Sijaona andiko la Uislamu linalokataza kula mbele ya mtu aliyefunga

Ile ni sheria ya zenji ila ingiea twitter uone watu wanavyotukana uislamu.

Sikiliza nikuambia kuna sheria za eneo fulani ,mbona Tanga ,Mtwara ,Lind hapa kuna migahawa kibao inapiga kazi 🤣🤣🤣.

Ingia Kule X uone uislamu unavyotukanwa.
 
Usichanganye mambo mnamu! Kula ni jambo la halali kidini iwe hadharani au kwa siri lakini kwa mwezi wa ramadhani linakuwa ni halali kwa mwenye dharura... Hiyo wala haina shida na ni sheria inayowahusu waislamu pekee

Kwa sababu serikali ina jukumu la kuhakikisha watu wake wanakuwa huru katika kutekeleza ibada zao ndipo kwa Zanzibar wakaamua kupiga marufuku watu wote kula hadharani muda wa kati ya alfajiri na magharibi bila kujali mlaji ni mwislamu mwenye dharura au siyo mwislamu kabisa. Ndiyo maana nikasema HIZO NI SHERIA ZA SERIKALI KATIKA KUWARAHISISHIA WATU WAKE KUTEKELEZA IBADA YAO

Tukirudi kwenye hoja kuu ya uzi huu sijajua unazungumzia kwa nani? Kama unamaanisha hakuna dalili ya kuzuia kwa yule asiye muislamu basi ni kweli hakuna lakini jibu nilishatoa hilo hapo juu kwenye herufi kubwa. Kama unasema kumaanisha waislamu basi ndugu utakuwa unapotea au umekwishapotea

Wanazuoni wote wanaona kuwa mtu muislamu asiye funga basi ikifika muda anataka kula asile hadharani. Hekima yao ni moja tu katika hili nayo ni kuepusha mikanganyiko, sintofahamu na dhana mbaya kwa wasioelewa vizuri dini.

Imagine mama aliye kwenye siku zake ale hadharani unafikiri mtoto wake wa miaka 7-9 atamuelewaje? Si kesho naye hataona haja ya kufunga (kumbuka kuanzia miaka saba wanafundishwa kuswali na kufunga). Au chukulia unafakamia hotelini je huoni yule asiye mwislamu atautafsiri uislamu vibaya pamoja na waislamu wenyewe na mwisho hata kukata tamaa na uislamu kabisa

Inawezekana sijaeleweka kabisa lakini kwa ufupi ni kwamba huyu bwana mleta uzi anapinga ijitihad za wanawazuoni. Tumuulize tu mbona akioga mtoni nguo anaziweka mbele yake ili azione vizuri je, aya na hadithi inayoelekeza hivyo kaipata wapi?
 
Ni kweli hakuna mafundisho ya kuchukia mtu akila mbele yako wewe uliyefunga (kwanza ni kichekesho hiki) lakini tukuulize je kuna sehemu umeona au kusikia kwamba wanafundishwa wafungaji wawachukie wanaokula mbele yao? Maana ulivyoileta hii hoja ni kanakwamba umekutana na mafundisho hayo

Kwa nilivyokusoma unataka watu wasiofunga wale tu kwa kujiachia na sisi tuliofunga tukae nao wakila tusichukue hata hatua ya kuwaepuka wamalize kula!
 
Huko Zanzibar Serikali inafurahia kuona raia wake wanafanya doria za kjinga kukamata watu wanaokula mchana. Hivi kuna mtu analazimishwa kula jamani ama kufunga?
 
Hatua ya kuchukua kwa mliofunga mkiona wenzenu wasiofunga wanakula ni kuondoka hiyo sehemu, si lazima mkae mkishuhudia watu wanakula na kutamani vyakula vyao. After all, hakuna aliyewalazimisha kufunga, mnajitakia wenyewe.
 
Hatua ya kuchukua kwa mliofunga mkiona wenzenu wasiofunga wanakula ni kuondoka hiyo sehemu, si lazima mkae mkishuhudia watu wanakula na kutamani vyakula vyao. After all, hakuna aliyewalazimisha kufunga, mnajitakia wenyewe.
Kwani mimi nimeandikaje?
 

UNAPOKULA WAKATI SISI TUMEFUNGA UNATUTIA HAMU YA KULA.
 

Kwanza wanapokula wanatutia hamu na kukutesa kwa kihisia. Ni bora tuteseke wote. Wao kwa nini wajichane hadharani?
 

Serikali iende mbele zaidi na msikitini iwe lazima kwenda. Asiyeenda aadhibiwe kobe
 
Nakala aione bin haroub dos.2020 Maghayo FaizaFoxy
 
Hivi yule Afande Rama shoga aliyekuwa anakatikia kabisa naye amefunga? 🤣
 
Anakula saa 12 jioni, anakula saa 3 usiku anakula na saa 10 asubuhi...😁
 
Hivi kumbe kumbe Zanzibar ni nchi ya kiarabu. Sikuwa nalifahamu hili.
 
Katika Imani Unafuata Sheria ya nchi au Sheria ya Allah iliyopo katika Quran?
Allah gani wewe kaandika sheria? Hayo ni ma moseic old ,draconian law ya tamaduni ya far east ,nchi nyingi za kisaarabu zilishaachana na huo utopolo.

Unapokuwa majority sehemu wewe ndio una duty ya kuheshimu haki za minority.

Dunia nzima inapambana na wahindi ambao ni majority India jinsi wanavyoua waislamu na kuwalazimisha wafuate dini Yao ya kihindi ya kuabudu ngombe. Je! Unaona wapo sawa?

Kule Ireland ambalo majority ni wakristu uliwahi kuona wanalazimisha waislamu ambao ni minority wasile nyama siku ya ijumaa kuu kwa kuhamasisha vijana wawasake mitaani na kuwapiga viboko au kuulazimisha hoteli zifungwe au zisiuze nyama siku hiyo?

Hivi ninyi mna ubongo kweli ? Hata amri za KUFUNGA hoteli mchana ni za hovyo kabisa. Mungu gani huyu mnayemwabudu?

Suala la Imani ni Mila tuu hizo. Wakati wewe unafunga unaamini kabisa kwa maneno ya propaganda unayoambiwa kuhusu mwezi huo kuwa labda ambaye hafungi ,atakufa, hatapata riziki, labda atakufa au kuteseka Sana lakini wapo wenye mifumo MINGINE ya Imani na mambo Yao yanasonga vizuri tena wanawashangaa ninyi

Kadhalika siku ya ijumaa kuu, wapo wakristu wanaamini ukila nyama unaweza kufa au kupata laana kubwa, ila wapo wakristu wanaitafuna vizuri tena ya nguruwe achilia mbali wasioamini ukristu na mambo Yao yanasonga . Heshimuni haki za watu, anayefunga afunge anayekila ale. Mungu ndiye muhukumu was haki.

THERE IS NO MORAL POLICE
 
Zanzibar ni nchi ya kiarabu i can smell it
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…