Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Urejeshwaji wa vifaa na mitambo hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Kadogosa, aliyesisitiza umuhimu wa kuhakikisha rasilimali zote zinazohitajika katika utekelezaji wa miradi zinapatikana na kubaki katika maeneo ya kazi ili kuepusha ucheleweshaji.
Pia soma ~ Kadogosa amwambia Mkandarasi wa Barabara ya Kahama–Bulyanhulu JCT - Kakola kuwa hataongezewa muda, mradi ukamilike Desemba 2026
Alifafanua kuwa tabia hiyo inaweza kusababisha miradi kutokamilika kwa wakati, pamoja na kuisababishia Serikali hasara kutokana na kulazimika kulipa tena gharama za usafirishaji na uletaji wa vifaa na mitambo hiyo.
Katika hatua nyingine, utekelezaji wa agizo hilo umeanza pia katika mradi wa ujenzi wa barabara ya mchepuo ya Iringa (Iringa Bypass), yenye urefu wa kilomita 7.3, ambapo hadi Oktoba 29, 2026, mkandarasi alikuwa amerejesha mitambo 41 kati ya 65 inayohitajika kwa mujibu wa mkataba, sawa na asilimia 63.