Sijawahi kuona haya mashirika ya umma yakitangaza kazi

Peleka barua na uzoefu wako wa kazi moja kwa moja hata kama hawajatangaza pale mlangoni kwa mlinzi juu ya bahasha andika kwa gavana bank kuu halafu jieleze humo na kuacha macontacts yako. Huwezi jua japo ni nje ya utaratibu
Niliwahi kufanya km ulivyosema nikapeleka barua nikampa mlinzi getini, siku zikasogea siitwi ila boss wa ofisi nilikua namfahamu ni Rafiki na brother yangu waliwahi kusoma pamoja miaka yao basi brother akapiga simu dogo ameleta barua hapo ila hajaitwa bwana wee nikaambiwa kesho njoo ofisini tuhakiki km kweli ulileta barua, kesho yake nikaenda ofisini boss nikamkuta akaitwa HR kisanga kikaanzia hapo, nikaulizwa na HR (mdada wa makamo) barua yako uliiacha wapi na jina lako ni nani nikataja, HR akaenda kupekua barua hola akarudi akasema barua yako haipo, naomba huu ushauri muuache km ulivyo..
 
Walikuambiaje baada ya barua kukosekana?
 
Walikuambiaje baada ya barua kukosekana?
Yaan hapo watu washaingia kazini interview ishapita ndio nikaitwa baada ya brother kumpigia simu, HR akaitwa boss akamueleza akaniuliza jina akaniuliza barua ulikabidhi wapi baada ya kujibu akachukua jina akaenda kuangalia kwenye barua alizopokea, akarudi akasema barua yangu haipo na nafasi zilikua tayari zishajaa walitaka watu 5 tu na walishapatikana kwa hio nikarudi nikaambiwa next time nisiache barua getini kwa mlinzi may be niache kwa secretary pale mapokezi nimwelezee anaweza akanielekeza wapi kwa kupeleka sio mlinzi, mlinzi hajui mambo ya ofisi ye kazi yake ni kulinda usalama tu basi
 
Kijana jaribu kufanya tafiti ndogo ndogo achana na maneno ya vijiweni.. BOT wanatangaza nafasi sana tu.. wameajiri vijana wadogo wadogo wengi sana siku za hivi karibuni.. kuanzia Banks supervisor, HR, IT, Madereva, Watu wa masoko ya fedha, Finance officers, engineers.

Na hakuna mtoto wa kigogo wala, ni washkaji tu nawajua watoto wa wakulima
 
Mlinzi alienda kuchambia barua hiyo๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜…
 
Mlinzi alienda kuchambia barua hiyo๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜…
Hatari sana mlinzi alinifanyia ovyo yaan sina hamu nilipata funzo, usiache barua kwa mlinzi peleka mapokezi acha kwa secretary na umuelezee vizuri maana hawakawii kuitia kwenye 'dust bin'
 
taasisi za kiserikali zinajiendesha zenyewe chache sana zinazotangaza
 
Ni ya wakubwa Hawa ambao kitumbua Chao Cha Bandari kinataka kuota nyasi wamefura huko..

Wewe endelea kutumiwa na hao Jamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ