Sijawahi kuona nchini yenye amani na usalama kama Zambia

Sijawahi kuona nchini yenye amani na usalama kama Zambia

Sudan kaskazini naona ni mara 100, achilia mbali kuiba huku hata mtu akusaidie kitu na umuachie tip ya dola 500 hapokei anakushukuru tu unaendelea na mambo yako
Ya mkuu Nigeria ni nchi ya kwanza yenye idadi kubwa ya watu, na asilimia kubwa ya raia wake hawana kazi. Kwahiyo ili mtu uweze kuishi na kujikimu kimaisha ni lazima ujiongeze kwa njia mbali mbali kama vile rushwa, utapeli, ufisadi nk.
 
Sudan kaskazini naona ni mara 100, achilia mbali kuiba huku hata mtu akusaidie kitu na umuachie tip ya dola 500 hapokei anakushukuru tu unaendelea na mambo yako
Kumbe Sudan nayo ni miongoni mwa nchi zenye raia waaminifu sana mkuu!!
 
Habari zenu wana JF wenzangu, kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Katika zunguka zunguka yangu yote katika nchi mbali mbali nikianza na nyumbani Tanzania, kwa kweli sijawahi kuona nchi yenye amani na usalama wa hali ya juu kama Zambia.

Kwa wale wenzangu waliowahi kuikanyaga nchi hii bila shaka wataleta ushuhuda wa hiki ninachoongea. Zambia ndio nchi ambayo unaweza kununua kitu njiani huku basi linakwenda, cha ajabu kama ulitangulia kumpa muuzaji hela kubwa, basi muuzaj atalikimbilia hilo basi hadi ahakikishe amekurudishia chenji yako, kitu ambacho kwa nchi nyingi including Tanzania hakipo. Yani ukinunua kitu ukatangulia kutoa hela na basi likaanza kwenda, basi uhesabu ushapigwa, maana muuzaji hatokupa chenji yako, badala yake atakimbia zake akijua hauna uwezo wa kutoka ndani ya basi linalotembea ili umkimbize yeye.

Hiyo tisa, kumi ni pale unapofika Lusaka katika ile stand yao kuu inayoitwa Kaunda bus terminal. Aisee pale utakuta wale jamaa wanaochenji hela wakiwa na maburungutu ya dola za mia mia, hamsini hamsini nk wameziweka mezani kwa ajili ya kuwachenjia wasafiri mbali mbali wanaoshukia pale kutoka nchi mbali mbali. Lile soko liko wazi masaa 24, na hakuna anaeingia kuwasumbua au kuwaibia wale wanao anika madola yao hadharani kwa ajili ya chenji. Kwa Tanzania ukiwa na sh laki 1 ukienda kariakoo kununua kitu, basi muda wa kulipa inabidi usogee kona kidogo ndo uchomoe hela, tena kimagutu magutu unaangalia huku na kule ili usije fatwa na vibaka. Kwa Zambia hiyo haipo.

Kuna siku nilishuka pale na mzigo wa maana, kwa vile nina mjomba wangu anaishi pale ikabidi na mimi nichukue hata wiki moja ili niuze mzigo wangu mdogo mdogo. Aisee nilishangaa kuona jamaa amekuja na zaidi ya dola 2500 tena kaziweka mfukoni tu, hana wasi wasi wowote mpaka pale town lilipo duka la mjomba wangu, akanipa changu na mimi nikamkabidhi mizigo yake akaita gari akapakia akaondoka.

Mimi mcheche ukanishika nikifikiri labda kuna watu wametuona kwahiyo wanaweza kuja kutupora yale madola aliyoniachia jamaa, mjomba wangu akacheka na kuniambia kuwa hapa watu huwa wanatembea mpaka na dola elf 7 town, itakuwa mimi wa dola elf 2 bwana.

Ki ukweli style ya maisha ya pale niliipenda sana haswa kwa upande wa usalama, sema ndo hivyo sehemu ambayo haukuanzia maisha ukisema uende kuanza tena itachukua muda kutoka.

Hizi nchi zetu zingine usalama ni zero, mpaka inafika kipindi wengi wetu tunakuwa tunatembea na kadi za bank tu mifukoni, ili kuepusha wizi wa fedha unaoweza kutokea wakati wowote. Mpaka sasa sijajua ni mbinu gani wanayotumia hawa jamaa kudhibiti wizi na ujambazi katika maeneo mbali mbali ya mji wa Lusaka na Zambia yote kwa ujumla.
Wazambia nadhani ni utamaduni wao... Hata habari kubagain kushushushiwa bei wakati wa manunuzi hawanaga sana.
Ni watu wa tofauti ukilinganishaa na sisi wabongo kilife
 
Mr Dudumizi usitumie nguvu kuandika vitu usivyovijua kumuelewesha anaekijua nakwambia tena majambazi walikua wanakuja Tunduma kufanya uharifu na kurudi upande wa Nakonde ambako ndio Zambia walikua wanajificha huko ila baadae kutokana na ushirikiano wa Nchi mbili ilikua rahisi kuwakamata na wengine walikua Watanzania walionyeshwa pale Hospital ya Rufaa mbeya miaka ya nyuma huko mimi mara nyingi naandika vitu nilivyoviona ni vile nimesahau mwaka wenyewe waliuawa karibu majambazi saba walikua hatari sana mpaka ile tabia ya watu wa Nakonde kulala na hela nyumbani au kwenda kwake kubadilisha dola huo mfumo ulikufa kabisa...
Mkuu Isanga family mbona hoja yako nimeshaijibu kitambo kwenye post namb #287. ikichek utaiona.
 
Wazambia nadhani ni utamaduni wao... Hata habari kubagain kushushushiwa bei wakati wa manunuzi hawanaga sana.
Ni watu wa tofauti ukilinganishaa na sisi wabongo kilife
Ya ni kweli mkuu, jamaa wako smart sana aisee.
 
So ni majambazi ya Tanzania ila yanajificha zambia...!! Aisee tz noma sanaa
Ya hao wako wengi. Tatizo mwana hakufafanua kama hao majambazi walikamatiwa Zambia au Tanzania. Ni ngumu kwa mimi kuamini tu moja kwa moja kama polisi wa Tanzania waliingia Zambia kuwakamata hao wahalifu. Ni kwa vile jamaa alisikia tu kwenye news akajua kuwa hao wahuni walifuatwa wakakamatwa na polisi wetu. Ila kwangu mimi naona hao wahalifu walikamatwa na polisi wa Zambia kwa kushirikiana na mamlaka ya Tanzania, kisha wakakabidhiwa kwa polisi wa Tanzania pale mpakani Tunduma. Polisi wa Tanzania nao wakafanya yao kama kawaid yao.
 
Ya umenikumbusha hayo hayo ya Burundi mkuu. Mwaka 1995, wakati huo serikali ilikuwa chini ya raisi Ally Hassani Mwinyi majeshi hayo hayo ya Burundi yalivuka boda kuingia Tanzania kwa lengo la kuja kuwaangamiza waasi wa Burundi waliofanya maafa kwa askari wa Burundi na kukimbilia Tanzania. Basi bwana warundi wakapiga hatua ya kwanza ktk ardhi yetu wakaona kimya, wakapiga ya pili kimya, ya tatu na kuendelea kimya. Basi wakaona kumbe Tanzania iko wazi namna hii haina hata jeshi la kuangalia mipaka yake, jamaa wakazidi kuingia tu kwa wingi katika ardhi ya Tanzania na vifaru vyao wakiamini kuwa wako katika ardhi ya shamba la bibi hakuna atakaewafanya kitu. Basi ndugu wale warundi walishtukia kitu kimeanguka ghafla kati kati yao, wakati wao wanatafakari ili kujua kitu hicho kimetokea wapi, ghafla wakajikuta tayari washanyanganywa silaha zao zote na wanaamrishwa warudi huko huko walipotoka bila silaha hata moja. Baada ya kuhakikisha jeshi la Burundi lote lishaingia ktk ardhi yao, jeshi letu lilitupa kiazi kimoja tu cha kuwaonya kwamba wasirudie tena ujinga ule. Unaambiwa hilo eneo lililotupwa kiazi hadi leo hakujawahi kuota chochote, yani eneo limebaki wazi kama ukumbusho.
Duh ndo maana Kagame alifyata kwa Kikwete. Maana anaifahamu Tanzania vizuri zaidi ya watanzania wenyew wanaoshinda kweny vijiwe vya kahawa. Jeshi la Tanzania halijawahi kushindwa ktk oparation yoyote tangu kuumbwa kwa dunia hii.
 
Jeshi letu halijawahi kushindwa katika oparation yoyote ya moja kwa moja.

Ni umahiri, umakini, ujuzi, uzoefu na jitihada za jeshi letu ndio zilizoweza kuleta ukombozi katika nchi za Zimbabwe, Msumbiji, Namibia, Kaburu, Comoro na kwengineko. So Kagame asingeweza kuthubutu kutuletea unyonge kama ule anaouleta kwa Congo na wakati mtoto wetu mwenyew hayati Ngulunziza wa Burundi alimshindwa.
 
Hata Tunduma pale Mkuu kwenye ishu ya kubadili fedha palikuwa na usalama wa kutosha mtu yupo na mamilioni kwenye kifungashio na hakuna mporaji ila ni miaka minne tangu nitoke pale sjui kwa ss hali ikoje
 
Tatizo la Tunduma usalama upo katika maeneo yale ya kubadilishia hela tu, kwa sababu maeneo hayo yamezingirwa na askari polisi wengi pamoja na askari wa uhamiaji. Ila utapomaliza kubadili hela zako na kutembea mwendo wa dakika 10 tu kutoka eneo la mpakani, lazima ushikishwe adabu na vibaka uchwara.
 
Miaka ya nyuma watu wametekwa sana kwa njia hiyo yaani anapanda bus la Lusaka huku kabadili lundo la hela kaweka kwrnye begi Wezi walikua wanaongea na wana usalama wasio waaminifu upande wa mpika huko bus linasimamishwa unaambiwa wewe ushuke na begi lako una tatizo la Passport wale polisi na wale wahuni walikuja kukamatwa siku moja dereva wa bus alipogoma kushusha begi la abiria wakashushie kituo cha polisi au begi libaki waende na mtu wao maana palikua na dola za kutosha baadae walipostukiwa wengine wakakimbia ila walikuja kuksmatwa na kuishia jela na hizo mambo ndio ukawa mwisho wake...harafu ramani ilikua inasomwa uhamiaji wao wanamlazimisha msafiri aonyeshe hela ya safari wengine wanaonyesha nyingi ili agongewe kumbe unaingia kwenye mtego wa kuibiwa...
 
Duh kumbe miaka ya nyuma ilikuwa balaa, ila askari uhamiaji wengi wanatamaa. Nafikiri huwa wanakamilisha ule msemo wa kila mtu ale kwenye kazi yake, na wanakula kweli 😀😀😂😂
 
Wale walifuta 000 zile ile hela haina thamani hata kuizidi Tsh ila kuelewa hapo kwa watu wengine mtakesha...
Mzee naelewa na najua maana ya 1 Kilometre is equal to 1000 metres Mzee. Kuna mtu aliyekimbia 1 km then akamcheka aliyekimbia 1000 metres akidai amekimbia umbali mfupi.
 
Naamini ipo siku ntatembelea nchi zetu jirani hizi aisee.

Ni majirani zetu ila daah tupo tofauti saana.

Mfan kipindi cha nyuma kidg mji wa tunduma ulikua unasifika kwa wizi, udokozi, ujambazi, magendo na uhalifu mwingine lakini cha ajabu ndo hapo karibu na hiyo Zambia isiyo na hizo sifa. Na wakazi wa hapo wengi shughuli zao hufanyia hiyo nchi jirani!!.

Ama kweli jasiri haachi asili, pamoja na kukaa na uaridi bado hatujanukia.
 
Back
Top Bottom