Siku hayati Magufuli aliposimama imara kutetea wamachinga, mbele ya Samia

Siku hayati Magufuli aliposimama imara kutetea wamachinga, mbele ya Samia

Bado sijaona sababu ya msingi kabisa ya kuwaondoa wamachinga barabarani.

Kama wanaziba njia na wanakaa kwenye mifereji ilo linazungumzika na inawezekana kuwasogeza sio kuwafukuza kama mbwa. Hii nchi ni ya kila mmoja.

Kuna watu nimeona wanasema nchi za weupe hakuna wamachinga....nawaambia watembee waone kuna nchi wamachinga mpaka kwenye reli.
Hamna aliyesema wafukuzwe kama mbwa..waondolewe barabarani
 
Wavuvi wanalipa kodi?
Wakulima wanalipa kodi?
Wafugaji wanalipa kodi?

Mnachekesha na vijisababu vyenu [emoji23][emoji23]
Afadhali hao wanafanya uzalishaji kuliko hawa machinga hawazalishi chochote..wakawe wakulima, wavuvi wazalishe
 
Thanks Mama D....uko sahihi Sana kwa. andiko lako hili....sisi wengine tumebahatika kuona awamu zote zauongozi wa nchi hii..kwangu Mimi baada ya Nyerere kiongozi anayefuatia kwa mikakati ya dhati kwa nchi yake na hasa maendeleo ya watu wake ni JPM...this man was a true son of Tanzania and Afrika....Binafsi huwa namfananisha na Thomas Sankara aliyeuawa kwa mbinu za kijasusi za ufaransa...JPM alikuwa anaipenda nchi hii kwa dhati...ila yeye mwenyewe alijua asingedumu kwa muda mrefu na ndiyo maana alikuwa anasema amejitoa mhanga...mabeberu siku zote hawako tayari kumuona kiongozi wa nchi ya dunia ya tatu na mwenye msimamo Kama wa JPM...ndiyo maana viongozi Kama Chavez, Sankara, Ghadafi, Lumumba na wengine waliuawa...
Tanzania tulibahatika kuwa na JPM na itachukua miaka mingi TZ na Afrika kumpata Kama yeye....

Zetu dua🙏
 
Serikali isikwepe wajibu wake, kama haiwezi kutafuta permanent solution basi itafute temporary solution. Hawa watu wanafukuzwa wanaenda wapi?
Warudi walikokua kabla, wote wale walioko mabarabarani wana meza zao katika masoko na minada, wameziacha wamezikodisha kwa machinga wengine, hivyo hakuna ambae hana pa kwenda, hata hivyo si jukumu la mamlaka kuwatafutia mahali pa kuenda , sababu hapo walipo siyo mahali sahihi na ni kinyume na taratibu za mipango miji.
 
Kumbe hata Mwendazake aliona kwamba wamachinga wanahitaji kuwekewa utaratibu mzuri ndio wahamishwe. Ndio agizo la Mama Samia pia. Hawatofautiani.
Nani kasema wanatofautiana? Waguse wamachinga isivyo halali uone muziki wake !
 

Siweki neno:

Lakini ukitaka kujua kwa nini wamachinga walimlilia sana, kujitokeza kwa wingi njiani kumzika ni hii hapo juu

Hata Rais wa awanu ya pili mzee Ali Hassan Mwinyi wakati akisoma Tanzia yake huko Chato, alimsifu Hayati kwa kutowasumbua wamachinga kwenye utawala wake!

Wamachinga wanatafuta hela ya kula, Wasaidiwe kwa kujengewa miundombinu kwanza na siyo kufukuzwafukuzwa kama mbwa
Jifunze kuishi bila mwendazake. Kila nabii na zama zake ndugu.
 
Bado sijaona sababu ya msingi kabisa ya kuwaondoa wamachinga barabarani.

Kama wanaziba njia na wanakaa kwenye mifereji ilo linazungumzika na inawezekana kuwasogeza sio kuwafukuza kama mbwa. Hii nchi ni ya kila mmoja.

Kuna watu nimeona wanasema nchi za weupe hakuna wamachinga....nawaambia watembee waone kuna nchi wamachinga mpaka kwenye reli.
Huko kwa weupe ni kwao, ndio maana hata Mkuu wao kasema tusijifananishe nao kwa kutoa mfano wa coca cola.
 
Hivi ni jukumu la nani hasa kuwatafutia watu sehemu za kufanyia biashara zao?
 
Mleta mada unadhani maamuzi yalikuwa sahihi? Unaweza kusolve tatizo kwa njia rahisi lakini ukafanikiwa kwa muda tu. Kwa hali ilivyo kuacha biashara hii bila mpangilio ilikuwa ni kosa kubwa sana na sasa linaigharimu serikali. Hii biashara imekuwa kichaka cha wanaokwepa kodi pia.

We unadhani kila mfanyabiashara akifanya umachinga serikali itatekeleza vipi shuhuli za maendeleo. Maji, Elimu, Barabara, Afya na miundombinu mingine itagharamiwa na nini.

Tuache kuleta kauli za nyuma na kutaka zifuatwe kama msahafu au Biblia. Zilikuwa na mashiko kwa kipindi kile na si sasa.

Raisi alishaweka wazi hataki kukusanya kodi ya dhuluma bali kodi ikusanywe kwa haki. Hivyo tutengeneze mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara waweze kulipa kodi. Tulipe kodi kwa maendeleo yetu wenyewe
 
Ubunifu wa Morogoro ulitakiwa kuwa applied nchi nzima .... andaa mazingira then waelekeze watu kwenda sehemu sahihi. JPM namkubali sana kwa kudeal na viongozi wasio wabunifu wasio na mawazo endelevu, wazembe na waoga.
 
Labda utakuwa unaishi Afghanistan wewe... Huwezi kuvua bila leseni, mkulima kuna ushuru wa mazao kwa gunia ukipeleka sokoni, mfugaji ukipeleka mifugo mnadani kuuza unalipa ushuru pale mnadani...
Rudi shule utoe umbumbumbu...kwani machinga si wanalipia vitambulisho
 
Back
Top Bottom