyoona na wanaturudisha nyuma,” Mbunge Eng. Chiwelesa.