Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

17th Portion:

.... Mzee Dingi alimtumia msg Mzee KY kumtaarifu kuwa ndio wanakaribia, so tujiandae.

Plan ilivyokuwa ni kwamba, wakishafika pale center, Mzee Dingi alitakiwa kumpigia simu Mzee KY ili aje awapeleke kwenye eneo lake analouza. Wakishafika kwenye hiyo eneo, Mzee KY anatakiwa kuwaita majirani zake aliopakana nao kwenye ilo eneo analouza, ili waje kutambua na kuthibitisha mipaka.

Wakishaoneshana mipaka, na kuelewana katika kila kitu, hapo ndio wanatakiwa kuniita mwenyekiti, niende mpaka pale site, ili kuona eneo linalouzwa na mipaka yake. Nikishajiridhisha kuwa kila kitu kipo sawa, hapo wote kwa pamoja tunatakiwa kwenda ofisini ili kuandikishiana na kukabidhiana hela.

Kuhusu ofisi, Mzee KY angeshauri twende tukaandikishiane nyumbani kwake. Nyumba hii ambayo tulikuwa tumefikia, na ilikuwa na muonekano kuwa inakaliwa na familia so ni rahisi kuaminika. Pia mihuri yote muhimu nilikuwa nimeshapewa, hadi nyalaka za mauziano zilizoandaliwa na Mzee KY nilikuwa nimekabidhiwa. Kiufupi, nyalaka zote sahihi zilikuwepo na baada ya mauziano, yule mstaafu angepewa. Kasoro pekee iliyokuwepo, ni kwamba eneo linalouzwa sio letu.

Takribani nusu saa tokea atume ile msg, Mzee Dingi akapiga simu. Baada ya salamu na maongezi kidogo, Mzee KY akaenda kuwapokea. Kisha akaenda nao hadi eneo linalotakiwa kuuzwa.

Wakiwa pale, majirani wakapigiwa simu. Akaanza kwenda yule mwanasheria feki, robo saa mbele, huyu Mzee Kidevu nae akaenda. Nikabaki mwenyewe, mwenyekiti ndani ya ile nyumba.

Baada ya kama dakika 45 tokea yule Mzee Kidevu aniache kwenye ile nyumba, Mzee KY akanipigia simu niende. Moyo ulikuwa unadunda kuliko kawaida, ila kila nikifikiria mgao wangu nitakaopata, nikajipa moyo. Nikawafata walipo.

Wale wengine wote, hakuna aliyekuwa kabeba begi lake pale site, ni Mimi peke yangu ndio nilienda na kibriefcase changu pale site. Nilivyofika tu site, nikapatwa na mshangao baada ya kumuona mtu tunayetakiwa kumliza.

Unajua katika maisha, coincidences zipo, lakini kuna baadhi ya coincidences hata ujielezee vipi, ni ngumu watu wengine kukuamini.

Alivyogeuka yule mama tunayetaka kumuuzia eneo, nikajikuta nipo uso kwa uso na Mama mwenye nyumba niliyohama siku iliyopita. Binafsi kutokea moyoni, sikuwa nafahamu kama mlengwa ni yeye. Na hata sababu iliyonifanya nihame pale kwake, wala haikuhusiana na yeye kuwa target yetu.

Ila unadhani ni nani angeweza kuamini maelezo yangu?. Yani leo nimehama, then kesho tunaenda kumpiga tukio, alaf niseme nilikuwa sijui kitu? Mtu yeyote mwenye akili timamu na reasoning capacity ya kawaida tu, asingekubali.

Yule mama alivyoniona kwa mbali, akanitambua. Nikawasogelea mpaka pale. Akanipokea kwa bashasha sana.

"Mwanangu ni wewe? Siamini macho yangu, kumbe ndio umepata kazi huku?". Nikamjibu ndio. Akanichangamkia sana, "Mungu mkubwa, na wakati wa Mungu ndio wakati sahihi, angalia ulivyoinuliwa mwanangu". Muda huo anaongea yote, wale washirika wangu wote wapo kimya, kila mmoja kapigwa butwaa kivyake, kasoro Mzee KY, yeye alikuwa neutral.

Yule mama akaendelea, "Unaona mwanangu kuishi na watu vizuri ilivyo ni jambo jema? Mfano ungeondoka kwa ugomvi, leo hii tungetizamana usoni? Nadhan hata jambo langu leo lingekuwa gumu". Mzee Dingi ikabidi aingilie yale maongezi yetu, "Kwani nyie mnafahamiana?". Mstaafu akamjibu, "Ndio, huyu ni kijana wangu kabisa, nimefahamiana nae miaka mingi, na leo ona Mungu amenikutanisha nae tena, ili aweze kuwa msaada wangu kwenye huu ununuzi"

Mzee Dingi: "Ni jambo jema, basi hapa shughuli yetu itaenda kwa urahisi sana"

Mstaafu: "Yani hapa Sina mashaka kabisa, nipo kwenye mikono salama ya kijana wangu"

Yule mstaafu akanigeukia Mimi na kuniambia "Tena tukitoka hapa unikumbushe nikurudishie Kodi yako iliyokuwa imebaki, maana ulivyotoka tu, dalali akaleta mtu mwingine atakayeingia leo. Ilikuwa halali yako kuhama pale. Huku ni mbali mwanangu."

Akili ikaanza kunizunguka kuliko kawaida, hapa nisimame upande wa nani?, wa huyu mama, au wa ile timu?. Upande wowote ambao ningechagua lazima kuna consequences ningekutana nazo. Nikisema nisimame na kina Mzee Dingi, basi uhaminifu kwa huyu mama ningekuwa nimeuvunja. Nikisema nisimame na huyu mama, basi nijiandae kuingia kwenye vita na kina Mzee Dingi, maana nitakuwa nimewaingiza kwenye hasara kubwa sana. Dili za hela ndefu kama hizi, huwa zinamaandalizi mengi, na gharama kubwa inatumika, mfano ile nyumba ambayo tungeenda kuandikishiana, ilikuwa imekodiwa, na iliwekwa vitu vyote vya ndani ili ionekane kama ni makazi halisi.

Kufanikiwa Kwa Ili dili, ndio hela ya kucover hizi gharama zote ingepatikana. Kufeli Kwa Ili dili ni hasara, hasara ambayo hakuna aliyekuwa anataka itokee, na ndio maana maandalizi yake yalikuwa deep. Mpaka kufikia muda ule, hatma ya kufanikiwa au kufeli Kwa lile dili zilikuwa mikononi mwangu. Nikawa najiuliza, hawa watu watanielewa kweli??. Wote nikiwaangalia, they mean business, hakuna aliyekuwa na mzaha. Katika ile timu yote, nilikuwa namuhofia sana yule Mzee KY, ukiachana na yeye kuwa kiongozi, ila pia ni mtu fulani aliye serious sana muda wote. Macho yake yameingia kwa ndani, alafu makali sana. Akikuangalia sana unaweza hisi anachuki na wewe.

Wakati naendelea kuwaza hayo. Mzee KY akaamua kuchukua nafasi yake kama muuzaji wa ile ardhi, akamgeukia Mzee Dingi na kumwambia:

"Hebu tumalize ili swala, kuna sehemu natakiwa kuwahi"

Mzee Dingi
: "Haya mama, twende mkaandikishiane, ila tufunge ili swala"

Mstaafu: "Sawa hakuna shida"

Mwanasheria feki na yule Mzee Kidevu kama wanaweza kuondoka, maana kazi yao ya kutambua mipaka wameshaifanya. Mzee KY akawazuia kuondoka, kwamba wao kama majirani na mashahidi, watatakiwa kuweka Saini zao kwenye zile nyalaka za mauziano.

Baada ya kuwaambia hivyo, akashauri twende nyumbani kwake tukasainishane. Nikamkatisha, kwamba kuna shida kidogo imejitokeza.

Wote wanne kasoro yule mama mstaafu, walinigeukia kwa mshangao, maana nilienda nje ya script. Yule Mzee KY alinikata jicho, ambalo lilinipa tafsiri kwamba nikizingua nimekufa.

Akili ikaanza kunizunguka kwa haraka, maana nilitakiwa kufanya maamuzi ndani ya muda mfupi, uhamuzi ambao ungeweza kuwa na impact kwangu, kwa muda mrefu ujao...

Baada ya kufikiria kwa haraka, kuna wazo likanijia kichwani. Wazo ambalo niliona lingesaidia kudelay ile process kwa siku chache. Nikawashirikisha nilichokuwa nawaza

Analyse: "Wazo la kwenda kuandikishiana kwako muuzaji, ni zuri, ila sio sahihi. Kiofisi zaidi, inatakiwa kila kitu kikafanyikie ofisini, ili baada ya hapo niweze kuacha nakala za haya mauziano pale, sitakiwi kuzunguka nazo"

Aisee wale jamaa walinikata macho ya chuki, hadi nikaingia ubaridi. Unajua nature ya hii kazi, maandalizi yake hayakutakiwa kuhusisha ofisi. Ndio maana hata ofisi feki haikuwa imeandaliwa. Kitendo cha kusema tuandikishiane ofisini, maana yake hizo ni gharama zingine za haraka ambazo tutaziingia.

Ajabu ni kwamba, Mimi wakati najaribu kitengua lile zoezi lisifanyike siku ile, yule Maza ambaye tunataka tumpige hela akaanza kunibembeleza nifanikishe mauziano siku ile ile.

Mstaafu: "Mwanangu hebu nisaidie Mama ako, nipate ili eneo siku ya leo, nimelisumbukia sana"
Analyse: "Naelewa mama, lakini haya ni maswala ya kiofisi, leo mkiuziana alaf nikapoteza nyalaka. Inaweza kuniweka hatiani huko mbeleni"
Kesho Yetu: " Kwanini upoteze nyalaka, serikali imekuamini kukupa hiyo nafasi, mbona unashindwa kujiamini?"
Mstaafu: "Wewe mbona ni kijana smart sana, acha kuniangusha bhana"
Mzee Dingi: "Kama wasiwasi ni huo, basi tukishaandikishiana, tutaenda kuzipitisha chini ya mlango wa ofisi. Jumatatu utawahi mapema ili uziweke kwenye mafaili"
Mstaafu: "Hela ya soda ipo kijana wangu, naomba sana unisaidie"

Huyu mama ndio alikuwa anazidi kunipa ugumu. Najaribu kutaka kumsaidia. Lakini yeye anazidi kuniwekea ugumu. Baada ya majadiliano ya dakika kadhaa, Mzee KY ikabidi aingilie kati;

Mzee KY: "Nakubaliana na mwenyekiti, yupo sahihi kwa anachokisema. Ili ni jambo nyeti sana, halitakiwi kupelekwa kiholela."

Wote tukabaki tunamwangalia kwa mshangao, sikutarajia kama angeniunga mkono. Inamaana huruma imemuingia au kuna kitu kingine anafikiria?

Akaendelea:

Mzee KY: "Nashauri tufanye mambo kiofisi zaidi, Jumatatu mpaka Jumatano sitokuwa na nafasi, ila naomba wote kwa pamoja tukutane ofisini siku ya Alhamisi ili tumalize ili swala. Na kuhusu gharama zenu za usumbufu nitazirudisha, wala msiwe na hofu"

Tukawa tumekubaliana hivyo, lakini sisi wengine wote tulibaki na maswali kichwani, Mzee KY anawaza nini?. Mbona tumeenda nje ya plan lakini hajapanick?

Kiukweli nilishindwa kabisa kumuelewa. Ikabidi nimwambie yule mstaafu anipe lift mpaka Dar, maana kuna mambo yangu nilitakiwa kuyaweka sawa kule. Mzee KY akaniangalia jicho lenye kuuliza "Huondoki na sisi?". Nikampotezea.

Kwenye gari ya yule mstaafu, nikapanda na Mzee Dingi. Wale wengine wakarudi kivyao. Tukiwa njiani yule mstaafu alinibembeleza sana nisimamie swala lake lifanikiwe ile. Nikamwambia asijali. Mzee Dingi akawa anachombeza hapa na pale, lakini tukikutanisha macho yake yananiambia "ntakuua apostle". Pamoja na jicho la chuki alilokuwa ananiangalia nalo, lakini alikuwa haruhusu nimguse hata kidogo. Kiufupi alikuwa ananitisha, lakini at the same time ananiogopa.

Baada ya kufika mjini, kila mmoja alienda na njia yake. Yule mama mstaafu alitaka kunipa lift ila nikahofia Mzee Dingi anaweza kutufatilia nyuma nyuma alafu apajue ninapoishi, so nikakataa. Wote akatushushia sehemu moja. Kabla hatujaachana Mzee Dingi akaanza kunipa makavu;

Mzee Dingi: "Apostle Unazingua sana ujue? Dili ilikuwa imeshaisha hii"
Analyse: "Ila kumbuka huyu mama Mimi ananifahamu vizuri tu, dili likiisha msala unabaki kwangu"
Mzee Dingi: "Msala ubaki kwako, kwani bado unaishi kwake? Tanzania mapori mengi sana, nenda hata Mtwara huko, sio lazima wote tuendelee kuishi mjini".
Analyse: "Nirahisi kwa wewe kusema hivyo, lakini pia tambua yule mama.....". Kabla sijamalizia kauli yangu, akanikatisha.

"Acha useng* apostle, kwani Mama ako yule?". Aliongea kwa nguvu na jazba kiasi kwamba watu waliokuwa karibu wote wakatugeuzia sisi macho. Ukimuona Mzee Dingi alivyokuwa kavaa na yale maneno aliyoongea, ilikuwa halali wapita njia kutushangaa.

Nikaamua kuondoka, nikachukua uelekeo wangu, Mzee Dingi nae akaeleka upande wake.

**************

Kuna jambo moja ngoja niliongelee japo wakati naanza kusimulia, sikuplan kabisa kuweka details zake.

Nilivyokuja kuzinguana na kina Mzee Dingi hadi ikafikia kuachana nao (nitasimulia mbeleni) niliendelea kuwa na mawasiliano na Mzee KY kwa muda kidogo. Katika huo muda, ndio alikuja kuniambia vitu ambavyo hata kwangu havikuwa clear. Tokea mwanzo nimekuwa nikisema tu, tukapiga dili ili au lile, lakini sikuwahi kusema how. Ngoja walau nielezee dili la huyu mstaafu ilikuwaje mpaka ikafikia hatua ya kwenda kuuziana ardhi kule vigwaza.

Mzee KY anawatu anaofahamiana nao sehemu kadhaa, kuna mtu alimpa tip kuhusu huyu mama mstaafu na mafao yake. Yeye siku zote huwa anahitaji info hiyo tu, kwamba pale kuna hela kiasi kadhaa inaweza kupatikana, then mengine yote anafanya mwenyewe.

Alivyopewa hiyo info, akaja kuoneshwa muhusika mwenyewe alivyo. Baada ya hapo akaandaliwa mtu wa kumfatilia na kukusanya taarifa zake za kutosha. Zikishapatika, analetwa mtu wa kuja kukuvuta kwenye himaya yao. Kama unayetaka kutapeliwa ni mtu mzima sana, basi katatumwa katoto, kama wewe ni kijana, atatumwa mtu mzima au mzee nk. Kwa huyu mstaafu, kalitumwa katoto kakiwa na sare za shule ya msingi. Mtoto alipewa namba ya simu imeandikwa kwenye kikaratasi, akaambiwa amfate yule mama mstaafu kisha amuombe simu ili ampigie mama yake, maana amechanganya magari (just imagine unakutana na mtoto wa primary maeneo ya kkoo, alafu anakuomba umpigie mama yake, huwezi chomoa. In reality hako katoto kanakuwa sio mwanafunzi, au hata kama ni mwanafunzi basi anakuwa planned).

Sasa ile namba ukiipiga, haitokaa ipokelewe. Itaita sana mpaka ukate tamaa wewe. Kinachofatia, utamsaidia yule mtoto kupanda gari za kumfikisha kwao. Itakapofika mida ya usiku, mwenye ile namba itakupigia na kusema amekuta missed call yako. Ukikumbuka tukio na kumuelezea, atakushukuru, Kisha atakwambia nilikuwa sehemu fulani ndio maana sikuweza kupokea. Hii sehemu fulani atakayoitaja, lazima iwe inaendana na wewe maana taarifa zako za kutosha zinakuwepo. Anaweza kusema nilikuwa kwenye ibada kwa Mwakasege, Kakobe au Mwamposa, or chochote ambacho ukikisikia kitaendana na wewe. Hapo ndio utamwambia "Ooh kumbe na wewe unapata huduma kwa huyo mtumishi?".

So kutokea hapo, hamtojadili habari za mtoto tena. Next mtajikuta mnaanza kukutana physically huko kwenye huduma za kiroho. Atazidi kuwa karibu na kujenga uhaminifu, mpaka kuna siku utaongea kitu kitakacho kuja kukuliza. Haya yote yanachukua muda mrefu sana, na ndio maana Mzee KY kwa mwaka alikuwa hafanyagi dili nyingi.

Sasa kwa huyu mstaafu ilikuwa kama hivi. Alikuja akaongea habari zake za kuhitaji kufanya mradi wa greenhouse na kilimo cha umwagiliaji katika mtindo wa kisasa. Hii ndio taarifa aliyokuwa anaisubiria Mzee KY. Alivyoipata, ndio akaanza kuweka plan ni kwa namna gani akamilishe plan. Wakati anaendelea na kuweka mipango yake sawa, ndio kuna siku aliniona na yule mama mstaafu kabla sijahama kwenye nyumba yake. Na kwavile alishawahi kuniona na kina Mzee Dingi, basi akapendekeza Mimi niwe included ili ku-smoothen the process.

So, kwenye lile dili sikujumuishwa kwavile waliniona smart na mchangamfu, bali ukaribu wangu na yule mama. It was not a coincidence, everything was planned. Na Mzee KY alikuwa ahead of time.

Pamoja na hayo yote, Kunishirikisha Mimi ilikuwa ni plan A, lakini haikuwa plan pekee. Na kitendo cha Mimi kuonekana na yule mstaafu pale site, dili lilikuwa tayari limeshafanikiwa kwa 80%, either niendelee nao au nikatae.

So muda ule nilipoachana na Mzee Dingi baada ya kushushwa kwenye gari na mstaafu, Mimi nilianza kufikiria ni jinsi gani naweza kumsaidia yule mstaafu bila kuingia kwenye utata na kina Mzee Dingi.

Wakati Mimi nafikiria hayo, Mzee KY kwa upande wake alikuwa ashanitoa kichwani kwake. By the moment tumeachana kule site, yeye tayari alisha-execute plan B. Plan ambayo timu nzima hatukuwa tunaifahamu, isipokuwa yeye. Kama ushawahi kuangalia movie, huwa kuna wale extra characters, wanaonekana kwenye vipande kadhaa ili kukamilisha matukio, baada ya hapo hawaonekani tena hadi movie inaisha. Hivyo ndivyo Mzee KY alivyotufanya timu nzima. Yani kipindi Mimi na Mzee Dingi tunatukanana barabarani kisa dili limedelay, kumbe kwenye dili lenyewe wote tumeshatolewa.

Kwa ufupi Mzee KY aliamua kuwa Solo.......

Mzee KY kama Scoffield [emoji23]


Kuna watu bado wamekaza fuvu kwenye ATM na 1.5M wakat mzee dingi yupo Vigwaza
 
7th Portion:

... Mzee Dingi akaniambia "Hela ikishafika mkononi mwako, alaf ukairudisha ilipotoka, utasumbuka sana kupata hela tena. Hela hairudishwi apostle"

Ilo jina apostle lilishaanza kunikera. Japo wanasema jina ukilikataa ndio linakua, ila sikuwa na namna, nikajikuta namjibu kwa hasira "Yule anafamilia inamtegemea, sio haki kumdhurumu, alafu na ilo jina la apostle sitaki kulisikia tena, umesikia we Mzee?". Mzee Dingi akabaki ameniangalia tu, alaf nae akawaka "Sikia apostle, nani ambae hana familia hapa?, Mimi mwenyewe napambania familia yangu vile vile". Akaendelea "Nyumbani hawajali hela naipataje, wao wanachohitaji ni matunzo, hata kama siipati kwa njia halali, ila nyumbani ikifika, inatatua shida zao, na wananishukuru kama Baba"

Nikamkatisha "Utajisikiaje unampa mkeo hela kwa ajili ya ada ya watoto, alaf anatokea mtu anamtapeli?". Wote wawili wakacheka, alaf Mzee Dingi akaniambia "Hiyo ndio itakuwa tiketi ya kurudi kwao, maana siwezi kuwa na mke mwenye tamaa. Huwezi kutapeliwa kama huna tamaa". Nikataka kuongea kitu, yule mwanasheria feki akaingilia "Apostle, kama unamuonea huruma, kamrudishie walau hiyo laki, haya shuka kwenye gari". Sikutaka kuendelea kuongea nao, nikashuka.

Nilivyoshuka kwenye ile gari yao, wao wakaondoka bila kuniambia wanaelekea wapi. Ila Mimi niliendelea kubakia eneo lile lile, nikiwa natafakari nini cha kufanya. Yule jamaa wa mkaa nilikuwa namuonea huruma, ila hapo hapo upande wangu nilikuwa nimefulia sana, kiasi kwamba nafsi ikawa inagoma kurudisha ile hela, jobless upate laki alafu urudishe? Labda Ulaya. Lakini upande mwingine nikajifikiria, endapo nitamrudishia ile laki, basi hapo nitakuwa nimejiingiza matatizoni. Potelea pote, nikaamua kurudi zangu gheto.

Ila nikawa nimepitisha uhamuzi wa kuwapotezea kina Mzee Dingi, maana kampani yao niliiona ni kama ticket ya jela.

Kesho yake mida saa sita, Mzee Dingi akanipigia simu, sikupokea, akapiga tena, sikupokea. Akaamua kutuma msg "Apostle, njoo mtaa wa Msimbazi na Lindi, kuna Kijiwe wanauza kahawa, fanya haraka". Nikaisoma, alaf nikaipotezea, nae akakausha. Ilivyofika wik end, siku ya jumapili, akaniita tuongee. Ila hakutaka tuongelee pale nyumbani, tukaenda kwenye kipub fulani hivi.

Kufika pale, ndio akaanza kuniambia "Sikiliza mdogo wangu, haya maisha yanahitaji kupambana, najua umesoma na unaelimu nzuri, lakini hiyo sio njia pekee ya ww kuingiza hela. Kama kuna kitu hujui ni kwamba, unakismart cha kuaminiwa, nyota yako inang'aa Apostle. Ni rahisi sana mtu kukuamini wewe, alaf na ulivyo muongeaji, na unavyojua kupangilia maneno, wewe ni mtu sahihi kabisa ambaye ofisi yetu ilikuwa inamkosa"

Nikamwangalia yule Mzee wee, sikusema chochote. Mzee aliongea vyote anavyojua ila kwa upande wangu nilishadhamiria siingii kwenye kazi zao. Nikaamua kuondoka eneo lile. Wakati naondoka, akawa ananisindikiza na maneno, "Ulivyokuja kuniomba nikuunganishie michongo, ulitegemea ufanye kazi ikulu? Au ulitaka ofisi yenye A.C? Mshamba sana we mtoto"

Sikumjibu kitu, nikamuacha kwenye ile pub, nikaelekea zangu betting center kupoteza muda.

Siku zilisogea, niliendelea na harakati zangu za kuunga unga kama kawaida, ila Mzee Dingi aliendelea kunishawishi nijiunge na timu yao. Ilifikia hatua ikawa kero sasa, hadi nikaanza kujutia kwanini nilimfataga kumwambia aniunganishie mchongo.

Nilivyoona usumbufu umezidi, nikaamua kuhama eneo lile. Nikahamia sehemu moja Tabata chang'ombe, karibia na hospital ya Kundy. Mimi na yeye tukawa tunaonana mara chache chache sana, hasa kwenye vituo vya dalala au njiani.

Kiuhalisia, baada ya kuhama, hata yeye akaamua kunipotezea kabisa. Ila miezi kama minne tokea nihame pale nilipokuwa nakaa mwanzo, Mzee Dingi akanipigia simu, mpaka kufikia pale, niliamini alishakubaliana na msimamo wangu, so sikuona tabu kupokea simu yake.

Nilivyoipokea, after salamu akaniambia "Apostle, fanya mpango tuonane wik end hii, kuna kitu nataka tujadiliane". Nikamuuliza "Kitu gani?". Akajibu "Usiwe na wasi, sio zile dili za kipindi kile, hii ni issue nyingine, wik end fanya unitafute". Nikamwambia fresh.

Ilivyofika jumapili tukakutana bar. Story mbili tatu, ndio akaniambia alichoniitia. "Sikia apostle, kuna kiasi fulani cha hela ninacho, nataka nianze kufanya biashara halali, sitaki tena dhuluma". Nikamjibu "Ni jambo zuri, ila sijaelewa Mimi nahusika vipi hapa?". Akasema " Sikia apostle, nahitaji mawazo ya biashara na mtu ambae naweza kufanya nae. Nahitaji tushirikiane"

Baada ya blah blah hapa na pale, kuna wazo nikalitoa, ambalo nililifikiriaga muda mrefu, ila mtaji ikawa ndio shida

Na ilo wazo lilikuwa kutoa mkaa vijijini, kisha unakuja kusambaza mjini, kama jinsi alivyokuwa anafanya yule jamaa aliyetapeliwa na kina Mzee Dingi. Nilipomuelezea, akafikiria kwa muda kidogo, Kisha akaniuliza vitu kadhaa kuona uelewa wangu kwenye hiyo biashara. Alivyoona maelezo yangu yapo clear, akasema ngoja atafakari zaidi, huku akiwa anaangalia uwezekano wa kupata madalali hapa mjini, ili mzigo ukifika, tusisumbuke kupata soko.

Tukaagana, nikaondoka eneo lile.

Baada ya kama siku tatu, akanipigia tena. Akaomba tuonane, ila safari hii akaja mpaka nilipohamia. Baada ya maongezi ya hapa na pale, tukawa tumekubaliana kufanya biashara. Kwavile sikuwa na mishe ya kueleweka, hii niliichukulia kama nafasi pekee ya kunitoa kwenye ukata. Nikadhamiria kuifanya kwa moyo na uaminifu, ili kujitengenezea kipato, lakini pia kumuonesha Mzee Dingi kuwa inawezekana kuingiza hela kwa njia halali.

Nilijidanganya. Nilichokuwa nawaza Mimi, sicho alichokuwa akiwaza Mzee Dingi.....


Endelea hapa Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, Mpaka siku niliyokutana na yule Mzee
Pole apostle
 
18th Portion:

Baada ya kuachana na Mzee Dingi, nilirudi gheto direct. Siku hiyo hiyo mida ya jioni, yule mama mstaafu akanipigia simu;

Mstaafu: "Hujambo mwanangu?"
Analyse: "Mzima mama, shikamoo"
Mstaafu: "Marahaba. Vipi utakuwepo mjini mpaka lini?"
Analyse: "Kuna vitu naweka sawa, vikikamilika nitaondoka. Inaweza ikawa Jumatatu au Jumanne"
Mstaafu: " Tunaweza kuonana kabla hujaondoka?"
Analyse: "Sawa hakuna shida, nadhani Jumatatu jioni nitakuja".


Baada ya kuongea na yule mstaafu, jioni hiyo hiyo, Mzee KY nae akanipigia simu, kuniambia tuonane siku ya Jumatatu jioni bila kukosa, ili tuweke sawa mambo kadhaa. So, ndani ya siku moja nikawa na appointments mbili, na zote jioni.

Wa kwanza kuonana nae ni Mzee KY, tulikutana mida ya saa kumi kumi.

Mzee KY: "Umeshaongea na yule mama au kuonana nae tokea ufike mjini?"
Analyse: "Hapana, kwanini?
Mzee KY: "Ulimwambia chochote labda kuhusu huu mpango?"
Analyse: "Hapana, vipi kwani?"
Mzee KY: "Oky Vizuri, sasa shika hizi hesabu" (akatoa hela na kunipa).

Nikahesabu, zikafika laki 3 na nusu. Nikamuuliza za nini hizi?

Mzee KY: "Huo ndio mgao wako, kwenye ili dili haupo tena"

Nikabaki nimeshangaa, sipo Kivipi?. Maana kama sipo basi dili limekufa, ila yeye mbona anaongea as if dili bado lipo?.

Ni kama vile aliyasoma mawazo yangu, akaniambia "Wewe ulikuwa plan A, haikuwa plan pekee. Kwahiyo kama nilivyokwambia, naomba ukae pembeni, dili litaenda bila uwepo wako. Na usije kumwambia chochote yule Mama"

Nikabaki na mwangalia tu. Hapa ndio alikuja kunipa maelezo ambayo nilikuja kuhitimisha kuwa, uwepo wangu kwenye lile dili haikuwa coincidence, kila kitu kilikuwa planned. Aliifahamu connection yangu na yule mama, na dhumuni la kunifanya Mimi kuplay role ya mwenyekiti, ili niweze kugain trust ya yule mama Kwa urahisi. Na hata kile kitendo cha Mzee Dingi Kuni unblock na kunitaka nipige nao kazi, yote ilikuwa ni maandalizi ya ili dili. Halikuja ghafla kama nilivyodhani. Baadhi ya maelezo aliyonipa, ndiyo niliyaelezea jana. Japo kuna mengine niliyaelezea jana, ila yeye alikuja kuniambia mbeleni kabisa wakati dili limeshafanyika.

Baada ya kumaliza mazungumzo yetu, tukaagana. Sikuwa na sehemu nyingine ya kwenda zaidi ya kule kwa mstaafu, ikabidi nielekee kule.

Nikiwa zangu mdogo mdogo nishakaribia kwa yule, Sina ili wala lile. Kumbe Mzee KY alikuwa ameniungia tela. Sikujua kama dhamira yake ilikuwa kupajua ninapoishi au alitaka kujua nitaelekea wapi baada ya sisi kuachana pale kwenye ile Pub. Naingia tu kwenye ile nyumba, na yeye huyu hapa. Kwa haraka haraka, mtu angeweza kuhisi kuwa tulikuwa tumeongozana wakati tunaenda pale.

Nilishtuka kumuona, japo sikuwa na uwezo wowote wa kumzuia yeye kuwa pale. Yule Mama mstaafu alipotuona wote alifurahi sana;

Mstaafu: "Naona watu muhimu mmeamua kunijia kwa pamoja, karibuni sana"
Analyse: "Asante sana"
Mzee KY: "Kijana alinipigia simu niungane nae kuja kukuona. Vipi za tokea siku ile?
Mstaafu: "Salama tu, Tunamshkuru Mungu uzima upo kama unavyotuona"

Kisha akanigeukia Mimi;

Mstaafu: "Karibu tena nyumbani, ila this time karibu kama mwenyekiti"

Aliniambia hayo maneno huku anacheka, Mzee KY nae akacheka kidogo. Tukaingia na kukaa sebleni kwake. Maongezi yote kayatawala yule mama tu. Kuna muda akaingia chumbani huko, kisha akatoka na hela;

Mstaafu: "Nilikwambia nitakurudishia hela ya Kodi uliyoacha, chukua laki mbili yako. Sitaki dhulma Mimi, najua kijana ndio kwanza unaanza kujijenga".

Mzee KY akamakinika kuona nitafanya nini. Binafsi nikaamua kuzikataa zile hela;

Analyse: "Hapana mama, nilihama kwa hiari yangu hii hela wala sio deni kwako"
Mstaafu: "Chukua mwanangu, hii haiusiani na kule kusainishiana, maana kule najua huwezi kuniangusha. Nakupa kama kijana wangu tu".

Unajua siku zote wakati nakua, kuna methali ilikuwaga maarufu sana.

"Sikio la kufa halisikii dawa"

Ukikanywa, usiposikia lazima uambiwe. Siku zote nilikuwa naichukulia kama methali tu, lakini in a real sense kwa mara ya kwanza nimekutana na ilo "Sikio la kufa". Unajua ili umuokoe mtu anayezama, sharti awe mtulivu vinginevyo mtazama wote. Au la, basi mpe kijiti, akishike umvute. Sasa huyu mama kila nikimpa kijiti, anakikataa. Kimoyo moyo nikajisemea atajijua mwenyewe.

Analyse: "Usijali mama, hiyo hela wewe Kaa nayo. Nimeondoka kwa amani kabisa, nikiichukua nitajisikia vibaya".

Akabaki na hela yake. Baada ya maongezi ya hapa na pale, Mzee KY akaomba niwapishe waongee kidogo. Sikuwa na namna, nikatoka zangu nje, wakaongea mambo yao kwa takribani nusu saa au dakika arobaini na tano. Baada ya hapo Mzee KY akatoka nje, tukaondoka wote.

Baada ya kutoka pale, akatafuta sehemu. Akaniweka kikao tena;

Mzee KY: "Sikia kijana, hivi unaweza kukadilia gharama kiasi gani imetumika kuandaa Ili dili?".

Ni kama alikuwa anaongea peke yake, maana kabla sijamjibu akaendelea tena;

"Mlivyokuja kule site, uliwaona wale majirani niliosalimiana nao?. Wale wote nimetoka nao huku. Uliwaona wale watu wanaolima pale?. Sijui hata wanalima nini, ila nao nimewaweka Mimi."

Akaendelea;

"Dili lifanikiwe au lisifanikiwe, hao wote lazima wapate hela yao. Sasa hebu niambie, lisipofanikiwa hela za kuwalipa zinatoka wapi?"

"Kuna watu huwezi kuwasaidia hata ufanye vipi, they are destined to lose. Hata ukisema umuache na hela zake akanunue eneo halali, still zile hela ataenda kuzifukia chini akitegemea zitachipua, ila ataambulia hasara. Najua hukuchukua ile laki mbili yake, sio kwamba huitaki au unamuonea huruma, bali you feel guilty. Nitakupa Mimi ile laki mbili, soon after dili kufanikiwa, ila for now naomba usinizibie njia, maana siwezi elezea nitakachokufanya. Umenisikia..........?'' Akataja jina langu halisi.

Nikashtuka, amelijuaje jina langu?.

Mzee KY
: "Wote mliopo kwenye Ili dili hakuna nisiyemjua, kuanzia anapokaa au sehemu zake za kwanza kukimbilia hapa mjini, kwahiyo kabla hujafanya jambo utakalokuja kulijutia, ni heri ujifikirie mara mbili"

Nikabaki nimeduwaa tu Kwa muda, sielewi what next. Akaniambia, "Huna haja ya kuendelea kubaki hapa, wahi ukapange vitu kwenye makazi yako mapya, japo nakushauri hama". Hakusubiria jibu langu, akaondoka.

So, he knows me well?. Why nihame wakati ndio kwanza nimehamia au kuna msala unanisubiria? Wazo likanijia, kwanza yule mstaafu tumejuliana mjini hapa hapa, atajijua mwenyewe, ngoja nijihangaikie Mimi.

Nilivyofika ghetto, Yale maneno ya Mzee KY kuwa nihame pale, yakawa yananijia. Nikajikuta njia panda, nipange vitu au nijiandae kuhama?. Ila nimetoka kulipa Kodi ya miezi 6 siku chache tu zilizopita, nahamaje? Mbona ntakuwa nafaidisha wenye nyumba?. Lakini taswira ya Mzee KY ikawa hainipi picha nzuri ya yajayo. Akili ikaniambia nisipange vile vitu, nihame.

Nikampigia simu mwenye nyumba, kumuomba kesho tuonane kama ataweza. Akakubali.

Asubuhi nilivyoonana nae, nikampanga kuwa nimepata dharura natakiwa kusafiri haraka nje ya mkoa, anirudishie hata nusu kodi. Akanijibu "Mwanangu Cha kukusaidia hapa, labda nikuhifadhie vitu vyako kwahiyo miezi 6 utakayokuwa unapambana na hiyo dharura yako"

Nikaona hapa siwezi ambulia hata mia, cha zaidi nitapoteza muda tu kumbembeleza.

Kipindi Mimi nawaza namna ya kuhama pale. Mzee Dingi akanipigia simu na kuomba tuonane.

Nikafikiria huyu nikutane nae maeneo yapi?. Kipindi kile maeneo ya Tabata kuna mashindano ya mpira wa miguu yalikuwa yanaendelea. Viwanja vilivyokuwa vinatumika ni kile Cha Sigara na cha Tabata shule. Nikaona option ya Tabata shule ndio sahihi, maana ni mbali kiasi na ninapoishi. Lakini sababu nyingine iliyofanya nisione shida kukutana nae Tabata, ni kwavile nilikuwa natarajia kuhama.

Nikamwambia tukutane Tabata shule. Mzee Dingi akagoma, na hii ni kwavile pale ni karibu sana mitaa anayoishi yeye. Nilivyóona bado anakomaa tuchange location, nikamwambia basi sitaki kuonana na wewe. Endelea na mishe zako.

Nilipata ujasili wa kumwambia vile kutokana na sababu Kuu mbili, kwanza kwenye dili lao sipo tena, alafu pili sijui anataka tuongee nini. Alivyoona nimekataa kuonana nae, hakuwa na choice zaidi ya kukubali tukutane maeneo yale.

Mida ya jioni nikasogea pale Tabata shule. Mzee Dingi alikuwa ameshafika kabla yangu. Mara zote ambazo tumekuwa tukikutana, vikao vilikuwa vinafanyikia either bar, pub or kwenye mgahawa. Ila this time hakutaka tukutane maeneo hayo. Akapendekeza tukutane kwenye yale majengo ya shule ya Kijapan (kuna shule ilijengwa na Wajapani maeneo yale). Nikajiuliza mara mbili mbili, why kachagua kule?. Ila kimoyo moyo nikajisemea akileta za kuleta, nitamfumua. Hasira zangu zote ziishie kwake.

Akanielekeza alipokuwa amesimama, nikamfata. Kufika pale, navikuta vizee vyote vitatu vipo. Mzee Dingi, Mzee Kidevu na Mwanasheria feki. Nikajiuliza vinanitakia nini?.

Nilivyowaona, sura zao zote ziliakisi shari, ila sikuwa na namna zaidi ya kuwasogelea. Zikapigwa story za hapa na pale, lakini Unaona kabisa hapa kuna jambo litatokea muda sio mrefu. Na Mimi kwa hasira nilizokuwa nazo, nikawa nasubiria kwa hamu ilo jambo litokee. Kwa jinsi tulivyokuwa tumejipanga, Mzee Kidevu alikuwa nyuma kidogo upande wangu wa kushoto, alafu mwanasheria feki na Mzee Dingi walikuwa mbele, tupo face to face. Tukiwa tunaendelea kuongea upande, kwa ghafla sana yule Mzee Kidevu akanirukia horizontally na kunipiga kichwa cha mbavu. Ni kitu ambacho sikuwa nimekitarajia, nikajikuta nayumba yumba. Kitendo cha kuyumba yumba, wale wazee wote wakanivamia kwa pamoja.

Nikajisemea hapa ndio nilikuwa napataka, ngoja nipunguze hasira zangu. Unajua Kwa jinsi nilivyokuwa nawakadiria, nilihisi dakika 10 nyingi wangesanda kwenye lile valangati. Ila yule Mzee Kidevu sijui hata anakulaga nini aisee, maana kuna muda nilimrushia ngumi, lengo nimpige shingoni, ila at the same time nae akanirushia ngumi. Ngumi kwa ngumi zikakutana, nilipatwa na maumivu kiasi kwamba nikahisi nimepiga mti. Kibaya zaidi yule Mzee hata akuugulia chochote, ndio kwanza anakuja tu.

Kipindi hicho chote, Mzee Dingi na Mwanasheria feki wameshasanda, wameniacha Mimi na Mzee Kidevu. Raia wamejaa wanauliza kuna nini?. Mzee Dingi linawajibu "Mambo ya kifamilia, tuachieni wenyewe". Yule Mzee Kidevu kama angekuwa na pumzi ya kutosha, angeniaibisha pale, kitu pekee kilichofanya akachemka ni pumzi. Nilivyóona kazidiwa, nikaanza kumpelekea punch mfululizo. Kumbe bwana vile vizee vilikuja na back up. Muda wote tokea nimewakuta, kuna jamaa kipande alikuwa amekaa kwa pembeni anachezea simu.

Walivyoona hadi Mzee Kidevu kazidiwa, Mzee Dingi akaita "We Beka fanya kazi yako". Aisee nilivyomuona huyo Beka mwenyewe, sikuwa na namna zaidi ya kukimbia. Nilifungua turbo kuelekea kwenye makazi ya watu, yamekaa kama kota hivi. Nilidhani watanipotezea, nashangaa Beka kaniungia tela, Mzee Kidevu na wale wazee wengine nao wakaanza kuja nyuma yetu. Raia nao hawana dogo, baadhi wameacha kuangalia mpira, wametuungia tela.

Nikipiga hatua zangu mbili, ndio hatua moja ya Beka. Sikwenda mbali sana akanishika. Nikataitishwa. Mwanasheria feki akawa anafanyakazi ya kufukuza watu walau wasogee mbali ba tulipo. Nilivyokuwa chini pale, Mzee Dingi akawa anasema;

Mzee Dingi: "Mvue hivyo vitu alivyovaa ndio vinamtia kiburi"

Beka akanichukulia ile pete yangu yenye kihirizi. Kisha akataka kunivua na kacha niliyokuwa nimevaa mkononi

Mzee Dingi: "Hiyo muachie, haina madhara. Yupo nayo hata kabla hajaoneshwa Dunia ilivyo"

Baada ya kuichukua ile pete, akamkabidhi Mzee Dingi, alafu wakaanza kuondoka. Kwenye wallet nilikuwa na 70k, hawakuigusa kabisa. Yani Wazee shida yao ilikuwa ile pete tu. Nilikuwa bado nimekaa chini nikiwa na hasira, maana yule kipande aliniumiza. Ghafla kuna wazo likanipitia kichwani, sikujiuliza mara mbili, nikanyanyuka na kuanza kuwafata. Nilivyowakaribia nikainama chini na kuchota mchanga, Mzee Kidevu akawa ameniaona;

Mzee Kidevu: "Apostle umenichota unyayo, apostle umenichota unyayo?"

Kiukweli nilifanya vile kama kuwatisha tu, ila Mzee Kidevu akalichukulia serious.

Mzee Kidevu: "Apostle unachotaka kukianzisha unakimudu?. Kumbe mtoto mshenzi sana wewe"

Kabla sijamjibu kitu, yule Beka kipande akawahi kunikamata, akaniminya mkono hadi nikaachia ule mchanga. Nikabaki nimesimama tu. Kila Wakitaka kuondoka, natishia kama nainama kuzoa mchanga, wanarudi.

Mzee Dingi: "Huyu mtoto sio wa kumfanyia mzaha kabisa"

Jamaa kila wakipiga hesabu, walipoacha gari yao ni mbali lazima watembee. Lakini hapo hapo wanahofia huku nyuma naweza fanya jambo baya. Ghafla Mzee Kidevu akanirukia, tukaanguka wote chini. Kisha wakamwambia Beka anibebe mpaka kwenye gari yao.

Muda huo wote raia full kucheka, kelele na kuzomea. Jamaa ikabidi wanipe lift kwa lazima, wakaenda kunishushia Ilala Boma.

Nilichokuja kugundua, kumbe ile Jana nilivyoacha na mzee Kesho Yetu, alimpigia Mzee Dingi na kumwambia Mimi sitoshiriki tena kwenye lile dili, nikiendelea kuwepo kuna uwezekano mkubwa sana wa dili kufeli. Ndio maana kina Mzee Dingi wakaamua kuja kunishikisha adabu na kunipora kile kihirizi, maana waliona sihitajiki tena.

Ambacho Mimi na wale wazee hatukujua ni kwamba, wakati sisi huku tunashikana mashati, upande wa pili Mzee Kesho Yetu alikuwa anakamilisha dili. Jana yake wakati tupo kwa yule mstaafu, walivyo baki peke yao sijui hata alimwambia nini, ila chochote alichomwambia ndicho kilichopelekea wao kwenda kukamilisha dili.

Walau Mimi nilishajua kuwa kwenye lile dili sipo tena, ila kina Mzee Dingi wao walikuwa wanasubiria siku mbili mbele wakakamilishe dili.

Wamechukua pete yangu, na kuondoka kishujaa, kumbe upande wa pili Mzee Kesho Yetu anasepa na mkwanja peke yake.

Kibaya zaidi, anaacha msala ambao ni wetu wote, ilhali sisi wengine hatujajiandaa....
Kula chuma hiyo
20221111_144143.jpg
 
Mkuu, wewe unaweza kwenda kununua shamba au kiwanja alafu usiende na mtu wako wa karibu? I mean rafiki/mke/kaka/dada/ndugu wa karibu??

Tuendelee na story tusije maliza utamu mkuu!!
Yule mama alikuwa tayari Chini ya himaya yao na ndio maana mzee KY Ali execute plan B

Kumbuka pia KY ndie alimpeleka Mwamba kwa mganga Moro
 
Dah ila Apostle unazingua, kwanin haumtonyi mmama wa watu mwenye moyo mwema,

maana hao wapigaji wao wanataka kumpiga izo million 40 wakale bata tu na sio kingine.

ila aisee wazazi wanajua unapambana mjini kumbe unanyang'anyana mchanga na wakina mzee dingi
 
9th Portion:


.....Bi Mkubwa ikabidi aniulize kwa upole tu "Tuambie mwanangu, huyu jamaa unashida nae ipi?". Nikaendelea kuwa kimya tu kwa muda. Fikra ndio zikaanza kunituma, huenda kuumwa kwangu yule Kisauti akawa anahusika. Nilikuwa nishamsahau kabisa. Nilipatwa na hasira kuona nateseka kwa kosa lisilokuwa langu. Mshua alivyoona bado nipo kimya, sijamjibu Mama chochote, akanyanyuka na kuanza kuondoka. Bi mkubwa akamuuliza

Bi Mkubwa: "Baba nanii unaenda wapi sasa?

Mshua: "Sasa mtu haongei, nitakaa hapo siku nzima?"

Bi Mkubwa: "Unajua ili ni tatizo kubwa sana, usilifanyie mzaha"

Mshua: "Mzaha anaufanya huyo hapo, katibua watu mjini huko, karudi kutupa sisi shida"

Bi Mkubwa: "Kwahiyo tumuache afe"

Mshua: "Na akiendelea kukaa kimya, atakufa kweli"

Nilivyoona mzozo utaenda kuwa mkubwa, ikabidi niwafungukie issue nzima ilivyokuwa. Baada ya hapo wakaanza kujadiliana nini kifanyike. Bi Mkubwa akashauri wampigie simu Kisauti ili kumuomba msamaha, Kisha waangalie namna gani wanalimaliza lile jambo. Ila Mshua akagoma.

Bi Mkubwa: "Mwanao hali yake sio nzuri huyu, tuwasiliane na mdeni wake, tumlipe yaishe"

Mshua: "Hatuwezi lipa hela ambayo hatujachukua. Huo ni unyonge, na siwezi kuufanya. Dawa ya moto ni moto, kwavile kaanza yeye, acha tuendeleze, ngoja niwasiliane na Mzee Taba, ili tumpeleke kwa mtaalam"

Bi Mkubwa: "Mwanangu haendi kwa mtaalam wala kilingeni, kesho asubuhi naenda nae kanisani kwenye maombi"

Mshua: "Kwa hali ilivyo, lazima twende tu, na ilo halina mjadala"

Ukatokea mvutano mwingine pale, wapi nipelekwe hiyo kesho. Ila Mshua kutokana na commanding force yake, ikaamriwa nipelekwe kwa mtaalam. Kesho yake asubuhi na mapema tukaenda hadi kilingeni. Bi Mkubwa nae hakutaka kubaki nyumbani, alitaka awe na Mimi muda wote ili kujua hatma yangu.

Kufika kwa mganga tukapokelewa vizuri. Kutokana na hali niliyokuwa nayo, nikapewa kipaumbele kuonana na mtaalam. Tulivyoingia ndani, akaanza kuweka vitu vyake sawa, ongea ongea mambo yake pale.

Kuna muda nadhani alipandisha mashetani, maana lafudhi ilibadilika. Yeye ni mtu wa Kanda ya ziwa, ila ghafla akaanza kuongea lafudhi ya kimasai. Kuna mtu mwingine ambae ni msaidizi wake, ndio akawa anasaidia mwongozo wa yaliyokuwa yanaongelewa. Zoezi lilidumu kama nusu saa, then akarudi normal. Bila hata sisi kuongea sana, akaniambia, "Kijana unabahati sana kuendelea kuliona jua mpaka muda huu. Wapinzani wako, dhamira yao ni ya dhati". Mshua akauliza, kwahiyo nini kifanyike?. Yule mtaalam akasema kwasasa kuna kitu inabidi nimfanyie ili kudhibiti maumivu, alaf usiku ndio tutafanya zoezi kamili la kumtoa kwenye hii hali". Mshua akasema sawa, hakuna shida.

Mtaalam akaanza kufanya kazi yake pale. Mle ndani kulikuwa na kinu kikubwa kama vile wanavyotwangiaga wanawake, ila chenyewe kimechakaa sana, yawezekana ni cha muda mrefu, na rangi yake ilikuwa nyeusi tii, na mistari mistari myeupe. Sasa baada ya mtaalam kufanya mambo yake, akataka kupanda juu ya kile kinu, sikujua dhumuni lake lilikuwa ni lipi, maana wote mle tulibaki kuwa watazamaji tu. Wakati yupo juu ya kile kinu, alianguka yeye na kinu chake na kutanguliza uso chini. Alivyofika chini, kimya kikatawala. Urefu alioanguka ulikuwa mdogo sana, hata mtoto mdogo angeweza kusurvive, ila cha ajabu mganga alizimia. Yule msaidizi wake ndio akamkimbilia ghafla na kumnyanyua. Akachovya ule usinga kwenye kibakuli fulani kilikuwa pembeni, alaf akaanza kumpiga nao, huku anaongea maneno ambayo sikuyaelewa. Baada ya muda, mtaalam akaamka, anaongea ila sauti inatoka kwa mbali sana kama kakabwa au ametoka kukabwa.

Muda huo wote, sisi tupo kimya tu. Fahamu zilipomrudia vizuri na kuwa na utimamu wake. Akatwambia kwa upande wake, ili zoezi lipo nje ya uwezo wake, yani limemshinda. Akatuelekeza kwa mtaalam mwingine, aliyekuwa kijiji cha pili ambaye anaweza kutusaidia. Mshua na Bi Mkubwa wakawa wanajadiliana, Mshua anauliza kama twende siku hiyo hiyo, au kesho yake, ila Mama anataka turudi nyumbani. Yule mtaalam akawaambia, kadiri mnavyochelewa, ndivyo mnavyojisogeza kwenye kilio. Muwahisheni huyu, vinginevyo mtamkosa.

Bila kupoteza muda, tukafunga safari mpaka kwenye hicho kijiji. Tukaulizia hadi tukafanikiwa kumfikia yule mganga. Kutokana na miundombinu ya kijijini ilivyo, tulijikuta tunafika pale jua likiwa limeshaanza kupungua nguvu.

Tulipokelewa vizuri na msaidizi, tukakaa foleni kusubiria zamu yetu ifike.

Mida ya saa kumi na mbili kasoro, ndio tukafanikiwa kuonana nae. Hapo Bi Mkubwa nafsi haijamtulia kabisa. Muda wote kama ana mashaka na mganga. Ile hali ya Bi Mkubwa ikawa inamkera yule mtaalam. Akatwambia "Kuna hii dawa, ili zoezi lifanikiwe, inabidi wote watatu muilambe". Akaanza kutaka kumpa Bi Mkubwa, Mama akasita kidogo. Yule mganga akamkata jicho. Ikabidi Bi Mkubwa akubali kuilamba. Cha ajabu baada ya Bi Mkubwa kuilamba, sisi wengine hatukupewa. Bi Mkubwa akahoji kulikoni? Yule mganga akatoa usinga na kumpiga nao kichwani, Bi Mkubwa akasombwa na usingizi. Mimi na Mshua tukajikuta tunatazamana tu bila kusema chochote.

Baada ya salamu, akatwambia "Poleni sana na safari, maana huku tulipo ni mbali sana na mlipotoka". Baada ya kumuelezea dhumuni letu la kuwa pale, nae akafanya standard procedures zao (naziita standard procedure maana kote nilipoenda naona wanafanya hivyo). Baada ya muda kidogo akaanza kutwambia. Akaendelea "Tatizo lililowaleta hapa nimeliona vizuri sana, ila kwa bahati mbaya lipo nje ya uwezo wangu"

Mshua akamuuliza "Unamaanisha nini?". Yule mganga akasema "Aliyemfanyia hivi kijana wako, ni mtu aliyedhamiria sana, na hata huko alipoenda, ni Kwa mtu mwenye uwezo wa juu kuliko wangu. Hapa ninaweza kuliona tatizo, lakini uwezo wa kulitatua ndio sina"

Mshua akawa kama mtu aliyekata tamaa, akamuuliza yule mtaalam "Sasa unatusaidiaje au unatushauri kitu gani?. Yule mganga akamjibu "Kitu ninachoweza kuwasaidia kwasasa ni kuwapa sehemu ya kupumzika usiku wa leo, na kesho patakapokucha, nawashauri mtafute mganga mwingine".

Kusikia vile, hata Mimi nikajihisi kukata tamaa, Kisauti amedhamiria kunipoteza.

Mshua akamuuliza, dhumuni la yeye kumfanyia vile Bi Mkubwa ni lipi?. Mtaalam akamwambia "Huyu hakuwa na utulivu wa nafsi, kadiri muda unavyoenda angeweza kunikwaza, ila msiwe na wasi, ataamka ndani ya muda mchache ujao.

Mshua akaomba tuondoke siku ile ile. Wakasaidiana kumuweka Bi Mkubwa ndani ya gari, na kumlaza siti za nyuma. Mimi na Mshua tukawa mbele, safari ikaanza.

Tukiwa njiani, Bi Mkubwa ndio fahamu zikamrudia, akajiinua na kukaa. Mshua akageuka na kumuuliza anajiskiaje? Bi Mkubwa hakujibu kitu, ila likamtoka fyonyo moja refu. Kiasi kwamba kule mbele tukapatwa na hali ya kutaka kucheka. Kuzuga ikabidi nigeukie nje, maana ningecheka yangezuka mengine. Mshua sababu ya kuendesha, plus ubovu wa barabara hakuweza kugeukia nje,alaf kicheko kikataka kumponyoka. Akazuga kupiga chafya na kujikoholesha. Picha nzima Bi Mkubwa akawa kaisoma. Bi Mkubwa ni dizaini ya wale wa wamama ambao Ukifanya kosa anaweza akakukata jicho kali hata kwa dakika 5 nzima, sasa ndicho kilichotokea kwenye gari. Alimkata jicho Mshua, kiasi kwamba kule mbele Mshua akawa anahisi ile hali. Ila hapo hapo anajizuia kucheka tena, maana heri ya Mimi, yeye angecheka tena ile safari ingekuwa chungu kwake.

Wote tukawa kimya, unasikika mziki tu kwenye radio. "Zima mamiziki yako inaniumiza kichwa Mimi" Bi Mkubwa akawaka ghafla, Mshua wala hakuongea kitu, akazima, safari ikaendelea.

Njiani nzima akawa anasikika Bi Mkubwa tu, anatusema weee, alaf anakaa kimya. Baada ya muda kidogo anatusema tena, Kisha anakaa kimya.

Mshua yeye yupo kimya tu, macho yako mbele muda wote. Kadiri gari inavyonesa nesa kwenye ile barabara mbovu, na Mimi ndivyo ninavyozidi kugugumia maumivu, Mama nae anakunja sura kwa uchungu, kama vile na yeye anaumia. Mshua yupo kimya, hana story na mtu. Ila kila Bi Mkubwa akimsema, yeye ananikata jicho Mimi, kujaribu kunionesha kuwa Mimi ndio chanzo.....

Endelea hapa Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee
Aise pole sana unajua kwanini ulikuwa una pumua mpaka muda nikwasababu haukula hiyo pesa.
 
10th Portion:

.....Tulifika nyumbani usiku ukiwa umeshaingia. Ila mpaka muda huo, hawakuwa wamekubaliana hatua gani ifuate. Wakati Mimi nakula, Mshua akaomba namba ya Kisauti ili ampigie. Bi Mkubwa akakataa, akasema kama tunampigia, basi yeye (Mama) ndio aongee nae, na sio Mshua. Na hii inatokana na kwamba Mshua hapendagi mambo ya kubembelezana sana, haijalishi nani yupo sahihi. Sometime huwa nahisi ikitokea nimetekwa, alaf watekaji wakampigia simu Mshua kumpiga mikwara awape hela ili waniachie, najiona kabisa nikifa [emoji28][emoji28][emoji28]

Bi Mkubwa akapiga, simu alafu akaweka loudspeaker. Kisauti akapokea. Bi Mkubwa akajitambulisha.

Bi Mkubwa: "Mimi Mama ake fulani..."

Kisauti: "Anhaa, vipi anaendeleaje?"

Bi Mkubwa: "Hali yake bado sio nzuri, tunahitaji msaada wako"

Kisauti: "Dah, mtoto anaroho ngumu sana huyu, bado yupo? "

Bi Mkubwa: " Hakuna haja ya kumfanyia hivyo mwenzako, tutakulipa hizo hela, ila usimfanyie hivyo"

Kisauti: "We hujui alichonifanyia huyo, hujui kabisa. Jeuri sana huyo mtoto"

Kitu ambacho sikukielezea hapo mwanzoni ni kwamba, Mzee Dingi alivyopotea na zile hela, msala aliniachia Mimi. Na Mimi kitendo cha kuondoka kule porini, msala alibaki nao Kisauti. Ule mkaa wote tuliochukua, haukuwa mali ya Kisauti peke yake, yeye alikuwa kama mwakilishi tu au kiongozi, plus hela za wale vibarua. Sasa sikujua walimfanya nini baada ya huu msala kutokea, ila alikuwa na hasira sana.

Sasa wakati Bi Mkubwa anaendelea kuongea nae, Kisauti akasema "Huyo msihangaike nae, muacheni tu, maana hakuna mtakachoweza kufanya". Alafu akakata simu kama kawaida yake.

Simu ilivyokatwa, pakafatiwa na ukimya kidogo. Kisha Bi Mkubwa akaanda chakula kwa ajili yao. Walivyomaliza kula, ndio mjadala ukaanza upya, nini kifanyike. Bi Mkubwa akaendelea kusisizita, wanipeleke kwenye maombi, ila Mshua ni kama mtu ambae akili yake haikuwa pale home, maana alikuwa kwenye mawazo mazito sana.

Pasi na kuongea na mtu yeyote, Mshua akachukua simu yake, Kisha akatoka nje. Alikaa huko muda mrefu kidogo, alirudi ndani kipindi Mimi nishaingia chumbani kulala. Chumba nilichokuwemo, kilikuwa karibu zaidi na sebule, hivyo niliweza kuwasikia wakibishana kuhusu siku ya kesho. Mshua alikuwa anasisitiza asubuhi na mapema ataondoka na Mimi kuna sehem anatakiwa anipeleke. Ila Bi Mkubwa akawa hataki. Ila baada ya mzozo wa muda mfupi, Bi Mkubwa akakubali yaishe.

Palivyokucha, safari ikaanza hadi ziwani, then kutokea pale, tukapanda mtumbwi mpaka kwenye kisiwa fulani hivi cha wastani kwenye ziwa Victoria, ambacho makazi ya watu yalikuwa ya kuhesabu sana. Kwa kupitia maelekezo ya wenyeji, tukafanikiwa hadi kufika sehemu ambayo Mshua aliikusudia. Tukapokelewa vizuri. Hapakuwa na watu wengi, ila tulilazimika kusubiria muda mrefu, maana mtaalam alikuwa kaenda porini kutafuta dawa kwa ajili ya kazi zake.

Alivyorudi, tukaambiwa tuingie ndani.

Akatwambia :

Mtaalam: "Taja majina matatu ya mgonjwa, pamoja na jina la mama yake". Mshua akataja, alafu mganga akaanza kufanya madude yake aliyoyajua mwenyewe. Baada ya muda akaanza kuongea na Mshua.

Mtaalam: " Tatizo lenu nimeshalijua, ila ningependa kujua nyie mnahitaji nini"
Mshua: "Nataka mwanangu apone, lakini pia ningependa kujua amefanywa kitu gani"
Mtaalam: "Waliofanya hivi, dhamira yao ni kumuondoa huyu kijana, lakini hawakutaka aondoke mapema"
Mshua: "Kivipi?"
Mtaalam: "Walitaka apitie mateso makali sana, alafu ndio afe. Ni kama waliamua kumuadhibu kwanza. Maana vilichukuliwa vitu kama mfuko au maputo matatu, yakasomewa kisomo, alafu yakavalishwa moja juu ya jingine. Yote matatu kwa pamoja yakatengeneza puto moja, ndani yao kikawekwa kitu chenye ncha ncha, mfano wa mbegu ya mbigili. Baada ya hapo likajazwa hewa,likafungwa na kwenda kuning'inizwa porini juu ya mti mrefu kabisa. Yale maputo ndio yanawakilisha mwili wa huyu kijana. Kadiri upepo unavyo vuma, lile puto linapepea, na ile mbigili ndani yake inafanya kulichoma puto. Siku puto litakapopasuka, ndio siku atakayoaga Dunia"

Hayo maelezo ya yule mganga, yalininyong'onyesha sana. Nikajiona hapa sitoboi. Kwenye kile kichumba cha mganga palikuwa na hali ya hewa ya joto sana, ila maelezo yake yalifanya nikatokwa na vipele vya baridi. Mshua ikabidi amuulize kuwa Kwa hali hiyo tunafanyaje sasa?

Mtaalam: "Kitu cha kufanya ni kwenda porini kulitafuta ilo puto, kulitoa juu ya mti,kulifungua na kutoa ile bengu. Hakuna njia nyingine ya tofauti". Mtaalam akaendelea "Angetaka kummaliza haraka, puto moja lingetosha, huyu alidhamiria kumtesa kwanza"

Mshua akabaki ameduwaa tu. Kila mganga akiongea, yeye anashtuka tu "Duh, duh, aisee". Yani zile duh duh zilikuwa nyingi hadi msaidizi wa mganga akamkata jicho. Yule mganga ikabidi amwambie, "Ilo zoezi lote inabidi lifanyike usiku wa leo, kabla hapajakucha, ngoja niandae vitendea kazi"

Muda ule ule, kuna mambo baadhi yalifanyika ili kuweka maandalizi sawa Kwa ajili ya zoezi la usiku. Nilichanjwa chanjwa baadhi ya maeneo, nikapakwa vitu ambavyo sikuvielewa, lengo ilikuwa ni kuniweka tayari.

Kuna mambo mengi sana yalifanyika usiku ule, ambayo sitoweza kuyaandika hapa, maana sio dhumuni lake. Ila zoezi lilifanikiwa, ile mbegu ilitolewa ndani ya puto. Ile hali ya mwili kuchoma choma, nayo ikakoma. Ila nikabaki na maumivu ndani ya mwili, mfano nikimeza chakula, nilikuwa nahisi maumivu kila kinapopita hadi kufika tumboni. Tuliendelea kukaa pale kwa siku zingine tatu, alafu ndio tukaruhusiwa kuondoka. Ila kabla ya kuondoka, mtaalam akanisisitiza sana nisije kumtafuta tena Kisauti, na hata ikitokea amenipigia simu, basi nisipokee. Kiufupi alisema nikate kabisa mawasiliano nae, na pia ikitokea tumekutana uso kwa uso, nisikubali kabisa kumpa mkono. Maana dhamira yake juu yangu ni ya dhati sana, na haiwezi kukoma kirahisi.

Tukaanza safari ya kurudi nyumbani. Njia nzima hatukuongea chochote na Mshua. Tulivyofika home, baada ya chakula, Mshua akataka kuniweka kikao, Bi Mkubwa akakataa "Subiri basi apate hata nafuu, kwani anahama huyu". Mshua hakumjibu chochote, akanikata jicho, nikazuga kama sipo nao, nikaangalia pembeni. Baada ya siku tatu, hali yangu inaendelea kuimarika taratibu, Mshua akataka tuongee, Bi Mkubwa akakataa tena,

Bi Mkubwa: "Mimi baadae natoka, naenda kumwangalia mke wa Mzee K anaumwa, hamuwezi kufanya mazungumzo nikiwa sipo"
Mshua: "Tena ukitoka ndio vizuri, maana haya mazungumzo ni kati yetu sisi"
Bi Mkubwa: "Sitaki kuanza kuuguza upya hapa, nikiwaacha peke yenu najua kitakachotokea"

Mshua hakumjibu tena, akawa ametoka nje, akaelekea kwenye bustani na gazeti lake mkononi. Bi Mkubwa akaniambia kwavile toka nimefika pale, nimekuwa mtu wa kushinda ndani tu sababu ya kuumwa, basi nimsindikize huko ninapoenda, ili ninyooshe miguu. Nikawa nimetoka na Bi Mkubwa, siku tukaimalizia huko.

Kwavile hali yangu bado haikuwa vizuri sana, niliendelea kukaa nyumbani kwa wiki zingine mbili. Siku niliyowaambia nia yangu ya kurudi Dar, Mshua akasema "ushapona eeh? Sasa nina maongezi na wewe."

Safari hii, Bi Mkubwa hakuweka pingamizi. Mshua alikuwa amevaa suruali, akaenda kubadili na kuvaa bukta, Kisha akaniambia twende tukazungumzie nje. Nikabaki nashangaa tu, haya ni maandalizi ya mazungumzo au kuna kitu kingine hapa?... ..

Endelea hapa Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee
Dingi mtata
 
Back
Top Bottom