Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

6th Portion:

.... I was a bit disappointed. Tukaongea story zingine mbili tatu, alafu tukaagana. Niliendelea kulifikiria lile swala, mwisho wa siku nikadhamiria nijipange Kisha niende mpaka kijijini, walau nipate kuongea nao ana kwa ana, maana dhamira yangu ilikuwa thabiti. Tofauti na wao walivyohisi, Mimi sikuwa napanga kuoa shangazi, kuna binti nilikuwa nae kwenye mahusiano ambayo kwa kiasi fulani yalikuwa serious.

Wiki moja baadae, sister angu akawa ameniita niende kumtembelea Mwanza, lakini pia aweze kuniunganisha na mchongo fulani. Nilivyoenda akafanikisha kuniunganisha na ilo deal, japo halikuwa na muda mrefu, maana nilikaa kule takriban mwezi mmoja.

Kumbe ukiachana na huo mchongo, sister alikuwa na mission nyingine. Nyumbani, wazazi walimpa jukumu la kumfahamu mwanamke wangu, Kisha awape taarifa. Sister nae alichokosea, badala walau aniulize, akawa anapitia simu yangu kimya Kimya. Simu yangu haikuwa na password, fingerprint wala patterns, so ilikuwa rahisi kuaccess information.

Katika mapenzi kuna muda wapenzi huwa wanachatig ujinga ili kusogeza siku. Sasa kuna chatting fulani nilikuwa nachat na shangazi, kiutani utani nilimwambiaga "Yani wewe ningefanikiwa kukuoa, ningekuwa na raha sana", ilikuwa ni chatting za kupoteza muda tu, ila sister akaichukulia serious. Na kwenye gallery alikuta picha zake kadhaa, akajirushia Kisha akakausha, maana hakuwa na namna ya kuniambia, kwasababu info amezipata kwa njia isiyo halali.

Siku zikaenda, na ule mchongo ukafika tamati, nikarudi Dar. Sasa kuna siku yule shangazi alitaka nimpost kwenye status, baada ya kuvutana sana, nikaona isiwe case, nikawahide watu wote muhimu, Kisha nikampost nakuweka caption ya kawaida tu. Sasa kumbe sister alikuwa ameinstall Whatsapp mbili kwenye simu yake, na Mimi sikugundua. Akaiona ile status. Nashangaa kuona amereply "Mdogo wangu ndio maana hata uleje haunenepi, mzigo wote huo kweli?"

Ikabidi nijaribu kumkataa:

Analyse: "Huyo ni Mama wa rafiki yangu"
Sister: "Kwenda huko, niliona picha zenu kwenye simu yako, nikahisi ni yaliyopita, kumbe ndiyo yaliyopo?
Analyse: "Haipo hivyo dad... "
Sister: "Huyo ndio mwanamke unataka kumpeleka nyumbani bila aibu? Hivi akili zako zipoje lakini?"

Ikabidi nikaushie msg zake, akaamua kunipigia simu, alinisema sana siku hiyo, hadi nikahisi kizungu zungu. Nikaanza kujihisi sasa hapa nilipofikia pashakuwa pabaya, wanaonizunguka wote hawana utulivu wala amani, inabidi niachane na haya mambo sasa.

Hata lile wazo la kumpeleka yule binti home, ikabidi nilisimamishe kwa muda. Maana mazingira hayakuwa supportive tena, na Kwa jinsi ninavyomjua Mshua, panaweza pakatokea ngumi nikienda, alaf sikutaka tufikie huko.

Huyu manzi, kipindi namwambia nataka nikamtambulishe nyumbani, alikuwa anasita sita, mara aseme nivute subira kidogo, muda bado. Alivyosikia nimesitisha kumpeleka nyumbani, ukawa ugomvi sasa, maana akawa ana push sana nimpeleke, hadi nikawa najiuliza, hiyo subira aliyokuwa anasema niivute, imekatika au?.

Fast forward kidogo. Niliendelea kufanya mishe zangu za kuunga unga mjini, huku nikipata nafasi, nazungusha bahasha maofisini. Pale gheto nilipokuwa nimepanga, kuna Mzee fulan smart, amechomekea muda wote, ni mtu mzima, ila hana mvi hata moja, panki lake muda mwingi limepakwa super black, nae alikuwa amepanga pale. Sema tofauti yetu, Mimi nilikuwa nimepanga chumba kimoja, yeye alichukuwa vyumba viwili na sebule, maana alikuwa na familia.

Mzee sikuwa na mazoea nae sana, hata jina lake halisi nilikuwa silifahamu, nilizoea kusikia mkewe anamuita baba fulani (jina kapuni), au vijana wengi pale mtaani walipenda kumuita Mzee Dingi (na Mimi humu nitapenda kutumia ilo ilo jina la Mzee Dingi). Huyu Mzee kwa mtazamo wa nje, alikuwa na muonekano fulani wa kimamlaka, yani ukimuona tu kwa mara ya kwanza, unahisi atakuwa mtu mzito au yupo kitengo nyeti somewhere. So, kutokana na mambo yangu kuwa magumu, nikapata wazo la kuongea nae, pengine anaweza akaniunganishia mchongo wowote hapa mjini. Siku ya siku nikamkabili, ilikuwa siku ya jumapili, maana huwa anashindaga home tu.

Nilivyomuelezea shida yangu, kabla ya yote akaniuliza kwanini nimemfata yeye?. Nikamjibu nimejaribu tu, maana siwezi jua nani anaweza nisaidia, maana mjini Sina connection ya maana. Mzee Dingi akaniuliza elimu yangu na taaluma niliyonayo. Nikajielezea vizuri pale. Tukaongea mambo mengi, mwishowe akaniambia, kesho nivae vizuri, Kisha nimpigie simu anielekeze nitakapomkuta. Tukabadilishana namba za simu, nikarudi ghetto kwangu.

Kesho yake nikajiandaa vizuri, Kisha nikampigia simu anipe direction. Akanielekeza niende mpaka city center, maeneo ya Samora, kuna bustan fulani ipo opposite na NBC, nimsubirie pale. Nikabeba copy za vyeti vyangu kwenye bahasha, nikaanza safari ya kuelekea town. Nilivyofika, nikamjulisha, akaniambia nimsubirie atakuja. Nikatulia.

Nilikaa sana pale, karibia masaa mawili, Mzee hajatokea, wala hajanicheki. Sema sifa kubwa ya jobless ni uvumilivu, nikaendelea kuvumilia. Baada ya muda, pembeni yangu alikuja akakaa jamaa, ambae alionekana kama Yuko stressed hivi. Kila muda anapiga simu, na ukimuangalia vizuri kama anataka kulia. Sasa katika kupoteza time maana nilikuwa bored, nikajikuta namuuliza kilichomsibu. Jamaa ndio kunipa story kuwa huwa anafanya biashara ya mkaa, analeta na kuuza kwa jumla, kisha anarudi mkoani. Hii ilikuwa ni trip yake ya kwanza tokea aanze biashara kwa upande wa Dar, mzigo wote umekamatwa na maliasili maana pia alikuwa amebeba vitu ambavyo hakuwa na vibali navyo, So upo kituo cha polisi. Haelewi afanye nini, na wale waliomshika, wanataka mpunga mrefu ili aachiwe. Ndani ya muda ule mfupi, alijikuta tu ananiamini, tukawa tunaongea kama watu ambao tumefahamiana kwa muda mrefu.

Binafsi sikuwa na cha kumsaidia, nikabaki nampa pole na kumtia moyo tu. Ghafla Mzee Dingi akawa amefika, nikanyanyuka kumsalimia, alafu nikawa nasubiria anioneshe direction tunayoenda, ila yeye akawa amemakinika sana na yule jamaa niliyekuwa naongea nae. Akaniuliza "Huyu mwenzako ana Nini?". Nikashangaa kwann amemuita mwenzangu, ila sikujali sana, nikampa briefly tu.

Baada ya kuisikia story ya jamaa, pale pale Mzee Dingi akasema anafahamiana na mwanasheria ambae alishamsaidiaga rafiki yake kwenye mzozo na maliasili. Akamwambia yule jamaa aongozane na sisi wakati yeye anampigia simu mwanasheria. Kilichonishangaza, wakati tunaondoka, ile simu aliyopiga, ikaita kwa Mzee mwingine ambae alikuwa eneo lile lile anakunywa kahawa, sema kakaa benchi jingine. Yule jamaa wa mkaa hakuusoma mchezo, sijui ni stress au vipi.

Mzee Dingi aliongea huku simu kaiweka loudspeaker wote watatu tunasikia, mwisho wa siku mwanasheria akasema yupo maaneo ya stesheni,kuna mgahawa anapata chai, so tumfate pale. Tukaongozana Mimi, Mzee Dingi na jamaa wa mkaa. Stesheni kuna mgahawa upo unaface stand direct, ndio tukaingia hapo. Tukamkuta huyo mwanasheria, nilivyoiangalia ile sura, ni Mzee ambae tokea nilivyofika kwenye bustan pale Samora, nilimkuta, muda wote alikuwa anasoma gazeti, story kidogo huku anakunywa kahawa. Yani kiufupi hakuwa na haraka yoyote. Ila tulivyomkuta hapo kwenye mgahawa, akatwambia tuongee tunachotaka kuongea, hana zaidi ya dakika 15, anawahi mahakamani.

Kuna kengele Fulani ikalia kichwani mwangu. Zilipigwa sound za kutosha pale, sound nyingi sana. Mpaka ikafikia hatua, yule jamaa wa mkaa akahitajika kutoa laki 5 ili issue yake iwe solved siku ile ile. Jamaa wa mkaa akawa anajaribu kubargain yule mwanasheria feki akanyanyua briefcase yake akatishia kuondoka, Mzee Dingi akawahi kumtuliza kuwa amsaidie jamaa issue yake, jamaa nae kwa kuhofia kupoteza mtu wa kumsaidia, akakubali kutoa hiyo 500k. Pale pale akili ikaniambia, kuna mtu anatapeliwa muda sio mrefu.

Kati ya wote pale, yule jamaa wa mkaa, alionekana kuniamini Mimi kuliko wengine. Hata ile 500k waliyokubaliana atoe, akanitupia Mimi jicho fulani kama vile kuomba ushauri au kuuliza atoe au asitoe?. Kwa mazingira yalivyokuwa, nikajikuta nampa ishara atoe hela, asiwe na wasi wasi, ila nafsi ilikuwa inanisuta sana.

Wote wanne, tukatoka nje ya ule mgahawa, tukapanda gari ya yule mwanasheria, mpaka ATM, jamaa wa mkaa akatoa hela. Kisha tukarudi mpaka karibu na jengo la mamlaka ya bandari, kufika pale, yule mwanasheria na jamaa wa mkaa wakashuka na kuingia ndani, Nia ni kwenda kuandikishiana hela walizipeana, then ndio waende polisi. Baada ya dakika kama 15, yule mwanasheria akarudi peke yake, akazama kwenye gari haraka, Mzee Dingi akang'oa.

Akili yangu ikawa wazi, kuwa Mzee Dingi ni tapeli tu, yeye na mwenzie. Ikabidi nivunje ukimya ndani ya gari, kwamba kilichafanyika haikuwa haki. Hakuna aliyenijibu, Mzee Dingi akapaki gari kituo cha mnazi mmoja pale, then Mzee Dingi akawa ananiambia "Bahasha wanazunguka nazo vijana wanaotafuta kazi, wewe umeshapata kazi tayari, tafuta briefcase au begi la kubeba mkononi, kesho usije tena kazini na hiyo Bahasha". Nikamwangalia yule Mzee, hana hata chembe ya huruma au kujutia. Yule mwanasheria feki, akaniuliza "Kwani bwana mdogo unachotaka hasa ni nini?". Nikamjibu " Tumrudishie jamaa hela zake". Mzee Dingi akadakia "Sikia apostle, Ungetaka kumsaidia, ungemsaidia kipindi tupo pale mgahawani, acha kutia huruma wakati hela unaitaka"

Nikajikuta hasira zinazidi, hasa alivyoniita apostle, maana ilikuwa ni kama kebehi fulani hivi. Yule mwanasheria feki kwenye ile 500k, yeye akachukua 200k, Mzee Dingi akapewa 200k, alafu akachukua 100k na kunikabidhi Mimi,kisha akanipa na namba ya simu kwenye kikaratasi. Akaniambia "Hiyo ndio namba ya yule jamaa, hiyo 100k ndio mgao wako, mtafute umrudishie walau nusu hasara"

Nikabaki nimetoa macho tu.....

Endelea hapa Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu. Mpaka siku niliyokutana na yule Mzee
 
Back
Top Bottom