Sijaona andiko la Uislamu linalokataza kula mbele ya mtu aliyefunga

Sijaona andiko la Uislamu linalokataza kula mbele ya mtu aliyefunga

Hiyi ni sheria ya nchi husika ,tena wamesema kula hadharani .

Kuvaa nguo hata chupi ni ruksa ukiwa kwako ila sio hadharani kama barabarani ,kufanya mapenzi ni ruksa sio kosa ila kufanya kweny hadhara na kujirekodi kurusha mtandao ndio kosa
Andiko langu linahusu uisilamu na sio nchi fulani.

Ujumbe wangu ni kuwa sijaona katazo la uisilamu wenyewe likisema kwamba ni dhambi kula mbele ya mtu aliyefunga.

Elewa ninaposema uisilamu,sijataja nchi.

Kama kuna Nchi inakataza ijue tu keamba inakataza kwa utashi wake na sio sheria ya Dini inasema hivyo
 
Isitoshe kama unaongelea hilo kwa muktadha wa kinachoendelea zanzibar,sheria inayotumika pale ni ya jinai na sio ya kidini.
Andiko langu liko wazi kwamba sijaona katika maandiko ya kiisilamu katazo la kula mbele ya aliyefunga na kwmaba eti kitendo hicho ni dhambi,sijaona katazo hilo.

Mbona wewe unaitaja zanzibar wakati andiko langu nimetaja uisilamu mkuu.

Ni vizuri tukawa tunaelewa makusudio ya maandiko,sio vizuri ukawa mtu wa kusom ili ujibu bali uwe mtu wa kusoma ili uelewe.

Hao zanzibar wanaokataza watu watajua wenyewe
 
Ni sheria za nchi husika
Kula, Kutafuna, Kunywa maji kwenye mazoezi, au kula mchana hadharani wakati wa Ramadhani ni uhalifu katika nchi za kiarabu UAE.

Wakati wa Ramadhani, hairuhusiwi kula, kunywa au kuvuta hadharani nyakati za mchana

Adhabu kwa mtu anayeonekana kukiuka sheria inaweza kuwa kifungo cha hadi mwezi mmoja, au faini ya Dirham 2,000.
Mimi nazungumzia uisilamu sijazungumzia nchi husika.

Makusudio yangu ni kufikisha ujumbe kwamba sijaona andiko katika UISILAMU(sio katiba ya watu fulani)
 
Kule zanzibar wame kamatwa watu 12 kwa kula hadharani yani walivyo kua na akili fupi kama njia ya kwenda chooni wanaona eti kula hadharani kipindi hiki ambacho wao wana jishindisha njaa ni dhambi na ni makosa kisheria alafu ushoga uliojaa kule wanaona kawaida tuu na wala huwezi kusikia wanakemea na kusema ni dhambi
🤭🤭🤭🤭
 
Hiyi ni sheria ya nchi husika ,tena wamesema kula hadharani .

Kuvaa nguo hata chupi ni ruksa ukiwa kwako ila sio hadharani kama barabarani ,kufanya mapenzi ni ruksa sio kosa ila kufanya kweny hadhara na kujirekodi kurusha mtandao ndio kosa
Hoja inauliza kuhusu Dini... Sio nchi au Taifa?!
 
Andiko langu linahusu uisilamu na sio nchi fulani.

Ujumbe wangu ni kuwa sijaona katazo la uisilamu wenyewe likisema kwamba ni dhambi kula mbele ya mtu aliyefunga.

Elewa ninaposema uisilamu,sijataja nchi.

Kama kuna Nchi inakataza ijue tu keamba inakataza kwa utashi wake na sio sheria ya Dini inasema hivyo
😅😅Kwani hapa unaongelea nn ? Na majority wa nchi hizo wanafuata sheria ya dini...Nchi imeamua yenyewe ndio sheria hiyo
 
Tukiwa tuna masiku kadhaa tokea mfungo uanze nimejaribu kukutana na changamoto kadhaa kwa baadhi ya watu wakikereka na watu wanaokula mbele yao huku wakiwa hawajafunga.

My take
Sijaona andiko linaloashiria kuonesha kwamba ni vibaya kula mbele ya mtu aliyefunga.

Dhambi ipo kwa mtu ambaye anatakiwa afunge na hajafunga na wala hana sababu ya msingi.

dhambi hiyo itakuwa ni kwa sababu hajafunga na wala sio dhambi kwa sababu ya kula mbele ya mtu aliyefunga.

Na wala sijaona andiko linalomlazimisha mfungaji ati achukie kitendo cha mtu kula mbele yake.
WAfungaji hawana nguvu ya kuvumilia wengine wanaokula wakati wao wanakula milo mitatu usiku
 
Ni sheria za nchi zinawekwa ili kuwarahisishia watu kutekeleza sheria za mwenyezi Mungu bila bugdha. Hakuna sheria inayokataza mtu kujiremba awezavyo lakini unaonaje leo ukiamua kuvua nguo zote utembee barabarani je utakamatwa au hutakamatwa?
Mbona mfano wako hauendani kabisa na hoja ya mtu kula hadharani.
 
lakini unaonaje leo ukiamua kuvua nguo zote utembee barabarani je utakamatwa au hutakamatwa?

Tofautisha kati ya kitendo ambacho ni halali kukifanya iwe sirini ama hadharani kama kula chakula,kunywa maji,kufua n.k

Na kuna vitendo ambavyo ni halali sirini lakini hadharani havifai kama vile kuvaa kichupi kama unavyosema.

Kula ni kitendo cha halali iwe hadharani ama sirini.
 
Kuna vijisheria vinatungwa huku uswazi kuhusu kufunga.
We acha zimebaki siku 12
Waisilamu wa Zanzibar wanatapatapa ni wajinganga sana uwezi kumkata anae kula mchana anawaacha wanakopa na kukopesha kwa riba ukawacha wazungu wanaotembea matako nje
 
Dini

Kuwa kwao kwamba majority ni waiisilamu hakuondoi uhalisia wa kwamba bandiko langu linahusu dini(usilamu)
Hakuna kweny uislamu ila huwezi kupangia watu wafanye nn,katiba wanaandika watu kutokana na mahitaji yao.

Kama ingekuwa ni uislamu mbona pombe wanaingiza ndani ya nchi yao?... Uislamu hausiki kabisa
 
Huyu mleta Mada ni fuasi wa Dini ya Kiqadiani/ Ahmadiyya wenyewe Uislamu wao wana uduplicate ila ukiwafuatilia sana sio Waislamu sahihi ila tu wanajuficha katika Uislamu kwa kupotosha wengine..........wana Nabii wao alijitokeza baada ya Mtume Muhammad (saw) wa kwao anaitwa Mirza ghulamu Qadiani wa kutoka India.
 
Ni sheria za nchi zinawekwa ili kuwarahisishia watu kutekeleza sheria za mwenyezi Mungu bila bugdha. Hakuna sheria inayokataza mtu kujiremba awezavyo lakini unaonaje leo ukiamua kuvua nguo zote utembee barabarani je utakamatwa au hutakamatwa?
Sifa kubwa ya imani ni kuvumilia na kuyashinda majaribu sasa kama mtu anajiona ni mwepesi kuingia dhambini kisa kakutana na majaribu huyo aachane na mambo ya imani asichoshe wengine
 
Hakuna kweny uislamu ila huwezi kupangia watu wafanye nn,k
Ni kweli na ndio maana hata mimi sijawapangia nini wafanye,au nimewapangia wapi ?
Kama ingekuwa ni uislamu mbona pombe wanaingiza ndani ya nchi yao?..
Sasa kitendo cha wao kuingiza pombe hakituzuii sisi kusema pombe haifai katika uisilamu.

Wao acha waingize pombe ila na sisi tutaendelea kuhubiri kwamba uisilamu umekataza pombe.

Wao acha waendelee kuzuia watu mambo kadhaa katika ramadhani ila na sisi haituzuii kusema kwamba uisilamu haujakataza hayo.

Hivyo basi uhuru wa watu kujipangia mambo yao hautufanyi sisi tusibainishe uhalisia wa uisilamu
 
Huyu mleta Mada ni fuasi wa Dini ya Kiqadiani/ Ahmadiyya wenyewe Uislamu wao wana uduplicate ila ukiwafuatilia sana sio Waislamu sahihi ila tu wanajuficha katika Uislamu kwa kupotosha wengine..........wana Nabii wao alijitokeza baada ya Mtume Muhammad (saw) wa kwao anaitwa Mirza ghulamu Qadiani wa kutoka India.
Hii ndio mpya naiisikia leo kuhusu mimi 😂😂,kuna file langu unalo ambalo mimi silijui hongera sana.

Jambo la msingi ni kujibu hoja yangu na sio kuanza kunipakazia vitu ambavyo havina ushahidi wowote.
 
Back
Top Bottom