Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Sijaridhishwa na namna Mbowe anavyoiongoza Chadema, chama chetu kinahitaji mwelekeo mpya na uongozi wenye maono mapya," alisema Tundu Lissu leo akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Mlimani City. Lissu alitumia fursa hiyo kutangaza rasmi nia yake ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema, akisema ni wakati wa mabadiliko ya kiuongozi ili kuimarisha chama kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.