Tashacobbs
JF-Expert Member
- Jun 18, 2022
- 572
- 1,559
Story nzuri
Big up
Big up
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shukrani sana mkuu ngoja nitulie niisome vizuri!!
Wabheja sana sis story nzuri sana!!!
Itoshe kusema wewe na mshua wako mmepitia mengi [emoji28][emoji28]4th Portion:
.... Sikuelewa alimaanisha nini, na yeye hakuwa tayari kutoa ufafanuzi mpaka apate jibu langu. Sikutaka kukubali kichwa kichwa kujibu kitu ambacho sijaelewa, niliyoshapitia yanatosha, sikutaka kupitia mengi zaidi. Ikabidi nizuge kwa kumwambia inaelekea Mimi na yeye tunamengi sana ya kuzungumza, na kwavile mitihani inakaribia, basi asubirie nimalize, then tuyajenge kwa kirefu. Hakuwa na pingamizi, sana sana akaniambia kuwa yeye yupo, haendi popote, nikiwa na muda nisiache kumtafuta. After that day, sikujisumbua nae tena.
Baada ya kufanya necta, niliendelea kubaki Tanga kwa wiki kadhaa, maana ile sio sehemu unayoondoka tu kizembe. Kwa hizo wiki nilizoendelea kuwepo nikawa naaga makoloni yangu na kufanya utalii wa ndani. Hata baada ya mitihani, Mshua hakuwahi kunicheki hata mara moja, isipokuwa kuna siku inaonekana alisikia mazungumzo yangu ya simu na Mama. Mama alinipa pole na mitihani, alaf akataka kujua narudi lini nyumbani, nikamjibu kuwa kesho yake nitaelekea Dar, alaf kutokea pale nitapanda bus la kuelekea nyumbani. Akawa ananisisitiza nisikae Dar, nipafanye kama njia tu ya kurudia home. Nikamtoa hofu, maana hata hivyo sikuwa na mpango wa kukaa Dar kwa nyakati zile, nilihitaji kupumzisha akili na mwili.
Mida ya usiku, wakati nipo hostel, napiga story na madogo wa form 5, maana pakikucha naondoka mazima, ghafla ikaingia msg toka kwa Mshua. Kwenye ile msg alikuwa ananiambia kuwa amenitumia laki 3 kwenye account yangu. Lakini badala ya kufurahi, nikajikuta napigwa na bumbuwazi, maana maelezo aliyotoa kuhusu ile laki 3, ni kwamba itanisaidia katika kipindi chote cha kusubiria matokeo, maana hataki kuniona nyumbani mpaka matokeo yatoke. Nikaona huyu Mzee vipi? Inamaa Bado anakinyongo na Mimi? Nikampigia simu, iliita kwa muda mrefu, wakati inakaribia kukatika, akapokea.
Analyse: "Shikamoo Baba"
Mshua: "Marahaba"
Analyse: "Naomba nirudi nyumbani, hii hela haiwezi kunitosha kwa kipindi chote cha kusubiria, maana sina pa kulala wala kula, mahitaji ni mengi"
Mshua: "Kwani si una baba mwingine huko? Ukikwama atakusaidia, wewe ni jembe lake"
Analyse: "Naomba nije tukizungumzie ili swala, maana hatukupata muda wa kuongea kabisa"
Mshua: "Kama unahisi utapata zero kwenye hiyo mitihani, niambie mapema nijichange, nikuongezee hela utokomee huko huko"
Analyse: "Dah, lakini Ba...."
Mshua: "Katika ukoo wetu hakuna wasomi wengi, ila sijawahi sikia mtu yeyote aliyepata sifuri, sitaki rekodi za ajabu ajabu zianzie kwenye familia yangu"
Analyse: "Ni kweli mitihani ilikuwa migumu, siwezi bashiri matokeo, lakini siwezi kupata sifuri Baba"
Mshua: "Kama huwezi pata sifuri, basi usiwe na wasi, hiyo hela itakutosha kusubiria matokeo"
Analyse: "Haiwezi kutosha Baba"
Mshua: "Siumezoea kutembea na wamama? tafuta mmoja, msaidiane kutumia mafao yake. Tena nakutahadharisha, haya tuliyoongea ole wale ufungue mdomo kumwambia Mama yako, ukinigombanisha tena na mke wangu, hutoamini nitakachofanya"
Kabla sijajibu, akakata simu. Nikaona hapa shughuli imeshajifunga, Sina ninachoweza kufanya. Mtetezi pekee ni Mama, nae nishapigwa pini kumwambia. Hapo ile balance niliyokuwaga nayo kwenye account, nilikuwa nishaibabua ovyo ovyo, nisingeweza kuendelea kubaki Tanga.
Kesho yake nikaelekea Dar, nikaacha vitu vyangu kwa bi mkubwa yule. Nikaanza harakati pale pale mjini, nikatoka na kwenda maeneo tofauti tofauti. Mama niliendelea kumpiga kalenda kuhusu kurudi nyumbani, hadi matokeo yakatoka. Hayakuwa mazuri, lakini pia sio mabaya, yalitosha kunifanya niendelee na chuo.
Baada ya kuona matokeo, ilibidi nimpigie Mshua. Nilipiga mara 3 hakupokea, alivyoona nimepiga mara ya 4, akakata simu,Kisha akaniandikia msg, "Tuma namba ya shule na namba ya mtihani". Ikabidi nimtumie. Kesho yake akanitumia nauli, nikafanya mchakato, nikarudi zangu nyumbani.
Home nilipokelewa vizuri tu, japo nilijitahidi kuact normal, ila ndani kwa ndani nilikuwa nimemkunjia Mshua. Sikuweza kumwambia Mama kuhusu kukatazwa kurudi home mpaka matokeo yatoke. Na yeye alivyoniona tu, akasahau yote, wala hakuulizia sababu.
Siku zilipita tukiwa katika utulivu, Mshua alikuwa anajaribu kuniweka karibu, nahisi Sometime alikuwa akijisikia vibaya, ila niliendelea kuwa dry tu. Kusoma PCM mimi nilikuwa nafata ndoto zangu, sikuona mantiki ya yeye kunilazimisha nisome alichoona yeye kinafaa. Na kitendo cha kuniambia nisirudi home mpaka matokeo yatoke, niliona haikuwa fair. Hata kama mwanzo nilishawahi kuondoka home na nikasurvive, basi haikutakiwa anichukulie kama mtu ninayeweza kuwekwa kwenye hard time na nikatoboa.
Usajili wa vyuo ulivyoanza, nikajisajili. Vilipofunguliwa nikaelekea Dar kuanza maisha ya chuo. Mwaka wa kwanza na wapili sikuwahi kurudi likizo kabisa. Ila kwenye likizo ya kuingia mwaka wa 3, nikaona ngoja niende home kuwajulia hali. Niliwabebea na vizawadi kadhaa. Kwenye bus, nilikaa na Maza mmoja hivi wa makamo, Yuko vizuri kiasi chake, kama zilivyo pigo zangu. Katika story za hapa na pale, ndio nikagundua anafahamiana na Mshua. Walishafanya pamoja biashara mara kadhaa, ila walipotezana kitambo kirefu.
Kwavile huyu Maza alikuwa anafata bidhaa karibia na Kijiji chetu, akaniambia tuongozane mpaka nyumbani walau akamuone Mzee kabla hajaendelea na shughuli zake. Nikataka nimpigie Mzee kumpa taarifa za ujio wa mgeni wake, ila yule Maza akanizuia. Akasema anataka amfanyie surprise maana ni kitambo sana hawajaonana. Nikaona sio kesi.
Tulivyofika kwenye wigo wa pale nyumbani, palikuwa na utulivu. Tulivyoingia, wa kwanza kutoka alikuwa Mama. Nilifurahi sana kumuona, nikajikuta natabasamu. Ila alivyomuona yule Maza niliyekuja nae, akazubaa kidogo, akajishika kifua kama vile mtu mwenye maumivu. Alaf akakaa chini taratibu, as if miguu haina nguvu.
Nikamgeukia yule Maza nikamwangalia kwa macho yenye mchanganyiko wa kuuliza na kushangaa, huyu Maza ni nani????? [emoji1751][emoji1751]
Mwendelezo basi aseeOngeza siku za kuishi mkuu 😅😅
Nyakibimbiri hii hii ya Izimbya?[emoji38][emoji38]Hahahaaa..nimecheka hapo Ochu alivyoumbuka!!
Hio wanafunzi wanaifanya sana huku mashuleni...kuna siku mwanafunzi mmoja alimleta mzazi wa mchongo ivoivo mtoto anatokea Arusha kazoa kijana Nyakibimbirii hukuuu [emoji23][emoji23] kumbe yule kijana wanajuana vizuri na mwalimu fulani!
Sasa watoto wengine hawawapangi na kuwamezesha vizuri wakifika shule Maelezo wanajichanyanya!