Mahondaw
JF-Expert Member
- Apr 9, 2013
- 67,252
- 168,563
Wabheja sana sis akee ngoja nitulie niisome vizure!!
Wapiii Tayukwa baby zu mtzmweusi Kigi Makasi Unforgettable mmash S V Surovikin
Mlishaisoma hii???
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wabheja sana sis akee ngoja nitulie niisome vizure!!
hahahaha yule mzee ni balaa sanaKy hana akili ya hata mmoja hapoo.....
We hukumbuki kuna episode Raymond alifulia akawa mwizi wa Magari ika hakuchukua mda mrefu akarudi Top
21st Portion:
...Nyumbani nilipokelewa vizuri tu, tena kwavile safari walijua nimekuja kuwaangalia sababu ya ugonjwa wa Mama, hivyo Mshua hakuwa mkaksi kwangu. Hali ya Mama ni kweli haikuwa nzuri, alikuwa haishi kulalamika maumivu na vichomi vya mara kwa mara. Mwanzoni walivyompeleka hospitali, alipewa tu dawa ambazo walidhani zingeweza kulitatua tatizo lake. Ila alitumia mpaka zikaisha, ila tatizo likaendela.
Nilivyofika ikabidi nishauri turudi tena hospital kwa uangalizi zaidi. Na kweli tulivyoenda tena, wale madaktari baada ya vipimo vyao, wakasema Mama anasumbuliwa na appendix na kwa stage iliyofikia, inatakiwa afanyiwe upasuaji haraka sana. Binafsi nikishasikia habari za upasuaji, huwa naichukulia kama habari nzito hata kama ni upasuaji mdogo. Ikabidi tushauriane kama familia nini kifatie, maana Kwa mazingira ya hospital ya pale kijijini, haikunipa amani kabisa kuwaruhusu wamfanyie upasuaji Mama. Mshua akabisha bisha sana pale, Mama nae asivyopenda kusafiri, akawa anasisitiza tufanyie pale pale. Kwavile watoto tuko wengi kuliko wazazi wetu, mawazo yetu ndio yakapita, kuwa upasuaji usifanyikie pale kijijini.
Baada mjadala huo kuisha, ukaibuka mjadala wa hospital gani aende. Nikashauri twende Bugando Mwanza, kwanza ni karibu lakini pia pale Mama atakuwa chini ya uangalizi mzuri wa Dada. Mshua akashauri twende Dar, kule huduma ni nzuri na kuhusu sehemu ya kufikia atafikia kwangu.
Analyse: "Kule Mama hawezi kuwa comfortable tofauti na kwa Dada"
Mshua: "Kwanini asiwe comfortable?"
Analyse: "Sasa unadhani Mimi na wewe tutaweza kumpa uangalizi mzuri kuliko Dada?"
Mshua: "Kwani mpaka tumuangalie Mimi na wewe?"
Analyse: "Sasa nani mwingine atamuangalia?"
Mshua: "Mkeo"
Analyse: "Mke yupi Mzee?. Sina mke mjini Mimi"
Mshua: "Huna mke, au huwa anakuja na kuondoka?"
Mama: "Nyie mkishaanza kubishana hapo, mpaka apatikane mshindi Mimi ntakuwa nishajifia hapa"
Ikabidi mazungumzo na Mshua yakome kwa muda. Tukaadhimia Mama aende Bugando. Tulisafiri nae mpaka kule, Mshua yeye alibaki. Kufika Bugando tukawaelezea tuliyoambiwa hospital kule kijijini, tukawapa na makaratasi ya vipimo vyao walivyofanya. Wakayasoma, kisha wakashauri afanyiwe vipimo upya, baada ya hapo ndio taratibu zingine zifatie.
Majibu ya vipimo vyao pale Bugando yaliporudi. Mama akaonekana hana tatizo appendix, isipokuwa kwenye mifupa ya nyonga uloto ndio umepungua (sababu ya umri), hivyo mifupa inasagana na kumletea maumivu. Akapewa dawa na ushauri wa baadhi ya vyakula anavyotakiwa azingatie, Kisha tukaruhusiwa. Hakufanyiwa upasuaji. Tukaendelea kukaa Mwanza, tukishangaa Jiji kidogo. Mshua akawa anataka turudi;
Mshua: "Ameshapewa dawa, fanya mpango arudi sasa"
Analyse: "Ngoja walau tufanye utalii kidogo kwa wiki hii kisha tunarudi"
Mshua: "Umenisikia vizuri nilichokwambia?. Nimesema fanya mpango Mama arudi, wewe hata ukiendelea kukaa mwaka, Sina tatizo"
Sister: "Lakini Baba, ungemuacha hata siku chache, huko anawahi kufanya nini?"
Mshua: "Hivi nyie sijui hata kama mnanielewa. Yani mnanipangia juu ya mtu ambae mmezaliwa mkanikuta nae?. Nimesema namuhitaji mke wangu"
Tulianza tunajadiliana kawaida tu, ila Mshua akaenda anabadilika mdogo mdogo. Kesho yake tukarudi nyumbani. Home Sweet Home.
Mshua: "Kwahiyo hawa madaktari wa hapa kijijini walikuwa wanataka kufanyia mazoezi mwili wako?"
Mama: "Yameshapita hayo, makosa hutokea"
Mshua: "Ni kwavile huo upasuaji haukufanyika tu, ila nadhani wangeomba uhamisho. Lakini hata hivyo lazima niwafate tukaambizane ukweli"
Analyse: "Hata ukiwafata itabadili nini, acha tu yapite"
Mshua: "Ili limepita, lakini maradhi hayaishi kuja, nataka siku nyingine wakiiona hii sura, wakumbuke notsi zote walizosoma hadi wakahitimu"
Nikamkubalia tu, then nikaingia jikoni kutaka kusaidia kupika maana hatukula njiani. Mshua akaniambia nijipikie mwenyewe tu, maana chakula cha Mama ameshakipika. Nilijua asingeniruhusu kula kile chakula, ila nikamjaribu tu;
Analyse: "Lakini wote tumetoka safari"
Mshua akacheka kwanza, "Yani ninunue mahitaji yote humu ndani, pia nikupikie. Huyu ni mke wangu"
Analyse: "Na Mimi ni mwanao"
Mshua: "Nani kakwambia?. Una uhakika gani wewe ni mwanangu?. Ukiachana na sisi kufanana maana hata Mimi na Mama yako tunafanana, una ushahidi gani mwingine?. Huyu ni mke wangu, ukitaka cheti Cha ndoa kipo, wasimamizi wapo. Wewe unachochote cha kuthibitisha wewe ni mwanangu?.
Mama yeye anacheka tu, wala hachangii chochote. Mshua najua alikuwa katika mood ya utani, lakini kwenye mood ile ile ya utani, nilikuwa na uhakika kile chakula siwezi kula, otherwise mood yake ingechange. Maana nakumbuka kipindi niko O level, Mshua alikuwa na kawaida ya kutupikia. Tukitoka shule tunakuta chakula tayari. Ilitokeaga nikasingiziwa mimba, Mshua alimaindigi kwamba anatupikia chakula (Mimi na mdogo wangu), tukishiba tunaenda kusumbua watoto wa watu. Alisema hatokaa atupikie tena maana tushakuwa vidume. Japa lile soo, baada ya mtoto kuzaliwa iligundulika sihusiki, ila Mshua aliendelea kunimaindi, yeye msimamo wake siku zote ilikuwa mwanamke hawezi kukusingizia mimba kama hujalala nae.
Nikaingia zangu jikoni kupika.
***** ****** *****
Siku zilisogea sana, nilikaa takriban mwezi na nusu. Mpaka jioni moja Mshua aliniomba tuongee mida ya usiku shughuli za nyumbani zikiwa zimepoa.
Siku hiyo hiyo, baada ya kula chakula cha usiku, tukaenda kukaa nje kwenye bustani. Tukiwa pale nje akaniuliza "Vipi unashida gani safari hii?"
Nilikaa kimya kwa muda, nilikuwa najaribu kutafakari, nianzie wapi kumuomba msamaha? Au nifunguaje haya mazungumzo?
Alivyoona nipo kimya sana, akabaki ananiangalia tu bila kusema chochote. Kisha akanyanyua simu yake, na kuniuliza:
Mshua: "Najua unatatizo, vipi niende ndani, alaf tuongee kwa njia ya simu?
Nikatabasam tu.
Analyse: "Nilionana na yule Mzee"
Mshua: "Aliniambia kuwa ulienda shambani kwake"
Analyse: "Kwanini hukuwa niambia yeye ni nani, au mipango uliyokuwa nayo juu yangu?"
Mshua: "Unadhani hiyo ingeweza kubadili kitu?"
Analyse: "Sio kubadili kitu tu, bali ingebadili maisha yangu yote"
Mshua: "Kwani sasa hivi huwezi kubadili hayo maisha yako?"
Analyse: "Sio kiwepesi kama ambavyo ingekuwa mwanzo"
Mshua: "Unapenda kufanya mambo kiwepesi au kwa njia ulizochagua wewe?
Analyse: "Hakuna anayependa kupita njia ngumu, ni matokeo tu ya machaguo yetu ndio yanaweza kutupitisha huko"
Akakaa kimya kwa muda. Alaf kabla hajaongea chochote, nikaona niutumie ule ukimya kumuomba msamaha.
Analyse: "Najua nimeku disappoint sana, nimefanya maamuzi mengi ambayo yameuvunja sana moyo wako na wangu. Ila...."
Kabla sijamalizia, akanikatisha.
Mshua: "Mimi ndio mwenye makosa hapa. Kama kuna anayetakiwa kuomba msamaha kwa kuivunja mioyo yetu, basi ni Mimi"
Akaendelea:
"Unajua katika maisha yangu, sikuwahi kabisa kufikiria kujiunga na jeshi. Ndoto na mipango yangu mingi ilikuwa sehemu nyingine kabisa. Mimi kujiunga na jeshi, ilikuwa ni ndoto ya Babu yako, yeye ndiye aliyenipush sana kuingia kule, japo nilikataa kwa nguvu zangu zote.
Kama ilivyokuwa kwako, nilivyomalizaga kidato cha nne, sikutaka kuendelea zaidi, nilitaka kuwa mfanyabiashara, ila Babu yako alitaka niendelee zaidi, ila kwa kupitia jeshini. Palitokea sintofahamu nyingi kati yetu, hadi ikapelekea Mimi kuondoka nyumbani na baadhi ya mifugo yake
Siku niliyorudi nyumbani, japo nilirudi na zaidi ya nilichoondoka nacho, ila Babu yako hakutaka kunipokea. Ilibidi wazee wa Kijiji wahusike katika kutupatanisha. Pamoja na adhabu ya bakora nilizopogwa mbele yao, Babu yako aliweka sharti la Mimi kujiunga na jeshi, hapo ndio ataweza kunisamehe kabisa na kunichukulia tena kama mwanae.
Sikuwa na jinsi, ilibidi nikubali, japo kutoka moyoni nilijenga chuki na yeye, kwa kunilazimisha kitu nisichotaka. Nilivyoingia jeshini, baada ya muda nikachaguliwa kwenda kozi Urusi. Hapo kidogo ndio nikaanza kulipenda jeshi. Kabla sijaondoka nchini, Babu yako akataka niache nimeoa kabisa. Hapo ukatokea ugomvi mwingine, maana sikuwa tayari kwa jambo lile kwa muda ule.
Nikaambiwa kama sipo tayari kuoa, basi inabidi niache nimechumbia. Pia nikakataa. Wakati najiandaa na safari, Babu yako akaniambia atamchumbia mwanamke kwa niaba yangu. Nikamwambia sitomtambua. Nikaondoka tukiwa hakuna maelewano mazuri.
Nilivyohitimu na kurudi Tz, nilikuwa sitaki kwenda kusalimia nyumbani, maana ningekabidhiwa mke ambae sio chaguo langu. Nilikuja kupata matatizo ya kiafya jeshini, kwa mara nyingine tena Babu yako akaingilia kati kinyume na matakwa yangu, nikajikuta rasmi nimetoka jeshini. Nilivyorudi nyumbani, mwanamke niliyechaguliwa na Babu yako, ndio akapewa jukumu la kuniuguza kwa ukaribu. Kitendo cha kuwa nae karibu kwa muda mwingi, kikajenga mazoea kati yetu. Nikajikuta naanza kumkubali."
Kufikia hapo nikaanza kujiuliza maswali, huyu mwanamke anayezungumziwa hapa ndio Mama yetu au? Ikabidi nimuulize,
Analyse: "Huyo mwanamke aliyekutafutia Babu, ndio Mama?"
Mshua: "Ndio. Kwani vipi?"
Analyse: (nikacheka kidogo) "Kumbe ulitafutiwa mke na Babu?"
Mshua: (akanikata jicho) "Acha dharau kijana, kuna baadhi ya mambo yako nje ya upeo ,huwezi kuelewa sawa?"
Nikawa, mpole, Kisha nikawa najizuia kucheka. Mwisho wa siku tukajikuta wote tunacheka 😅😅😅😅.
Akaendelea na story:
"Kabla afya yangu haijatengamaa vizuri, ile biashara aliyopanga kunipa Babu yako, ikapata ajali ya moto. Nikajikuta sina kazi, Sina kiwanda. Hapo ndio hasira juu ya Babu yako zikazidi. Nikaamua kuondoka pale kijijini, na kwenda mbali nao kuanzisha maisha yangu mengine, kivyangu, bila wao. Mwaka 82 nikaamua kumuoa rasmi Mama yenu, kipindi ana ujauzito wa dada yenu.
Majukumu yalipozidi kuongezeka, ikabidi nisogee sehemu za mbali zaidi ili kutafuta kipato. Niliamini umri niliokuwa nao, ndio wakati sahihi wa kupambana. Hakuna sehemu katika hii nchi ambayo sijafika. Nimenusulika kufa mara kadhaa huko migodini, nilishawahi kufukiwa hadi na kifusi. Huu mguu niliomia kipindi nipo jeshini, katika harakati za utafutaji, umeshavunjika tena mara kadhaa. Lakini pamoja na yote hayo, sikufikiria ku-make peace na Babu yako.
Sikuwahi kuwasiliana nae wala kurudi tena pale kwake. Kwa muda mrefu nilikuwa nikimchukia kwa maamuzi aliyoyafanya juu yangu, maana ni kama yaliniharibia maisha. Nilitamani sana angesimama upande wangu, au kusimamia yale niliyojipangia, na sio kunilazimisha kuwa vile anavyoona yeye inafaa.
Ila Mwenyezi Mungu ana njia nyingi sana za kutuonesha mambo ambayo sio rahisi kuelezeka. Hata uwe na moyo mgumu kiasi gani, akiamua kukufikishia ujumbe wake, basi jua atakufikishia tu, hata kwa namna ambayo hukuitarajia
Baada ya miaka mingi kupita, chuki na hasira juu ya Babu yako zikiendelea kuwepo. Alikuwa akinitafuta na kunitumia barua kupitia kwa wafanyabiashara waliokuwa wanatembea vijiji kwa vijiji, ila sikuwahi kumuandikia chochote. Ujumbe wangu nilikuwa naurudisha kwa mdomo tu, japo wahusika waliufikisha.
Mwenyezi Mungu akaamua kunionesha jambo. Mimi nilizaliwa kabla ya Uhuru wa nchi hii, ila macho yangu yangu yaliendelea kuwa gizani kwa muda mrefu.
Ile siku ambayo wewe uliyozaliwa, ndio siku ambayo macho yangu yalianza kuona. Ujio wako, ulifanya hasira zote nilizokuwa nazo juu ya Babu yako kufutika. Pengine usingezaliwa, ningeendelea kuwa kipofu, japo macho yangu hayakuwa na tatizo. Ningeendelea kuamini nipo sahihi"
Sikuelewa anamaanisha nini, ikabidi niendelee kumsikiliza. Hapo ndio akanifunulia kurasa za kitabu ambacho sikuwahi kukisoma kabla. Kurasa ambazo zilikipa thamani kubwa sana kile kitabu. Kurasa zilizofanya niyatazame baadhi ya mambo, kwa mtazamo tofauti kabisa....
Endelea hapa https://www.jamiiforums.com/threads...liyokutana-na-yule-mzee.2079499/post-46025799
Shukrani sanaa kwa kutoa muda wako kutusimulia story nzuri ya kutufunza na kutuburudisha piahh Analyse22nd Portion (Portion Finale)
.... Tuliongea mengi sana usiku ule. Ngoja nikusimulie machache ya alichonisimulia. Alisema hivi;
"Mpaka wewe unakuja kuzaliwa, kiuchumi walau nilikuwa vizuri kwa kiasi fulani. Yale maisha ya kwenda sehemu za mbali kukaa muda mrefu sababu ya utafutaji nilikuwa nishaachana nazo. Mimi kama mzazi, sikutaka kabisa kuwa kama alivyokuwa Babu yenu, sikutaka kuwa mkoloni na kulazimisha mfanye vitu ambavyo havikuwa kwenye maono yenu.
Nilikuwa naamini kama nitawasupport kwenye vitu mnavyotaka, basi kuna uwezekano mkubwa sana wa kupiga hatua nzuri kwenye maisha. Nilikuwa naamini nimepitia njia ngumu za utafutaji sababu ya kumsikiliza Babu yenu. Laiti ningefatisha njia zangu tokea awali basi nisingepitia msoto kama niliopitia.
Ulipoamua kukimbilia Dar es salaam, pale ndio alarm ililia kichwani kwa mara ya kwanza, ila nikaamua kuipuuzia, kwa kuangalia hata Mimi kuna kipindi kwenye maisha nilishapitia hali ile.
Kwa namna zangu ninazozijua Mimi, niliamua kukusupport katika njia uliyochagua. Kukupa Uhuru ndio jambo ninalojutia mpaka sasa. Niliamini utakuwa unajua kitu unachohitaji, na ndio maana niliamua kukusupport.
Nilikuja kushtuka ikiwa too late, kwamba upo kwenye harakati ambazo hata wewe mwenyewe hujui nini hasa unahitaji. Kibaya zaidi, ukajiingiza kwenye mapenzi. Mapenzi na utafutaji ni vitu ambavyo kamwe haviwezi kwenda pamoja, hata ungejaribu vipi. Ndio maana hata baada ya miaka michache ya kupambana kwako, bado ulirudi nyumbani mikono mitupu, kama ulivyoondoka.
Ile hela niliyokupaga kama mtaji, ilisababishwa na majuto niliyokuwa nayo. Sikujua nini nifanye kwa wakati ule, ndio maana nikakupa ile hela walau ukaendeleze ulichokuwa umeanza. Mimi kama Baba nilitakiwa kuwa mwongozo wako katika kila kitu, kitendo cha kukuachia mtoto uongoze, kimetuingiza wote shimoni.
Niliishi muda mrefu nikiwa na hasira na chuki kwa Babu yako, niliamini yeye ndio alivuruga maisha yangu na kuyafanya yawe magumu. Ila ujio wako, ulionesha ni Kwa kiasi gani sikuwa sahihi. Na pia ikawa wazi Babu yako alikuwa sahihi kwenye mengi.
Hakuwa perfect, ila kwa kiasi chake palikuwa na jema katika kila alilokuwa ananifanyia. Mfano mdogo angalia maisha yangu sasa hivi, vitu vingi nilivyofanya na kuhangaikia, sipo navyo. Hata nyie watoto, wote mmetawanyika, kila mmoja yuko anapojua yeye. Hata hizi mali pengine mpo mnazipigia hesabu, na pia sitokuwa na namna zaidi ya kuwarithisha. Nimebaki na kitu kimoja tu, ambacho hakuna anayefikiria kukichukua toka kwangu, nacho ni Mama yenu. Nimebaki na Mama yenu tu hapa. Cha kustaajabisha ni kwamba, Mama yenu nilichaguliwa na Babu yenu, ambae siku zote niliishi nikimlaumu. Sijui kama unanielewa?.
Nikatikisa kichwa tu kukubali.
Akaendelea:
"Siku niliyokutana na wewe ukiwa kama kibarua kule kwenye tangawizi, ndio siku niliyotambua ni Kwa kiasi gani nilimkosea Babu yenu. Maumivu niliyoyahisi moyoni mwangu,siwezi kuyaelezea. Na ndio yalinipa picha, ni kiasi gani nilimuumiza Babu yenu. Hakuna maumivu makubwa, kama pale unapochukiwa na mtu ambae upo tayari kufanya lolote kwa ajili yake.
Nasikitika jaribio la mfumo wa maisha niliokuwa nautamani, limefeli, kibaya zaidi limefeli katika hatua ambayo hatuwezi kurekebisha. Sasa ndio naamini, unaweza ukampenda sana mtu, ila katika namna ya kumuonesha upendo wako ukajikuta unaharibu. Na ubaya ni kwamba jamii haiangaliagi nia, inaangalia matokeo. Watahukumu kulingana na matokeo ya ulichofanya, hata kama nia yako ilikuwa njema.
Mpaka kufikia ile siku tunakutana kule, japo ukaribu na Babu yako ulikuwa umerudi, ila nilijihisi mkosefu upya. Ukaribu uliokuwa umerudi, ilikuwa ni ile naturally tu kama watu wazima tuliamua kusahau yaliyopita. Ila kwa jinsi nilivyojisikia siku ile nilipokuona, nilitambua kuwa natakiwa kumuomba msamaha Mzee wangu, namshukuru Mungu kwa kunipatia ile nafasi, sijui kama Babu yenu angekuwa ameshafariki ningejisikiaje. Hakuna mzazi anayependa kumuona mtoto wake akiteseka"
Kufikia hapa, Mshua akanyamaza kidogo. Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu, nilishuhudia Baba yangu akitokwa na machozi. Tulikuwa tumeangaliana, akainama chini, na Mimi nikaangalia pembeni. Hata kwenye misiba ambayo nilishawahi kuhudhuria na yeye akiwepo, sikuwahi kumuona akilia. Ila usiku ule Baba alilia mbele yangu.
Siwezi elezea nilijisikia vipi, ila itoshe kusema I felt so bad. Akaniambia "Kuwa strong haimaanishi hatuumii, ila pia chozi kutoka sio symbol ya udhaifu. Tuna wengi tunaowaangalia, ila ni wachache wanaotuangalia na kuyaelewa yale tunayoyabeba, hata kama hatujawaambia"
Baada ya ukiwa wa dakika kadhaa. Nikauvunja ule ukimya
Analyse: "Nadhani hata Mimi natakiwa kukuomba msamaha Mzee. Maamuzi yangu mengi ndio yametufikisha hapa Mimi na wewe"
Mshua: "Sio Kweli. Maamuzi yangu Mimi mengi ndio yametufikisha hapa. Mimi ndio niliamua uje duniani, Mimi ndio nilitakiwa kuendelea kukusimamia mpaka pale utakapokuwa kuwa tayari kuanzisha maisha yako. Sikutakiwa kukusikiliza, hakuna ubishi juu ya ilo. Niliteleza, na nimegundua nikiwa nimeshachelewa sana, sema wewe bado hujachelewa. Una nafasi kubwa ya kuweka mambo vizuri. Hasa yale yaliyonishinda Mimi."
Akaendelea;
"Unajua unapokuwa mtoto, unakuwa sharp katika vitu vingi sana, kasoro vision tu. Upeo na maono yanakuwa wazi kulingana na umri unavyoongezeka Kadiri unavyokua, ndivyo unavyong'amua makosa uliyokuwa ukiyafanya katika umri uliopita. Usikubali maono ya siku chache mbele, watakayokuwa nayo vijana wako, yaharibu mipango yako juu yao ya miaka mingi mbele. Ndio maana jukumu la mzazi ni kumsimamia na kumuongoza mtoto mpaka akue. Niliweza kukusimamia, ila nikashindwa kukuongoza"
Analyse: "Sawa nimekuelewa Mzee. Naamini kila kitu kitakaa sawa siku moja"
Mshua: "Sawa. Vipi huko mjini, mambo yako yanaendaje?"
Analyse: "Mambo ni magumu sana Mzee, kila siku napiga hatua moja mbele, mbili nyuma"
Mshua: "Na hivyo ndivyo maisha yalivyo siku zote, ugumu wa maisha upo ili kutukumbusha namna ya kuishi na watu au kuwa na shukrani pale tunapofanikiwa. Yakiwa mepesi sana tungejisahau"
Analyse: "Ni kweli, lakini, hao watu tunaotakiwa kuishi nao vizuri, mbona hawanijali kabisa?"
Mshua: "Hawakujali kivipi?"
Analyse: "Hata yule unayeona anaweza kukusaidia, nae hakupi kabisa ushiriakiano"
Mshua: "Bwana mdogo, siku zote nakwambia hakuna aliyezaliwa kwa ajili ya matatizo yako. Mtangulize Mungu siku zote. Hata yule unayeona anatakiwa akusaidie, na yeye kuna sehemu anahitaji kusaidiwa. Usipolielewa ilo, utamchukia kila mtu"
Akaendelea, "Hivi huwa unasali?".
Kwa macho makavu kabisa, nikamjibu "Ndio"
Akacheka, "Tabia ya mwanadamu huwa haijifichi, tokea umekuja hapa, hakuna siku ambayo hukukumbushwa na Mama yako kwenda kanisani. Unajiweka mbali sana na Mungu, hivi hizi Baraka anazokuombea Mama yako kila siku zitakufikia vipi?".
Nikabaki kimya. Akaendelea na punch zake;
"Jitihada bila Nuru, utazidi kupotea. Jiweke karibu na Mungu, kisha fanya mambo yako, ongea na watu, wapigie simu, omba kuonana nao hata kama hawataki, maana kwenye haya maisha tunawahitaji hata wale ambao hawatuhitaji"
Analyse: "Nimefanya hivyo sana Mzee, lakini hata wale waliokuwa rafiki zangu, hawapo tena karibu na Mimi kama zamani. Maisha yao yanaenda ila yangu yapo vile vile"
Mshua: "Ukisema hivyo unakosea sana, alafu utaonekana kama ni mbinafsi. Vipaumbele vinabadilika kadiri umri unavyosogea. Kama kuna watu ulikuwa unashinda nao siku nzima mkiongea na kufurahi, usitarajie wakishaoa/kuolewa au kuwa na watoto/familia, wataendelea kukupa uzito kama ilivyokuwa zamani."
"Hao unaowasema, jaribu siku kuwapigia simu alafu uone kama kuna atakayekukatia, mtaongea vizuri tu, na hata wasipopokea, waelewe. Hawajakutenga, ila kawaida umri unaambatana na majukumu. Ukilielewa ilo, hutoumia juu ya ukimya wao"
"Maisha yetu hayana tofauti na safari, mliopo kwenye safari moja ndio mtakutana ndani ya bus. Kuna bus la elimu, bus la kazi, bus la semina nk. Na kwenye hayo mabus, kila mmoja atashukia sehemu yake. Ikitokea mtu ameshuka, mtakie kila la kheri huko aendako maana safari yenu ya pamoja inaishia hapo. Ila ukitaka aendelee kuwepo, utajikuta unashukia njiani au unamlazimisha apitilize vituo. Huko mbeleni lazima hamtoelewana, kuna mmoja kati yenu hiyo safari ya kulazimishana itamchosha, maana utajaribu kumuonesha uzuri wa mandhari nje ya dirisha, ataangalia lakini mawazo yake yatakuwa kwingine, mwishowe atashuka. Sasa kwanini usingeacha ashuke wakati ule?"
"Mliyenae safari moja, hawezi kushukia njiani. Na atakayeshukia njiani huyo hampo safari moja."
"Unakumbuka kipindi mnakua jinsi wewe na ndugu zako mlivyokuwa na furaha hapa nyumbani?"
Analyse: "Ndio?"
Mshua: "Mbona siku ya harusi ya dada yako ulikuwa unacheza mziki kwa furaha sana, ingali ukijua sherehe ikiisha hatokuwa hapa tena?"
Analyse: (Kimya).
Mshua: "Kuna muda unatakiwa ufurahi pindi uwapendao wakiwa wanaondoka"
Akakaa kimya kidogo kisha akaniuliza: "Hivi ishawahi kutokea umekutana na mtu katika jambo fulani, mkapoteana, baada ya muda mkaja kukutana tena sehemu nyingine?"
Analyse: "Ndio, ishawahi kutokea Kwa watu niliosoma nao"
Mshua: "Nadhani walau utakuwa umenielewa sasa, mnaweza mkawa ndani ya bus moja, ila safari zenu ni tafauti. Uliyekutana nae shuleni, usilazimishe aendelee kubakia kwenye maisha yako, wakati kusoma mmeshamaliza."
Akaendelea; "Kwahiyo unapokuwa huko mjini, basi jitahidi sana unapokuwa kwenye mihangaiko yako. Japo unahitaji watu, lakini pia uwe selective kwa kiasi fulani. Pia usijiweke mbali sana na Mungu, kuna wakati anatushindia magumu mengi pasipo sisi kujua, jitahidi usifanye mambo yasiyompendeza".
Analyse: "Sawa Mzee, me nimekuelewa, nitajitahidi kubadilisha baadhi ya vitu na mitazamo yangu pia"
Mshua: "Itakuwa ni jambo la kheri, maana usipokuwa makini utashangaa miaka inaenda ila mambo yako yamesimama."
Analyse: "Ila Mzee, umeniambia nina wahitaji hata wale wasionihitaji. Ila hapo hapo unaniambia sitakiwi kulazimisha watu wabaki kwenye maisha yangu"
Akasikitika kidogo kisha akaniambia, "Kuna tofauti kubwa kati ya sehemu ya kujiegesha, na sehemu ya kuegemea. Usichanganye hizo sehemu mbili".
Nikabaki kimya tu namsikiliza huku najaribu kuabsorb maneno yake.
Tukaendelea kuongea mambo kadha wa kadha, lengo ikiwa ni kucatch up with our past. Mwisho wa siku nikamuuliza:
Analyse: "Ulisema nikirudi bila mwanamke, utaniozesha binti yeyote wa hapa kijijini, vipi kuna yeyote uliyenichagulia?"
Mshua (akatabasamu kidogo): "Siwezi kukuchagulia mke"
Analyse: "Kwann? Huoni utakuwa unaenda kinyume na alivyofanya Babu?"
Mshua: "Babu yako alijua naweza kurudi na mzungu, ndio maana akafosi kunitafutia mke. Ila wewe leta yeyote tu, sisi fresh" (Alafu akageuka nyuma kuangalia kama Mama yupo karibu)
Nikajikuta nacheka. Alaf akaniuliza
"Au unawaogopa wanawake huko mjini? Ukihitaji msaada wewe niambie"
Analyse: "Hao wote ambao niliokuwaga nao nimewapata vipi?
Mshua: "Siwezi jua, labda unatanguliza hela je?. Alafu zikiisha wanakuacha, unarudi huku kupumzika, tunajua unastress za maisha kumbe wanawake"
Wote tukaishia kucheka tu.
Mama akawa amekuja mpaka mlangoni, alafu akatuuliza "Mnahitaji chai?". Baba akajibu "Ndio"
Mama: "Analyse, njoo uchukue vikombe na chupa"
Mshua: "Siwezi kuandaliwa chai na huyu, haitokuwa tamu kama ikiandaliwa na wewe mke wangu"
Mama(akacheka) : "Sawa , basi ngoja niwaletee"
Mshua: "Ngoja tuje huko huko ndani, huku mazungumzo yameshaisha"
Mama: "Sawa"
Analyse: "Yani Mama na umri huo unakubali Baba anakuhadaa na vimaneno vyake?"
Mama: "Uongo wa mganga, ndio nafuu ya mgonjwa mwanangu" (Akacheka kisha akaingia ndani)
Nikafikiria kwa muda kidogo alafu nikamuuliza Mshua; "Kwahiyo chai isipoandaliwa na yeye haiwi tamu kwako?"
Mshua: "Mbona ulichofikiria, ni tofauti na ulichoniuliza?"
Nikastaajabu, anaongelea nini huyu Mzee? Amejuaje kama nilichomuuliza sicho nilichofikiria?. Ila kabla sijafungua mdomo wangu akaniwahi:
"Kuna muda binadamu wote ndivyo tulivyo"
Nikabaki namwangalia tu. Akanyanyuka, akanisogelea kidogo. Alivyofika usawa wangu, akaniambia "Unapokuwa mtoto, unatakiwa kumsikiliza mzazi wako. Unapokuwa mtu mzima, mnatakiwa kusikilizana wewe na mzazi wako, maana upeo wako pia unakuwa angavu na umekomaa. Ila kadiri miaka inavyozidi kusogea, wazazi wanatakiwa wakusikilize wewe mtoto wao, maana akili yao inakuwa tayari imechoka. Uwe umejiandaa au hujajiandaa, kuna siku nitatakiwa kukusikiliza mwanangu"
Akanipiga piga kwenye bega, kisha akaingia ndani.
Niliendelea kubaki pale nje kwa dakika kadhaa, nikifanya marejeo ya mazungumzo yetu. Kuna kitu nikagundua alikiongea kwa uwazi, ila nilichelewa kuking'amua. Kilivyokuwa wazi kwangu, nikajikuta nasikitika kwa tabasamu.
Nikanyanyua vitu na kuelekea ndani, tayari kwa kuanza chapter mpya ya maisha yangu.
*******************************************
Wakuu, kama ilivyo ada ya simulizi zangu. Lengo la hii story ilikuwa ni kuelezea mazungumzo yangu na yule Mzee wa Kongowe, niliamua kujumuisha na matukio yangu mengine walau kuweka uzito. Nashkuru kwa uwepo wenu tokea mwanzo mpaka sasa. Panapo majaaliwa, tukutane tena kwenye simulizi zijazo.
Wasalaam,
Analyse
Daah kweli tunajifunza kupitia wazee wengine... mi mzee wangu sijawahi kuongea nae lolote la maana yani tunakutana tu juu kwa juu kila mtu na mishe zake
Karibu tena mrembo. Tuombeane afya.
Nashkuru kwa baraka zako [emoji120]
Tokea story imeanza, kila anayeomba namba, akinipigia anaulizia waganga [emoji28][emoji28][emoji28]
Mzee Dingi na mstaafu sijawahi kabisa kuonana nao tena. Nilishawahi kukutana mara moja na Mzee Kidevu, sikutaka hata story nae, nikamkimbia tu.
Mzee Kesho Yetu nilikutana nae mara mbili, mara ya kwanza hatukuongea chochote, mara ya pili nilikuwa kwenye kikao cha harusi, akaja ili wajumbe wamuone, yeye ni MC
Acha basi hawapost wale 🙆🏼♂️🙆🏼♂️🙆🏼♂️Endeleeni na zile zingine, kuna story ya akinyi, Babu yangu mshikaji wangu, shada kwenye makaburi nk 😅😅😅😅
Haya sawa 🥹Wapo busy na majukumu, wataanza kupost soon 😅😅
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Antonnia hizo namba unazoomba huko PM unataka kunifanyaje???Baada ya kufika tamati kwa story hii, naomba kuweka maangalizo yafuatayo:
1. Huwa nasimulia story zangu kwa vipande. Na kila kipande kinabeba kisa kimoja ambacho huwa nimeamua kukiwasilisha kwenu. Kusimulia kwangu kwa vipande, haimaanishi matukio kwenye visa ambavyo nimeshawahi kusimulia au nitakayokuja kusimulia huwa yapo separate. Ni mambo yanayotokea simultaneously.
2. Dhumuni la kusimulia haya matukio ni ili, tujifunze, tuburudike au zitusaidie kupoteza muda. Ndio maana kuna sehemu tunacheka, tunahudhunika au kuwa neutral.
3. Haya matukio ni past life, ndio maana napata courage ya kuyasimulia bila shida. Tokea nimeanza hii story, nimepokea requests nyingi sana za wanaoomba either namba za waganga au niwaunganishe na waganga. Wakuu, sina connection yoyote na waganga kwasasa, na pia nisingependa kurudia hayo maisha. Kuniomba nikutafutie hizo namba au nikuunganisje na timu ya wale wazee, hapo ni kujaribu kunirudisha kwenye maisha ambayo nilishatoka.
Ukija PM njoo na mishe zingine, niko social na siwezi kujibu ovyo au kutoa lugha kali, lakini hiyo isiwe kigezo cha kunipush.
[emoji109][emoji109][emoji109][emoji109][emoji109]
Nimeshajibu kwenye comments za huko juu mkuuSawa mkuu Kama umemaliza, lakin hujatuwmbia ule msala wa mstaafu uliishia wapi
Vipi mzee kesho yetu na mzee dingi, mliishia wapi au hujawah kukutana nao Tena? Mana nakumhuka kuna sehemu ulisema mpaka Leo mzee dingi anakumind