Sijavutiwa na Toyota Harrier a.k.a Tako la Nyani

Kwa wingi wa haya magari barabarani, jinsi watu wengi wanavyoyazungumzia na wengine wakiyataja Kama magari ya ndoto zao, nilikuwa Napata sana Shauku ya kuyaendesha, Ama kuyatumia Na ku feel ile Taste iliyomo ndani yake.

Juzi kuna Jamaa akaniletea Moja akiwa anaiuza.

Katika kuendesha hii gari nimegundua, yafuatayo:

1. gari ni nyepesi sana unapofika speed kuanzia 120, inahitaji uwe makini sana kuicontrol ..

2. Gari iko juu na inakosa balance kiasi kwamba kwenye kona kali ni msala mtupu kama ukiingia kichwa kichwa..

3. Haikupi comfortability nzuri ukilinganisha hata na Brevis...Yaani ukiwa kwenye Brevenga au Crown unasikia raha zaidi ya Harrier.

4. Ina fuel consumption kubwa tofauti na perfomance yake. (Yaani haina nguvu wala ubora mkubwa kulinganisha na utumiaji wake wa mafuta)

5. Bei Yake nadhani ilipanda kutokana na demand ya watu sababu ya kuigana ila ni gari ya kawaida sana....i would rather go for a cheaper Subaru forester XT than Harrier.

N:B matamanio yangu kwenye Hii gari yameisha Rasmi na sijaandika uzi huu kuziponda, ila tu nilikuwa na over Expectations. ASALAM ALLEIKUM.

Kijana umezoea baby walker hizi hutaziweza. Majibu ya mwaswali yako matano haya hapa.

1. Gari ni nyepesi (sio kwa uzito) ni nyepesi inachomoka sana. Hilo librevis lako linachukua muda kuchanganya.

2. Gari iko juu sio kwamba haina balance umezoea vigari vya chini kwa hiyo hii unajiona kama uko juu ya mti[emoji38][emoji38]. Hata ukiendesha Range Rover utalalamika hivihivi. Hakuna kesi nyingi za Harrier kupinduka.

3. Comfortability ya gari kubwa huwezi kulinganisha na hiyo brevis yako. Watu wana akili zaidi yako ndio maana Harrier inauzwa Mil 38 na Brevia Mil 15. Hiyo tofauti kubwa ya bei ni pamoja na comfort utakayoipata kwenye Harrier.

4. Kwa hiyo unataka kulinganisha spidi ya mnyama harrier na hako ka brevis kako..[emoji38][emoji38][emoji38]

5. Niliwahi kuwa na Harrier na sasa nina hiyo XT. Harrier ni noma aisee. Ukiona gari imenunuliwa sana we nunua tu, kuna watu walishafanya analysis na kuipitisha.
 
Point number 4 naomba nikuweke sawa.

Harrier engine 2AZ-FSE inazalisha 160HP
Brevis Ai250 1JZ-FSE inazalisha 197HP

Hapo numbers dont lie, Brevis itaichapa harrier katika namna yeyote ile when it comes to power.
 
Kwa wingi wa haya magari barabarani, jinsi watu wengi wanavyoyazungumzia na wengine wakiyataja Kama magari ya ndoto zao, nilikuwa Napata sana Shauku ya kuyaendesha, Ama kuyatumia Na ku feel ile Taste iliyomo ndani yake.

Juzi kuna Jamaa akaniletea Moja akiwa anaiuza.

Katika kuendesha hii gari nimegundua, yafuatayo:

1. gari ni nyepesi sana unapofika speed kuanzia 120, inahitaji uwe makini sana kuicontrol ..

2. Gari iko juu na inakosa balance kiasi kwamba kwenye kona kali ni msala mtupu kama ukiingia kichwa kichwa..

3. Haikupi comfortability nzuri ukilinganisha hata na Brevis...Yaani ukiwa kwenye Brevenga au Crown unasikia raha zaidi ya Harrier.

4. Ina fuel consumption kubwa tofauti na perfomance yake. (Yaani haina nguvu wala ubora mkubwa kulinganisha na utumiaji wake wa mafuta)

5. Bei Yake nadhani ilipanda kutokana na demand ya watu sababu ya kuigana ila ni gari ya kawaida sana....i would rather go for a cheaper Subaru forester XT than Harrier.

N:B matamanio yangu kwenye Hii gari yameisha Rasmi na sijaandika uzi huu kuziponda, ila tu nilikuwa na over Expectations. ASALAM ALLEIKUM.
Mkuu nakuunga mkono. Ila ungejaribu na zile harrier hybrid ndo ulete hii mada.
 
Hiyo gari ni nyepesi sana. Kwenye hii video kuna toureg. Ukiipigisha harrier test kama hiyo itakula mzinga huo haujawahi kutokea.

Asante sana nimeona utofauti gari nyepesi kwenye kukata kona sio ya kuamini yaweza binuka anytime. Na watu wanavyoipenda sasa sijuhi kama wanafahamu hili au ubishi tu ila wanajua?
 
Point number 4 naomba nikuweke sawa.

Harrier engine 2AZ-FSE inazalisha 160HP
Brevis Ai250 1JZ-FSE inazalisha 197HP

Hapo numbers dont lie, Brevis itaichapa harrier katika namna yeyote ile when it comes to power.

Na mimi naongezea...

Harrier ina gearbox ya U141e na ina gear 4 tu.
Brevis ina Gearbox ya A650e na ina gear 5.

Hii ligi inaishia tu kwenye makaratasi kabla hata ya kuingia barabarani.
 
Hapana ndugu yangu, hii ni kutake care tu.
Safari ndefu unatakiwa kuweka na kamzigo at least 100kg kwenye eneo la mzigo, na gari inakamata chini.
Raha ya Forester ni valves zake zote zikifunguka after 120km/hr, cha ajabu katika spidi hiyo unaweza accelerate tena mpaka 160km/hr kiurahisi sana.
Wazee wa forester kwanini barabarani nyinyi ni mbio tu?
 
Sasa braza mpaka uanze kugara gara na gari kiasi hicho ni nini hasa unakuwa unatafuta?

Hapo mzee tunazungumzia stability barabarani, its sad kwamba kwenye hiyo segment ya pick up, Hilux ndio gari imeperform vibaya kuliko popular pickups unazozijua.

Tena imeperform vibaya kwenye speed ndogo kuliko hao wenzake.

Hapo wametest popular pickups karibu zote kuanzia Ford Ranger, VW Amarok, Nissan Navara, Dodge Ram, Mitsubishi L200, Isuzu D-max, n.k.
 
Niliishuhudia hii mwigumbi nilikuwa nyuma ya LC70 kwenye roundabout tairi mbili za upande mmoja zilinyanyuka kabisa zikaiacha lami, ila ali recover.

Mbele alipaki pembeni. Na hakuwa kibati.

Huyo alihisi Lc70 series ni Porche 911 kwamba kwenye roundabout atapita na 150kph.

Kiukweli gari nyingi za juu na mbio havipatani.
 
Back
Top Bottom