Siku 2 ofisini, mama Stergomena Tax naye kafanya kosa lilelile la Mulamula

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
6,661
Reaction score
21,656
Nimeshtuka Sana juu ya hiki kilichotokea.

Ujumbe wa Bunge la Marekani umekuja Afrika mashariki ukiongozwa na senator John Inhofe, umeenda kwanza Kenya ukaonana na Ruto Kisha ukaruka kwenda Kigali kukutana na Kagame, yaani umetupita hapa katikati Kama sisi sio watu, Mama hapendi hii kitu, wanakuwa Kama hawajaiona Royal tour, waziri changamka.

Mama anataka kuturudisha kwenye ramani ya Dunia US na Ulaya kituo Chao kiwe Tanzania kwanza, nasi pia tujulikane kwao.

Sio waziri anapokelewa na Biden halafu rais anapokelewa na Mange.
 
Kuna ukweli ndani yake..
Lakini vichwa box watakushambulia
Maana yake TZ haina uzito kwa nchi za East Africa, ni kama li Tembo fulani lizembe na lizito kuelewa au kupiga nalo dili.......
Tuliogopa kwenda Msumbiji, Rwanda akajitosa, Tukajipelka na kiherehere Congo kwenda kuwavurugia dili zao, tukaambulia kichapo na vifo, tukaufyata na kufunga virago...
Kuna tatizo hapa....
 
Mwanzoni nilitaka kuandika huu ni ujinga,lakini baada ya kupitia na kutazama katika jicho la tatu nikagundua huu ni moja ya nyuzi bora kabisa lakini kwa watu wenye akili kubwa.
 
Ing'otanyi Kagame
 
Kosa lake lipi?
 
Mkuu MSAGA SUMU, sasa huu ni ujinga tuu!. Anayeamua aende wapi ni mgeni mwenyewe!, anayepanga safari ni msafiri mwenyewe na sio mwenyeji, sasa hapo kosa la Dr. liko wapi?!, tusiwashobokee sana hawa jamaa, usikute ni hawa ndio walimnanilii yule naniliu wetu kama nilivyowahi kuuliza hapa US/EU Walimtoa Saadam, Ghadafi na Mugabe? Je, wanapanga kumtoa Rais Magufuli madarakani? Watanzania wazalendo tutakubali?
P
 
Wanajua aina ya rais tuliyenaye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…