20th Portion:
... Nikiwa pale kwenye kiti, Mzee Kesho Yetu alibaki ameniangalia kwa muda mrefu, Kisha akaniambia
Mzee KY: "Sikia bwana mdogo, nakushauri upotee mjini kwa muda. Hivi pale ulishahama?"
Analyse: "Ndio"
Mzee KY: "Vizuri, sasa inabidi usionekene Dar kwa kipindi fulani, ili upishe hali ya hewa itulie."
Analyse: "Natamani kufanya hivyo, ila hela ndio sina. Kule kuhama hama, kumenipotezea hela sana. Hata huku kukutafuta wewe nako kumenirudisha nyuma"
Mzee KY: "Enhee Hapo hapo kwenye kunitafuta, naomba tukiachana leo nisikuone tena hata kwa bahati mbaya. Nisingependa unifatilie tena"
Analyse: "Sasa naondoka vipi na Sina hela?"
Mzee KY: "Unapoanza jambo lolote, lazima uwe umepanga namna ya kulimaliza. Vinginevyo utajikuta unaingia matatizoni kama hivi sasa"
Analyse: " Basi nifanyie mpango hata wa kiasi kadhaa walau kiniwezeshe kupotea"
Mzee KY: " Sina hela kwasasa"
Analyse: " Hela zote ulizopiga Mzee?"
Mzee KY: " Hela zote kiasi gani?. Hivi unajua nyuma yangu kulikuwa na watu wangapi hadi dili likafanikiwa?"
Akaendelea, " Nitakupa ile laki mbili niliyokuahidi wakati ule, nitakuongezea na elfu hamsini. Zaidi ya hapo, sina."
Nikabaki nafikiria tu pale, natokaje salama kwenye huu msala?
Akaendelea, "Tena kitu unachotakiwa kukikwepa sana, ni kuonana na wale wazee wengine. Ni rahisi wao kukuchoma, ili wao wajiweke on safe side".
Analyse: " Sawa nimekuelewa, ila nina ombi moja la mwisho"
Mzee KY: "Ombi gani?"
Analyse: "Unajua wale wazee walinipora ile hirizi niliyopewa na yule mtaalam wako, kama inawezekana unidirect kwake akanipatie nyingine"
Yule Mzee aliniangalia kama vile nimeongea kitu ambacho hakukitarajia kabisa.
Mzee KY: "Ilo haliwezekani kabisa. Alafu nilijua utaongea kitu cha maana, kumbe kujichanganya na wazee akili yako ndio ishavurugika hivyo?"
Analyse: "Sina akiba Mimi, alaf natakiwa kujificha. Najifichaje sasa?"
Mzee KY: " Hayo ilibidi uyawaze kabla hujaamua kuingia kwenye hizi kazi"
Analyse: "Ila nyie ndio mlionishawishi kuingia kwenye hizi kazi"
Mzee KY: "Ila hakuna aliyekulazimisha"
Maneno yake yanazidi kunikata moto, maana bila hela ya maana ni ngumu kutoboa mafichoni.
Analyse: "Basi nisaidie jambo jingine?"
Mzee KY: "Lipi?"
Analyse: "Kwavile wewe unabiashara nyingi genuine mjini, basi nifanyie hata mchakato nifanye kazi kwako"
Akanishangaa tena;
Mzee KY: "Bwana mdogo kumbe hauko smart kama nilivyodhani. Umefikiria kabla hujatoa ilo ombi?"
Analyse: "Nimefikiria, ila sina namna ya kusurvive"
Mzee KY: "Sikia, Mimi na ww kitendo cha kufahamiana kwa njia hii, basi hatuwezi tena changamana nje ya hapa. Na kama tungejuana nje ya hapa, basi hakuna uwezekano ungeweza kunifahamu namna hii. Wakati unajiunga ulijua unachokuja kukifanya, na ukaamua kujiunga, tafuta namna ya kujitoa"
Yaliongelewa mengi, lakini hapakuwa na lolote ambalo lingeweza kumfanya either aniongezee hela au hata anipe ajira. So, tukamalizana kwa yeye kutoa hela kwa wakala, na kunipatia. Hakutaka kabisa kunipa namba yake aliyokuwa anatumia pale. Baada ya kunipa hela akaniambia;
"Kubali hasara, badili simu na hiyo line. Usivitumie tena. Narudia, Simu na line, sio line peke yake"
Tukaagana, nikaamsha.
Nikazunguka, upande wa parking. Nika nakili namba za lile gari lao, kisha nikadandia usafiri wa kurudi Dar. Nikiwa ndani ya coaster, Mzee Kesho Yetu akanitext kwa ile namba yake ya siku zote, "Nimeambiwa umenakili plate namba za hii gari, fikiria mara mbili kabla hujafanya ulichokusudia, maana hakuna kurudi nyuma baada ya hapo".
Nikajifikiria kwa muda, ila nikaamua kumpotezea. Maana hata Mimi mwenyewe sikujua kwanini nimenakili ile namba, ila nilipata hisia inaweza kuja kuwa na msaada mbeleni.
Sababu iliyosababisha nirudi Dar, kwanza sikuwa nimeplan niende wapi, pili sikuwa nimejipanga vizuri namna ya kuondoka.
Nilivyokuwa ndani ya gari, ile simu nikaamua kumuuzia abiria aliyekuwa pembeni yangu. Niliiuza kwa bei ya hasara, ila sikujali. Line nikafuta majina yote, kisha nikaitupa mle mle ndani ya gari.
Nikanyoosha moja kwa moja mpaka gheto. Naanza kutafakari wapi nitaenda. Kesho yake nikanunua simu ndogo ya batani na kusajili line mpya, kisha nikarudi ghetto. Sikuwa napenda kushinda sana nje. Giza likishaanza kuingia, ndio nilikuwa nautumia huo muda kutembea tembea.
Zilipita kama wiki mbili, bila kash kash yoyote au kukutana na mtu yeyote wa kunipa mashaka. Nilivyohisi kama kumetulia, kuna jamaa yangu nikaenda kuonana nae maeneo ya Mikocheni, sasa muda narudi nimefika pale mwenge mataa. Nilisimama karibia robo saa nzima, natafuta timing ya kuvuka barabara, maana gari zilikuwa speed sana.
Zilivyopungua nikawa navuka. Sasa wakati navuka, kuna Mzee nae akawa anavuka kutokea upande opposite na wangu. Ikatokea ile hali ya kugonganisha njia. Yani wewe ukitaka kupita upande wa kulia, wa mbele yako nae anakua kaamua kupita upande huo. Ukisema ushift kushoto, unakuta na yeye karudisha mawazo ya kupita upande huo. Mpaka mnajikuta mnagongana. Icho ndicho Kilichotokea kwa yule Mzee.
Kila nikimkwepa na kwenda kulia, nae anakuja huko, nikirudi kushoto nae huyo kushoto. Binafsi nikikutanaga na situation kama hiyo, huwa nasimama, ili huyo mtu mwingine apite, ila Cha ajabu kwa yule Mzee, nilivyosimama na yeye akasimama. Alafu muda huo huo, kuna gari ipo kibati inakuja upande wetu. Nilivyóona simuelewi yule Mzee, nikaamua liwalo na liwe, kwa nguvu zangu zote nikaamua kumpush ili tuangukie anapotoka yeye. Cha ajabu, nilitumia nguvu nyingi sana, ila nikajikuta napush hewa, hapakuwa na mtu mbele yangu. Nikaangukia upande wa pili, ile gari ikapita speed bila hata kusimama.
Haya yote yalitokea ndani ya muda mchache sana. Cha kushangaza, watu waliokuwa jirani, wao walichukulia kile kitendo kama nimejirusha ili kulikwepa lile gari, kumbe mwenzao niliona vitu tofauti. Na kati yao waliokuwa wanaongea, hakuna aliyezungumzia habari za kumuona mtu mwingine mbele yangu. Waliishia kunipa pole, wengine hongera kuwa siku yangu ya kufa bado nk. Lile tukio lilinifikirisha sana. Kwanini limetokea? Linahusiana na issue tuliyofanya kwa yule mstaafu?. Au ndio ndugu zake wameamua kunifanya kama alivyofanya Kisauti?. Kama ni hivyo, why Mimi niwe napataga adhabu tu, alaf wanaofaidika ni wengine?. Najitoaje kwenye Ili?
Akili ikaanza kuniambia niondoke mjini haraka sana. Ila naenda wapi?. Home nikienda, lazima niulizwe kwanini nimeenda, maana wao wanahisigi nikishazingua ndio huwa naenda. And this time ni sahihi, nishazingua, je niende au nisiende?
Ila hata nikienda, kama jamaa wameniamulia, wanaweza kunidhuru nikiwa kule kule. Nikaanzr upya vurugu za kwenda kwa waganga na Mshua?. Mawazo yakanijia nimpigie Kisauti, dhumuni ikiwa walau anipeleke hata kwa mtaalam wake nikajikinge kwanza. Ila kuna sauti ndani yangu ikawa inanikumbusha maonyo ya mtaalam kuwa nisije kumtafuta tena Kisauti. Ila nitafanyaje?. Namtafuta vipi huyo Kisauti
wakati namba yake sikuwa nayo, niliifuta nilivyouza simu?.
Na kusema niende mpaka kule walipo kabla sijaongea nae itakuwa uongo. What if hasira zao hazijaisha? Na zinaishaje ikiwa hawajapata hela zao?.
Ndani ya wiki nilishaanza kukonda kwa mawazo, maana pia hela Nazo zinaisha tu Kwa matumizi, ila siingizi hata 100.
Wiki mbili tokea lile tukio la pale mwenge litokee, sister akanipigia simu kuwa Mama anaumwa sana, alafu sijawahi hata kuwajulia hali. Ofcourse kichwa changu kisipokuwa na utulivu, huwa kuwatafuta watu inakuwaga issue sana. Na mtu asiponielewa, tutagombana mara kwa mara, ndio maana mahusiano yangu mengi yanavunjikaga kwa mtindo huu. Tokea nibadilishe simu na line, nilivyowapigia ndugu zangu kuwataarifu kuhusu namba yangu mpya, sikuwahi kuwatafuta tena.
Na hapo ulishapita karibia mwezi mzima. Baada sister kunipigia na kunipa ile taarifa, nikajiona nishapata sababu ya kwenda home. Nikaamua kumpigia Mama home, simu alipokea Mshua. Baada ya salamu za hapa na pale, ikiwa ni pamoja na kunielezea hali ya Mama. Nikamwambia kuna kazi ya watu naiweka sawa, kisha baada ya wiki moja nitaenda kuwaona. Hakunipinga.
Sikuwa na kazi yoyote, ila Mshua namjua hivyo sikutaka maswali mengi. Ningemwambia kesho yake naanza safari, angetaka kujua kwamba Sina mishe huku mjini? Maana haiwezekani taarifa upewe leo, then kesho upo ndani ya bus. Sikuwa nimejiandaa namna ya kudanganya, nilihofia ningebabaika alaf akahisi kuna jambo haliko sawa.
Ile wiki nzima ya kusubiria safari, sikutaka hata kutoka nje na pale nilipokuwa naishi. Muda wote nipo ndani, au chooni. Ndani au dukani. Kiufupi niliishi kama digidigi.
Baada ya wiki, nikafunga safari kwenda home. Punch alizoenda kunipa Mshua, zilikuwa ni mara mia ya alizonipa Mzee wa Kongowe.
Walau Mzee wa Kongowe alikuwa ni mtu baki, maana kuna baadhi ya maneno ukiambiwa na mtu wa karibu sana, yanachoma kuliko hata msumari. Mzee wa Kongowe alinifanya nikaanza kumuangalia Mshua kwa namna ya tofauti. Ila maneno ya Mshua yalinibadili mtazamo wangu kabisa.
Kauli za Mshua Ziliniumiza sana, ila naweza kusema zilinisaidia sana kurudi kwenye mstari. Zilinifanya nikaanza kuyaangalia baadhi ya mambo kwa mitazamo tofauti sana. Au kuwachukulia watu kwa namna ya kipekee pia.
Niliufurahia uhamuzi wa kurudi nyumbani kipindi kile. Maana niliondoka nikiwa mtu wa tofauti ....
Endelea hapa
Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee