Sijawahi kuona nchini yenye amani na usalama kama Zambia

Sijawahi kuona nchini yenye amani na usalama kama Zambia

Habari zenu wana JF wenzangu, kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Katika zunguka zunguka yangu yote katika nchi mbali mbali nikianza na nyumbani Tanzania, kwa kweli sijawahi kuona nchi yenye amani na usalama wa hali ya juu kama Zambia.

Kwa wale wenzangu waliowahi kuikanyaga nchi hii bila shaka wataleta ushuhuda wa hiki ninachoongea. Zambia ndio nchi ambayo unaweza kununua kitu njiani huku basi linakwenda, cha ajabu kama ulitangulia kumpa muuzaji hela kubwa, basi muuzaj atalikimbilia hilo basi hadi ahakikishe amekurudishia chenji yako, kitu ambacho kwa nchi nyingi including Tanzania hakipo. Yani ukinunua kitu ukatangulia kutoa hela na basi likaanza kwenda, basi uhesabu ushapigwa, maana muuzaji hatokupa chenji yako, badala yake atakimbia zake akijua hauna uwezo wa kutoka ndani ya basi linalotembea ili umkimbize yeye.

Hiyo tisa, kumi ni pale unapofika Lusaka katika ile stand yao kuu inayoitwa Kaunda bus terminal. Aisee pale utakuta wale jamaa wanaochenji hela wakiwa na maburungutu ya dola za mia mia, hamsini hamsini nk wameziweka mezani kwa ajili ya kuwachenjia wasafiri mbali mbali wanaoshukia pale kutoka nchi mbali mbali. Lile soko liko wazi masaa 24, na hakuna anaeingia kuwasumbua au kuwaibia wale wanao anika madola yao hadharani kwa ajili ya chenji. Kwa Tanzania ukiwa na sh laki 1 ukienda kariakoo kununua kitu, basi muda wa kulipa inabidi usogee kona kidogo ndo uchomoe hela, tena kimagutu magutu unaangalia huku na kule ili usije fatwa na vibaka. Kwa Zambia hiyo haipo.

Kuna siku nilishuka pale na mzigo wa maana, kwa vile nina mjomba wangu anaishi pale ikabidi na mimi nichukue hata wiki moja ili niuze mzigo wangu mdogo mdogo. Aisee nilishangaa kuona jamaa amekuja na zaidi ya dola 2500 tena kaziweka mfukoni tu, hana wasi wasi wowote mpaka pale town lilipo duka la mjomba wangu, akanipa changu na mimi nikamkabidhi mizigo yake akaita gari akapakia akaondoka.

Mimi mcheche ukanishika nikifikiri labda kuna watu wametuona kwahiyo wanaweza kuja kutupora yale madola aliyoniachia jamaa, mjomba wangu akacheka na kuniambia kuwa hapa watu huwa wanatembea mpaka na dola elf 7 town, itakuwa mimi wa dola elf 2 bwana.

Ki ukweli style ya maisha ya pale niliipenda sana haswa kwa upande wa usalama, sema ndo hivyo sehemu ambayo haukuanzia maisha ukisema uende kuanza tena itachukua muda kutoka.

Hizi nchi zetu zingine usalama ni zero, mpaka inafika kipindi wengi wetu tunakuwa tunatembea na kadi za bank tu mifukoni, ili kuepusha wizi wa fedha unaoweza kutokea wakati wowote. Mpaka sasa sijajua ni mbinu gani wanayotumia hawa jamaa kudhibiti wizi na ujambazi katika maeneo mbali mbali ya mji wa Lusaka na Zambia yote kwa ujumla.
kma ni suala la kuonyesha maburungutu ya fedha chunya,mkwajuni ,saza na tunduma mbona kawaida tu. Kurejeshewa chenji incase gari limetangulia pande za tukuyu kiwira ni kawaida. Changamoto inakuja uaminifu ni zero hapa kwenye jiji la makala plus panya road attacks
 
Mr.Dudumizi umehamia na kuwa balozi wa Amani wa Zambia,Ile habari ya nchi yako ni kisiwa cha amani imeishia wapi🥱
Habari ipi hiyo mkuu? Afu tofautisha amani na usalama. Hivi ni vitu viwili tofauti ndio maana hata maneno yake pia yako tofauti.

AMANI: Mfano naweza kusema Burundi sasa hivi ni nchi ya amani kwa maana hakuna vita.

USALAMA: Ila pia naweza kusema Burundi hakuna usalama, kwa maana watu wamekuwa wakiuwawa, kutekwa, kufungwa, kubambikiwa kesi, kuingiliwa usiku majumbani kwao, kuporwa barabarani, kupigwa hovyo nk.

Kwahiyo Tanzania ni nchi ya amani, ila kwa upande wa usalama tunalega lega kidogo. Sema jeshi letu la polisi limejitahidi kurudisha usalama kwa kiasi kikubwa baada kuyangamiza yale magenge ya panya road nk.
 
kma ni suala la kuonyesha maburungutu ya fedha chunya,mkwajuni ,saza na tunduma mbona kawaida tu. Kurejeshewa chenji incase gari limetangulia pande za tukuyu kiwira ni kawaida. Changamoto inakuja uaminifu ni zero hapa kwenye jiji la makala plus panya road attacks
Tunduma burungutu unaweza kutembea nalo ukiwa maeneo ya mpakani pale border kwa sababu askari polisi na wa uhamiaji ni wengi sana maeneo yale. Ila ukitoka kidogo tu nje ya hapo. Watu watakusaula hadi nguo ya ndani wakuache kama ulivyozaliwa.
 
Back
Top Bottom