Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

Mkuu baada ya kuacha mishe na kina mzee dingi ila mzee KY ulisema kuwa uliendelea kuwasiliana nae kwa muda fulani

Mbona sijaona umetolea maelezo sababu ya kuendelea kuwasiliana na mzee KY
Baada ya kuachana nae kule maeneo ya Chalinze, before sijarudi nyumbani kwa wazee, nilionana nae kama mara mbili hivi. Na hizi zote ni Mimi ndio nilikuwa nafosi mazungumzo.

Na dhumuni la kufosi hayo mazungumzo, ni kwamba nilikuwa naamini yupo katika position ya kunisaidia kupata mchongo halali, maana alikuwa na maisha mazuri tu. Ila yeye hakuwa tayari kuendeleza ukaribu kati yetu
 
Niliwahi kupeleka mzazi feki pia kumbe huyo mzazi feki alishawahi kucheza dili na yule discpline Master na wakadhurumiana. Aisee sitosahau niliishi maisha magumu sana kipindi kile
Itakuwa ulipata tabu sana 😅😅
 
Mkuu hongera kwa simulizi hii, nimejifunza mengi.Ile simulizi ya kwanza ya maisha yako nilipata hamu ya kujua kazi alizowahi kufanya babako kwa ukaksi aliokuwa nao.
Kwa sasa najua kuwa ni mjeda mstaafu.
Congrats kwakuwa na baba huyo.
 
Mkuu nakumbuka kipindi hicho nipo form two ndio kipindi cha kufanya mtihani wa Necta. Aisee sitosahau niliyakoroga mpaka tukashauriana na mshikaji niliyefanya nae ule msala twende kwa Mganga wa kienyeji
Mkuu form two ulishaanza kufikiria habari za waganga 😅😅😅
 
Mkuu hongera kwa simulizi hii, nimejifunza mengi.Ile simulizi ya kwanza ya maisha yako nilipata hamu ya kujua kazi alizowahi kufanya babako kwa ukaksi aliokuwa nao.
Kwa sasa najua kuwa ni mjeda mstaafu.
Congrats kwakuwa na baba huyo.
Shukrani master 👊
 
Baada ya kuachana nae kule maeneo ya Chalinze, before sijarudi nyumbani kwa wazee, nilionana nae kama mara mbili hivi. Na hizi zote ni Mimi ndio nilikuwa nafosi mazungumzo.

Na dhumuni la kufosi hayo mazungumzo, ni kwamba nilikuwa naamini yupo katika position ya kunisaidia kupata mchongo halali, maana alikuwa na maisha mazuri tu. Ila yeye hakuwa tayari kuendeleza ukaribu kati yetu
Aha nimekupata mkuu
 
2nd Portion:

... Ilivyofika siku aliyosema ataenda pale shule, niliwasiliana nae mapema tu asubuhi, akaniambia nitangulie shule, anikute ofisini.

Nikasubiria wanafunzi wengine wametoka assembly na kuingia madarasani, Kisha mdogo mdogo nikaingia eneo la shule. Kufika ofisini, Mwalim ananiuliza umefata nini bila ya mzazi?. Nikamjibu kuwa baba Yuko njiani, amesema anikute ofisini. Hapo namjibu, ila nina hofu ya kutosha, kwanza sielewi yule mchaga akija atasema Nini, tusije umbuka kama Ochu. Sasa ile hofu niliyokuwa nayo, ikamhadaa Mwalim, akaona kijana nipo serious, nimeshikika. Nikaambiwa nikae kwenye benchi nje ofisi pale.

Kama dakika 45 hivi, mchaga hatokei. Head Master akanimind, walim nao wakaanza kunisema (siunajuaga walim wakiwa wengi ofisini). Ghafla naona yule mchaga kaja, begi lake mgongoni kama vile katoka safari. Kufika karibu, akapokewa na head Master. Wakati wanasalimiana, nikageuza shingo ili nimsalimie, maana alinipita wakawa kama wamesimama nyuma yangu. Kumbe wakati nageuka, nae alikuwa ameplan kunipiga kofi, kwahiyo kile kitendo cha kugeuka, nilikutana na kofi Kali la uso, hadi nikachanika kidogo mdomo wa chini.

Hata Head Master hakuwa ametarajia lile swala, akawa ameshtuka, akamuuliza "We Mzee unafanya nn? Hebu tulia, usije kusabisha majanga hapa"

Yule mchaga akamkunjia sura Head Master "Huyu ni mwanangu, Nina haki ya kufanya lolote". Head Master akavunga. Mchaga akaomba taarifa kamili ya kilichotokea, akakaribishwa ofisini kwa Mkuu. Kikao kikaanza, Mchaga, Mkuu, Mwalim wa nidham, pamoja na Mwalim aliyetushika siku ile. Muda huo nimepigishwa magoti. Mchaga akaelezwa issue nzima ilivyokuwa. Alikuwa amekaa, akasimama kwanza, akawa kama anataka kutoka nje ya ofisi, alafu akarudi. Walim wanamtuliza "Mzee hebu tulia kwanza" alaf mkuu akamuagizia maji walau yamsaidia kupunguza presha. Yule dingi baada ya kunywa maji, aliinama kama dakika 5 yupo kimya tu. Baada ya hapo akaomba fimbo. Alininyuka hadi fimbo ikaisha, akaanza kunipiga makofi. Walim wanafanya kumzuia.

Sijawahi kupatwa hasira kama niliyopata siku ile, maana alinibutua sana, alaf sikuwa na lolote ninaloweza kufanya. Maana ningemdindia, maana yake msala wa kuleta mzazi ungeendelea kuwepo. Mwisho wa siku wakayaongea pale, nikapungiziwa adhabu, badala ya miezi mitatu, nikaambiwa nirudi baada ya mwezi mmoja na nusu alaf siku ya kuripoti nije na 150k kama faini.

Tukatoka nje ya shule, mdogo mdogo tukaizunguka shule, tukachukua uelekeo zilipo hostel za nje. Kwenye zile hostel ng'ambo ya barabara kulikuwa na bustan, tukaenda kukaa pale. Hapo njia nzima tupo kimya, hakuna anayeongea, maana nilitaka kuongea akaniambia nitulie, tutaongea tukifika. Sasa tumefika pale, cha kwanza kuniambia "Pole sana kijana, wale ni watu wazima, kugain trust yao sio kazi ndogo"

Nikawaka, "hata kama, sio unipige vile". Mchaga nae akawaka "Kwanza uliniongopea, ulisema kesi ya uzushi, kumbe umeiba mahindi ya shule? Sasa unataka wenzako wafe njaa?" Nikaanza kujiuliza huyu jamaa vipi, mzima kweli? Mchaga akaendelea "Watoto kama wewe ndio wanasababisha watoto wetu wanafeli, mnaenda shule kusumbua wengine, kama hutaki shule acha, ila usiwape wakati mgumu watoto wa wengine, kwanza naomba hela yangu iliyobaki".

Yani kunipiga kote kule, Bado unataka hela nyingine? Akaniambia "Dogo sijaja Tanga kusoma kama wewe, nimekuja kutafuta hela, usijitoe akili, ntarudi shule nikakuharibie". Nikaona isiwe kesi, nikatoa 20 nikampa akate 15k, mchaga akasema hapa hairudi chenji, ile 25k ilikuwa ni makubaliano kwavile ulisema wamekusingizia kesi, ila ungeniambia ukweli, dau lingepanda.

Nikataka kubisha, ila sikuona dalili za kuipata hiyo elfu 5, so ikabidi nipigie kimya tu. Akaniambia "Usihudhunike sana, nimekusaidia sana, tena next time nitakupunguzia, sitokufanyia Bei kubwa, tushakuwa wana". Nikaona huyu Mzee mbona kama ananichulia? Next time ipi?. Akaniuliza shule unamaliza lini kwani? Nikamjibu mwakani. Akatabasam kidogo, Kisha akaniambia "Kwa jinsi ninavyokuona, ni mbali sana, tunza namba yangu utanihitaji tena kabla hujamaliza shule". Akaamsha.

Alivyoondoka, nikaanza kujiuliza huo mwezi mmoja na nusu naumaliza vipi bila sehem rasmi ya kuishi? Maana sikutakiwa kuonekana hostel. Na kwavile Mzee ameshakuja, hivyo walim wanaamini nitaondoka nae, hakuna mzazi anayeweza kumuacha mwanae arande rande tu. Nakusema kukaa kwa mwanamke mwezi na nusu, bila kuwa na hela, isingekuwa rahisi.

Nikafikiria kwenda kwa ule mshangazi wangu wa buguruni sokoni, ila nikaona nitapoteza. Nikajikuta out of options, ikabidi niamue kurudi Dar kwa muda. Dar sikuwa na sehemu ya kufikia zaidi ya kwake. Hata hivyo sikuwa na mpango wa kukaa sana pale, baada ya kama siku 4 nikapanda bus kwenda Mbeya, kuna jamaa yangu nilikuwa nafahamiana nae mtu wa migodini, sema sio mchimbaji, yeye anafanya biashara ndogo ndogo kama kuuza sigara, bangi, mirungi, boxer n.k

Kitu ambacho najilaumu mpaka sasa, ule muda niliokuwa nimepewa suspension, walau ningeutumia kupiga pindi mchikichini, au hata kujisomea, ndio kwanza nazurura. Nikafika mpaka Mbeya, then nikachukua gari za kunifikisha Songwe, kule nilienda sehemu moja inaitwa Ngwala, jamaa ndio alikuwa kule. Nilivyofika, sikukaa siku nyingi, jamaa akasema kwa kipindi kile, pale hakuna hela, akasema twende kwenye migodi mingine tucheki harakati. Tulikuwa tunazunguka na kukaa sehemu kutegemeana na movements za wachimbaji. Ukiachana na uuzaji wa zile bidhaa, lakini pia sometime nasi tulikuwa tunajumuika na wadau wengine waliokuwa wanachambua chambua mabaki ya mchanga wa madini, au pia kufanya kazi zingine zinazojitokeza. Makapi makapi tuliyokuwa tunaokota na kuuza, yalikuwa yanatupa vihela viwili vitatu vya kusogeza siku.

Ubaya wa migodini, kuna watu tangia wameenda kule, hawajawahi kurudi makwao, kibaya zaidi wengine hata hawajulikani kwa majina yao halisi, ni mwendo wa nicknames tu. Nakumbuka kuna mwamba mmoja aliugua hadi akafa, ila hakuna aliyekuwa anamjua ndugu yake hata mmoja. Jamaa ilibidi azikwe kule kule tu, unaweza kuta ndugu zake mpaka leo wanaimani ndugu yao kaenda kutafuta, atarudi, kumbe jamaa hadi kuoza ameshaoza tayari. Lile tukio lilinifikirisha sana, itakuwaje likinitokea Mimi? Ndo yale mambo, unaangalia zako taarifa ya habari, unasikia kifusi kimefunika watu machimboni, mzazi unachukulia kawaida, unawapa pole wafiwa, ukiamini mwanao yeye yupo shule, kumbe ni miongoni mwa majeruhi au waliofukiwa.

Katika uokotaji kwenye yale mabaki, kuna siku jamaa yangu alibahatisha kajiwe fulani hivi kadogo. Kwavile Giza lilikuwa lishaanza kuingia, tukaamua kwenda kumcheki yule anaeyanunua, tupate hela ya kula then tulale. Jamaa kale kajiwe alikachukua kwa milioni mbili na nusu. Nikamwambia jamaa silali huku leo, naamsha usiku huu huu. Tukachukua pikipiki zikatupeleka mpaka center, lengo ni tulale pale, alaf asubuhi tuchukue gari za kutupeleka mjini. Mpaka muda huo, ile hela tulishagawana pasu kwa pasu, kila mtu anayake.

Kufika center, tukachukua room moja kwenye bar tuliyofikia. Jamaa yangu ni mtu wa tungi, so after kuoga, akashauri tuchukue bia kadhaa tunywee room. Binafsi sikuwa mnywaji pombe, ila nikaona sio kesi, jamaa kaagiza Serengeti, Mimi nikachukua safari 5 tu maana sikuwa mzoefu, tukarudi gheto. Ila binafsi sikuwa na amani kabisa, maana yule jamaa ni mzoefu, nikahisi naweza nikalewa, alaf akapita na hela zote nisijue nampatia wapi. Maana tumefahamiana kwenye harakati tu, tena niliunganishwa na jamaa mwingine ambae ndio alikuwa rafiki yetu wote. Nikawa namtegea jamaa anywe, ila nae akauchuna. Ananiuliza "Mbona hunywi?", Namjibu nitakunywa. Kiufupi mpaka kunakucha, hakuna aliyegusa bia hata moja, kulala yenyewe ilikuwa unasinzia kidogo, then unashtuka. Kulivyokucha, Mimi ndio nilianza kuondoka, maana safari yangu ilikuwa ndefu, nilitaka niunge Dar moja kwa moja, bia zote nilimuachia yeye.

Mbeya mjini, nikaweka kiasi cha zile hela kwenye account, then nikachukua chuma ya kwenda Dar. Hapo ni mwezi mzima unaenda kuisha tokea nitoke Tanga. Baada ya kufika Dar, plans zangu ilikuwa nikanunue materials alaf hizo siku chache nikazimalizie Galanosi kwa jamaa yangu. Nikiwa ndio bado nazunguka kwenye centers tofauti tofauti kununua past papers, Mshua akanipigia simu. Tukaongea fresh, akaniuliza maendeleo, nikamjibu kila kitu kinaenda vizuri, baada ya story mbili tatu tukaagana.

Usiku huo huo, akanipigia simu head prefect kwamba kuna usajili unaendelea pale shuleni kwa wanafunzi wa kidato cha 6, hivyo nifanye mpango niende haraka. Akaniambia pia kuhusu suspension, kwavile siku zimebaki chache, niende na mzazi wangu tena pale shuleni na hela ya fine, atafanya mpango nitapokelewa tu.

Nikaona wazo zuri, kumpigia simu yule Mchaga, akasema aina noma, kesho yake nirudi Tanga, then siku inayofatia twende wote shule akamalizie msala.

Ambacho Mimi na yeye hatukukijua, kumbe Mshua wangu akiwa kwenye kufatilia biashara zake, aliamua aje pale shule kuniangalia kabla hajarudi kijijini. So, muda wote tulioongea na simu Jana yake, tayari alikuwa na taarifa zangu full.

Mimi na yule Mchaga tulikuwa tumeandaliwa mtego. Kilichoenda kutokea, Mchaga alisema hatonisahau........

Endelea hapa Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu. Mpaka siku niliyokutana na yule Mzee
Ndugu wasomaji, kivumbi leo
 
20th Portion:

... Nikiwa pale kwenye kiti, Mzee Kesho Yetu alibaki ameniangalia kwa muda mrefu, Kisha akaniambia

Mzee KY: "Sikia bwana mdogo, nakushauri upotee mjini kwa muda. Hivi pale ulishahama?"

Analyse: "Ndio"

Mzee KY: "Vizuri, sasa inabidi usionekene Dar kwa kipindi fulani, ili upishe hali ya hewa itulie."

Analyse: "Natamani kufanya hivyo, ila hela ndio sina. Kule kuhama hama, kumenipotezea hela sana. Hata huku kukutafuta wewe nako kumenirudisha nyuma"

Mzee KY: "Enhee Hapo hapo kwenye kunitafuta, naomba tukiachana leo nisikuone tena hata kwa bahati mbaya. Nisingependa unifatilie tena"

Analyse: "Sasa naondoka vipi na Sina hela?"

Mzee KY: "Unapoanza jambo lolote, lazima uwe umepanga namna ya kulimaliza. Vinginevyo utajikuta unaingia matatizoni kama hivi sasa"

Analyse: " Basi nifanyie mpango hata wa kiasi kadhaa walau kiniwezeshe kupotea"

Mzee KY: " Sina hela kwasasa"

Analyse: " Hela zote ulizopiga Mzee?"

Mzee KY: " Hela zote kiasi gani?. Hivi unajua nyuma yangu kulikuwa na watu wangapi hadi dili likafanikiwa?"

Akaendelea, " Nitakupa ile laki mbili niliyokuahidi wakati ule, nitakuongezea na elfu hamsini. Zaidi ya hapo, sina."

Nikabaki nafikiria tu pale, natokaje salama kwenye huu msala?

Akaendelea, "Tena kitu unachotakiwa kukikwepa sana, ni kuonana na wale wazee wengine. Ni rahisi wao kukuchoma, ili wao wajiweke on safe side".

Analyse: " Sawa nimekuelewa, ila nina ombi moja la mwisho"

Mzee KY: "Ombi gani?"

Analyse: "Unajua wale wazee walinipora ile hirizi niliyopewa na yule mtaalam wako, kama inawezekana unidirect kwake akanipatie nyingine"

Yule Mzee aliniangalia kama vile nimeongea kitu ambacho hakukitarajia kabisa.

Mzee KY: "Ilo haliwezekani kabisa. Alafu nilijua utaongea kitu cha maana, kumbe kujichanganya na wazee akili yako ndio ishavurugika hivyo?"

Analyse: "Sina akiba Mimi, alaf natakiwa kujificha. Najifichaje sasa?"

Mzee KY: " Hayo ilibidi uyawaze kabla hujaamua kuingia kwenye hizi kazi"

Analyse: "Ila nyie ndio mlionishawishi kuingia kwenye hizi kazi"

Mzee KY: "Ila hakuna aliyekulazimisha"

Maneno yake yanazidi kunikata moto, maana bila hela ya maana ni ngumu kutoboa mafichoni.

Analyse: "Basi nisaidie jambo jingine?"

Mzee KY: "Lipi?"

Analyse: "Kwavile wewe unabiashara nyingi genuine mjini, basi nifanyie hata mchakato nifanye kazi kwako"

Akanishangaa tena;

Mzee KY: "Bwana mdogo kumbe hauko smart kama nilivyodhani. Umefikiria kabla hujatoa ilo ombi?"

Analyse: "Nimefikiria, ila sina namna ya kusurvive"

Mzee KY: "Sikia, Mimi na ww kitendo cha kufahamiana kwa njia hii, basi hatuwezi tena changamana nje ya hapa. Na kama tungejuana nje ya hapa, basi hakuna uwezekano ungeweza kunifahamu namna hii. Wakati unajiunga ulijua unachokuja kukifanya, na ukaamua kujiunga, tafuta namna ya kujitoa"

Yaliongelewa mengi, lakini hapakuwa na lolote ambalo lingeweza kumfanya either aniongezee hela au hata anipe ajira. So, tukamalizana kwa yeye kutoa hela kwa wakala, na kunipatia. Hakutaka kabisa kunipa namba yake aliyokuwa anatumia pale. Baada ya kunipa hela akaniambia;

"Kubali hasara, badili simu na hiyo line. Usivitumie tena. Narudia, Simu na line, sio line peke yake"

Tukaagana, nikaamsha.

Nikazunguka, upande wa parking. Nika nakili namba za lile gari lao, kisha nikadandia usafiri wa kurudi Dar. Nikiwa ndani ya coaster, Mzee Kesho Yetu akanitext kwa ile namba yake ya siku zote, "Nimeambiwa umenakili plate namba za hii gari, fikiria mara mbili kabla hujafanya ulichokusudia, maana hakuna kurudi nyuma baada ya hapo".

Nikajifikiria kwa muda, ila nikaamua kumpotezea. Maana hata Mimi mwenyewe sikujua kwanini nimenakili ile namba, ila nilipata hisia inaweza kuja kuwa na msaada mbeleni.

Sababu iliyosababisha nirudi Dar, kwanza sikuwa nimeplan niende wapi, pili sikuwa nimejipanga vizuri namna ya kuondoka.

Nilivyokuwa ndani ya gari, ile simu nikaamua kumuuzia abiria aliyekuwa pembeni yangu. Niliiuza kwa bei ya hasara, ila sikujali. Line nikafuta majina yote, kisha nikaitupa mle mle ndani ya gari.

Nikanyoosha moja kwa moja mpaka gheto. Naanza kutafakari wapi nitaenda. Kesho yake nikanunua simu ndogo ya batani na kusajili line mpya, kisha nikarudi ghetto. Sikuwa napenda kushinda sana nje. Giza likishaanza kuingia, ndio nilikuwa nautumia huo muda kutembea tembea.

Zilipita kama wiki mbili, bila kash kash yoyote au kukutana na mtu yeyote wa kunipa mashaka. Nilivyohisi kama kumetulia, kuna jamaa yangu nikaenda kuonana nae maeneo ya Mikocheni, sasa muda narudi nimefika pale mwenge mataa. Nilisimama karibia robo saa nzima, natafuta timing ya kuvuka barabara, maana gari zilikuwa speed sana.

Zilivyopungua nikawa navuka. Sasa wakati navuka, kuna Mzee nae akawa anavuka kutokea upande opposite na wangu. Ikatokea ile hali ya kugonganisha njia. Yani wewe ukitaka kupita upande wa kulia, wa mbele yako nae anakua kaamua kupita upande huo. Ukisema ushift kushoto, unakuta na yeye karudisha mawazo ya kupita upande huo. Mpaka mnajikuta mnagongana. Icho ndicho Kilichotokea kwa yule Mzee.

Kila nikimkwepa na kwenda kulia, nae anakuja huko, nikirudi kushoto nae huyo kushoto. Binafsi nikikutanaga na situation kama hiyo, huwa nasimama, ili huyo mtu mwingine apite, ila Cha ajabu kwa yule Mzee, nilivyosimama na yeye akasimama. Alafu muda huo huo, kuna gari ipo kibati inakuja upande wetu. Nilivyóona simuelewi yule Mzee, nikaamua liwalo na liwe, kwa nguvu zangu zote nikaamua kumpush ili tuangukie anapotoka yeye. Cha ajabu, nilitumia nguvu nyingi sana, ila nikajikuta napush hewa, hapakuwa na mtu mbele yangu. Nikaangukia upande wa pili, ile gari ikapita speed bila hata kusimama.

Haya yote yalitokea ndani ya muda mchache sana. Cha kushangaza, watu waliokuwa jirani, wao walichukulia kile kitendo kama nimejirusha ili kulikwepa lile gari, kumbe mwenzao niliona vitu tofauti. Na kati yao waliokuwa wanaongea, hakuna aliyezungumzia habari za kumuona mtu mwingine mbele yangu. Waliishia kunipa pole, wengine hongera kuwa siku yangu ya kufa bado nk. Lile tukio lilinifikirisha sana. Kwanini limetokea? Linahusiana na issue tuliyofanya kwa yule mstaafu?. Au ndio ndugu zake wameamua kunifanya kama alivyofanya Kisauti?. Kama ni hivyo, why Mimi niwe napataga adhabu tu, alaf wanaofaidika ni wengine?. Najitoaje kwenye Ili?

Akili ikaanza kuniambia niondoke mjini haraka sana. Ila naenda wapi?. Home nikienda, lazima niulizwe kwanini nimeenda, maana wao wanahisigi nikishazingua ndio huwa naenda. And this time ni sahihi, nishazingua, je niende au nisiende?

Ila hata nikienda, kama jamaa wameniamulia, wanaweza kunidhuru nikiwa kule kule. Nikaanzr upya vurugu za kwenda kwa waganga na Mshua?. Mawazo yakanijia nimpigie Kisauti, dhumuni ikiwa walau anipeleke hata kwa mtaalam wake nikajikinge kwanza. Ila kuna sauti ndani yangu ikawa inanikumbusha maonyo ya mtaalam kuwa nisije kumtafuta tena Kisauti. Ila nitafanyaje?. Namtafuta vipi huyo Kisauti
wakati namba yake sikuwa nayo, niliifuta nilivyouza simu?.

Na kusema niende mpaka kule walipo kabla sijaongea nae itakuwa uongo. What if hasira zao hazijaisha? Na zinaishaje ikiwa hawajapata hela zao?.

Ndani ya wiki nilishaanza kukonda kwa mawazo, maana pia hela Nazo zinaisha tu Kwa matumizi, ila siingizi hata 100.

Wiki mbili tokea lile tukio la pale mwenge litokee, sister akanipigia simu kuwa Mama anaumwa sana, alafu sijawahi hata kuwajulia hali. Ofcourse kichwa changu kisipokuwa na utulivu, huwa kuwatafuta watu inakuwaga issue sana. Na mtu asiponielewa, tutagombana mara kwa mara, ndio maana mahusiano yangu mengi yanavunjikaga kwa mtindo huu. Tokea nibadilishe simu na line, nilivyowapigia ndugu zangu kuwataarifu kuhusu namba yangu mpya, sikuwahi kuwatafuta tena.

Na hapo ulishapita karibia mwezi mzima. Baada sister kunipigia na kunipa ile taarifa, nikajiona nishapata sababu ya kwenda home. Nikaamua kumpigia Mama home, simu alipokea Mshua. Baada ya salamu za hapa na pale, ikiwa ni pamoja na kunielezea hali ya Mama. Nikamwambia kuna kazi ya watu naiweka sawa, kisha baada ya wiki moja nitaenda kuwaona. Hakunipinga.

Sikuwa na kazi yoyote, ila Mshua namjua hivyo sikutaka maswali mengi. Ningemwambia kesho yake naanza safari, angetaka kujua kwamba Sina mishe huku mjini? Maana haiwezekani taarifa upewe leo, then kesho upo ndani ya bus. Sikuwa nimejiandaa namna ya kudanganya, nilihofia ningebabaika alaf akahisi kuna jambo haliko sawa.

Ile wiki nzima ya kusubiria safari, sikutaka hata kutoka nje na pale nilipokuwa naishi. Muda wote nipo ndani, au chooni. Ndani au dukani. Kiufupi niliishi kama digidigi.

Baada ya wiki, nikafunga safari kwenda home. Punch alizoenda kunipa Mshua, zilikuwa ni mara mia ya alizonipa Mzee wa Kongowe.

Walau Mzee wa Kongowe alikuwa ni mtu baki, maana kuna baadhi ya maneno ukiambiwa na mtu wa karibu sana, yanachoma kuliko hata msumari. Mzee wa Kongowe alinifanya nikaanza kumuangalia Mshua kwa namna ya tofauti. Ila maneno ya Mshua yalinibadili mtazamo wangu kabisa.

Kauli za Mshua Ziliniumiza sana, ila naweza kusema zilinisaidia sana kurudi kwenye mstari. Zilinifanya nikaanza kuyaangalia baadhi ya mambo kwa mitazamo tofauti sana. Au kuwachukulia watu kwa namna ya kipekee pia.

Niliufurahia uhamuzi wa kurudi nyumbani kipindi kile. Maana niliondoka nikiwa mtu wa tofauti ....

Endelea hapa Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee
Sehemu ya 19 sijaiona nimeitafuta mpaka nimechoka
 
Nimejaribu kuangalia, pia sijaiona. Itabidi mods Moderator YinYang Invisible au Maxence Melo waje wakupe jibu kwanini imeondolewa.

Hiyo portion ya 19 ilikuwepo
Aisee! Yani nimesoma kipande cha 20 kama nikiwa nimeshikiwa fimbo na kujaribu kuungaunga kila tukio la kuunganisha hiyo part ila sijafua dafu! Nikakosa ladha ikabidi nipumzike kidogo! Ndio nimerudi nikiwa na matumaini flani ambayo sijayakuta!


Kiweke hapa mkuu au nitumie PM kama kilikua na ukakasi mpaka kimeondolewa
 
Wamefanya vibaya sana! Yani sijaona hata mtu kui quote hiyo part, kilikua na shida gani!!?
 
Wamefanya vibaya sana! Yani sijaona hata mtu kui quote hiyo part, kilikua na shida gani!!?
Wametoa vyote hadi ambavyo mtu aliquote, sijajua shida ni nn. Haikuwa na contents zozote mbaya
 
Back
Top Bottom