Siku aliyozaliwa Yesu bado Kitendawili

-Hawa/eva siyo mwanamke wa kwanza inamaana adam alikua na mke zaidi ya mmoja hata kama siyo kwa kipindi kimoja.
- Daudi alichepuka waziwazi
-Joshua aliua watu wengi kisa kuipata nchi ya ahadi, badae unakutana na amri usiue 😀😀
 
Siku zikipatikana page zilizotolewa kwenye biblia basi tutaenda sawa

Kitabu cha Enoch wamekipiga chini makusudi
 
Ukiwaambia wakariri dini, kuwa hizi ni biashara kama biashara nyingine wanaona umekengeuka
Dini ni biashara,ukichukua hata mia kwenye kile kikapu ndo utajua pesa na huyo mungu wa kanisani nani mkuu[emoji23][emoji23]utapigwa kipigo mpaka utahisi sio kanisa ni polisi

Mapadre wanazini,one time kabla sijaacha tungi shakunywa nao na masister bia sehemu flani pande za tegeta,anyways sitaki kuzama deep ila dini ni siasa na biashara period .Mungu wa ukweli hayupo kwenye dini yeyote anatafutwa na mtu binafsi ndo SIRI.
 
Wanakunywa sana tuu, tena kuna fungu la bia za baba......😀😀 Sijataja jina ila mkija na mahasira nitataja mpaka sharika nilipopata kamnyweso
 
-Hawa/eva siyo mwanamke wa kwanza inamaana adam alikua na mke zaidi ya mmoja hata kama siyo kwa kipindi kimoja.
- Daudi alichepuka waziwazi
-Joshua aliua watu wengi kisa kuipata nchi ya ahadi, badae unakutana na amri usiue [emoji3][emoji3]
Biblia ni kitabu cha fasihi kilichoandikwa kwa ustadi mkubwa na kilikuwa na nia nzuri tu ya kuwafanya wanadamu wajitambue na kujua wananguvu kiasi gani,kila mtu anaweza kuwa kama yesu,jiulize kwanini mabuddha wamefukuzwa india na vitabu vyao vimechomwa na ndo huku yesu alipokuwako toka udogoni?kwa maana wanaijua siri ya kweli na dunia inapenda ufahari na utawala na sio watu kuwa huru.ndo hivyo wakatokea wahuni wengine wakabadilisha nyaraka,wengine wakaedit,wengine wakaongeza yao wengine wakachana ,wakatengeneza mfumo wa hierachy yani viongozi na watumishi ilikuwa ni siasa ndo maana wanapenda sadaka bila sadaka hakuna kanisa broh,hivi si ukichaa biblia unayo eti unaenda kanisani kusomewa aya tatu,unajisalisha pale we mwenyewe,unatoa kibunda halafu unarudi home..kwanini usinunue samaki wako fresh ukamuunga halafu ukashukuru tu kimoyomoyo kuliko kupoteza muda
 
20 years to come kama hizi historia hazitatunzwa (hata yale masalia) basi hakuna atakayejua ukweli

Ama waikatae dini au waendelee kuburuzwa kama mazombi
 
20 years to come kama hizi historia hazitatunzwa (hata yale masalia) basi hakuna atakayejua ukweli

Ama waikatae dini au waendelee kuburuzwa kama mazombi
Waache kwenda kwa mwamposa au mwakasege au kumsikiliza sijui papa weeeeee washakuwa mazombi hakuna namna sana sana labda mtu akiamua kufanya tafiti atatoka kwenye huu mtego
 
Mkuu kwanini unapenda kufikiriwa bila kufanya tafiti,fikra zako ni za nini?unatakiwa usiamini unatakiwa ujue
Natakiwa nijue nini?mambo ya kiroho ni imani,haya tuambie wewe unachojua juu ya miaka 18 ya Yesu ambayo haijaandikwa,umetafiti ukajua nini?
 
Maelezo mengi ya tafiti sijui Nini? Ukweli ni kwamba tarehe zote ulizotaja au zilizotajwa na watafiti siyo za kweli.
Sema nini, hizi dini zimetufanya waumini wake kushindwa kuchambua mambo ya dini bila kujali umri,elimu zetu nk.
Biblia au vitabu vinaeleza kabisa kwamba wakati wa kuzaliwa, Yesu alizaliwa kwenye zizi la mifugo(ngombe,mbuzi,kondoo) na zizi hilo lilikuwa tupu kwani mifugo hiyo ilikuwa malishoni au makondeni(maana yake walikuwa wanalishwa kwenye mabaki ya mazao baada ya kuvunwa ambapo kwa haraka haraka kipindi cha mavuno ni kuanzia April hadi Julai kwa maeneo karibia mengi ya ulimwengu)
Vilevile, kipindi cha mwezi wa 12 au Januari kwa maeneo mengi ya Ulaya ni kipindi cha baridi hivyo hatutegemei wachungaji au mifugo kuwepo makondeni kwa malisho maana watu na mifugo huwa ndani kwa ajili ya kujikinga na baridi na mvua. Na, kama shambani kulikuwa na mazao basi ni yale yanayoanza kuota au kuchipua.
Kwa hoja hizo chache itoshe kusema na tukubali ile nadharia ya kwamba X mass ilikuwa ni sikuu ya kusherehekea Mungu Jua ambayo ilikuwa maarufu wakati huo kwa watu wasio wakristo hivyo ili kuwaingiza kwenye ukristo ilibidi kuwashawishi kwa kujiunga nao kwenye sherehe zao ambapo matokeo yake ni waliokuwa wakristo kumezwa kwenye Imani zisizo za kikristo hadi wakati huu.
 
Nipo kampuni moja hivi ya ku supply vinywaji ,,nimejionea kwa macho yangu masister wananunua bia za kuzidi
 

Maneno hayo kuwa alitwaa mwili aliyatoa biblia ipoi ?? hebu tuwekee nukuu tafadhali
 
Kwanza uyo yesu aliwahi kuwepo hapa duniani? isije ikawa hata habari zake ni za kutungwa tu
 
Ndipo hapo wanaobuka watu wanadai huyu jamaa hakuwai kutokea hapa duniani story yake ni tungo tu za watu maana nje ya masimulizi ya kwenye biblia uwezi kupata habari zake kwengine kama kweli alikwepo basi watu wengi wangemsimulia katika nyanja tofauti tofauti cha kushangaza mtililiko wa atory zake ni ule wa kwenye biblia na sio zaidi ya hapo
 


Ni dhana potofu iliyozoeleka miongoni mwa Wakristo kwamba Paulo na Mitume wa Kristo walikuwa na kauli moja katika mahubiri yao ya Yesu aliyesulubiwa.

Wakristo wanafikiri kwamba mitume na Paulo walikuwa wakihubiri fundisho moja na kila mtu alimwamini Yesu wa kimungu ambaye alikuja kusulubiwa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu. Walakini, ikiwa mtu anachunguza bibilia kwa uangalifu, mtu huyo angeona kwamba Paulo na wanafunzi hawakuwa wakihubiri fundisho moja na hawakumwamini Yesu yule yule.

Mitume kule Yerusalemu walisikia kwamba Paulo amekuwa akihubiri mafundisho tofauti huko Galatia na Korintho.

Paulo alikuwa anawaambia wasifuate sheria tena na kwamba hawapaswi kula tena nyama ya kosher au kutahiriwa (kulingana na Mwanzo 17::14, agano linavunjwa kama hakuna tohara) n.k. Kwa hiyo Mitume wakaenda Galatia na Korintho na kuwahakikishia watu wote kwamba Paulo amekosea,

Paulo aliposikia hayo alirudi moja kwa moja mijini ………

Wagalatia 1:6

6 Nastaajabu kwamba mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita kwa neema ya Kristo na kugeukia Injili nyingine.


Inasema Injili tofauti, kwa hiyo ni wazi wanafunzi walikuwa wakiwafundisha mafundisho tofauti na haikuwa tu masuala madogo.

Wagalatia 2:11-21

Paulo Anampinga Petro

11 Petro alipofika Antiokia nilimpinga usoni kwa maana alikuwa amekosea waziwazi.

12 Kabla ya kufika watu fulani waliotoka kwa Yakobo, alikuwa akila pamoja na watu wa mataifa mengine. Lakini walipofika alianza kujitenga na watu wa mataifa mengine kwa kuwaogopa wale waliokuwa wa kundi la tohara. ( kwa nini watu kama vile mtume Yakobo bado waliamini kwamba sheria kuhusu chakula ingepaswa kutumika bado? Ikiwa Yesu alikuja kuchukua nafasi ya sheria, basi kwa nini bado wanaifuata sheria?)

13 Wayahudi wengine walijiunga naye katika unafiki wake. kwa unafiki wao hata Barnaba alipotoshwa. (kwa hiyo, Petro, Yakobo na Barnaba wamekosea?)

14 Nilipoona kwamba watu hawaishi kulingana na ukweli wa Injili, nilimwambia Petro mbele ya watu wote, "Wewe ni Myahudi, lakini unaishi kama Myunani na si kama Myahudi. , kwamba unawalazimisha watu wa mataifa mengine kufuata desturi za Kiyahudi?

15 "Sisi tulio Wayahudi kwa kuzaliwa na wala si 'watenda dhambi Mataifa'

16 tunajua kwamba mtu hahesabiwi haki kwa kuishika sheria, bali kwa imani ya Yesu Kristo. Vivyo hivyo na sisi tumemwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki. kwa imani katika Kristo na si kwa kushika sheria, kwa maana kwa kushika sheria hakuna mtu atakayehesabiwa haki (kwa nini wanabishana juu ya kufuata sheria au la? Kwa nini hawapatani na mafundisho?)

17 "Ikiwa tunatafuta kuhesabiwa haki katika Kristo, inaonekana kwamba sisi wenyewe ni wenye dhambi, je! hiyo inamaanisha kwamba Kristo anaendeleza dhambi? Sivyo hivyo!

18 Nikijenga upya kile nilichobomoa, nathibitisha kwamba mimi ni mvunja sheria.

19 Kwa maana kwa njia ya sheria naliifia sheria ili nipate kuishi kwa ajili ya Mungu.

20 Nimesulubiwa pamoja na Kristo, wala siishi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu.Uhai ninaoishi katika mwili, ninaishi kwa imani ya Mwana wa Mungu. ambaye alinipenda na kujitoa nafsi yake kwa ajili yangu.

21 Siibatili neema ya Mungu, kwa maana ikiwa haki inaweza kupatikana kwa sheria, Kristo alikufa bure.


Paulo anawashutumu Wakristo wote wa Kiyahudi akiwemo Petro na Barnaba. Tuna upande wa Paulo tu wa hadithi lakini ukumbusho wa Petro wa hadithi hii haujatolewa kwetu katika Agano Jipya.

Petro angemjua Yesu vizuri zaidi kuliko Paulo.

Kuna mabishano iwapo 1 Petro ni barua iliyoandikwa na Petro na karibu wasomi wote, wa kale na wa kisasa wanakubali kwamba 2 Petro si barua iliyoandikwa na Petro.



Matendo 4:31

31 Baada ya kusali, mahali walipokuwapo pakitikiswa. Na wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.

Ikiwa Petro alijazwa Roho Mtakatifu kwanini Paulo anamwita Petro mnafiki kwa kula na watu wa mataifa halafu watu walipotoka kwa Yakobo aliinuka. Yakobo ni ndugu wa kambo wa Yesu, aliishi na kukaa pamoja na Yesu.

Kwa nini bado alifikiri kwamba watu wanapaswa kula nyama ya kosher?

Hatuna maelezo yoyote ya hadithi ya Peter kuhusu tukio hili.

Barnaba pia anaitwa mnafiki katika mstari wa 13. Angalia jinsi katika mstari wa 15 mawazo 17 Paulo anabishana nao kuhusu sheria.

Hiyo ina maana kwamba wanafunzi walitaka kufuata sheria na kupendekeza kuifuata.

Vinginevyo Paulo hangeitaja. Angewezaje kumwambia Petro mambo hayo na kuangalia kile ambacho Yesu alisema kuhusu Petro.
 
Achana na tarehe 25 Desemba hiyo ni sikukuu ya wapagani walioamua sherehe za miungu yao na kuipa hadhi kuwa siku ya kuzaliwa Yesu.
 
Ufafanuzi mzuri sana, Mkuu hakuna muendelezo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…