Sijawahi kumsikia MAKONDA akiongea Kiingereza

Unataka aongee kiingereza kwani anaowaongoza ni wazungu?
 
Mmh ila wewe bwana..🤣🤣🤣😆
 
Ila wewe sina adabu kabisaa
 
Anaongea kiingereza cha tabu sana. Akiongea kiingereza na mtu asijejua kiswahili itakuwa ngumu kuelewana, maana kiingereza chake kinaeleweka kwa mtu anayejua kiswahili. Mfano, kama umekaa badala ya kukumbia stand up ili usimame, atakwambia stop.

Msemaji mkuu wa serikali ya Tanzania Dr. Gerson Msigwa akinadi bandari kavu ya Kwala mkoa wa Pwani


View: https://m.youtube.com/watch?v=dW3OOkY2sVY
 
Makondo na kingereza wapi na wapi wakati hata jina siyo la kwake. Yeye anaitwa Daud albert bashite.
 
....kutema yai si mchezo. ni adhabu inayosulubu mioyo ya wanasiasa na watawala wengi sana. imagine una hela, cheo, na umaarufu, ila ikifikia hatua ya kupiga un,'gen'ge, Unaanza vizingizio ooh, eti kiingereza sio akili, akili ni kujua mambo.

kwani lugha sio miongoni mwa mambo?...tusijifariji lugha za kimataifa bado tunazihitaji ili kujifungasha kwenye utandawazi na teknolojia.
 
Mleta mada hebu weka Uzi wako Kwa kiingereza kilichonyooka ili wajuvi wa hii lugha tukupime kwanza wewe kama unaimudu
 
Viongozi wa Urusi,India,Korea,japan,nk umewahi kusikia wanaongea kiingereza wanapotekeleza majukumu yao?au umesikia kiingereza ni almasi?

Mama na baba yako wanaoongea kiingereza wamewahi kuwa hata wenyeviti wa mitaa??
 
Mmeanza nongwa eeeh🤣🤣
 
Ni lazima kuongea kiingereza?
 
Tuma kwa namba hii


View: https://youtu.be/mJ4wUQ8THhc?si=FXpCCkugb2-_ihQX
 
Ni lazima kuongea kiingereza?
ulazima unategemeana mazingira, sasa unatarajia nani akuongelee mambo muhimu yanayokuhusu ikiwa haujui lugha ya mwenzako?

mfano, wewe ni kiongozi una kikao cha wawekezaji, utaita wakalimani kila hatua?

mnasemaga china imepiga hatua na haijawahi kutinga kwenye ukoloni wa lugha... na tujiulize ni kwanini sasa wanajifunza kiswahili kwa kasi. kwanini hawajatosheka na kichina chao?'

mnadhani kutojua lugha za wengine ni uzalendo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…