Domhome
JF-Expert Member
- Jun 28, 2010
- 3,198
- 3,950
Tanga raha Sana..Kijana wa Tech, Tanga raha [emoji28][emoji28]
Tanga Tech, Makorola hadi Kwanjeka !
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tanga raha Sana..Kijana wa Tech, Tanga raha [emoji28][emoji28]
uliingia mtegoni kijinga sana chief[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], tapeli huwa haachi utapeli.......7th Portion:
... Mzee Dingi akaniambia "Hela ikishafika mkononi mwako, alaf ukairudisha ilipotoka, utasumbuka sana kupata hela tena. Hela hairudishwi apostle"
Ilo jina apostle lilishaanza kunikera. Japo wanasema jina ukilikataa ndio linakua, ila sikuwa na namna, nikajikuta namjibu kwa hasira "Yule anafamilia inamtegemea, sio haki kumdhurumu, alafu na ilo jina la apostle sitaki kulisikia tena, umesikia we Mzee?". Mzee Dingi akabaki ameniangalia tu, alaf nae akawaka "Sikia apostle, nani ambae hana familia hapa?, Mimi mwenyewe napambania familia yangu vile vile". Akaendelea "Nyumbani hawajali hela naipataje, wao wanachohitaji ni matunzo, hata kama siipati kwa njia halali, ila nyumbani ikifika, inatatua shida zao, na wananishukuru kama Baba"
Nikamkatisha "Utajisikiaje unampa mkeo hela kwa ajili ya ada ya watoto, alaf anatokea mtu anamtapeli?". Wote wawili wakacheka, alaf Mzee Dingi akaniambia "Hiyo ndio itakuwa tiketi ya kurudi kwao, maana siwezi kuwa na mke mwenye tamaa. Huwezi kutapeliwa kama huna tamaa". Nikataka kuongea kitu, yule mwanasheria feki akaingilia "Apostle, kama unamuonea huruma, kamrudishie walau hiyo laki, haya shuka kwenye gari". Sikutaka kuendelea kuongea nao, nikashuka.
Nilivyoshuka kwenye ile gari yao, wao wakaondoka bila kuniambia wanaelekea wapi. Ila Mimi niliendelea kubakia eneo lile lile, nikiwa natafakari nini cha kufanya. Yule jamaa wa mkaa nilikuwa namuonea huruma, ila hapo hapo upande wangu nilikuwa nimefulia sana, kiasi kwamba nafsi ikawa inagoma kurudisha ile hela, jobless upate laki alafu urudishe? Labda Ulaya. Lakini upande mwingine nikajifikiria, endapo nitamrudishia ile laki, basi hapo nitakuwa nimejiingiza matatizoni. Potelea pote, nikaamua kurudi zangu gheto.
Ila nikawa nimepitisha uhamuzi wa kuwapotezea kina Mzee Dingi, maana kampani yao niliiona ni kama ticket ya jela.
Kesho yake mida saa sita, Mzee Dingi akanipigia simu, sikupokea, akapiga tena, sikupokea. Akaamua kutuma msg "Apostle, njoo mtaa wa Msimbazi na Lindi, kuna Kijiwe wanauza kahawa, fanya haraka". Nikaisoma, alaf nikaipotezea, nae akakausha. Ilivyofika wik end, siku ya jumapili, akaniita tuongee. Ila hakutaka tuongelee pale nyumbani, tukaenda kwenye kipub fulani hivi.
Kufika pale, ndio akaanza kuniambia "Sikiliza mdogo wangu, haya maisha yanahitaji kupambana, najua umesoma na unaelimu nzuri, lakini hiyo sio njia pekee ya ww kuingiza hela. Kama kuna kitu hujui ni kwamba, unakismart cha kuaminiwa, nyota yako inang'aa Apostle. Ni rahisi sana mtu kukuamini wewe, alaf na ulivyo muongeaji, na unavyojua kupangilia maneno, wewe ni mtu sahihi kabisa ambaye ofisi yetu ilikuwa inamkosa"
Nikamwangalia yule Mzee wee, sikusema chochote. Mzee aliongea vyote anavyojua ila kwa upande wangu nilishadhamiria siingii kwenye kazi zao. Nikaamua kuondoka eneo lile. Wakati naondoka, akawa ananisindikiza na maneno, "Ulivyokuja kuniomba nikuunganishie michongo, ulitegemea ufanye kazi ikulu? Au ulitaka ofisi yenye A.C? Mshamba sana we mtoto"
Sikumjibu kitu, nikamuacha kwenye ile pub, nikaelekea zangu betting center kupoteza muda.
Siku zilisogea, niliendelea na harakati zangu za kuunga unga kama kawaida, ila Mzee Dingi aliendelea kunishawishi nijiunge na timu yao. Ilifikia hatua ikawa kero sasa, hadi nikaanza kujutia kwanini nilimfataga kumwambia aniunganishie mchongo.
Nilivyoona usumbufu umezidi, nikaamua kuhama eneo lile. Nikahamia sehemu moja Tabata chang'ombe, karibia na hospital ya Kundy. Mimi na yeye tukawa tunaonana mara chache chache sana, hasa kwenye vituo vya dalala au njiani.
Kiuhalisia, baada ya kuhama, hata yeye akaamua kunipotezea kabisa. Ila miezi kama minne tokea nihame pale nilipokuwa nakaa mwanzo, Mzee Dingi akanipigia simu, mpaka kufikia pale, niliamini alishakubaliana na msimamo wangu, so sikuona tabu kupokea simu yake.
Nilivyoipokea, after salamu akaniambia "Apostle, fanya mpango tuonane wik end hii, kuna kitu nataka tujadiliane". Nikamuuliza "Kitu gani?". Akajibu "Usiwe na wasi, sio zile dili za kipindi kile, hii ni issue nyingine, wik end fanya unitafute". Nikamwambia fresh.
Ilivyofika jumapili tukakutana bar. Story mbili tatu, ndio akaniambia alichoniitia. "Sikia apostle, kuna kiasi fulani cha hela ninacho, nataka nianze kufanya biashara halali, sitaki tena dhuluma". Nikamjibu "Ni jambo zuri, ila sijaelewa Mimi nahusika vipi hapa?". Akasema " Sikia apostle, nahitaji mawazo ya biashara na mtu ambae naweza kufanya nae. Nahitaji tushirikiane"
Baada ya blah blah hapa na pale, kuna wazo nikalitoa, ambalo nililifikiriaga muda mrefu, ila mtaji ikawa ndio shida
Na ilo wazo lilikuwa kutoa mkaa vijijini, kisha unakuja kusambaza mjini, kama jinsi alivyokuwa anafanya yule jamaa aliyetapeliwa na kina Mzee Dingi. Nilipomuelezea, akafikiria kwa muda kidogo, Kisha akaniuliza vitu kadhaa kuona uelewa wangu kwenye hiyo biashara. Alivyoona maelezo yangu yapo clear, akasema ngoja atafakari zaidi, huku akiwa anaangalia uwezekano wa kupata madalali hapa mjini, ili mzigo ukifika, tusisumbuke kupata soko.
Tukaagana, nikaondoka eneo lile.
Baada ya kama siku tatu, akanipigia tena. Akaomba tuonane, ila safari hii akaja mpaka nilipohamia. Baada ya maongezi ya hapa na pale, tukawa tumekubaliana kufanya biashara. Kwavile sikuwa na mishe ya kueleweka, hii niliichukulia kama nafasi pekee ya kunitoa kwenye ukata. Nikadhamiria kuifanya kwa moyo na uaminifu, ili kujitengenezea kipato, lakini pia kumuonesha Mzee Dingi kuwa inawezekana kuingiza hela kwa njia halali.
Nilijidanganya. Nilichokuwa nawaza Mimi, sicho alichokuwa akiwaza Mzee Dingi.....
Nilikuwa nahitaji kufanya biz ili niingize hela. So ilikuwa rahisi kunichota, maana plan ilikuwa genuineuliingia mtegoni kijinga sana chief[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], tapeli huwa haachi utapeli.......
tapeli na biashara halali wapi na wapi?
raia za hivyo huwa wahuni sana, ukikataa kujiunga nae basi anakufanyia ushetani (kwa kumtumia third party) ili na wewe ugeuke shetani, at the end anakua kafanikiwa lengo lake,Nilikuwa nahitaji kufanya biz ili niingize hela. So ilikuwa rahisi kunichota, maana plan ilikuwa genuine
Halafu Hostel za Advance Usagara sec zipo katikati ya Jiji la Tanga....jirani kabisa na stesheni...Mikanjuni, Raskazone, Chichi, Sahare, barabara ya 14 ndio ilikuwa mitaa yangu
hivi pale chichi madada poa bado wapo?Mikanjuni, Raskazone, Chichi, Sahare, barabara ya 14 ndio ilikuwa mitaa yangu
Sasa hivi ndio wamezidi kuwa wajanja. Chichi na La Casa, vile viwanja haviwezi kufa. Nilikuwa naendaga maeneo hayo kuangalia mechi za UEFA, ila muda wote macho yanashangaa totoz tu 😅😅😅hivi pale chichi madada poa bado wapo?
long time sijaenda tanga......
ila ule mji ni balaa, alafu wenyeji wanasema eti miaka hii (2000-to date) mahaba hamna kabisa[emoji849][emoji849][emoji849]....... najaribu kuwaza ilikuaje zamani
Kwani na yeye alivokufanyia mwanzo ilikuwaje!!!! Vizuri nayeye kapata portion yakeMchaga aliingia 18 za Mshua [emoji28][emoji28]
Nipo nipo mkuuu. Ndio nimeingia hivi baada ya kumalizana na story ya Goba.
Nakutag sana nikajua funga ipite kwanz
Ila kama ni wewe una vituko 😂😂😂Naishusha muda Sio mrefu mkuu
Swaumu Kal najua 😀😃😄Halaf nimeona lakin sijapata notification 🫣🫣
Samahan
Si umeona hapo nimekulaumu kuwa hujanitag wakati jina lipo hapo ila sijaona nyieeSwaumu Kal najua 😀😃😄