Siku aliyozaliwa Yesu bado Kitendawili

Siku aliyozaliwa Yesu bado Kitendawili

Embu tupanue mjadala. Uyo Yesu ni kweli alishawahi kuwepo duniani, Kuna ushaidi wowote wa kihistoria kwamba Yesu aliishi hapa duniani na sio fictional tu
 
Pitia na hii[emoji1541]

SIKUKUU YA CHRISTMAS (Sehemu ya 5)

TAREHE 25 DECEMBER

Tuanze na majira ya kipindi alichozaliwa YESU
Luka 2:8
[8]Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku.

Kipindi pekee ambacho Wachungaji wanaweza kukaa makondeni na kuacha mazizi yao yakiwa tupu hata usiku ni majira ya baridi kali. Kasababu kipindi hiki ni kipindi ambacho majani yanaungua na kukauka kabisa kutokana na baridi kali. Hivyo kulazimu kuyafuata malisho sehemu zenye miinuko midogo ambayo kwa hakika itakua sehemu za bahari sehemu ya Gaza, au bahari ya chumvi, au pembezoni mwa mto Yordani kwa mujibu wa jografia ya eneo husika.

Sasa tutazame kwa mujibu wa kalenda ya kiyahudi msimu wa baridi unaanza lini?

Amosi 3:15
[15]Nami nitaipiga nyumba ya wakati wa baridi pamoja na nyumba ya wakati wa hari; na hizo nyumba za pembe zitaangamia, nazo nyumba kubwa zitakuwa na mwisho, asema BWANA.

Andiko hili linaonesha kua wana wa Israeli walikua wana tabia ya kujenga nyumba mbili za kuishi. Nyumba moja ni ya kukaa majira ya baridi na nyumba za wakati wa joto. Sasa tuangalie majira haya ya baridi ambayo mtu analazimika kuhamia kwenye nyumba ya wakati wa baridi ni yapi?

Yeremia 36:22
[22]Basi mfalme alikuwa ameketi katika nyumba iliyotumika wakati wa baridi, mwezi wa kenda; na pale palikuwa na moto wa makaa mbele yake.

Mwezi wa kenda (9) ni mwazo wa msimu wa baridi kali, kila mwenye uwezo wa kuwa na nyumba mbili ilimlazimu kuhama nyumba ya wakati wa joto na kuhamia nyumba ya wakati wa baridi (A warm apartment). Sasa kama umefuatilia kwa umakini mkubwa kwenye somo langu hili sehemu ya 3 utakua umejua kua tunaposema mwezi wa kenda (Tisa) kwa kalenda ya kiyahudi inaangukia katikati ya mwezi wa 11 hadi katikati ya mwezi wa 12 (November - December) kwa kalenda yetu ya sasa. Sasa kwa kua msimu huu wa baridi kali ambao ndio kwa hakika tunaona kua MASIHI alizaliwa kilichobaki ni kuitafuta tarehe 25 ya December inayosherehekewa sasa.

Kabla ya kuielezea tarehe 25 nijikite na utata wa kimaandiko ambao umekua ukipoteza wengi hata wakafikia kusema kua YESU hakuzaliwa tarehe hiyo.

Andiko linalotumiwa zaidi ni

Luka 1:26-28
[26]Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti,
[27]kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu.

Andiko hili hutumiwa sana kupinga hoja ya 25 December. Wanadai kua kama mimba iliingia tumboni mwa Mariamu mwezi wa 6 na akakaa nayo kwa miezi timilifu (miezi 9) basi ni ukweli usiopingika kua YESU alizaliwa mwezi wa 3 ndani ya mwaka uliofuata. Wanaongeza kwa kusema kua, kama YESU atakua amezaliwa 25 December basi ni kusema kua YESU alizaliwa njiti wa miezi 6 kitu ambacho haimkiniki kufanyika kabisa. Na isitoshe jambo hilo litakua limepingana na maandiko matakatifu yanayosema;

Luka 2:6
[6]Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia,

Andiko hili linaonesha kua YESU hakuzaliwa njiti bali siku zilitimia na siku zinatimia kwa kutimiza miezi 9 tumboni. Wanasema kua kama ukisema YESU alizaliwa December unapingana na maandiko, maana YESU alitimiza siku za kukaa tumboni.

Lakini twende taratibu na andiko hili hili tuone, huu mwezi wa 6 ulimaanisha nini?

Sasa ukitaka kupata maana halisi ya mwezi huu wa sita ulimaanisha nini anzia kusoma mstari wa 24 ndipo usome mstari huo wa 26 unaosema mwezi wa 6 kisha unganisha mistari yote miwili.

Tuanze na mstari wa 24

Luka 1:24-25
[24]Hata baada ya siku zile mkewe Elisabeti alichukua mimba akatawa miezi mitano, akisema,
[25]Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana katika siku zile alizoniangalia ili kuniondolea aibu yangu mbele ya watu.

Hebu rudia Mara mbili mstari huo wa 24 na 25 ili ujifunze kitu. Elisabeti ni mke wa Zakaria aliyekua KUHANI. Akabeba mimba AKATAWA (yaani akawa katika hali hiyo ya ujauzito) kwa miezi mitano (5).
Zingatia neno "AKATAWA MIEZI MITANO" na usilisahau hilo.

Baada sasa ya kushika neno hilo "AKATAWA MIEZI MITANO" unganisha na mstari wa 26 ili upate maana halisi ya neno "MWEZI WA SITA" na itasomeka hivi;

Luka 1:24-26
[24]Hata baada ya siku zile mkewe Elisabeti alichukua mimba akatawa miezi mitano, ..........

[26]Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti,

Kama umekua makini na maneno ya msisitizo niliyoyaweka utakua umegundua kitu hapo. Ukiunganisha hayo maandiko utagundua kua, sio mwezi wa sita unaoitwa JUNE kama wasomaji wengi wanavyodhani. Lakini ukweli ni kwamba Elizabeti alibeba mimba kwa muda wa miezi mitano, na mwezi wa sita sasa tangu Elizabeti abebe hiyo mimba ndipo Malaika wa BWANA alipoenda kwa Mariamu.

Ili kuthibitisha zaidi na kuuongezea nguvu ushahidi huu ongezea mstari wa 36 wa sura hiyohiyo.

Na utasomeka hivi;

Luka 1:36
[36]Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa;

Nakuomba usichoke kusoma maandiko hayo.
Hebu tuyaunganishe maandiko haya kwa mtiririko.

Luka 1:24-38
[24]Hata baada ya siku zile mkewe Elisabeti alichukua mimba akatawa miezi mitano,.....

[26]Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti,

Luka 1:27
kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu.

Luka 1:28
Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe.

Luka 1:29
Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani?

Luka 1:30
Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.

Luka 1:31
Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.

Luka 1:32
Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.

Luka 1:33
Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

Luka 1:34
Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume?

Luka 1:35
Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.

[36]Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa;

Zingatia hilo andiko la mwisho kwa mara nyingine.
Luka 1:36
Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa;.

MWEZI HUU NI WA SITA KWAKE YEYE (Elezabeti) ALIYEITWA TASA.

Mpaka hapo hoja ya mwezi wa 6 wakimaanisha JUNE imeshakufa kabisa, sasa tutafute tarehe 25 maana tuna hakika kabisa msimu wa baridi ambao YESU alizaliwa ni mwezi wa 9 kwa kalenda ya kiyahudi ambayo ni kati November na December kwa kalenda yetu ya leo.

Tuanze na kilichomleta YESU duniani.

Luka 4:18-21
[18]Roho wa Bwana yu juu yangu,
Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema.
Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao,
Na vipofu kupata kuona tena,
Kuwaacha huru waliosetwa,
[19]Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.
[20]Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho.
[21]Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.

Kuna mengi ameeleza katika mistari hii michache. Lakini Mimi nitaweka mkazo kwenye mstari wa 19 na 21 maana andiko kwenye mada yetu. Zingatio hapo ni "KUWATANGAZIA WAFUNGWA KUFUNGULIWA KWAO" na "MAANDIKO HAYA YAMETIMIA MASIKIONI MWENU". Kulikua na desturi kwa wafalme na watawala wa zama hizo na kurudi nyuma, ya kuwaachilia huru au kuwauwa baadhi ya wafungwa siku za sikukuu.
Na siku anayozaliwa mtu mkuu kama YESU inapaswa kuingizwa katika hesabu ya siku ya sikukuu.

Mathayo 14:6-7
[6]Hata ilipofika sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti Herodia alicheza mbele ya watu, akampendeza Herode.
[7]Hata akaahidi kwa kiapo ya kwamba atampa lo lote atakaloliomba.

Sikukuu ya sherehe ya kuzaliwa kwa Herode mfalme ndio siku Yohana alichinjwa.

Mathayo 27:15-17
[15]Basi wakati wa siku kuu, liwali desturi yake huwafungulia mkutano mfungwa mmoja waliyemtaka.
[16]Basi palikuwa na mfungwa mashuhuri siku zile, aitwaye Baraba.
[17]Basi walipokutanika, Pilato akawaambia, Mnataka niwafungulie yupi? Yule Baraba, au Yesu aitwaye Kristo?

Sikukuu ya Pasaka ndio siku aliyoachiwa huru Baraba aliyekua MWANAHARAKAT wa kiyahudi kimwili na kuuwawa YESU MWANAHARAKATI wa kiroho.

Kwahivyo uzoefu unaonesha kua siku ya sikukuu kuna kuachwa huru au kuuwawa. Japo maandiko yote hayo hayataji tarehe moja kwa moja mpaka uitafute kwa mahesabu.

Sasa hebu tuone mahali inakotajwa tarehe ya hukumu moja kwa moja.

Yeremia 52:31
[31]Hata ikawa, katika mwaka wa thelathini na saba wa kuhamishwa kwake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na tano ya mwezi, Evil-merodaki, mfalme wa Babeli, katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, akamwinua kichwa chake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, akamtoa gerezani.

Andiko hilo linataja moja kwa moja tarehe 25 mwezi wa 12. Japo hoja hiyo ni dhaifu mno, maana mwezi wa 12 unaotajwa hapo haumaanishi December. Lakini naweza kulitumia andiko hili kama spana ya kufungulia nati ngumu za wale wanaodhani miezi iliyotajwa kwenye biblia inalingana na miezi yetu leo. Kwahiyo uking'ang'ania kuinasibisha miezi hii ya kibiblia na miezi yetu nitakwambia hivi;- 25 December imetajwa ikihusika na kuwaachilia wafungwa, na YESU amekuja kufungulia wafungwa. Lakini ukielewa kuhusu kalenda ya kiyahudi tunaachana kabisa na andiko hilo. Na tutaanza kujadili kuhusu "MWAKA WA BWANA ULIOKUBALIWA".

Acha niliweke tena hapa andiko hili.

Luka 4:19
[19]Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.

Mwaka wa BWANA uliokubaliwa una tafairi 2 za kushabihisha maana ya andiko hili.

(1) Mwaka wa kuwaachilia huru watumwa wote.

Mambo ya Walawi 25:8-10
[8]Nawe utajihesabia Sabato saba za miaka, maana, miaka saba mara saba; zitakuwa ni siku za Sabato saba za miaka kwenu, maana miaka arobaini na kenda.
[9]Ndipo utakapoipeleka pande zote hiyo baragumu yenye sauti kuu, siku ya kumi ya mwezi wa saba; katika siku hiyo ya upatanisho mtaipeleka baragumu katika nchi yenu yote.
[10]Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kupiga mbiu ya kuachwa mahuru katika nchi yote kwa watu wote wanayokaa; itakuwa ni yubile
kwenu; nanyi kila mtu atairudia milki yake mwenyewe, nanyi mtarejea kila mtu kwa jamaa yake.

Kwa sheria ya torati mwaka wa hamsini ulihesabiwa kua ni mwaka wa BWANA na ulikua ni mwaka wa kuwaachi huru watumwa wote na kila mmoja ayarudie makazi yake. Mwaka huu ulikua wa maana sana kwa watumwa waliochoshwa na utumwa. Kuwaachi huru haikua hiyari ya MTU Bali ilikua ni amri ya BWANA. Lakini ilimpa nafasi mtu aliyetaka mwenyewe kuendelea kua mtumwa kuendelea na utumwa wa hiyari. Na mwaka unaofuata (baada ya yubile) wanaanza kununua watumwa upya.
Sasa YESU anatangaza yeye ni YUBILE ya milile yaani baada ya kutangaza Uhuru wa watumwa wa kiroho hakutakua na utumwa milele.

(2) Maana ya pili ya KUTANGAZA MWAKA WA BWANA ULIOKUBALIWA ni.

Lazima kue na hesabu ya mwaka itakayotambua ujio/kuzaliwa kwa KRISTO.

Leo hii tunasema ni mwaka 2023, lakini kwanini iwe 2023 na isiwe 3000 wala isiwe 5000 wala sio mwaka wa 1000? Kinachoamua huu usemi wa kusema huu ni mwaka 2023 na isiwe vinginevyo ni neno linalofuatia baada ya kutaja mwaka. Yaani utasema, huu ni mwaka 2023 BAADA YA KRISTO (BK). Yaani hii ni kusema kua, baada ya kumpata KRISTO duniani sasa imepita miaka 2023.
Au ni sawa na kusema kua KRISTO tumeanza kuishi nae hapa duniani tangu tarehe 1 mwezi wa 1 mwaka wa 1. Yaani tarehe 1 January ya mwaka wa kwanza ndipo kristo ameanza kuwepo.

Acha tuone maandiko yanasemaje.

Mwanzo 17:10-13
[10]Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa.
[11]Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi.
[12]Mtoto wa siku nane atatahiriwa kwenu, kila mwanamume katika vizazi vyenu, mzaliwa nyumbani, na mnunuliwa kwa fedha, kila mgeni asiyekuwa wa uzao wako.
[13]Mzaliwa nyumbani mwako, na mnunuliwa kwa fedha yako, lazima atahiriwe; na agano langu litakuwa katika mwili wenu, kuwa agano la milele.

Agano la MUNGU linaanzia hapa. Ili MWEBRANIA atambulike kua binaadamu kamili ni lazima atahiriwe na liliitwa agano la milele. Kabla ya siku ya nane ya tohara mtoto wa familia ya Kiebrania hakutambuliwa kama binaadamu aliyekamilika na ndio maana hakupewa jina kabla ya kutahiriwa. Baada ya kutahiriwa ndipo alipewa jina. Akifa kabla ya siku nane hawahesabu kama ni MTU amekufa Bali ni kama mimba tu imeharibika.

Luka 2:21
[21]Hata zilipotumia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; kama alivyoitwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba.

Hapo anakua mtu/Myahudi kamili. Sasa tangu awe myahudi kamili ndipo tunapoanza kuhesabu miaka. Hii ni kusema kua kuna sherehe mbili hapo, sherehe ya kuzaliwa na sherehe ya kutahiriwa yaani kua mtu/Myahudi kamili.

Tarehe 1 January mwaka wa kwanza ni siku ya tohara ya YESU. Sasa kama kungekua na tarehe za kuhesabu kabla ya tarehe hiyo tungehesabu hivi.

Tarehe 1 January ni siku ya nane (8)
Tarehe 31 December ni siku ya saba (7)
Tarehe 30 December ni siku ya sita (6)
Tarehe 29 December ni siku ya tano (5)
Tarehe 28 December ni siku ya NNE (4)
Tarehe 27 December ni siku ya tatu (3)
Tarehe 26 December ni siku ya pili (2)
Tarehe 25 December ni siku ya kwanza (1)

Kama tukikubaliana kua huu ni mwaka wa 2023 Bk, basi ni wazi kua tunapaswa kukubaliana kwamba YESU alizaliwa tarehe 25 ya mwezi December.

Lakini kuna wanaosema kua tarehe 25 December ni tarehe ya kuabudu miungu ya kirumi na Wakristo wakaiga hiyo tarehe. Acha nijibu kwa kifupi sana, na nitajibu kwa kirefu pindi nikiandika rasmi somo hili. Wanathiologia wakubwa wa Kikristo ndani ya Afrika ndio walioweka sawa tarehe hii 25 December baada ya Wakristo wa ulaya kusherehekea tarehe 11 September huku Asia na Africa wakisherehekea tarehe 6 January. Na hesabu hii ya tarehe 25 December waliipiga mnamo mwaka wa 200Bk, wakati huo hao waabudu miungu wa rumi (wanaonasibishwa na hiyo tarehe 25 December) wakisherehekea ibada za miungu yao tarehe 17 hadi 23 ya December. Ilipofika mwaka wa 274Bk waabudu miungu wa huko rumi wakahamisha tarehe kutoka 17 hadi 23 na kua 25 December. Baadae Wanathiologia wa Ulaya (rumi) wakajaribu kuhakiki upya tarehe ya kuzaliwa YESU na kugundua kua Wakristo wa Afrika walikua sahihi kwa kusema kua YESU alizaliwa tarehe 25 December. Na wao wakaanza kuifuata hiyo 25 December. Hii ilikua mwaka 336Bk. Na hii ni kusema kwamba. KWA WAKRISTO WA AFRIKA WAMEKUWA WAKISHEREHEKEA SIKUKUU YA KUZALIWA YESU KWA MIAKA 74 KABLA YA WAPAGANI KUITUMIA TAREHE HIYO KWA SHEREHE ZA MIUNGU YAO. NA WAMEKUWA WAKISHEREHEKEA SIKUKUU YA KUZALIWA YESU KWA MIAKA 136 KABLA YA WAKRISTO WA ULAYA KUANZA KUISHEREKEKEA KWA TAREHE SAWA NA HIYO.

Sasa Wazungu kwa roho mbaya yao ya kutaka kuonekana kua wao ndio wamegundua hili wakaamua kwa gharama kubwa kuharibu histori. Ili vizazi vijavyo visije vikasoma kua waliogundua tarehe hii ni Waafrika wakiwatangulia Wazungu kwa miaka 136. Sasa wakasahau kua, kwa mwaka waliokubali tarehe wanayosherehekea Waafrika na kwenda sawa nao (yaani 336Bk) watakua nyuma ya wapagani wa Rumi.

Sasa hivi inawawia vigumu kuusafisha uongo walioutengeneza wa kugundua tarehe. Maana ama wakubali wameiga tarehe ya wapagani ili wasiwatukuze Waafrika. Au wakubali aibu ya kukubali waafrika ndio wa kwanza kugundua tarehe ya Christmas.

VIPI NIENDELEE SEHEMU YA 6 AU TUISHIE HAPO? KAZI NI KWAKO. NA MAONI YAKO NDIO YATAAMUA KAMA TUISHIE HAPO AU TUENDELEE.

Ni Mimi Mwalimu Omari Mnyeshani Mwalimu wa zamu (teacher on duty)
Source: fb
 
kuna ushahidi gani mwingine? maelekezo ya papa au
sasa papa kabariki ushoga lipokeeni na hilo
Hata maisha yangu ni ushahidi pia

Kwani hao walioandika Biblia si binadamu tu kama wewe? Iweje umfiche Mungu kwenye hivyo vitabu kadhaa vya Biblia unafikiri Mungu ni mdogo kiasi hicho?

Ushoga ulikuwepo kabla hata ya Yesu
 
Yesu alizaliwa tarehe moja siku ya kwanza na mwaka moja Baada ya Kristo.
Na ndio tarehe inayotumika duniani kote.
Wacheni ujinga ujinga wenu, someni
 
Siyo tu tarehe ya kuzaliwa Yesu, bali hata mwaka aliozaliwa haujulikani. Jambo lisilotia shaka ni ukweli kuwa alizaliwa na kuishi miongoni mwa Wayahudi. Na ipo sababu za kitheolojia kwa tarehe hizo kutokuwa wazi..!
Lakini pia Kalenda tunayotumia leo (Gregorian Calendar) ni ya Kirumi na imekuja baadaye sana wakati huyo Yesu alikwishaenda zake. Mpaka leo Kalenda ya Kiyahusi ni tofauti na hii ya Kirumi; maana wao huesabu tangu mwaka ule walioshushiwa torati; ambapo leo ni mwka 5781 (kama sijakosea). Hali kadhalika miezi ya Kiyahudi haikuwa hii tunayoijua leo. Wao walikuwa na miezi yenye majina ya Abibu/Nisani, Zivu/Ayani, Siwani, Tamuzi, Avu, Elali, Ethanimu, Buli, Kisleu, Tebethi, Shebati na Adari
 
Yesu alizaliwa wakati wazazi wake waliposafiri kwenda kuhesabiwa. Waroma hawakuwa wajinga kusafirisha maelfu ya watu wakati wa majira ya baridi ili kwenda kuwahesabu. Wenzetu wanafanya mambo kwa kuangalia majira. Baridi la huko si kama huku, ni barafu tupu. So wanapofanya mambo huangalia hilo. Yesu atakuwa alizaliwa wakati wa majira ya joto. Mwezi wa tano hadi wa tisa hivi.
 
Back
Top Bottom