Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

Well noted. Sitolisahau jina lako kwenye tags za simulizi zijazo πŸ™πŸ™
 
Pamoja mkuu πŸ‘Š
 
shamzugi hizo hapo
 
Hii story imenigusa sana,imenifundisha na kunichekesha at the same time,[emoji28]

Hivii vipande hapo chini nilivichukua na kusave kwenye notebook yangu ndo vilinikosha

Mzee Kidevu: "Apostle umenichota unyayo, apostle umenichota unyayo?"[emoji28][emoji28]


Mzee Dingi: "Msala ubaki kwako, kwani bado unaishi kwake? Tanzania mapori mengi sana, nenda hata Mtwara huko, sio lazima wote tuendelee kuishi mjini".[emoji28][emoji28]

Mzee Dingi: "Dogo mambo hayaendi hivyo, hakuna tuzo kwa ajili ya watu wanaopata hela kwa shida.

Mzee KY: "Tukiwa wadogo, ni ndoto ya kila mtoto kuwa rubani. Hii Dunia jinsi ilivyo, ukiteleza kidogo tu inakuchagulia njia


Mzee kesho yetu:Sikia bwana mdogo, hii Dunia inaweza kukuchapa alafu haikupi kabisa muda wa kujutia. Na hata ukiwa kwenye kujutia, inaweza ikakuchapa tena, kiasi kwamba ukiwa kwenye kujutia kwako, ndani yake ukapata majuto mengine".

Mshua: "Hivi nyie sijui hata kama mnanielewa. Yani mnanipangia juu ya mtu ambae mmezaliwa mkanikuta nae?. Nimesema namuhitaji mke wangu"


Mzee KY: "Sikia, Mimi na ww kitendo cha kufahamiana kwa njia hii, basi hatuwezi tena changamana nje ya hapa. Na kama tungejuana nje ya hapa, basi hakuna uwezekano ungeweza kunifahamu namna hii


Mshua: "Ili limepita, lakini maradhi hayaishi kuja, nataka siku nyingine wakiiona hii sura, wakumbuke notsi zote walizosoma hadi wakahitimu"[emoji28][emoji28]

Mshua: "Bwana mdogo, siku zote nakwambia hakuna aliyezaliwa kwa ajili ya matatizo yako. Mtangulize Mungu siku zote. Hata yule unayeona anatakiwa akusaidie, na yeye kuna sehemu anahitaji kusaidiwa. Usipolielewa ilo, utamchukia kila mtu"


Mshua: "Nadhani walau utakuwa umenielewa sasa, mnaweza mkawa ndani ya bus moja, ila safari zenu ni tafauti. Uliyekutana nae shuleni, usilazimishe aendelee kubakia kwenye maisha yako, wakati kusoma mmeshamaliza."



Harakati za mzee dingi kwenye daladala [emoji28][emoji28][emoji119]

Akapanda gari ya Mbagala, nikachukua pikipiki na kuanza kumfatilia. Alivyofika mivinjeni, akashuka, akapanda tena gari ya kurudi Kkoo. Nikaanza kujiuliza, huyu Mzee kasahau kununua kitu town au?. Alivyofika kkoo, akapanda gari za gongo la mboto, zikampeleka hadi bungoni, pale pia akashuka, akachukua gari za Tabata. Kumbe jamaa anakaa Matumbi pale"[emoji28]
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] hilo la mzazi feki aiseee daaah nimekumbuka mbali sana.
 
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… Noma sana mkuu
 
Mzee Dingi: "Dogo mambo hayaendi hivyo, hakuna tuzo kwa ajili ya watu wanaopata hela kwa shida.


[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Mkuu siku moja uje utembelee camp lako, kwa Sasa limepigwa msasa linawaka balaa, Ila hostel zenu zile za pale nje ndo uhuni unaendelea, vijana Kila siku wanakesha kwenye vigodoro, yaan Uhuru umepitiliza Kama vile wapo chuo, na kwa ufupi kabisa hawafanyi vizuri
 
Mkuu mwaka Jana nilikuwa maeneo yale. Shule imezidi kupendeza, fensi nzuri. Imepakwa rangi na baadhi ya majengo yamerekebishwa. Kwanza nilipasahau, nimefanya kuelekezwa mpaka kufika, maana ni kitambo sijaenda. Hostel za kule nje, uhuni hauwezi kuisha, Uhuru mwingi
 
Mzee kesho yetu:Sikia bwana mdogo, hii Dunia inaweza kukuchapa alafu haikupi kabisa muda wa kujutia. Na hata ukiwa kwenye kujutia, inaweza ikakuchapa tena, kiasi kwamba ukiwa kwenye kujutia kwako, ndani yake ukapata majuto mengine.


Tungo imejaa maneno ya kifalsafa.

Hongera sana mtunzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…