safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,837
- 17,412
- Thread starter
- #61
Naam ngoja nikusome zaidi nione wapi nimechanganya mambo.Usichanganye mambo mnamu!
naam haswaa.Kula ni jambo la halali kidini iwe hadharani au kwa siri lakini kwa mwezi wa ramadhani linakuwa ni halali kwa mwenye dharura.
Naam naam hakika.iyo wala haina shida na ni sheria inayowahusu waislamu pekee
Naam hakika ndugu yangu ndivyo ilivyo.Kwa sababu serikali ina jukumu la kuhakikisha watu wake wanakuwa huru katika kutekeleza ibada zao
Hapa ndipo shida inapoanzia,na nitakujibu katika nyanja mbili.ndipo kwa Zanzibar wakaamua kupiga marufuku watu wote kula hadharani muda wa kati ya alfajiri na magharibi bila kujali mlaji ni
1.KiDINI : unapokuwa umefunga alafu mtu akala unamuona basi ELEWA kwamba mtu huyo hakunyimi uhuru wa wewe kuendelea na ibada hiyoo ya kufunga,huo ufahamu haupo katika uisilamu ni madai ya kijinga ya baadhi ya watu wasioelewa mambo.
Ni kama mtu anayefanya ibada ya kusali aseme kwamba ananyimwa uhuru na mtu ambaye amemuona anapita na pikipiki wala hasali,haimake sense
2.KiSHERIA ZA NCHI : wataalamu kadhaa wa sheria wamwfafanua kwamba sheria ama katiba ya zanzibar haijataja jambo hilo kwamba ni kosa,na ndio maana watu wanaohukumiwa wanahukumiwa kwa makosa mengine kama vile ukorofi na uzururaji na sio kula hadharani mchana.
Mmoja ya wanasheria hao ni wakili maarufu zanzibar Ndugu kijogoo alifafanua hivyo,na kama wewe unaona kuna sheria iliyotaja wazi kosa hilo ilete hapa.
Kwanza serikali haijaweka bado hiyo sheria unaposema ni sheria unakuwa unakosea na ndio maana ukienda mahakamani ukaomba data za watu waliohukumiwa kwa kosa la kula mchana wa ramadhani huwezi kukuta hiyo kitu.Ndiyo maana nikasema HIZO NI SHERIA ZA SERIKALI KATIKA KUWARAHISISHIA WATU WAKE KUTEKELEZA IBADA YAO
Pili andiko langu limelenga KUBAINISHA KWAMBA DINI HAIJAKATAZA MTU ASIYEFUNGA KULA MBELE YA MTU ALIYEFUNGA,hivyo huku unakozunguka kote mkuu ni kwenda kimyume na maudhui yangu.
Jawabu lako sio la kweli kama nilivyotangulia kusema na sababu ni tatu nakuwekea.Kama unamaanisha hakuna dalili ya kuzuia kwa yule asiye muislamu basi ni kweli hakuna lakini jibu nilishatoa hilo hapo juu kwenye herufi kubwa.
1.hakuna sheria iliyitaja kosa hilo.
2.jambo hilo ni kuingilia uhuru wa wengine kwa sababu kula ni jambo lenye kufaa.
3.jawabu lako limeenda kinyume na maudhui yangu yaani umetoka nje ya reli.
Muisilamu ambaye hafungi bila udhuru wowote bila shaka anafanya makosa sio sawa na Allah ndio atamhukumu kwa kosa hilo,Kama unasema kumaanisha waislamu basi ndugu utakuwa unapotea au umekwishapotea
Muisilamu ambaye hafungi bila sababu akila mbele ya mwenzie aliyefunga jua tu kwmaba atakuwa makosani kwa sababu hajafunga na sio kuwa makosani eti kwa sababu tu anakula mbele ya mtu aliyefunga.
Unaposema wote bado unakanganya mambo kwa sababu neno wote ni pana sana kwani hatujui unakusudia wote wa kishia ?Wanazuoni wote wanaona kuwa mtu muislamu asiye funga basi ikifika muda anataka kula asile hadharani
Wote wa kisunni ?
Wote wa kiibadhi ?
Wote wa ki shaairah ?
Wote wa kiahmadiyyah ?
Hivyo basi kauli yako ya wanazuoni wote bado haina mashiko kwa sababu wote unayoisema haipo.
Hakuna mkanganyiko wowote,huo sio mkanganyiko wa uhalisia bali ni sababu iliyotengenezwa tu ili katazo hilo lipite.Hekima yao ni moja tu katika hili nayo ni kuepusha mikanganyiko,
Mtu ambaye hajafunga akila mchana haleti mkanganyiko kwa wasiokuwa waisilamu bali ataleta mkanganyiko kwa waisilamu WASIOJIELEWA kwa sababu waisilamu wasiojielewa wao hawajui kwamba kuna watu kwao kula ni ruksa mchana wa ramadhani.
Hekima hii ni feki kwa sababu ipo kinyume na malengo waliyoyakusudia.sintofahamu na dhana mbaya kwa wasioelewa vizuri dini.
Kitendo cha kulazimisha watu wasile hadharani ndio kunaleta dhana mbaya pamoja na sintofahamu kwa wasiokuwa waisilamu.
Na moja ya dhana mbaya zinazoletwa na katazo hili ni kudhani kwamba uisilamu ni dini isiyotoa uhuru kwa wasiokuwa waisilamu na pili watu wasioelewa uisilamu hudhani kwamba uisilamu unalazimisha watu kufanya ambbayo kwao sio wajibu,
Hivyo hekima hiyo iliyokusudiwa inakuwa kinyume chake na sio kama unavyotuaminisha hapa na jambo hilo liko wazi.
Suala la malezi baina yako na mwanao haliingilii uhuru wa watu wengine,watu wengine hawalazimiki kufuata yale unayomfundusha mwanao.Imagine mama aliye kwenye siku zake ale hadharani unafikiri mtoto wake wa miaka 7-9 atamuelewaje?
Hata ukiwa unamfundisha mwanao kusali unatakiwa na wewe mzazi ama baba ukasali naye msikitini.
I
Lakini kitendo cha wewe na mwanao kwenda msikitini hakitofanya uwalazimishe wasiokuwa waisilamu nao waende msikitini au wajifungie majumbani eti kisa unamfundisha mwanao kusali,
hiyo ni sababu dhaifu mkuu kwa sababu watu wengine wana uhuru wao ambao hauwezi kuvunjwa kwa kigezo tu kwamba unamfundisha mwanao.
Atautafsiri uisilamu vibaya endapo mtamlazimishe asile mchana mpaka ajifiche wakati yeye halazimiki kwa lolote juu ya mfungo huu.Au chukulia unafakamia hotelini je huoni yule asiye mwislamu atautafsiri uislamu vibaya pamoja na waislamu wenyewe na mwisho hata kukata tamaa na uislamu kabisa
Umeeleweka ila haujakubalika hoja zako ndio msana mimi mtoa uzi nakujibu nukta baada ya nukta.Inawezekana sijaeleweka kabisa
Jitihada za wanazuoni hazina nafasi katika Dini ya Allah ambayo imekamilika,wanachuoni hawana nafasi ys kuharamisha jambo ambalo Allah kanyamazia hakubainisha uharamu wake.lakini kwa ufupi ni kwamba huyu bwana mleta uzi anapinga ijitihad za wanawazuoni.
Rejea hadithi ya mtume ambayo mtume alifikia kusema...
".. وسكت عن أشياء رحمة لكم فلا تبحثوا عنها
.."Mungu amenyamazia baadhi ya mambo ili iwe rahma kwenu,basi msichunguzechunguze.."
Wanachuoni hawatakiwi kuharamisha mambo ambayo Allah ameyanyamazia kwani Allah hakuona ?
Au uisilamu haukukamilika ndio maana tunahitaji jitihada za wanazuoni ?
Asili kila ambacho hakikutajwa uharamu wake basi ni halali.Tumuulize tu mbona akioga mtoni nguo anaziweka mbele yake ili azione vizuri je, aya na hadithi inayoelekeza hivyo kaipata wapi?
Hivyo maadamu sikuharamishiwa kuweka nguo mbele yangu basi ni halali kwangu kuweka.
Elewa hiyo kanuni kwamba vitu vyote kwa asili ni halali,pale inapokuja dalili ya kuharamisha ndio kinakuwa haramu.
Hivyo usiniulize kwa nini naendesha gari wapi limetajwa kwamba uendeshe katika hadithi , jawabu langu ni rahisi kwamba hakuna aya au hadithi imeharamisha jambo hilo ndio maana tunachagua cha kufanya.
Elewa hii kanuni "الأصل في الأشياء الإباحة
Asili katika vitu ni kujuzu kufanyika kwake endapo haijsjs dalili ya kuharamisha.