Siku hayati Magufuli aliposimama imara kutetea wamachinga, mbele ya Samia

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054

Siweki neno:

Lakini ukitaka kujua kwa nini wamachinga walimlilia sana, kujitokeza kwa wingi njiani kumzika ni hii hapo juu

Hata Rais wa awanu ya pili mzee Ali Hassan Mwinyi wakati akisoma Tanzia yake huko Chato, alimsifu Hayati kwa kutowasumbua wamachinga kwenye utawala wake!

Wamachinga wanatafuta hela ya kula, Wasaidiwe kwa kujengewa miundombinu kwanza na siyo kufukuzwafukuzwa kama mbwa
 
Hata mababu zetu waliishi nyumba za nyasi ila mambo hubadilika na kwenda njia iliyo Bora zaidi!! Waende maeneo husika na Kama kuna Tatizo walalamikie maboresho na Kama wanalipa kodi ni rahisi kusikilizwa na sio kuziba mitaro na barabara na njia za watembea kwa miguu
 
Na wewe unaunga mkono wakapange biashara hata kwenye mlango wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya? Hilo litakuwa ni Taifa la namna gani? JPM anafahamika alikuwa mtu wa kupenda sifa za hovyo hovyo especially kutoka kwenye makundi ya watu wenye uelewa mdogo katika jamii
 
Bado sijaona sababu ya msingi kabisa ya kuwaondoa wamachinga barabarani.

Kama wanaziba njia na wanakaa kwenye mifereji ilo linazungumzika na inawezekana kuwasogeza sio kuwafukuza kama mbwa. Hii nchi ni ya kila mmoja.

Kuna watu nimeona wanasema nchi za weupe hakuna wamachinga....nawaambia watembee waone kuna nchi wamachinga mpaka kwenye reli.
 
Serikali ambayo haikusanyi Kodi,itaanguka.Sasa machinga wanaotaka wafanye biashara sehemu yoyote na pia wafanye bila kulipa Kodi.Hiyo haiwezekani.
 
Na wewe unaunga mkono wakapange biashara hata kwenye mlango wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya? Hilo litakuwa ni Taifa la namna gani? JPM anafahamika alikuwa mtu wa kupenda sifa za hovyo hovyo especially kutoka kwenye makundi ya watu wenye uelewa mdogo katika jamii
Sifa ambazo hazijengi taifa!! Hiyo hotuba ni kujichukulia madaraka mkononi na sio kuongoza
 
Bado sijaona sababu ya msingi kabisa ya kuwaondoa wamachinga barabarani.

Kama wanaziba njia na wanakaa kwenye mifereji ilo linazungumzika na inawezekana kuwasogeza sio kuwafukuza kama mbwa. Hii nchi ni ya kila mmoja.

Kuna watu nimeona wanasema nchi za weupe hakuna wamachinga....nawaambia watembee waone kuna nchi wamachinga mpaka kwenye reli.
Wewe nawe, wanapangwa na kuwezeshwa kuwa na anwani ili walipe kodi!! Katika ujenzi WA taifa lazima wananchi walipe kodi stahiki kulingana na kipato!! Unaziba mbele ya mlipa kodi na wewe hulipi kodi Unategemea maendeleo!?
 
Na wewe unaunga mkono wakapange biashara hata kwenye mlango wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya? Hilo litakuwa ni Taifa la namna gani? JPM anafahamika alikuwa mtu wa kupenda sifa za hovyo hovyo especially kutoka kwenye makundi ya watu wenye uelewa mdogo katika jamii
Kwenye hiyo video JPM anataka wapewe utaratibu mzuri wa kufanya biashara kabla ya kuwaondoa.
 
Waende wakafanyie biashara wapi?
Kwani unafikiri hawa machinga ni wageni basi, walikuwepo katika minada na baadhi ya masoko, sasa wakati Mwendazake matajiri hawakuzikubali sera zake akaona awauzie hifadhi za barabara wamachinga kwa shilingi elf 20,000. Huu ulikuwa ukiukwaji mkubwa wa sheria za miji.
 
Wewe utakuwa mgeni nchi hii au hujui historia ya wamachinga nchini
 
Mnawapigia kelele machinga watoke bara barani ili mpitishe magari yenu, yes mpo sahihi lakini kumbukeni kuwa kuna watu hawana ajira na wanafamilia, wanategemea wauze magazeti, wauze mahindi ya kuchoma bara barani walishe familia
 
Back
Top Bottom