Kwa kawaida mida hii huwa nakua kanisani ila kwa jinsi nilivyo depressed hata ningeenda Church nisingetoka na chochote.
Toka juzi nimekuwa naisoma MITHALI 31-10-31 kwa lengo la kujitathimini maana ndoto yangu ni kuwa huyu mwanamke anayeelezewa hapa.
Kila nikiisoma hii Methali najiona nikilandana na huyu mwanamke kwa 97% na tena nasema kwa kujiamini kuwa nimemzidi mwanamke wa Mith. 31-10-31 kwa ubora....(YES).
Mwanamke kuwa mwanamke wa MITH 31 huamki tu siku moja na kujikuta hivyo, wala huzaliwi hivyo na wala sio bahati bali ni kwa kujitengeneza kwa mchakato wa muda mrefu na kwa msaada wa roho wa Mungu.
Hata hivyo Mungu anaweza kukukutanisha na huyu mwanamke ila shetani atahakikisha anakutoa kwake kabla hujajua thamani ya mwanamke uliyenae.
Wanaume wengi mnakutana na hawa wanawake ila kwa vile shetani anapenda kusikia vitu kama KATAA NDOA atahakikisha hata Mungu akikuletea huyu mwanamke HUMUONI. Atahakikisha unaona vile anavyotaka yeye uone na ndio maana Biblia inasema 'MKE MWEMA, JE NI NANI AWEZAE KUMUONA?"
JE NI NANI AWEZAE KUMUONA?
Mwanaume jiulize, UKIMUONA mwanamke ambae kamwe hawezi kukusaliti hata uwe Impotent au atongozwe na Bill Gates au upoteze kazi au uumwe miaka 10 kitandani na hatasema siri hizo kwa yeyote zaidi ya kwa Mungu wake UTAMJUA? Utatumia vigezo gani KUMJUA? Kwanza kuna wanaume na baadhi ya wanawake hawaamini kama hawa watu wana exist ila wapo ila KUWAONA ni mpaka kwa neema.
Wanaume huwa mna vigezo vyenu vya kujua mke mwema ila Mungu akikuletea mwanamke ambae keshajiandaa na kujipa maarifa na uwezo wa kusimama kwa uaminifu bega kwa bega na atakayekuwa mumewe katika kuboresha maisha ya familia yao utatumia vigezo gani KUMUONA?
Je, UTAMUONA kwa zawadi anazokuletea wakati wa uchumba au utamuona kwa sababu haombi nauli au utamuona kwa ajira/biashara yake nzuri au utamuona kwa kuwa hata ukikaa wiki bila kumtafuta halalamiki au utamuona kwa degree yake au utamuona kwa sababu hana kasoro kama binadamu wengine au UTAMUONAJE?
Kwa jinsi ninavyoongoza maisha yangu sikutegemea ipo siku nitaambiwa maneno niliyoambiwa lakini yamenisaidia kujua nifanye nini ili nisije nikaambiwa tena.
NB: Sijaandika kutafuta mwenza ndio mana PM nimefunga. Kuandika ni njia yangu yakujifariji.
Mbarikiwe.
Mithali 31:10-31