Siku Chief Adam Sapi Mkwawa alipojiunga na TANU mwaka wa 1955

Uko sahihi Faiza ni kweli Mkwawa alikuwa Muislam na ndivyo sote tuliokulia na kuishi maeneno ya karibu kabisa na Kalenga tunajua hivyo na halina ubishi. Hata sasa wanafamilia wa Mkwawa wengi wao ni waislamu.
Tena hasa hawa wanaoanzia na ..... Sapi Mkwawa karibu wote ninaowajua Mimi ni Islam
 
Ngongo,
Mimi kwa kuwa umetaka darsa In Shaallah nitakupa darsa.
Lakini darsa lina taratibu zake.
Halichanganyi mambo kwa hiyo hayo ya utumwa yatafuata
baadae In Shaallah.
Sasa na tuanze hili la ''Ukristo kupewa nguvu.''
Ingia hapa:
Mohamed Said: KANISA KATIKA TANGANYIKA YA KIKOLONI
 


Hili ni kweli kabisa...Tosa was inhospitable and Mkwawa thought by giving it to Missionaries they would give up....a terrible mistake. Determination is so powerful
 

Nimekusoma Sheikh Mohamed Said ingawa andiko lako limejaa ukakasi nianze na hili Uislam ulitangulia kabla ya Ukristo sina ubishi nalo ninapokushangaa ni pale unapoonyesha jaribu kuonyesha Uislam ni dini ya asili ya Afrika (EA) wakati nayo ililetwa na majahari na waarabu.Dini za asili za Afrika zinajulikana wazi Uislam na Ukristo tuliletewa haijalishi ipi ilianza na ipi ilikuja nyuma zote zililetwa.

Umejaribu kuonyesha Ukristo ulifungamana na serekali za kikoloni na Uislam ulipingana na Ukoloni lakini tukichimbua historia ya kudai uhuru wa Tanganyika tunawaona wakristo wa maeneo tofuti tofauti wakipinga ukoloni akiwemo Baba wa Taifa Dr Mwl Julius Kambarage Nyerere.

Sheikh Mohamed Said umeonyesha kupendezwa na ujio wa waarabu/waajemi na Uislam kwa maana hiyo basi kama waaarabu wangebahatika kuitawala Tanganyika wazee wako wa Kiislam wasingekuwa na sababu za kudai uhuru ?????.Dhana hiyo naiona hata leo mnaishabikia huko Zanzibar kwamba Sultan hakuwa na shida utawala wake ulikuwa bora kwakuwa tu ndio walioleta dini ya kiislam na majahazi !.
 
HAPANA, labda wasomaji wengine watusaidie kuhusu hili suala
Biashara ya watumwa "slave trade" ilianzishwa na kuratibiwa na waarabu chini ya Oman sultanate rule.

Hii biashara ya watumwa lasted for 400 yrs. Waingereza waliongoza katika kuikomesha hii biashara,refer the following agreements:-

1: Sir fairtax moresby agreement,signed in 1822

2: Harmetony agreement,signed in 1845

3: Mission led by Sir Bartle Frere, signed in 1873, hapa sultan Barghash wa Zanzibar alilazimishwa kufunga soko kuu la watumwa huko Zenj.
 
Ngongo,
Unachoona wewe nii ukakasi kwa mwingine ni ukweli.
Hakuna mahali popote niliposema Uislam ni dini ya asili ya Afrika.

La kama papo na mimi nimeghafilika nionyeshe.
Hayo mengine naona labda wengine watachangia wakipenda.
 
Mkuu Ngongo kuna kitu hapa kinataka kisiwekwe sawa,Nimemsoma vizuri Mzee wangu Mohamed Said lkn kuna mahali kama anaparuka kupasema:


-Kwanza hapa tujue kuwa Mtwa Mkwawa mwenyewe hakuwa na dini kwa maana ya Muislam au mkristo
Yeye alikuwa mfuasi wa dini ya asili akiamini ktk mizimu na waganga wa kienyeji,baada ya kuwa ameli-
ga jeshi la Mjeruma Mtwa Mkwawa alikimbia na akawa anatafutwa sana na Wajeruma popote alipo.

-Baada ya Wajerumani kumkosa wakaamua kumteka mwanae Mtwa Mkwawa aliykuwa anaitwa Sapi Mkwawa
Wakamchukua na kumpeleka Kilwa,kumbuka Kilwa ndio ilikuwa "Escape area" ya Wajeruman wakati wote
Wa utawala wao.Hata Zelewisky anavyokwenda kupigana na Mkwawa alitokea Kilwa kupitia Usagala

Sapi alipelekwa Kilwa ili kumtumia ujumbe Mkwawa kuwa mtoto wake ametekwa hivyo ajitokeze.Baada ya
Kukaa na Sapi Wajeruman wakampenda kwa aina ya uwezo wake wa kuongoza,wakampeleka Ujerumani na
Baadae wakamfanya kuwa Liwali wa Kilwa,na ili awe Liwali ilibidi aendane na utamaduni wa watu wake,hivyo Sapi akaingia kwenye Uislam na akawa Liwali wa Kilwa.

Kuanzia hapo Sapi na kizazi chake cha kuja chini wakawa Waislam,hivyo hata mwanae Adam Sapi Mkwawa alipozaliwa akawa tu "by default" Muislam.Baada ya hapo wale walio ktk ukoo wa Chief kuanzia Sapi na Adam Sapi wakawa Waislam.Hata baada ya Waingereza kurudisha utawala wa machief,Adam na wasaidizi wakke baadhi walioitwa "Wanzagila" walikuwa waislam

Hivyo sehemu ndogo tu ya Wahehe wa kizazi cha Sapi na mwanae Adam ndio walikuwa Waislam,hata wasaidizi wengine na watu wa karibu na Mkwawa kama kina Mwamgongolwa hawakuwa Waislam na Msikiti Kalenga umekuja kujengwa na Chief Adam Sapi miaka ya 1950's

Muingiliano kati ya Wahehe na Waarabu ilikuwa ni sbb ya biashara,Mtwa Mkwawa alikuwa na "shamba lake la pembe za ndovu" ambazo aliwauzia Waarabu,eneo hilo la "shamba" ndio mbuga ya Ruaha National Park ya sasa(Utakumbuka ndio mbuga yenye tembo wengi kuliko zote)

Walichoinga wahehe kwa Waarabu ni vazi,lkn Muhehe hakutaka liwe kama kanzu,yeye aliita "mgolole" na kichwani alijivika kiremba huku chini akivaa "lubega" nyeupa,hili ndio vazi rasmi la Wahehe mpaka leo

Kumbukumbu za Maandishi ya Kiarabu ya Makumbusho ya Mkwawa,ni yale aliokuwa nayo Sapi wakati akiwa Liwali kule Kilwa,akiwasiliana na wafanyabiashara wa kirabu kwa niaba ya Wajerumani,na Adam ndio aliyejengea kaburi la baba yake Sapi kwa mtindo wa kiislam baada ya kurudi toka Makerere na kukabidhiwa Uchief

Wahehe waliupokea Ukristo Ukatoliki toka kwa Wamisionari,na hasa Wamisionari wa Consolata toka Italia mwaka 1896 eneo la Tosamaganga,baadae Wamisionari hao wakasambaa eneo la Madibira bonde la Ihefu,Rujewa eneo la Usangu,Nyabula,Ilole na Pawaga.Toka mwaka 1896 Vatican ilituma Padre Francesco Caligliero(Mwenye jina la shule ya Cagliero iliyopo Ipogoro Iringa) kueneza Ukristo na kuifanya Iringa kama sehemu ya Metroponia ya Nyanda za Juu za Tanganyika,baadae ilipokomaa ndipo Papa akateua Askofu toka Italy kuja kuwa askofu wa Iringa,huyu Mzungu aliitwa Attilio Betlamino na alifia Tosamaganga na kuzikwa ndani ya kanisa hilo.
Cc barafu UncleBen Ngongo Nyani Ngabu Mimi Mwanakijiji Tangawizi Yericko Nyerere naiman64
 
Ngaliba Dume,
Ahsante sana kwa maelez haya.
Mengi katika haya sikuwa nayajua.

Nakushukuru sana.
 
Ngaliba Dume asante sana kwa kuniita na kwa maelezo haya,ninaafikiana na wewe sbb maelezo yako kweli hayapishani sana na yale juu niliyotoa mimi.Na ukiona "gwiji" wa historia kama Mzee wetu Mohamed Said kaonekana kukushukuru basi safi
 
Na kwa kuongezea tu ni kuwa Sapi mwenyewe alikuwa kipenzi sana cha Wajerumani,hasa baada ya kuwasaidia sana ktk utawala wao akiwa kama Liwali kule Kilwa,Kilwa ndio ilikuwa ngome ya Jeshi la Wajerumani wakati wa WWI,na ndio hata Nyambizi ya Wajeruman wakati wa vita hivyo ilikuwa Kilwa,sbb ya Utawala wa Wajerumani ilikuwa "Direct Rule" na mtu wa kuwaongoza watu wa eneo la Kilwa alipaswa kuendana na utamaduni wao,Sapi alipaswa kuwa muislam na akawaongoza watu wa eneo la Kilwa Kivinje mpaka Kilwa Kipatini kwa "sharia"

Hii ilimfanya Sapi kuwa muelewa wa maandishi ya kiarabu,sharia na uislam wenyewe.Kati ya mwaka 1896-1898 Sapi aliishi Kilwa,na baadae kupelekwa Ujerumani baada ya baba yake Mtwa Mkwawa kuthibika ameuwawa.1908 Wajerumani ndio walimrudisha na kumpa u-Liwali huko Kilwa.Sapi Mkwawa hakuwataka kabisa Waingereza,na hata wakati wa WWII alikuwa amejiapiza kuirudisha Iringa na Uhehe chini yake kama Hitler angeiteka Dar na Tanganyika yote,Muingereza aliufuta kabisa uchief mpaka alipourudisha kati ya mwaka 1920's.Na Sapi alifia kizuizini huko Mwanza ambapo alikuwa amewekwa na jeshi la Serikali ya Muingereza,ndio maana ukifuatilia historia ya Chief Adam Sapi mtoto wa Chief Sapi Mkwawa utaona kuwa alikuwa na historia inayohusisha mkoa wa Mwanza au Nyanza Province.

Ni kweli Iringa imetawaliwa na Wakristo Wakatoliki,na kitovu cha Ukristo Iringa kipo Tosamaganga,na ndio yalikuwa makao makuu ya Kanisa Katoliki Iringa,mpaka sasa shughuli nyingi za hija na mambo ya Wakatoliki yapo Tosamaganga badala ya Iringa Mjini.Makaburi ya mapadre na watawa wote wa Iringa wanazikiwa Iringa,mashirika makubwa ya watawa Wakiume na kike kwa Jimbo la Iringa makao makuu yapo Tosamaganga.Kifupi Tosamaganga ni kama "Vatican ya Iringa",maana watawa na mapadre ni wengi kuliko raia.Asilimia 99% ya ardhi ya Tosamaganga ipo chini ya kanisa,na hapo ni kilomita chache kufika Kalenga ilipo "Lipuli" ya Mtwa Mkwawa.Kwa Wahehe "Lipuli" maanake "ngome" na ndio maana timu ya mpira ya Iringa iliitwa "Lipuli"

Cc Ngaliba Dume UncleBen Mohamed Said FaizaFoxy Ngongo
 
Ngaliba Dume asante sana kwa kuniita na kwa maelezo haya,ninaafikiana na wewe sbb maelezo yako kweli hayapishani sana na yale juu niliyotoa mimi.Na ukiona "gwiji" wa historia kama Mzee wetu Mohamed Said kaonekana kukushukuru basi safi
Barafu,
Mimi bado mwanafunzi nasoma na kuna walimu wangu wengi
hapa Barzani.

Ahsante sana.
 
Rumaliza atakuaje na "jina halisi" la Khalfan bin Khamis al Barwani?

Huoni kama ni aibu na kituko kwa Rumaliza kuwa na "jina halisi" la Kiarabu? Haiwezekani, unatudanganya!

You are betraying African pride, the Bantu identity. Kisa? Kukumbatia dini za watu wengine!

Huwezi kukuta Muarabu anasema eti anaitwa "jina halisi" Rwaitama Sikujua.
 
Kwameh,
Inataka ushujaa mkubwa kuandika uongo.
Mimi sijajaliwa uhodari huo.

Lakini umetoa fikra zako na hivi ndivyo binadamu tulivyo kughitilafiana
ni jambo la kawaida kwetu.
 

Dini za watu wengine wepi unazoziongelea mbona hueleweki?
 
Dini za watu wengine wepi unazoziongelea mbona hueleweki?
Waarabu.

Mtu anaeitwa "Rumaliza" hawezi kuwa na "jina halisi" na Kiarabu.

Waarabu na Wazungu wameleta dini zao, majina yao, tamaduni, mavazi, na lugha zao. Tumeyakumbatia kichwa kichwa.

Malcolm X alikuwa anasema ukienda China huwezi kukuta Mchina anaitwa Murphy, au Bunch.

Muafrika ambae hakuelimishwa thamani ya utu wake ndio anasema eti RUMALIZA jina lake halisi ni KHALFANI bin BARWANI.

I mean, kama jina lake halisi ni KHALFANI bin BARWANI amepata wapi jina la RUMALIZA?

Kama sio kumeza mi culture na mi dini ya watu wengine?
 
Kwameh,
Siku hizi ilm nyingi zipo mtandaoni.

Ungechukua tabu kidogo tu ya ku-Google ungesoma kila kitu kuhusu
Rumaliza.

China kuna Wachina wengi wana majina ya Nancy na John.
 


ndo maana nikasema "hili lizee" litakufa kihoro na huo udini wako na hii dhambi itakutafuna wewe na kizazi chako chote mpaka ukamilifu wa dahari!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…