Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

7th Portion:

... Mzee Dingi akaniambia "Hela ikishafika mkononi mwako, alaf ukairudisha ilipotoka, utasumbuka sana kupata hela tena. Hela hairudishwi apostle"

Ilo jina apostle lilishaanza kunikera. Japo wanasema jina ukilikataa ndio linakua, ila sikuwa na namna, nikajikuta namjibu kwa hasira "Yule anafamilia inamtegemea, sio haki kumdhurumu, alafu na ilo jina la apostle sitaki kulisikia tena, umesikia we Mzee?". Mzee Dingi akabaki ameniangalia tu, alaf nae akawaka "Sikia apostle, nani ambae hana familia hapa?, Mimi mwenyewe napambania familia yangu vile vile". Akaendelea "Nyumbani hawajali hela naipataje, wao wanachohitaji ni matunzo, hata kama siipati kwa njia halali, ila nyumbani ikifika, inatatua shida zao, na wananishukuru kama Baba"

Nikamkatisha "Utajisikiaje unampa mkeo hela kwa ajili ya ada ya watoto, alaf anatokea mtu anamtapeli?". Wote wawili wakacheka, alaf Mzee Dingi akaniambia "Hiyo ndio itakuwa tiketi ya kurudi kwao, maana siwezi kuwa na mke mwenye tamaa. Huwezi kutapeliwa kama huna tamaa". Nikataka kuongea kitu, yule mwanasheria feki akaingilia "Apostle, kama unamuonea huruma, kamrudishie walau hiyo laki, haya shuka kwenye gari". Sikutaka kuendelea kuongea nao, nikashuka.

Nilivyoshuka kwenye ile gari yao, wao wakaondoka bila kuniambia wanaelekea wapi. Ila Mimi niliendelea kubakia eneo lile lile, nikiwa natafakari nini cha kufanya. Yule jamaa wa mkaa nilikuwa namuonea huruma, ila hapo hapo upande wangu nilikuwa nimefulia sana, kiasi kwamba nafsi ikawa inagoma kurudisha ile hela, jobless upate laki alafu urudishe? Labda Ulaya. Lakini upande mwingine nikajifikiria, endapo nitamrudishia ile laki, basi hapo nitakuwa nimejiingiza matatizoni. Potelea pote, nikaamua kurudi zangu gheto.

Ila nikawa nimepitisha uhamuzi wa kuwapotezea kina Mzee Dingi, maana kampani yao niliiona ni kama ticket ya jela.

Kesho yake mida saa sita, Mzee Dingi akanipigia simu, sikupokea, akapiga tena, sikupokea. Akaamua kutuma msg "Apostle, njoo mtaa wa Msimbazi na Lindi, kuna Kijiwe wanauza kahawa, fanya haraka". Nikaisoma, alaf nikaipotezea, nae akakausha. Ilivyofika wik end, siku ya jumapili, akaniita tuongee. Ila hakutaka tuongelee pale nyumbani, tukaenda kwenye kipub fulani hivi.

Kufika pale, ndio akaanza kuniambia "Sikiliza mdogo wangu, haya maisha yanahitaji kupambana, najua umesoma na unaelimu nzuri, lakini hiyo sio njia pekee ya ww kuingiza hela. Kama kuna kitu hujui ni kwamba, unakismart cha kuaminiwa, nyota yako inang'aa Apostle. Ni rahisi sana mtu kukuamini wewe, alaf na ulivyo muongeaji, na unavyojua kupangilia maneno, wewe ni mtu sahihi kabisa ambaye ofisi yetu ilikuwa inamkosa"

Nikamwangalia yule Mzee wee, sikusema chochote. Mzee aliongea vyote anavyojua ila kwa upande wangu nilishadhamiria siingii kwenye kazi zao. Nikaamua kuondoka eneo lile. Wakati naondoka, akawa ananisindikiza na maneno, "Ulivyokuja kuniomba nikuunganishie michongo, ulitegemea ufanye kazi ikulu? Au ulitaka ofisi yenye A.C? Mshamba sana we mtoto"

Sikumjibu kitu, nikamuacha kwenye ile pub, nikaelekea zangu betting center kupoteza muda.

Siku zilisogea, niliendelea na harakati zangu za kuunga unga kama kawaida, ila Mzee Dingi aliendelea kunishawishi nijiunge na timu yao. Ilifikia hatua ikawa kero sasa, hadi nikaanza kujutia kwanini nilimfataga kumwambia aniunganishie mchongo.

Nilivyoona usumbufu umezidi, nikaamua kuhama eneo lile. Nikahamia sehemu moja Tabata chang'ombe, karibia na hospital ya Kundy. Mimi na yeye tukawa tunaonana mara chache chache sana, hasa kwenye vituo vya dalala au njiani.

Kiuhalisia, baada ya kuhama, hata yeye akaamua kunipotezea kabisa. Ila miezi kama minne tokea nihame pale nilipokuwa nakaa mwanzo, Mzee Dingi akanipigia simu, mpaka kufikia pale, niliamini alishakubaliana na msimamo wangu, so sikuona tabu kupokea simu yake.

Nilivyoipokea, after salamu akaniambia "Apostle, fanya mpango tuonane wik end hii, kuna kitu nataka tujadiliane". Nikamuuliza "Kitu gani?". Akajibu "Usiwe na wasi, sio zile dili za kipindi kile, hii ni issue nyingine, wik end fanya unitafute". Nikamwambia fresh.

Ilivyofika jumapili tukakutana bar. Story mbili tatu, ndio akaniambia alichoniitia. "Sikia apostle, kuna kiasi fulani cha hela ninacho, nataka nianze kufanya biashara halali, sitaki tena dhuluma". Nikamjibu "Ni jambo zuri, ila sijaelewa Mimi nahusika vipi hapa?". Akasema " Sikia apostle, nahitaji mawazo ya biashara na mtu ambae naweza kufanya nae. Nahitaji tushirikiane"

Baada ya blah blah hapa na pale, kuna wazo nikalitoa, ambalo nililifikiriaga muda mrefu, ila mtaji ikawa ndio shida

Na ilo wazo lilikuwa kutoa mkaa vijijini, kisha unakuja kusambaza mjini, kama jinsi alivyokuwa anafanya yule jamaa aliyetapeliwa na kina Mzee Dingi. Nilipomuelezea, akafikiria kwa muda kidogo, Kisha akaniuliza vitu kadhaa kuona uelewa wangu kwenye hiyo biashara. Alivyoona maelezo yangu yapo clear, akasema ngoja atafakari zaidi, huku akiwa anaangalia uwezekano wa kupata madalali hapa mjini, ili mzigo ukifika, tusisumbuke kupata soko.

Tukaagana, nikaondoka eneo lile.

Baada ya kama siku tatu, akanipigia tena. Akaomba tuonane, ila safari hii akaja mpaka nilipohamia. Baada ya maongezi ya hapa na pale, tukawa tumekubaliana kufanya biashara. Kwavile sikuwa na mishe ya kueleweka, hii niliichukulia kama nafasi pekee ya kunitoa kwenye ukata. Nikadhamiria kuifanya kwa moyo na uaminifu, ili kujitengenezea kipato, lakini pia kumuonesha Mzee Dingi kuwa inawezekana kuingiza hela kwa njia halali.

Nilijidanganya. Nilichokuwa nawaza Mimi, sicho alichokuwa akiwaza Mzee Dingi.....


Endelea hapa Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, Mpaka siku niliyokutana na yule Mzee
 
Back
Top Bottom